Mheshimiwa Michuzi,
Naomba nidondoshee swali langu kwa wanajamii wa blogu yetu ya jamii.
Naomba nidondoshee swali langu kwa wanajamii wa blogu yetu ya jamii.
Ulaya tunajua ni uvivu, diet mbovu, na ukosefu wa mazoezi huchangia asilimia kubwa kuleta unene haswa maeneo ya tumboni/kiunoni. Je Afrika kwetu, ambako watu hufanya mazoezi kila siku (kutembea), na hula nyumbani zaidi (sio fast food restaurants) nini kinawaletea vitambi?....
naongelea wanawake kwa wanaume. Sehemu ya pili ya swali: Ni jinsi gani ya kuwasaidia kutokwa na tatizo hilo....Inaelekea wengi huona ni sifa, siyo tatizo.
Asante.
Mfukuampunga.
Asante.
Mfukuampunga.
Ohoo! Swali zuri sana. Huku Africa vitambi huletu na vitu vingi ikiwepo hilo ulilolisema. Watu huku wanapenda kula nyama sana wakimezea bia baaaridi(Yaani the kili)! Haswa kanda ya kaskazini mwa TZ. Halafu mazoezi kwao ugonjwa. Pia mikuku yaliyototoliwa kwa njia ya umeme nayo inachangia sana. Na hii ni mbaya sana wadau kwani hii huongeza sana neutranti za uzazi na hivyo kusababisha watu kuzaa ovyo. Matokeo ni watoto wengi wa mtaani na kuchoropoa mimba kwa wingi. Natumaini nimejitahidi kutumia taaluma yangu ya udokta kutoka chini mti kukujibu Asante.
ReplyDeleteUtapiamlo, ngano (aka beer), mataputapu (aka local brew.
ReplyDeleteJe huko Yuropa kuna wanawake wenye vitambi????
Huko mbele nundu siyo dili ila kibongobongo nundu dili, mtu ukiwa na nundu unaoneka upo njema,ukichomekea hata zile dili zetu za kizushi mtaani unaaminiwa.
ReplyDeleteSasa ivi kwa miji iliyoendelea kuna sehem za mazoezi nyingi gym lkn bei zake ni kama mshahara wa kima cha chini kwa mwananchi wa kawaida labda ufanye joging kimtindo au waishio maeneo ya fukwe basi waendeleze matumizi yake.
Kimsingi wanashauriwa wafanye sana mazoezi, coz obesity inasababisha game kwa bi mkubwa iwe fake, unakaribisha sukari, presure na magonjwa ya moyo harafu....nundu ni mzigo wa mwiba, virungu haviishi uswazi coz wadau wanajua wewe upo njema...kwa wale wenye magari badala ya kukaa sana kwenye foleni unaweza ukapaki gari ukawa unatembea au ukakimbia mdogomdogo, wafanyao kazi ofisi zilizopo magorofani, tumieni ngazi badala ya lifti...vilevile game za kifo cha mende zinalemaza, amkeni mtaja megewa...teheteeee
WANAUME WANAVITAMBI KUPITA KIASI AFRICA.KUTOKANA NA MAMBO YA NYUMBA MBILI NA KUOA WANAWAKE AMBAO ELIMU YA CHAKULA HAWANA . HALAFU VILEVILE WANAWAKE WENGI SANA WANAFIKIRI NDOA NI MAPISHI YA MAFUTA NA SHURTI MWANAUME APIKIWE KWANZA . MIMI HAPA MUME WANGU ANANIPIKIA MIMI, NA ANAPIKA CHAKULA SIMPLE . NA WASHAURI WANAWAKE WENZANGU MWACHE MWANAUME WAKO AKUPIKIE UTAONA CHAKULA SIMPLE KINA NYANYA ORIGINAL NA KITUNGIUU NA MAJI . NA ANGALIA SISI WAKINA MAMA TUKIPIKA MARA NYANYA ZAKOPO, NAZI, SPICES MAFUTA AMBAYO NI GALLON . MWANAUME MAFUTA OLIVE OIL BABU .INAKUWA WORSE PALE KUNAPOKUA NA MWANAMKE MWINGINE MASHINDANO YA MAPISHI NDIO YANAPOANZA.
