
Naibu Waziri wa Habari na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (kulia) akifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain kwa watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Forodhani mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja Ununuzi, Uuzaji na Usambazaji wa Zain, Omar Zuberi

Baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Forodhani mjini Zanzibar wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain mjini Zanzibar juzi.

Baadhi ya akina mama wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Forodhani mjini Zanzibar juzi.

Meneja Ununuzi, Uuzaji na Usambazaji wa Zain, Omar Zuberi, akikabidhi jezi kwa Naibu Waziri wa Habari na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (kulia) wakati wa hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Zain kwa watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Forodhani mjini Zanzibar juzi. Jezi hizo zilitolewa na Zain kwa ajili ya timu ya Naibu Waziri Kombo.

Naibu Waziri wa Habari na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (kulia) akipokea juisi kutoka kwa Meneja Ununuzi, Uuzaji na Usambazaji wa Zain, Omar Zuberi, kwa niaba ya watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Forodhani wakati wa hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Zain kwa watoto hao mjini Zanzibar juzi. Zain ilitoa vyakula anuwai vyenye thamani ya sh. 500,000 ikiwa ni pamoja na sukari, mchele, unga wa ngano, mafuta na sabuni. Kushoto ni Mratibu Biashara na Maendeleo wa Zain Zanzibar, Aloyce Kimaro.
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeanza mazungumzo na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania, ili idhamini mashindano ya Ligi Kuu Zanzibar.
Hayo yalibainishwa mjini Zanzibar juzi usiku na Naibu Waziri wa Habari na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo wakati akipokea jezi zilizotolewa na Zain kwa timu yake, katika hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na kampuni hiyo ya simu kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Forodhani.
"Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, naishukuru Zain kwa msaada inaotoa katika miradi mbalimbali ya jamii hususan elimu, tunaamini bado mnaendelea kupanua wigo mpana zaidi wa kusaidia jamii pia katika sekta ya michezo.
"Hivi sasa tayari SMZ imeanza kufanya mazungumzo na Zain ili idhamini Ligi Kuu Zanzibar, mambo yakienda vizuri tutawatangazia," alisema Naibu Waziri huyo, kauli iliyopokewa kwa mayowe na vifijo kutoka kwa waliohudhuria hafla hiyo.
Zain, kampuni ya simu inayoongoza kwa kutoa huduma bora katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, mbali na kusaidia miradi mbalimbali ya jamii, pia imekuwa ikisaidia kuinua muziki, sanaa na michezo kwa ujumla.
Hivi karibuni, Zain ilisaini mkataba wa miaka minne wa kuidhamini timu ya soka ya taifa ya Saudi Arabia (SNFT) na pia Zain ilidhamini mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Beijing, China.
Naibu Waziri Kombo alisema anaamini endapo Zain itaridhia kudhamini Ligi Kuu Zanzibar, itakuwa ni mojawapo ya hatua ya kutimiza malengo yake na kutekeleza kauli mbiu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa).
MICHUZI HIYO PICHA YA TATU KUTOKA JUU HAO NI WATOTO YATIMA KWELI? MBONA NI WATU WAZIMA WENYE WAUME NA FAMILIA ZAO? NINI DEFINITION YA WATOTO YATIMA? AU HIZI FUTARI NI KUJIKUSANYA NA KUTAFUTA WATOTO WAWILI WATATU NA KUSEMA WATOTO YATIMA?
ReplyDeletekwa nini watoto wanashea sinia, kwa nini kila mtoto asipakuliwe kwa sahani yake? au kwa sababu ni yatima?
ReplyDeletewewe anon wa mwanzo namna gani? una matatizo gani? kwa nini husomi maelezo yaliopo chini ya kila picha ukafahamu kinachoendelea? kwa nini hukuuliza basi kama waliopo picha ya mwanzo kama nao ni yatima? ah hata sijui nikufahamu vipi, nadhani mwalimu wako wa shule alipata tabu sana.
ReplyDeleteanaon wa pili: kwanza kabisa hiyo sio sinia ni sahani! umeona wapi sinia kuwa size ndogo namna ile. pili labda wanakula pamoja kwa vile wao ni makobe ya mchana! :)
ReplyDeleteJAMANI UKUMWI SASA KWA NINI WATU WASHEE MASINIA . HAKUNA PAPER PLATES
ReplyDelete