KP NA CHUO
CHUO KIMYAAAAAAAAAAAAAAAAAA

CHUO KIKUU CHA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM KIMEFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUANZIA SAA SABA MCHA WA LEO.

MADENTI WAMEPEWA HADI SAA 12 LEO JIONI WAWE WAMENDOKA CHUONI HAPO KUFUATIA MGOMO WAO WA KUTOINGIA MADARASANI KWA MUDA WA SIKU TATU MFULULIZO WAKIDAI HAKI SAWA KWA WOTE KATIKA KUPEWA MIKOPO YA KUBUKULIA.

HABARI KAMILI NA PICHA ZINGNE BAADAYE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. TATIZO SERIKALI YA AWAMU YA NNE UMEKUMBATIA USWAHIBA BADALA YA UTENDAJI NA UTEKELEZAJI YA KERO YA WANANCHI, SUALA SERA YA MIKOPO IMEKUWA NI KERO YA MUDA MREFU KWA WANACHUO NA MALALAMIKO YAMETOLEWA SIKU NYINGI LAKINI UTEKELEZAJI NI USANII MTUPU. WACHE WANACHUO WAGOMA HII NI HAKI YAO YA MSINGI KATIKA KUDAI HAKI ZAO. NCHI IMETALIWA NA MIGOMO NI LAZIMA TUJIULIZE KUNA NINI KATIKA UONGOZI HUU.

    ReplyDelete
  2. Serikali ya Kikwete isifanye mzaha na suala la wanafunzi wa vyuo vikuu!Mgomo wao huo unaweza kusambaa nchi nzima katika sekta nyingine pia.Wanachogoma wanafunzi ni halali kabisa.Pesa wanayo pewa hawapewi bure bali ni mkopo watakao kuja kuulipa pindi wakianza kazi na kupokea mishahara.Kuna tatizo gani katika hilo?Hivi kweli Nchi yetu haina uwezo wa kuwagharamia wanafunzi wote wa vyuo vikuu kwa kukopeshwa kila kitu na pesa hizo wakaja zilipa pindi watakapo maliza masomo?Pesa ngapi inafujwa na serikali pamoja na CCM kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile marudio ya chaguzi ndogo na huku ukiwa umebakia muda mfupi sana kabla ya uchaguzi mkuu ujao?Huo sio Utaaahira huo?Ni kitu gani?Hivi gharama yote ya kuwasomesha wanafunzi wote Vyuo Vikuu thamani yake ni sawa na Dhahabu Kilo ngapi?Hatuwezi kuichimba dhahabu hiyo ikalipia wanafunzi hao ambao watakuja ikomboa nchi yao siku za usoni?Kuna mtu serikalini mwenye hoja ya maana kuhusu pingamizi hiyo?Au UFISADI unawatokea nyongo sasa hata busara zimenyauka?Fanyeni haraka wanafunzi hao warejeshwe Vyuoni mara moja vinginevyo mgomo huo utafufuka upya kwa Wastaafu,Walimu,Madaktari na Wauguzi kote nchi nzima!Pesa ya kuchezea ipo,lakini ya mambo muhimu ya maana hakuna,ngoja kesho!Juzi hapa meshikishwa adabu kufuru iliyofanyika ya kupewa Nusu Bilioni na mfanya biashara mmoja,kwa biashara gani hiyo?We haya we!Ngoma mlioipiga mtaicheza wenyewe!

    ReplyDelete
  3. suali dogo tu kwa wanaojua yanyoedelea chuo kikuu, ni kwa nini kila mwaka ni kama mila lazima patokee migomo? yaani tangu niko mdogo nasoma magazetii mambo ya migomo, hii nni jadi?

    Pia inakuwaje kuwaje kwa wale wanafuzi wa kujitegemea? wasiotegeme serikali au kwa wanafunzi wageni? au hapo chuoni hakuna wanafunzi kutoka nchi za jirani? kama wapo inakuwaje kwa upande wao? wamelipa fees na madarasa yamefungwa?