ReplyDeleteHALAFU WANAUME HAWAJUI UKIWA NAKITAMBI UJUE MWANAMKE ATAKUCHEAT SASA , HIVYO VITAMBI NI KARAHA KWENYE MAPENZI
ReplyDeleteNILIMUACHA MUME WANGU MAANA ALIVYOONZA KUWA NAKITAMBI SHUGHULI SIKUIWEZA KABISA .NIKICHEFUCHEFU MWANAUME KUWA NA KITAMBI
ReplyDeletePombe nyingi na vyakula vya mafuta, chumvi na sukari zaidi. Vile vile Kuchelewa kula jioni halafu kwenda kulala mara baada ya kula.
ReplyDeleteWatu wengi wanaona fahari kula nyama zenye mafuta mengi. Angalia wavuvi ambao wanakula sana samaki, huwezi kuwaona na vitambi.
Vitambi na uzito mkubwa vinaharibu unyumba na kuleta msingi wa magonjwa mengi. Vyakula vyetu vingi ni vya kukaanga, kuanzia maandazi ya chai ya asubuhi na manyama ya vyakula vya mchana na jioni. Tuongeze kula mboga za majani na nyama kula kwa wastani. Soda vile vile zio nzuri kwa afya.
KITAMBI ASILI YAKE NI KULA NA KUNYA HUMO HUMO! haaaa., mtanisamehe wenye vitambi! YUCK!
ReplyDelete...Mada nzuri sana, lakini majibu mengi hayajasaidia watu. Naomba mdau anayweweza anipangie menu simple kabisa toka asubuhi nadi usiku mimi mfanyakazi wa kawaida wa jiji la Dizim ambayo itanisaidia kupiga vita kitambi. Nitashukuru!
ReplyDeletenyumbani kwanza ni culture mbovu tuliyonayo
ReplyDeleteUkiwa na kitambi au mwanamke mnene basi wewe una hela au unatunzwa vizuri na mumeo
Pili watu wanakula nyumbani lakini most of the time ni unhealthy food
- Nazi kwa wingi,
- tunakula too much curbs kuliko greens and proteins,
-mafuta ya chakula mengi ni from animal products,
-maziwa yetu ni full cream nayo ni balaa bora sio kila mtu anajua kutengeneza cheese na hayo maziwa ingekua hivyo tungeshaisha wote
- watu hawajui umuhimu wa kula matunda
- tunakula chakula kizito very late at night
hebu angalia wahindi diet yao ni mbovu sana tu kama yetu lakini wao kinachowasaidia ni kuwa wengi vegetarians. Hivyo wanakula sana mbegu na majani kuliko sisi na nyama kwanza bila nundu mtu hajaridhika na nyama ya mbuzi choma, kuku za kuchoma,
Wewe unayetaka menu ya subuhi mpaka jioni ni vigumu mtu kukupangia bila kukufahamu....labda kama ukienda kwa nutritionist...ndio akupangie individual. Unatakiwa ujue kuwa chakula kinatakiwa kuliwa tofauti kati ya mtu na mtu. Na nikutokana na gender, age, height na shughuli unazozifanya kwa siku.....Lakini callories intake per day kwa mwanaume hata kama ni nini zisiwe zaidi ya 2500
ReplyDeleteKuna hii calculator inasaidia kujua uhahitaji ngapi per day
calucator
kwa vile vyakula vyetu havina kuandikwa kuwa vinaprovide calories ngapi kwa siku cha muhimu ni kuwa greens first.....
Ukiwa unakula mlo wowote anza kwanza na majani...asubuhi matunda kwanza kabla ya kunywa chai yako au ni bora ule matunda tu bila chai....na kama ni mnywaji wa sukari kata half of what you normal take...tunakula sana sukari bongo...
Mchana na jioni...anza na kachumbari, mchicha, salad etc hizo zinajaza tumbo mapema ..halafu unakula proteins kwa wingi then kama ni starch ndio unakula mwisho...heh hehe heheheh....sasa kama ni ugali unaulumanga bila mboga mwishoni....teh teh teh teh tet .....well nadhani hapa kwa vyakula vyetu ni heri ule mchicha mwingi na maharaje lakini ugali uwe kidogo sana ....that will do it
Move around ....watanzania wengi wa mjini siku hizi hatujui kutembea tunazania kupanda vibasi toka posta mpya kwenda ya zamani ni umaarufu ......tembea as much as possible
maji kwa wingi kunywa kila siku. Achana na soda na beer punguza.....Utashangaa jinsi mahipsi na kitambi vinavyoisha bila hata wewe kujua....
