Dar es Salaam, Tanzania
Oktoba 15, 2008
Vodacom ikishirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa GSMA na kampuni ya Qualcomm, kupitia mkakati wa Wireless Reach imeunganisha migahawa mitatu ya intaneti katika miji mikubwa mitatu nchini kupitia mtandao wake wa mawasiliano, ili kuziwezesha jamii za ndani kunufaika na kasi kubwa ya kupata habari kutoka vyanzo mbalimbali vya huduma kwenye tovuti.
Ikiwa inaendeshwa na wajasiriamali wa ndani kila mgahawa wa intaneti una vifaa mbalimbali vilivyounganishwa na mtandao wa Vodacom wa HSPA ambao unaweza kupata mawasiliano kwa kasi ya megabaiti 7.2 kwa sekunde.

Watanzania watamudu kulipia ada kidogo kwa kutumia njia ya kompyuta ambayo itawawezesha kufikia mtandao wa Intaneti katika kuitafuta habari muhimu kuhusu kila jambo kuanzia kwenye elimu hadi kwenye afya, bei za bidhaa na hata utabiri wa hali ya hewa.

Katika nchi ambayo njia za kawaida za simu na kompyuta ni migahawa hiyo itawawezesha watanzania wa kawaida kufurahia kupata mawasiliano ya intaneti na faida nyingi zinazohusiana kwa mara ya kwanza katika maisha yao.

Migahawa mitatu ya kwanza ya intaneti katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma, na Arusha, itafuatiwa na mingine mingi katika maeneo mbali mbali ya Tanzania.
Migahawa hiyo ikiwa kwenye makontena yaliyotengenezwa kwa ajili ya shughuli hiyo maalum, migahawa hiyo pia itauza bidhaa nyingine na huduma zinazotolewa na Vodacom kama vile vocha, kulipia miito ya simu na kuchaji simu pamoja na kutumika kama wakala kwa ajili ya huduma ya kutuma pesa kwa njia ya simu ya M-pesa.

Tanzania hivi sasa ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazoendelea kwa kasi zikiwa na wastani wa kukua kwa kiwango cha Pato la Ndani la Taifa kwa kiwango cha asilimia 6.5 kwa mwaka. Kutokan na hali hiyo upatikanaji wa habari na mawasiliano ni msingi wa kukua kwa mawasiliano zaidi.

Vodacom Tanzania, kupitia sauti na huduma zake kwa miaka minane iliyopita imekuwa kwenye mstari wa mbele kuhakikisha kuwa yanakuwepo mawasiliano muhimu kwa wananchi wa Tanzania.

“Tunajivunia kwamba katika kuongeza kwenye idadi ya watoaji wa mawasiliano suluhisho kwa wananchi wa Tanzania ushirika wetu mpya na GSMA na Qualcomm katika kuleta migahawa intaneti yenye kasi kubwa hapa nchini,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Dietlof Mare.
Migahawa ya Intaneti itahakikisha kufikiwa kwa huduma miongoni mwa wanafunzi, wafanya biashara na Watanzania wote wanaohitaji kuwasiliana na kuendelea kupata mawasiliano ya mamboyanayoendelekutokea nchini, Afrika na kwingineko duniani kwa kasi, kuaminika na kwa bei wanayoimudu.

Vodacom Tanzania imetumia utaalamu na rasilimali za Mfuko wa Maendeleo wa GSMA na mkakati wa Qualcomm wa Wireless Reach kuanzisha modeli ya kibiashara na teknolojia katika kupitia kwenye migahawa ya intaneti.

Mfuko wa Maendeleo wa GSMA una uzoefu mkubwa katika nyanja hii kwani umeshasaidia katika kuanzishwa na migahawa ya intaneti iliyounganishwa na mitandao nchini Bangladesh.

Qualcomm, imekuwa inaongoza kwenye kuanzisha na kubuni teknolojia za juu zisizotumia nyaya na upatikanaji wa takwimu ikiwemo HSPA imekuwa inachangia kuleta utaalamu wake kwenye miradi na kuwezesha zana za 3G na vipuli, huduma ya mtandao, mafunzo ya teknolojia na usimamizi wa miradi.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa GSMA Dawn Haig-Thomas alisema, “Mawasiliano mapana yanayohamishika yamekuwa ni muhimu katika kumudu kufikiwa kwa intaneti na mamilioni ya watu duniani ambao wanaishi kwenye mitandao ya intaneti ya kudumu.

“Ubunifu wa kushirikiana mtazamo wa kuufikia uliobuniwa na Vodacom unaonyesha jinsi gani waendeshaji wanavyoweza kuifanya huduma kubwa na muhimu inayotolewa na mtandao mpana wa mawasiliano unaohamishika kufikiwa na watu wengi zaidi.

“Qualcomm, ina furahi kuunga mkono mradi huu kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa GSMA kupitia mkakati wa Wireles Reach,” alisema Mkurugenzi mwandamizi wa masuala ya kimataifa kwa serikali wa Qualcomm.
“Kuanzishwa kwa mtanzao mpana wa teknolojia inayohamishika kama vile HSPA utawawezesha Watanzania kuunganishwa sehemu yoyote duniani na kuwezeshwa kuvifikia rasimali wanazozihitaji kwa bei wanayoimudu. Vikisaidiwa na Mtandao wa Vodacom wa migahawa ya intaneti itafungua mlango kwa habari za kielemu, tiba na habari nyingine muhimu kwa ajili ya kuboresha maisha.”

Kuhusu Vodacom
Vodacom Tanzania Limited (Vodacom) ni mtandao unaongoza nchini Tanzania kwa kutoa huduma ya GSM/3G na huduma pana ya mawasiliano ya HSPA kwa wateja zaidi ya milioni 4.5.

Vodacom inaongoza imetumia teknolojia hivyo kuwezesha kuweka bidhaa na yenyewe katika kutafuta suluhu kwa njia yoyote ya mawasiliano.

Vodacom inaendelea kutoa mitandao ya kipekee yakiwa yanenea kwenye eneo kubwa ikiwa na ubora wa hali ya juu na kwa viwango ambavyo wateja wanamudu kukiw ana mtazamo wa kuwawezesha mamilioni ya Watanzania kwa njia muhimu za mawasiliano ya simu.

Kuhusu GSMA GSMA ni kundi la kibiashara duniani likiwalisha waendeshaji wa simu selula ndnai nchi 218 duniani, umoja huu unawakilisha zaidi ya mikondo ya mawasiliano bilioni 3 ya GSM na 3GSM kwa zaidi ya asilimia 86 ya maunganisho ya simu selula duniani. Kama nyongeza watengenezaji na wasambazaji zaidi ya 200 wanaunga mkono mikakati ya umoja huo.

Malengo ya msingi ya GSMA ni kuhakikisha kuwa simu selula na husuma zisizo za nyaya zinafanya kazi sehemu mbalimbali duniani na zinapatikana au kufikiwa kwa urahisi kukuza thamani yake kwa wateja binafsi na uchumi wa taifa wakati zsiunda fursa mpya za kibiashara kwa waendeshaji na wasambazaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. where is the website you are advocating?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...