    ReplyDelete
  4. Sasa basi!! tumechoshwa kusikia Chuo kimefungwa eti wanafunzi wamegoma kuingia darasani kwa madai ya kutokopeshwa pesa za kubukulia... yaani Chuo kimekuwa kama umeme wa mgao!!mara upo mara upo mara haupo!!! Hivi tunafaidika nini sote wananchi. serikali na wanafunzi husika!!? Kwa nini pasitafutwe muafaka wa kudumu ambao utaongozwa na sheria na mara pakitokea hitilafu basi sheria ifuate mkondo wake na siyo kwa kusema samaki mmoja akioza basi no wote!!! Nani atalipia muda huu ambao unapotezwa bure na watu ambao hawataki kutafuta suluhu la swal zima la migomo na hasa Chuo kikuu!!!! Ajabu kwamba sasa hii migomo ya kufungwa Chuo imekuwa kama jambo la kawaida tuu!! Huu kama si uzuzu ni nini jamani??? (dRU)

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli hawa wanafunzi wanachofanya siwaelewi. Hivi hawaoni kuwa wanatwanga maji kwenye kinu? Na hawaoni wanaharibu chances zao za kuja kuajiriwa kwa sababu hakuna kampuni ya binafsi wala serikali ambayo wanaihujumu sasa kwa migomo yao kama itakubali kuwaajiri.Hivi sasa vyuo vikuu viko vingi wakati ajira haziko nyingi. Leo hii sio siri graduate wa chuo cha Tumaini ana nafasi nzuri ya kupata ajira kwa sababu hawana cv chafu kama hao wa UDSM. Masikini vijana hao sijui hawalioni hilo?

    ReplyDelete
  6. Sawa mgomo ila watakopeshwa wangapi? hizo pesa? kazi kweli kweli jamani tujisukume hivyohivyo kusoma wananchi wenye pesa zao wajitokeze ku sponsor kila tajiri vichwa vitatu sio tuna wazamini ma miss tu tanzania mara miss pombe gani hawa wasomi ndio wakuwazamini kwa nchi kama zetu za africa. Hafidh

    ReplyDelete
  7. walichokua wanakitaka ndo hicho sasa washafungiwa chuo na muda wakurudi haujulikani sijui hizo semister watakava vp? mgomo hauna mana mtaona baada ya hiyo miezi mingapi mtarudi chuoni HAKUTAKUA NA MABADILIKO YOYOTE mmepoteza muda wenu buuuuuuuuuure!poleni sana madenti wa bongo.

    ReplyDelete
  8. Bora wangegoma ili gharama zipunguzwe kufikia kiasi wanachomudu. Wenyewe wanataka pesa zaidi, hela tuu ndo tatizo hapo.

    Sasa hayo masomo mtafidiaje?

    Serikali ili kukomesha migomo inatakiwa mtu akigoma basi fukuza kabisa na funga mirija yoote ya baadaye. Yaani wanafunzi wakigoma wafukuzwe jumla halafu wasipewe tena admission kwenye vyuo vya serikali.

    Hawa wanagoma wanajuwa mtawafukuza kidogo na kuwarudisha tuu.

    Halafu ni wajinga saana jamaa hawa, utawaona wakati wa kurudishwa kila mtu ataomba msamaha binafsi na kukiri kutii sheria zoote ikiwemo kutokugoma na kupokea feza zilezile. Sasa mlikuwa mnagoma nini, hamna fikira za mbele au mnajaribu zali la mentali?

    ReplyDelete
  9. Kwa jinsi ninavyopafahamu hapo UDSM na mambo yake, hata kuwalaumu kwa mgomo wao nashidwa. Maana sisi enzi hizo tulikuwa tukikurupushwa wizarani, wakati huo Bilali ndiyo katibu mkuu. Vurugu na mji mzima unataaruki. Sababu ati pesa imetoka lakini Bilali kaiweka kwenye fixed account!

    bado tuna safari ndefu sana kuweza kufikia malengo mazuri ya serikali hii kuhusu elimu. Watu wa chini wanamwangusha sana mweshimiwa Rais.

    Kwa mfano mzuri, huwezi kusema serikali haina pesa wakati mashindano ya shimiwi week tatu pale Morogoro yamekula hela equivalent ya kujenga secondary nne zenye A level! Sasa hii wangepewa wanafunzi wa universities wanaodai pesa. Hawa wanafunzi hawawezi kuwa vichaa. wana kila sababu. wanajua vitu hivi. Sasa ukisimama ukasema hakuna hela, hawaelewi kabisa. Mimi pia sielewi.

