
Nakubaliana na wadau wote waliowahi kulisifia jiji la Kigali.Kwa kweli Abanyarwanda wametuacha wabongo na A. Mashariki kwa mbali!Jiji linakua kwa kasi ya ajabu na usafi mmhh!
Hata ukidondoshaa kapunje ka mchele utakaona!
Nauliza; hivi Ma Meya wetu na watendaji wao huwa wana utaratibu wa kutembelea majiji ya wenzetu??
Mdau Lilly,
Kigali
pumba tupu sasa kinachosifiwa hapa nini ni usafi au jiji kujengeka!kama jiji kujengeka mbona hatuoni chochote cha maana huyo dada me nadhani hana cha maana maana me naona kwenye hiyo picha hapo naweza kufananisha na jangwani halafu inaonesha hajui maana ya tambarare
ReplyDeleteMdau wa Kigali nakubaliana na wewe.
ReplyDeleteKila mkoa una mkuu wa mkoa, una meya, una madiwani...sijui kinachoshindikana ni nini kuweka mikakati ya kuweka miji katika usafi. Ukianza na baby steps mwisho tutafanikiwa. Hata ikibidi kuanzia kwa kampeni za kuwahimiza watu kutotupa taka ovyo kupitia vyombo vya habari..na baadae kudumisha usafi wa mitaa,wilaya na hatimae mji unasafishika. Na halafu kuhakikisha proper sanitation etc.. Mji kama Dar kwa kweli unatia hata KINYAA wakati wote ni mchafu, ikinyesha mvua ndio usiseme.....Jamani mawazo, kampeni chanya tutajikomboa...viongoz kama mnasoma na msikie hili. usafi utaepusha kuchukua maisha ya wengi hasa kutokana magonjwa yatokanayo na uchafu...Hivi kila diwani akianza kushughulikia eneo lake, wakisukumwa na meya vitashindikana kweli... MDAU big UP, mimi binafsi nakereka sana na UCHAFU acha tu...
Usiwachokoze kabisa mameya wetu kwa kuwapa mawazo ya kutembelea majiji ya wenzao. Watamaliza hela zote za walipa kodi kwa ziara za miji ya Marekani.
ReplyDeletemji wa kigali una watu 700000, nchi nzima watu milioni nne. dar in watu zaidi ya milioni sita. when you make any comparison you have to take into consideration populations, square kilometre and other habitat factors you thick heads!
ReplyDeleteMimi nakuunga mkono mdau ulio toa mada hii,lakini nadhani labda umependa tu kuuleta huu mjadala hapa, ukweli ni kuwa Meya maimuna kapachikwa tu, madiwani mambumbu, unadhani kitatendeke kitu gani.Huu ni wakati sayansi na teknogy viongozi darasa ziro, huo mji unautegemea uwe vipi.
ReplyDeleteKigali ni kuzuri na kusafi kwa kweli ila tu mdau umetusaliti kwa kuleta picha isiyofanana na maelezo yako. Nakumbuka tulikuwa Kigali mwaka 2004, wabongo kama kawaida yao wakawa wanatupa maganda ya matunda njiani. Cha kushangaza jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti safi sana akaja na kuokota maganda mawili ya ndizi yaliyotupwa na mbongo!! Aibu lakini ndio hivyo watu wanajua kujituma.
ReplyDeleteMdau wa Kigali asante kwa maoni yako,ila sijui kama unaelewa kuwa hiyo ni damu ya wakongo ndo maana hamtaki kuiachia.huo uchumi unaokwenda kasi Rwanda inaupata wapi??mi nimefanya kazi kule ,asikudanganye mtu,ni hao warwanda wanaomaliza watu congo,tutasafisha taratibu bongo yetu lakini si kwa pesa ya damu ya watu.
ReplyDeleteHuu mji utafikiri Iringa, au wanyalu mnasemaje?
ReplyDeleteHIVI HUU MJI UNAWEZA HATA KUULINGANISHA NA ARUSHA SIONI CHOCHOTE CHA KUSIFIA HAPA. DAR IS MUCH FAR HUWEZI UKALINGANISHA KABISA MJI NA JIJI, HII MAY BE ITAKUWA SAWA UKILINGANISHA NA MOSHI AU MBEYA SIJUI MACHO YA WATU WENGINE YANAKUWA VIPI KAMA WEWE KWELI BONGOZ VIPI MWANZA MBONA WABONGO HAWAPENDI VITU VYAO???DA
ReplyDeletekwani mayor ndio jiji..charity starts at home....ukisafisha jiji lakini wananci wanatupa matakataka kila mahaki, kutema mate hovyo na kukojoa tu.......watu wenyewe ndio wanatakiwa kuanza kusafisha na kuacha tabia ya kutupa takataka na hapo ndio tutaweza kuask for more help from our leaders
ReplyDeleteMichuzi usiiminye hii, ni facts. Mimi nashindwa kuelewa hawa Wajerumani. kwanini wasimkamate Kagame wanakamata yule mama?! Kagame hataondoka kwenye historia kuwa yeye ndiye aliyeanzisha mauaji ya Kimbari. Lakini history ina mambo sana. Inageuka haraka sana. kwani kuna mtu alitegemea Generali Karadzi akamatwe?? Nasubiri ya Rwanda. Ili mradi tu wasituguse sisi wa-TZ. hatuna haraka na nchi. kila siku sikukuu huku!
