Home
Unlabelled
lala unono salamanda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
tafadhali wacha kubomoa hizo nyumba jamani. hizo nyumba wazikarabati kama wanataka kujenga waende nje ya mji! kwasababu nyingi kwanza mji utakuwa , na msongamano mjini utapungua.
ReplyDeleteI object what is going on in Dar city centre! Why do we want to concentrate all skyscrappers in the city centre while other infrastructure e.g drainage systems, roads, etc haven't been upgraded to match up the new high rise buildings requirements? Can't those high-rise buildings be built a bit far from the city centre to avoid congestion? To my opinion, we can keep our old Dar as a touristic site and for the benefit of future generations!
ReplyDeleteMdau,
Gotheburg, Sweden.
hizo archictecture za zamani you can never find them duniani. wazikarabati tuu. viwanja viko vingi huko segerea, kibaha tegeta wapanue mji tuu nibora na maendeleo yataongezeka, kuliko kubanana hapo mjini na migorofa mingi barabara ndogo ,parking za magari hakuna foleni tele ,huo mji haukujengwa kuhost magari mengi naomba serekali wazingatie swala hilo!
ReplyDeleteMimi ninashindwa kuelewa bongo zetu wabongo tulizipata wapi? Tunaua, tunafuta historia hivi hivi! kwa nini hivyo vikwanguaanga visitafutiwe sehemu za nje kidogo ya katikati ya jiji (ikiwa ni pamoja na kukuza mji) ili pamoja na usasa ambao hakuna anayeupinga tuhifadhi ukale ambao utachangia kuhifadhi historia pamoja na kukuza utalii wa kiutamaduni (cultural tourism) kama si leo basi kwa vizazi vijavyo. Tatizo la watawala wetu ni kufikiri kuwa jiji ni Samora ave tu basi na itakuwa hivyo milele na milele!!! shame on us Bongoleses
ReplyDeleteJAMANI MIMI NASIKITIKA SANA SALAMANDA KUBOMOLEWA KAMA NI AMRI YANGU NINGESHAURI IWE KIVUTIO CHA UTALII WALETWE WAHANDISI WAZURI WASI NA VYETI FEKI WAIMARISHE MISINGI YA HILO JEGO LITUMIKE HATA MIAKA 50 SASA TANZANIA TUTABAKIZA JENGO GANI LA KIISTORIA KAMA YOTE TUTAYABOMOA? UTALII SIO SIMBA AU NGIRI TU JAMANI JAMANI TIZAMENI WAKUBWA.
ReplyDeletewww.kipepeotours.com
INANIKUMBUSHA ZAMANI SAANA ENZI HIZO FORODHANI PRIMARY LILIAN TAIRO, ZAKIA DINDII NA SADA SHAHA NA WENZIE WATEMI KWA SALAMANDER IECECREAM HAWAJAMBO WALIKUWA WANALETA KASHESHE HAO
ReplyDeleteHIYO NTUMBA NI MUHIMU SAANA MNABOMOA YA NINI. KILA MTU ANAPAJUA HAPO
ReplyDeleteInasikitisha sana kuondoa haya majengo ya kihistoria...Naamini ni hali ya ubinafsi ilyoyotawala watoa mamuzi wa jiji na tamaa za pesa. Kwa nini isianzishwe new DSM eneo la Kigamboni na DSM ya sas ibaki kwa ajili ya historia.....
ReplyDeleteWadau hakuna anayewasikia, hapa bongo ukiwa na fedha unaweza kuhamisha chochote ili mradi unaongea vizuri na wakubwa wala hutaulizwa fedha umepata wapi. Mfano huu unijieleza!!!
ReplyDeleteMichuzi unaweza kutusaidia kufikisha maoni haya kwa NGO yo yote inayohusika na hifadhi za utamaduni na kuwashauri waende mahakamani kuweka stop order kwa niaba ya wananchi. kwa hakika inasikitisha sana. wabongo tumerogwa na nani?
ReplyDeleteMambo ya kuiga kijinga. Tunalilia kupromoti utalii halafu vitu ambavyo tunavyo sisi wenzetu hawana tunabomoa ili tujenge sawa na walivyo navyo wenzetu. Sasa mtu akitoka Chicago au New York ataona nini cha ajabu na kikwangua anga chamtoto?
ReplyDeleteHalmashauri zetu za miji aibu tupu. Acheni uvivu wa kufikiria na kutafuta njia za mikato.
Hivi Lawyers Environmental Action Team LEAT hawawezi kuingilia sakata hili kwa gia ya mazingira? Tumeshaona matatizo ya maegesho kwenda jijini, thamani ya jengo hilo kihistoria, matatizo ya majitaka na majisafi, msongamano barabarani nk. LEAT, saidieni kuokoa jahazi kama mlivyofanya na mradi wa kamba mto Rufiji.