    ReplyDelete
  10. inasikitisha kwa taasisi kubwa namna hiyo kufungwa. sijui mambo haya ya ukiritimba yataisha lini. ninaunga mkono mgoma huo ijapokuwa wanaoumia ni wanafunzi wenyewe.

    ReplyDelete
  11. Hivi serikali hajui kama madawa na elimu ndio kitu muhimu nchini jamni? CCM watoke bwana! Wanahimiza primary tu! Mimi hata sielewi.

    ReplyDelete
  12. sasa wajemeni wasomi hawa wanagoma.
    sasa kama mimi mkulima nikigoma itakuwaje? Mbuzi wangu, kondoo wangu, nikogoma kuwafunga au kuwapeleka malishoni itakuwaje? nikigoma kulima itakuwaje? na hawa wanaogoma ndo tunawategemea kuwa watakuwa waendesha nchi baadaye. sasa kila mtu akigoma itakuwaje. Mimi nadhani kugoma sio suluhisho ni kupoteza muda. hata kama suluhisho litapatikana ujue kuwa muda umepotea bure wote pindi mtu ugomapo kufanya kitu au jambo.
    ni mimi mkulima yule yule

    asanteni sana Mkulima

    ReplyDelete
  13. KAKA MICHUZI YANI NIMEANGALIA HABARI ZA KUFUKUZWA CHUO IMENIKUMBUSHA ENZI ZILEEEEEE. WALLAH SHULE YA BONGO INATESA. PIA NIMEONA PICHA ZAIDI NA ZA KUSIKITISHA KATIKA WEBSITE MOJA INAITWA WWW.KODOA.COM "NGUVU YA JICHO AFRICA MASHARIKI". YANI PICHA ZA HIYO WEB ZIMENIKUMBUSHA ENZI HIZO TULIPOTIMULIWA NA MABEGI KICHWANI. HEBU WADAU WAPITIE HUO TUSHEE NA HIZI HALAFU TUKUMBUSHANE BAADA YA KUONA HIZO PICHA WANAKUMBUKA NINI?MACHUNGU, HUZUNI, RAHA AU NINI.

    ReplyDelete
  14. maisha bora ya Jakaya M.Kikwete

    ReplyDelete
  15. "Father, Father, Father help us
    Send us some guidance from above
    'Cause people got me, got me questionin'
    Where is the love"

    Maana hata Bongo yetu watu wamekosa upendo tumepoteza matumaini.Alijisemea Nyerere kwamba viongozi watumiao pesa kuingia madarakani hawatufai hata kidogo,sasa inadhihirika wazi kwa viongozi wetu tulionao wakijisahau na kutotatua kero za wananchi wake,wakiendekeza sera za kibaguzi.
    Kampuni iliyojitwalia shirika la reli TRC inakopeshwa pesa na serikali ili kulipa mishahara wafanyakazi wake ikiwa ni milioni 50 peke yake ikienda kwa MD! Wanafunzi ambao ni Taifa la Sasa wanaomba mikopo ya 100% wananyimwa na chuo kufungwa ili warudishwe kwa masharti kuwafunga midomo.
    Hakika "we need our father to send us some guidance from above" maana viongozi wetu wameshindwa kabisa kututatulia shida zetu wao kwa sasa wanafikiria 2010 tu, huku hari zetu zikizidi kua mbaya. Tunahitaji uhuru mwingine wa kututambulisha kwamba sie ni watanzania, raia wa nchi hii maana Taifa limekua likisikiliza wageni mno kuliko sie wazawa, Mfano raia wema wa Shinyanga wamekua kila kukicha wakiililia serikali iache kusafirisha mchanga wa madini kwani unatumika kutoroshea mali zetu lakini wapi,Hakuna hata kiongozi wa nchi aliyenyanyua mdomo wake kusema.
    Mtu kama Hosea kusema kwamba wahujumu uchumi aka Mafisadi wakishitakiwa nchi itayumba ni dalili nzuri inayotuonesha sura halisi ya viongozi wetu wasivyokua na hata chembe moja ya uzalendo.Nahisi kwa mtazamo wangu serikali itaishia kuwalipa fidia tu hawa mafisadi iliowapeleka mahakamani

    ReplyDelete
  16. Hivi jamani hakuna namna ya kuwafanya hawa ma sponsor wa "masupa modo" wawa fikirie kidogo hawa wanafunzi wetu? Maana shule haisomeki kama hujala. Na nyie mlie soma zamani kaeni kimya kabisa maana hamkawii kuanza kuwasema watoto wa watu. Ukweli ni kwamba wakati wa juliasi watu walikuwa hawana hela lakini mahitaji nyeti yalipatikana. Sasa hivi bila pesa hata kukohoa unaweza ukashindwa achilia mbali kusoma.