ReplyDeletekama kawaida wadau wengi mnatoa maoni bila kujua mnachozungumzia. si ajabu huwa mnalinganisha Dar na Paris . Kigali haiwezi kuwa sawa na Arusha kamwe .
ReplyDeleteukweli ni kuwa Kigali ni mji mdogo lakini msafi kuliko Dar . Inapokuja suala la population density , kigali una density kubwa kuliko Dar .
....sijui kama wanaendelea kufanya hivyo, lakini in early 80`s walkiuwa wanaustaarabu wa wafanyakazi wa taasisi za serikali kufanya kazi za maendeleo na usafi for few hrs once a week .
Enzi hizoKigali ulikuwa msafi mara 100 ya Dar. sijui dar inaonekana vipi sasa , lakini Kigali una reutation ya usafi for decades .
kuhusu tabia, wanyarwanda wanatabia ya uchafu kuliko watanzania, lakini viongozi wapo kidedea.
Viongozi wetu wamelala .
KWA KUKUSAIDIA TU WEWE ULIYETOA STATISTICS ZA POPULATION .
ReplyDeleteRWANDA IS THE MOST DESELY COUNTRY IN AFRICA.
KUNGELEA(KUBISHANA) VITU USIVYOVIJUA, NI DALILI YA UJINGA .
WEWE MDAU UNAYETUITA THICK HEADS, KWA KULINGANISHA IDADI YA WATU KATIKA MIJI. KWA KUWA DAR INA WATU WENGI THEN NI SAWA KUWA CHAFU...JAMANI JAMANI HII NI DHANA POTOFU. KUNA MIJI MINGAPI DUNIANI YENYE WATU WENGI NA BADO NI MISAFI???? TUSIUKUMBATIE UCHAFU ETI KWA KUWA POPULATION NI KUBWA. VIONGOZ INAWEZEKANA WANAJITAHIDI KATIKA KUHAKIKISHA MIJI NI MISAFI LAKINI HIYO HAIWEZI KUFANIKIWA UNLESS UNABADILISHA MINDSET ZA WATU. ONCE AGAIN, KAMPENI CHANYA KUHIMIZI WATU KUTOTUPA TAKA OVYO IKIWEMO NA KUTEMA MATE NA KUKOJOA THEN MIJI YETU ITATAKATA. LAKINI UKIZIDI KUSAFISHA WAKATI MWINGINE YUKO NDANI YA GARI NA KUTUMA GANDA LA CHUNGWA NA CHUPA YA MAJI NJE YA DIRISHA ANAONA SAWA...MJI HATA SIKU MOJA HAUTAKUWA SAFI. BADILISHENI TABIA ZA WATU KWANZA ILI USAFI UANZIE KWA WATU HALAFU HAPO SASA EMPLOY NJI MBADALA ZA KUSAFISHA MIJI..BILA HIVYO ITAKUWA TU NI KUPOTEZA HELA. MFANO RAHISI, UNAMALIZA KUDEKI, HALAFU MWINGINE ANAKUJA KUMWAGA TOPE ULIPODEKI..NDIO KINACHOENDELEA KATIKA MIJI YETU.....
ReplyDeleteHivi kweli mtu anaweza akatetea uchafu kwa sababu ya population? Kwani uchafu au usafi ni tabia au uchache wa watu? Anzia nyumbani tu, unaweza kukuta ndani ya ua wa nyumba ya mtu ni kuchafu lakini nyumba haina hata watu watano!
ReplyDeleteMimi nafikiri, kwa usafi tuanzie kwa mtu mmoja mmoja, kama watu tumejijengea tabia ya kukojoa barabarani mpaka watu wanaandikia bango ' USIKOJOE HAPA' kwa jinsi tabia ilivyokithiri...Kuna baadhi ya nchi za wenzetu ambazo kujisaidia hadharani kuna faini ya kutosha tu...Lakini TZ, akina baba zoezi la ukojoaji hadharani liko nje nje....and looks like nobody is bothered by it!
Kuna watu wabishi jst 4the sake of kubisha. Mdau yuko Kigali, kavutiwa na usafi wahali ya juu wa jiji hilo, na akaona Dar haioni ndani. Sasa wewe unapobisha labda utueleze kuwa ulienda huko na ukakuta pachafu tutakuelewa otherwise no research no comment, ebo! Mimi binafsi nilibahatika kwenda huko..aloo si mchezo.Mnakumbuka kale ka-kampeni ketu ka kutotumia mifuko ya plastic?Kaliishia wapi?Wenzetu kule mirambo unanyang'anywa toka airport.Ukubwa wa jiji la Dar si hoja, tatizo ni mipango mibovu.