...Hivi kwa nini watu hawamuigi yule aliyekwenda kujenga Ubungo Plaza kule Uungo? Amekosa nini? Mbona makampuni na mabenki kibao yamekimbilikia kukodi pale, ukiachilia mbali 4 star hotel iliyopo mule???? AACCHHHENI HIZOOO!
ReplyDeletehaha wanataka kutengeneza DOWN TOWN kama miji mingi ya nchi zilizoendelea....Ila cha kusikitsha ni kuwa hizo nyumba nyingine ni za kihistoria zingekarabatiwa na kutumika kwa shughuli nyingine... Da historia kwetu haina umuhimu kabisa!! Hii noma
ReplyDeleteMichuzi afadhali umeondoa yale maherufi yako bwana yalikuwa yananikera kweli nikiweka maoni
ReplyDeletetuko tunapinga kwa nguvu zote. kama wanataka waende kurasini acheni mjini kubakie kama kulivyo. jengo mali sana hilo. halmashauri iko wapi??????????????????????? uuuuuuuuuuiuuuuiiiiiiiiiiiii.mangi london
ReplyDeleteWadau kam unaweza kununua chochote naomba niuziwe ikulu........ Nawezapata cotact za anaye husika
ReplyDeletehizo nyumba 'made in india'...mie nasema 'good ridance of bad rubbish'...tunataka nyumba za kisasa!!!
ReplyDeletesi wajenge jiji jipya waache hayo majumba ya zamani yawe historical buildings?
ReplyDeleteWatu bwana ndio maana walichoma vitabu vya zamani....hatuna hata historia ya nchi na majumba pia tunayaangamiza......
MIMI NAONA BORA KUSHUSHWE MASKY MANKE HUMU WOTE SIJUI NISEME NI WARUNDI ??HAWATAKI MAENDELEO YETU YA DAR ES SALAAM KUWE CITY .TEREMSHA BABA YUSUF MANJI!!LAKINI TUHURUMIE SIMBA
ReplyDeletemade in india you are correct rafiki yangu, however, quality group is also made in india and many other building are made in india...what difference does it make to you...wewe una unabagua these buildings and i am sure you are like wakaburus unabagua watanzania wenzako...not good to be racist in these day and age,,,think again
ReplyDeletesasa balozi wa nani.. mimi nataka hicho kifusi. Kina DILI china ua kuna ufisadi?
ReplyDeleteHilo Jengo lisibomolewe ni la Kihistoria!Ligeuzwe kuwa Maktaba ya Kumbukumbu za Historia ya Tanganyika na Zanzibar kabla ya mwaka 1850 AD !Lifanyiwe ukarabati lakini bila kupoteza Uasilia wake ili kuhifadhi kumbukumbu za Historia ya nchi yetu.This is more important to our Kids and Friends from the rest of the world than The Money and The Sky Scrapers you would want to give us!Serikali ni nani?Ni sisi watanzania katika ujumla wetu au ni vikaragosi vichache vilivyokalia ofisi za umma?Wamewekwa na nani katika ofisi hizo na Wanalipwa Mishahara na nani kama siyo KODI ZETU WATANZANIA?Watawezaje kutusaliti na sisi tukibakia tunawaangalia wakiiharibu nchi yetu,wakijaribu kuifuta historia yetu kwa tamaa ya pesa?Wameshindwa kumsaidia DR.MASAO,BINGWA WA TIBA YA MOYO KWA KUMKABIDHI JENGO LILE LIWE HOSPITALI YA KUDUMU,lakini wanathubutu kucheza na Historia ya nchi yetu?Tafadhali chukueni hatua kusitisha Ubomoaji wa jengo hilo.Kama ni kujenga jengo lenye Orofa 250 kwenda hewani,viwanja vipo bwelele maeneo mbalimbaliya jiji!Sehemu za Kihistoria zihifadhiwe!Naona hii serikali yetu sasa Yeboyebo tu haieleweki inakwenda wapi!Wasije wakatupeleka kusiko pelekwa watu,Kuzimuni!
ReplyDeleteJamani viongozi wetu!acheni kuwa na mawazo mpauko, adam kimbisa ofisi yako inafanya shughuri gani?
ReplyDeleteDar kila kitu hovyo Uchafu umekidhiri,Msongamano, maji kujaa katikati ya mji,
na mara nyingi tunasikia mnaenda China kujifunza mnajifunza nini au mnajifunza kutengeneza bidhaa feki?
Mwambieni huyo Manji wenu akajenge bweni huko tupunguze msongamano wa kwenda katikati ya mji,
Kule ocen Road kuna ujenzi wa hospital pembeni ya ufukwe,hivi ni kweli nyie mafisadi mnataka kutuambia hakuna sehemu nyingine ya kujenga hiyo hospital ni mpaka mjenge hapo ufukweni,
Vp Alhaji kimbisa? na hiyo hospital ikizinduliwa tunaomba muiite HINDU MANDALI BEACH RESOURT
kazi ipo kwa viongozi wehu tulionao,,eee Mungu ingilia kati sema na awa viongozi butu waelewe umuhimu wa kupanua jiji nje na sii kubananisha watu apo samora,k/koo"
ReplyDeleteinanitia huzuni saaana dar hakufai now yan balaa tupu.Manji hakika utapigwa daflau ni mnyazi-Mungu ukiendelea na U-EPA wako kwa viongozi wenye uchu
ili jengo ithink last year kikundi fulan cha wanaharakatwalionelea sana kusimamisha ubomoaji ili jengo,,sijui walitishiwa??