    ReplyDelete
  17. Sio kufunga tu fukuza wote.

    Wanalalamikia srikali wakati kaka zao na dada zao wamemaliza hapo na hawajarudisha mikopo yao. Nendeni mkawaulize waliotangulia hapo hela zikuwapi.

    Kwanza mtuachie nafasi. Mimi nimeshapiga box kishenzi na nina hela ya kusoma sas narudi home. Najua nikiomba hapo nitaingia.

    Mmezidi sasa hiyo nauli ya kuwarudisha makwenu ndio mtamaliza na kile kidogo mlichopewa.

    Mimi sioni hata hicho chuo kwanini kinakuwa cha serikali. Privatize ndio watu wajue joto ya jiwe.

    ReplyDelete
  18. HII NI MIKOPO AMA SADAKA?

    KIPINDI CHETU PALE MAMUZUMBE CHUO KIKUU HATUKUWA NA MAUPUMBAVU KAMA HAYA TULIPOPEWA MIHELA TULICHUKUWA BILA MALUMBANO KWA SABABU MIKOPO NI IARI SIYO KULAZIMISHA. UTAMULAZIMISHAJE MUTU AKUPE MAMIKOPO? MAJEMEDALI HII MUMEIONA WAPI HATA NYIYE MULIYO MAULAYA NI KWELI MUNAGOMA KULAZIMISHA MAMIKOPO? HUU SI UCHIMVI JAMENI? MUMU ULIZE HATA KAKA YANGU NA SOMO YANGU PETER S NALITOLELA KAMA HUKO CANADA KUNA MAUBISHI YA NAMUNA HII KUANDAMANA KAMA PIMBI KULAZIMISHA MUTU AKUKOPE HALAFU HURUDISHI SASA MAJEMEDALI NI NINI HII MUKOPO AMA SADAKA?

    ReplyDelete
  19. Hii ni saa ya kuwafanya wafadhili wa michezo wafadhili elimu. Huu umasikini si saa ya mchezo. Badala ya kufadhili elimu tunakalia umisi je hatuhitaji madaktari bora?

    ReplyDelete
  20. MIGOMO SIKU HIZI SIO EFFECTIVE, NAOMBA WAKAMWULIZE KIONGOZI WAO WA NCHI WAKATI AKIWA PALE CHUO WALIKUWA WANAGOMA VIPI MPAKA MIGOMO INAKUWA EFFECTIVE??
    HIVI SI WALIGOMA MAJUZI TU (MWEZI WA 4)?

    WANAFUNZI PUMBAVU KABISA WANAPOPOZI KWENYE PICHA ZA MIGOMO, NA AKILI ZAO NA ZAKUFUNDISHWA DARASANI HAWAJUI KUWA HIVYO NI VIDHIBITISHO KWENYE BARAZA LA CHUO!
    SERIKALI INABIDI IAMKE KAMA INAWAPA MIKOPO AU HAIWAPI ISEME MOJA.

    MUKANDARA INABIDI UJIUZURU WADHIFA WAKO KWANI UMESHINDWA KAZI MAPEMA, KATAFUTE DESA KWA MMARI.

    HIVI MZEE PANCHI ALIFARIKI KWELI???? AU NAE NI MMOJA WA MAFISADI WA EPA.

    ReplyDelete
  21. Kuna watoto wa Tanzania waliokosa nafasi ya kuingia chuo kikuu, mmojawapo ni mimi. Nina akili na nina uwezo mkubwa sikuweza kupata nafasi kikwazo ni uwezo wangu wa kifedha. Nasikitika sana hawa ndugu zetu waliopata hizo nafasi halafu wanazichezea. Ningekuwa mimi ningepiga book vibaya sana.
    Kuhusu ada mbona ni kidogo tu, dunia ya leo imebadilika sana. Angalia ada za University za US au UK utachoka mwenyewe. Hawa jamaa wanachezea hizo nafasi bora tupewe sisi.