Unene kwenye familia....kama umeona ndugu zako wakiwa wakubwa hunenepa jitahidi uanze mapema kucontrol kwa vile na wewe chance ya kunenepa ni kubwa
kama una baba au mama amekufa na heart attack ....jitahidi kucheck bp yako kila maraukishafikia 35 and above kwa vile chance ya wewe kuwa na ugonywa wa moyo ni kubwa...na hii ni kwa wanaume sana. Wao dalili za HP hazijionyeshi mpaka iwe imeshakua mbaya sana..lakini wanawake wengi huumwa na kichwa, moyo unakwenda mbio, kizunguzungu, blind sport etc
I am serious kitu kimoja kwa siku ukianza kubadilisha katika life style yako kweli our life expectancy itapanda sana...Inasikitisha sana ukiangalia ati yakwetu ni 45 years
Kweli kitambi ni ugonjwa lakini wengi hatujui na wengi tunashindwa au tunaona karaha kufanya mazoezi! Pamoja na masuala ya upishi wa mafuta kupita kiasi kuna suala la desturi za kula! Sio siri nikiwa nyumbani kwangu nakula kidogo sana nafikiri kwakuwa nakuwa niko mezani; ukiacha suala la balanced diet!Jamani ukienda kijijini au ktk nyumba zetu nyingine za mjini chakula kinaliwa kwa pamoja (kwenye sahani moja)mkiwa mmekaa chini mpaka wengine wanavua mashati! Hapo ndugu yangu watu wanakula sana bila kipimo! Na Chajio kinaliwa usiku wa saa 3.00 baada ya hapo kulala kwahiyo hakipati nafasi ya kulainishwa!Lakini lingine ni kuwa ukiwa na kitambi na ukitaka kukipunguza! Subiria magazeti ya Udaku hasa kama wewe maarufu!
ReplyDeleteKweli kitambi ni ugonjwa lakini wengi hatujui na wengi tunashindwa au tunaona karaha kufanya mazoezi! Pamoja na masuala ya upishi wa mafuta kupita kiasi kuna suala la desturi za kula! Sio siri nikiwa nyumbani kwangu nakula kidogo sana nafikiri kwakuwa nakuwa niko mezani; ukiacha suala la balanced diet!Jamani ukienda kijijini au ktk nyumba zetu nyingine za mjini chakula kinaliwa kwa pamoja (kwenye sahani moja)mkiwa mmekaa chini mpaka wengine wanavua mashati! Hapo ndugu yangu watu wanakula sana bila kipimo! Na Chajio kinaliwa usiku wa saa 3.00 baada ya hapo kulala kwahiyo hakipati nafasi ya kulainishwa!Lakini lingine ni kuwa ukiwa na kitambi na ukitaka kukipunguza! Subiria magazeti ya Udaku hasa kama wewe maarufu!
ReplyDeleteOngeeni ki-takwimu. Watanzania wengi asilimia 96 hukaa vijijini, hula mlo mmoja kwa siku wenye thamani ya chini ya dola moja.
ReplyDeleteHao hawana nishati ya kuoikia wala mafita ya kukaangia mahanjumati manyozungumzia.
Asila mia 4 ta wabongo huishi mijini wengi wao kwa shida tupu.
Kwa wengi hasa watoto wa mjini na vijiji 'ukubwa' wa matumbo ni 'kwashakor' ua ugonjwa wa utapia-mlo.
Kuna sehemu ndogo ya jamii ya watu wa mijini hupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku na hao man wa ona na vitambi ni mafisadi au jamii ya mafisadi. Kwa hiyo vitambi ni ugonjwa wa mafisadi na huletwa na ufisadi kwa sababu ufisadi humsukuma mtu ale, afakamie, anywe, asombe, ahamishe, alimbikize, aharibu kila kizuri cha wengi.
Sifa kubwa ya fisadi ni ubinafsi wa kupindukia na kutojali wengine ila yeye na tumbo lake. Jirani alale na njaa lakini yeye ale mpaka vingine avitupe kwenye pipa la taka.
...Anony wa 1:34 angalau wewe umejaribu kutoa mwanga wa namna ya kuepuka kitambi. A Thousand Thanks!
ReplyDeleteJamani, mimi ni mswahili, nipo ughaibuni kwa takribani miaka kadhaa sasa, naomba nifahamishwe kuhusu hili neno KITAMBI au KITAMBIO. Je? ni swahih kusema Kitambio? kama kichwa cha habari ya mada hii kinavyojieleza?? Maana nielewavyo mimi Kiswahili ni lugha inayokuwa, sasa kwangu KITAMBIO ni msamiati bado.Sijui ndio kiswahili cha siku hizi!!! Naomba msaada wenu.
ReplyDeleteMdau Ughaibuni.