Hao wakaazi wa hio kikwangua anga watapaki magari yao wapi? hapa naona ndio mji utajaa kama nini.
ReplyDeleteKweli sisi ni wabongoless
Mimi nahakika kabisaaa, hapo watu washakula cha juu wajanja waweke vitu vyao waendelee kutesa. Nasema hivi, ufanyike uchumguzi wa kina, utakuta pana mkono wa mkubwa fulani ameshinikiza. AMA ni mkubwa huyo huyo alichelewa sasa anaona bora apachike kikwangua anga chake hapo avune mpaka wajukuuu na vilembwe kama si vining'ina. Tatizo tunadhani utalii ni kwenda Seronera au mikumi peke yake, na hata huko wameshindwa kupatangaza, na kidogo kinachopatikana wanagawana wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDelete"EE MUNGU, BABA YETU ULIYE MBINGUNI, MWENYEKUGAWA RIZIKI NDOGO NDOGO NA ZILE KUBWA PIA (sio za EPA), MWINGI WA REHEMA NA MWENYE KUREHEMU" tuepushe Watanzania na janga hili la ujinga wa mawazo; ufisadi na ubinafsi. AMEIN.
Watu wengine siwaelewi na nadhani ukisoma hapa maoni sitawaelewa tena milele. Yaani, kuna kitu gani muhimu cha jengi hili? Kweli tutawaleta watalii waione hili jengo liliooza? Kakuna kata nukta moja ya maana katika jengo hili. Natumaini wadau mamefika hapa kabla ya kufungua kinywa chao, kunanuka vumbi. Hio hoteli yenyewe ilikuwa haina service yoyote na chakula bikaya sio fresh ya shamba. Nasikitika kitu kimoja tuu, kuna mdau pale anauza magazeti ya nje siku nyingi, natumai atarudi katika dili yake, manake hakuna sehemu nyingine unaweza kununua magazeti ya kila aina ya dunia pale japokuwa atakugonga bei ukija macho juu.
ReplyDeleteNimepiyia comments mbali mbali, nimezielewa vizuri sana. Watu wanaposema utalii hawana maana ya kwenda kuona mbuga na wanyama peke yake, hata majengo ya zamani pia.
ReplyDeleteAnonym wa 10.20 Fika inaonesha u mshamba, tena mshamba haswa. leo nimekuhifadhi, bahati yako.
For your info, Salamander is no more, buriani.
ReplyDeletekuna watu wanaunga mkono huu ujinga na utakuta hao wao ndo ma planner wa jiji. zanzibar inauzuri ghani waulize?? roma au vatcan je?? regent street london ina vikwangua anga vingapi? angalia uzuri wa jengo la mamlaka ya reli, na lile la town hall ya jiji. kanisa la azania front, ikulu utalii si wanyama tu nyie nyumbu
ReplyDeleteHuyo jamaa wa 10.20 namjua sana, kwa sentensi alizoweka nimeweza kutambua ni nani, ni mtu wa karibu yangu sana, kwa kweli huwa ni mchemshaji wa kutupa, kwa kuwa ni jamaa yangu huwa inabidi nimvumilie tu, ila jamaa zangu wote hawampendi kabisa. Kibaya zaidi amesomeshwa na pesa za EPA, babake!!! saasa, JK amewatumbukia nyongo wazazi wake. Atakoma kuringa, anajua akitetea mambo zaidi hayatafichuka. Namuonea huruma kwa kuwa mzee wake ni mgonjwa wa kisukari tangu siku nyingi, hajakamatwa ila nimiongoni mwa watu wanaotajwa sana, piga ua, yule mzee akikamatwa atafia segerea tu. Naomba wadau wenzangu tusimsakame, yeye na familia yao wote wameshachanganyikiwa. Tumsamehe jamani, kwani hata demu wake kishamtosa.
ReplyDeleteNito- Dalas.
Ndugu Michuzi, nilidhani unachuja mani mengine ya wadau hapa. Lakini naona unaweka zote siku hizi. Huyu anony wa 2:00 hapo juu maoni yake hayana kichwa wala miguu. Sasa kama anamjua anony wa 10:20, tufanye nini?
ReplyDeleteYaani huwezi kutoa maoni bila ya kutishwa au kupigiwa mikwara ya kizamani... sijui maoni yake yanahusika vipi na ghorofa bofu la salamander. Wakati mwingine nilikuwa naomba urudi kuchuja watu, huyu anafaa kabisa kupiga maoni yake buti kwenye fumbi la trashbin la komyuta yako.