    ReplyDelete
  22. Watanzania tunatakiwa kujiuliza nini kiini cha tatizo hili badala ya kulaumu hasa kwa wale ambao hawajapitia hatua hii. Historia inaonyesha kwamba sera hii iliingizwa nchini kama sharti mojawapo la nchi kupatiwa mikopo na mashirika ya fedha ya kimataifa ( IMF na Benki ya Dunia ) mwishoni mwa miaka ya themanini ikiambatana na zile ya kuchangia huduma za afya , ubinafsishaji wa mashirika ya umma na mageuzi katika mfumo mzima wa uchumi , bila ya kufanya utafiti wa kutosha tulikubali kujiingiza kichwa kichwa ambapo sasa madhara yake yanaonekana dhahiri . Kumbukumbu zinaonyesha kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wakati huo waliitisha mgomo mkubwa kupinga sera hizo hali iliyopelekea kwa mara ya kwanza chuo kufungwa kwa mwaka mzima na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi wakati huo kufukuzwa kabisa , wakati huo hawa ambao leo wamefukuzwa walikuwa wadogo mashuleni wakalazimishwa kuandamana nchi nzima kuwalaani wale waliogoma chuo kikuu na kuwaimba nyimbo kadha wa kadha za kuwakejeli ,kitendo cha wao kugoma kupinga sera hiyo hiyo ni kielelezo tosha kwamba wale walioipinga wakati ule walikuwa sahihi, wito wangu kwao ni kwamba wasichanganyikiwe ni hali ya kawaida na kwamba haki haipatikani kirahisi kama ambavyo watanzania wengi tunadhani.

    ReplyDelete
  23. nyie hamtaki kusoma hakuna watu wanosumbua hapa mjini kama wanafunzi wa udsm wao ndio wahuni na hio mikopo ndio wanachukulia advantage ya kusumbua hapa mjini tupisheni sisi tusome bwana mkatafute umaarufu kwenu mtatulia wenywewe na mtaandika barua ya kuomba msamaha kwanza fukuza wote wakachunge ngombe kwao hakuna anaefurahi na mgomo wenu ajira kwenu ni shida sana mnajiaribia wenyewe.

    ReplyDelete
  24. KAKA MICHUZI NAOMBA UWEKE HAYA MAONI YANGU NI MSAADA TOSHA KWA SERIKALI NA WANACHUO.
    Sasa serikali inabidi ifanye maamuzi ya msingi swala la elimu ni la muhimu sana na si kila mwanachi anaweza kumudu gharama za chuo,niwazi wanafunzi wengi hawawezi na wanahitaji msaada ili wasome pia wazipe familia zao unafuu wa maisha na hivyo ndio usemi wa maisha bora kwa kila mtanzania utatimilika.Serikali lazima ipende watu wake kwanza ili kutengeneza national security,kama inchi kila sehemu itajaa migomo mwisho si amani itaoweka na watu wataamua kuwauwa viongozi waliopo madarakani.
    Serikali hela inayo sema kuna watu wapuuzi wachache wanaendesha serikali kibiashara zaidi mifano tunayo mfanya biashara mkubwa akitaka kuikopa serikali hamna shida procedures zinakuwa fasta fasta.leo mwanafunzi wachuo wanasema wanashindwa mmhh huo ni uongo internationally watu watatuona ni wapumbavu rasimali tulizonazo thamani yake ni takribani mara mia ya hizo pesa za wanafuzi wachuo.
    Wanachuo,serikali isiwafanye wajinga bwana kwa hesabu za haraka hara kumkopa mwanafuzi mmoja tu kwa mwaka assume ni Tsh.5 million na chuo kina wanafunzi 10000,kwahiyo jumla ya hela ambayo serikali itatoa kwa mwaka kuwasomesha watu wake ni Tsh.50000 Millions [50Billions].Ambayo kwa serikali yetu niela ndogo mafisadi wamechota karibu billion mia[100billions] na nchi haija shake kiuchumi na sio hizo tu zilizo chotwa ziko nyingi tu.Mgomo endeleeni mpaka kieleweka hata wakifungua chuo kama habari bado ni zile zile nyinyi endeleeni tu kwani mnachofanya ni kizuri si kwa faida yenu wenyewe pia hata ya vizazi vijavyo vitawakumbuka na mtatengeneza histiria njema ya nchi yetu,Lazima mjione nyinyi ni wapekee kwa sababu wakipit hapo wote waligoma na changes hazikufanyika sasa safari hii mjitoe mhanga muone changes zimefanyika hata mkifukuzwa na mabadiliko yametokea poa tu.
    Serikali,mfanye rescue plan wanafunzi wapate maisha yawe nafuu chuoni iyo dhana ya kushea gharama ya masomo ni nzuri lakini kwenye nchi yetu muda bado wa kuiapply wananchi wetu wengi bado maskini nyie kwa sababu mnalipwa vizuri na marupurupu juu mnaona maisha nimaraisi kwa kila mtu acheni bwana kuweni binadamu wakawaida.Sawa Bodi inalalamika watu hawarudishi mikopo ni kweli we unadhani usumbufu uliopo wakati wa kuomba mikopo na mkopo wenyewe unaupata kwa tabu na haukidhi mahitaji we unadhani hata mtu atakuwa na hamu ya kuurudisha,kama serikali inataka mikopo irudishwe kwa wakati watu inabidi waridhike na mikopo wanayopewa kama nchi nyingine zinavyofanya,Serikali lazima itambue mikopo kwa wanafunzi ni lazima kwa amani ya nchi yetu,nyie wote mliopo madarakani mmesomeshwa bure na serikali na tena sio kwa mkopo ,kizazi cha sasa inabidi wasome kwa mkopo hapo naungana na nyinyi lakini mkopo lazima itosheleze mahitaji na iwe fully 100 percent.