ReplyDeleteYaani jamani wenzetu wamepiga hatua kwa hili ule ukweli usemwe. Wana system kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi au mwanzo am not sure, watu wote manafanya usafi mitaani kwao kwa kusimamiwa na mwenyekiti wao. They do respect this na hakuna anaenung'unika. Kila nyumba lazima itoe mtu wa kuwakilisha katika zoezi hilo na wanafanya kwa furaha. Mimi mwenyekiti wangu wa mtaa sijui kazi yake nini, labda kunisainia form za kufungua akaunti.Jiji letu bwana linanuka kwa uchafu lazima tuchukue hatua za makusudi kurekebisha. Unakuta bonge la jumba lakifahari, ukitoka tu nje ya geti unakutana na mfereji wa maji machafu yananuka si mchezo!
ReplyDeleteNOV.11 5:49 PM NI MMOJA WA WALE WASIJALI USAFIWOWOTE ULE HATA WA MWILI KWANI YEYE HIYO NI TABIA YAKE ALIYOJIJENGEA, HIVYO UNAPOZUNGUMZIA SWALA LA USAFI ANAHISI UNAMSEMA YEYE.BAHATI NZURI HAKA KAMJAMAA NI KAJIRANI KANGU NINAKAFAHAMU SANA KAVUMILIENI TU.
ReplyDeleteJamani kwa kweli watanzania sisi ni wachafu hilo tusikatae. Hasa Dar kumezidi. Tusisingizie suala la population hapa. China pale Beijing kuna watu milioni 33 lakini angalia kulivyo safi. Sasa Dar population ni milioni 4 lakini tunashindwa. Kigali ni kusafi acha mchezo mi nilikuwa huko mwezi wa nne. Wenzetu kila Jumamosi ni siku ya usafi. Ukionekana unatembea siku hiyo utaeleza unafanya nini badala ya kufanya usafi. Tuwe wa kweli viongozi wetu wamelala kazi kwenda kwenye vikao vya mishiko tu. Fanyeni kazi acheni kula kodi zetu.
ReplyDeleteUsafi unaweza kua hata na chumba kimoja lakini kikawa safi.
ReplyDeleteWabongo bado tunatetea uchafu wetu ebo!
Kigali Bomba sana!WanyaRwanda makini mtu wangu.Karibuni sana Mwanza na Dar es salaam!Kizuri hujiuza,kibaya chajitembeza.Wanyarwanda BiguP babake!
ReplyDeleteTHANK U VERY MUCH!! wabongo sie ni WACHAFU sana hatuna hata soni!!! KIGALI mji mdogo sana na ni msafi sana,...ukubwa wa mji sio JUSTIFICATION ya kuwa wachafu!!!!!na wewe unaetuita THICK HEADS wewe ndo THICK HEAD KABISA ona unavoongea pumba
ReplyDeleteMwanangu mi nilienda huko...usafi wa mji sikumbuki vizuri ila kaudhaifu kangu kamoja tu ndo karibia kaniumbue...Eh bwana watoto wa kitusi ni bomba!Hakyanani unaweza utoe talaka hivi hivi kwa mai waifu wako wa kibongo bila kosa!Watoto wametulia nyanja zote si mchezo. Unamcheki binti juu mpaka chini huoni kasoro...Hakyanani tembeeni muone, yaani unatafuta mwenye sura isiyo na mvuto asubuhi mpaka jioni hupati, na uki pata basi mgeni!
ReplyDeleteUnakuta mtu yupo ndani ya gari, iwe ni private car au daladala, anakula embe,chungwa au ndizi akisha maliza anatupa maganda nje ya dirisha, mbayaaaa!!!!wengine wanatupa ovyo chupa za maji barabarani. Halafu wanabaki kuitupia serikali lawama; wao ndio wanaochafua mazingira kuliko mifugo!!
ReplyDeleteAngalia wabongo walivyo wachafu..
utasikia mtu anasema mimi ni vile tu nimepanga chumba kimoja hapa, nikaa peke yangu, nyumba ya peke yangu check nitakavyokuwa msafi, utafurahi mwenyewe!! Sasa atapoingia kwenye nyumba ya pekee yake labda amepanga nyumba kubwa!!!ovyooo!!!ataanza kulalamika oo, oo, Hii nyumba sio yangu, nikihamia kwenye nyumba yangu niliyojenga itakuwa safi saana. Ngoja sasa ahamimie kwenye nyumba yao mpya! hakuna kilichobadilika, uchafu ni palepale.. ataanza kutafuta sababu zingine kibao mara maji, mara house-girl sijui nini!!!
USAFI NI TABIA YA MTU, TUNAWAWEZA KUBADILIKA, YES WE CAN. HEBU TUANZE KUWA WASAFI NA TUACHE KUOSHA VINYWA BILA MSINGI. RWANDA WANGEKUWA WAZUNGU TUNGESEMA WAO NI WAZUNGU. SASA NI WAAFRIKA WENZETU MAKELELE KIBAOOOOOOO