    ReplyDelete
  25. KAKA MICHUZI NAOMBA UWEKE HAYA MAONI YANGU NI MSAADA TOSHA KWA SERIKALI NA WANACHUO.
    Sasa serikali inabidi ifanye maamuzi ya msingi swala la elimu ni la muhimu sana na si kila mwanachi anaweza kumudu gharama za chuo,niwazi wanafunzi wengi hawawezi na wanahitaji msaada ili wasome pia wazipe familia zao unafuu wa maisha na hivyo ndio usemi wa maisha bora kwa kila mtanzania utatimilika.Serikali lazima ipende watu wake kwanza ili kutengeneza national security,kama inchi kila sehemu itajaa migomo mwisho si amani itaoweka na watu wataamua kuwauwa viongozi waliopo madarakani.
    Serikali hela inayo sema kuna watu wapuuzi wachache wanaendesha serikali kibiashara zaidi mifano tunayo mfanya biashara mkubwa akitaka kuikopa serikali hamna shida procedures zinakuwa fasta fasta.leo mwanafunzi wachuo wanasema wanashindwa mmhh huo ni uongo internationally watu watatuona ni wapumbavu rasimali tulizonazo thamani yake ni takribani mara mia ya hizo pesa za wanafuzi wachuo.
    Wanachuo,serikali isiwafanye wajinga bwana kwa hesabu za haraka hara kumkopa mwanafuzi mmoja tu kwa mwaka assume ni Tsh.5 million na chuo kina wanafunzi 10000,kwahiyo jumla ya hela ambayo serikali itatoa kwa mwaka kuwasomesha watu wake ni Tsh.50000 Millions [50Billions].Ambayo kwa serikali yetu niela ndogo mafisadi wamechota karibu billion mia[100billions] na nchi haija shake kiuchumi na sio hizo tu zilizo chotwa ziko nyingi tu.Mgomo endeleeni mpaka kieleweka hata wakifungua chuo kama habari bado ni zile zile nyinyi endeleeni tu kwani mnachofanya ni kizuri si kwa faida yenu wenyewe pia hata ya vizazi vijavyo vitawakumbuka na mtatengeneza histiria njema ya nchi yetu,Lazima mjione nyinyi ni wapekee kwa sababu wakipit hapo wote waligoma na changes hazikufanyika sasa safari hii mjitoe mhanga muone changes zimefanyika hata mkifukuzwa na mabadiliko yametokea poa tu.
    Serikali,mfanye rescue plan wanafunzi wapate maisha yawe nafuu chuoni iyo dhana ya kushea gharama ya masomo ni nzuri lakini kwenye nchi yetu muda bado wa kuiapply wananchi wetu wengi bado maskini nyie kwa sababu mnalipwa vizuri na marupurupu juu mnaona maisha nimaraisi kwa kila mtu acheni bwana kuweni binadamu wakawaida.Sawa Bodi inalalamika watu hawarudishi mikopo ni kweli we unadhani usumbufu uliopo wakati wa kuomba mikopo na mkopo wenyewe unaupata kwa tabu na haukidhi mahitaji we unadhani hata mtu atakuwa na hamu ya kuurudisha,kama serikali inataka mikopo irudishwe kwa wakati watu inabidi waridhike na mikopo wanayopewa kama nchi nyingine zinavyofanya,Serikali lazima itambue mikopo kwa wanfunzi ni lazima kwa amani ya nchi yetu,nyie wote mliopo madarakani mmesomeshwa bure na serikali na tena sio kwa mkopo ,kizazi cha sasa inabidi wasome kwa mkopo hapo naungana na nyinyi lakini mkopo lazima itosheleze mahitaji na iwe fully 100 percent.

    ReplyDelete
  26. KAKA MICHUZI NAOMBA UWEKE HAYA MAONI YANGU NI MSAADA TOSHA KWA SERIKALI NA WANACHUO.

  27. Anon wa 8.07 AM nimeshindwa kukupata, unasema umeshindwa kwenda chuo kwa kukosa fedha, na unatamani sana hiyo nafasi ya chuo ungepata wewe, sasa ungewezaje tena kulipa? Tatizo lako lilikuwa kukosa kabisa mkopo au ulipata mkopo wa asilimia iliyopelekea wewe kushindwa kumalizia ile asilimia ya stahiki yako?

    ReplyDelete
  28. Wengi ya walitoa comment either hawaelewi sababu ya kugoma or hawakusoma UDSM(kwa waliopitia wanajua hii ni wiki ya ngapi).Kwanza kugoma ni haki mradi taratibu za kuidhinisha mgomo zilifuatwa.Na si UDSM tu, vyuo kibao tayari vimegoma na baadhi washatimuliwa.Hivi Wizara husika haioni mapungufu kwenye sera ya mikopo kwa wanafunzi? Najua mgomo una athari kubwa lakini sauti ya mnyonge ni nini...kama sio kugoma? Mimi kwa miaka yangu minne pale Engineering tuligoma mara nne-ukiachilia vigomo vidogo vidogo vya pale CoET.
    Nawaunga mkono madogo,gomeni mpaka kieleweke.Kuna mifano kibao ya mapinduzi kwa kutumia migomo-so msiogope. Vinho

    ReplyDelete
  29. Fukuza mimi nasema hao wanafunzi fukuza kabisa. Wapuuzi wakubwa. Fukuza

    ReplyDelete
  30. Tuliosoma UDSM, tulikuwa wanaharakati, tuliwahi kufanya migomo mingi sana na hata pia kufanya chuo kifungwe.

    Kwa kila sababu ya mgomo tulihamasisha jamii na jamaa kwa hoja ya tulichogomea. Tuliweza pia kupata kuungwa wa mkono na wazazi, UDASA na vyombo vya habari.

    Lingine,tulikuwa pia na focus na kisomo chetu na taaluma. Sio visingizio baada ya kuona nondo kali.

    Sasa kizazi cha leo hakikumuandaa mtu yoyote kujali hoja, wakati wa kukoga, namna ya kugoma.

    Tilijipima na ikijir sawia tulikariri msemo wa Mw. JK wakati wa vita vya Kagera: Nia tunayo, sababu tunayo na uwezo tunao.

    Sasa, vilaza hawana nia thabiti, sababu ya msingi na hawezi kuhimili dhiki .... siku ya kwanza wameanza kulalama ... hatukupewa notisi ya kutosha, wengine wanasema nina elfu ishirini nk.

    ReplyDelete
  31. mdau hapo juu kabisa umenikumbusha jinsi mzee alivyokuwa anawaandaa wanafunzi kugoma sio kukurupuka tu bila kuanalyse vigezo vya kugomea. sio lazima kila isue iwe solved kwa mgomo, kakaeni tena chini ya mti na sio court yard mumsikilize mzee anasema nini kabla ya mgomo. msifanye migomo kwa jazba.good luck on ya long vacation!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...