Hello Kaka michuzi,
Pole sana na kazi za kutupa habari mbalimbali. Kaka michuzi mimi niko nchi fulani hapa Ulaya na nimeshangaa sana kuona kwamba mabenki ya hapa ukiwa na akaunti ya akiba(saving account) hakuna malipo yoyote kama ukichukua hela au hata mwisho wa mwezi hakuna malipo yoyote mteja anakatwa mwisho wa mwezi.
Pole sana na kazi za kutupa habari mbalimbali. Kaka michuzi mimi niko nchi fulani hapa Ulaya na nimeshangaa sana kuona kwamba mabenki ya hapa ukiwa na akaunti ya akiba(saving account) hakuna malipo yoyote kama ukichukua hela au hata mwisho wa mwezi hakuna malipo yoyote mteja anakatwa mwisho wa mwezi.
Ukifananisha na jina lenyewe, akaunti ya akiba inamsaidia mteja kutunza pesa kidogo alizonazo lakini Mabenki ya hapo Bongo wanakata hela kila unapochukua hela na pia mwisho wa mwezi. Yaani namaanisha hata kile kidogo mteja wa akina anachotunza kinachukuliwa.
Natumaini viongozi wetu wanasoma habari kwenye mtandao wako au labda kuna sababu ya kufanya hivyo ningepanda wachangiaji hasa wale wenye elimu kwenye mambo ya mabenki wanisaidie kuelewa.
Lakini nimeshangaa sana kwa sababu nimezoe kukatwa hela kila ninapochukua pesa na hata mwisho wa mwezi nilipokuwa Bongo.
Asante sana
Fredy
Asante sana
Fredy
Marekani wanakula kama kawaida, checking ndio hawachukui. Sijui nchi gani uliyopo, swiss?
ReplyDeleteYeah, ni kweli Freddy benki zilizo nyingi hapa kwetu zina tatizo hilo, mara monthly service charge, minimum balance, kuna benki nyingine hizo service charges unaweza kukuta zaidi ya mara tatu kwa mwezi hii ni besides atm charges. it really sucks.Kwa kweli hili linabidi litizamwe upaya.
ReplyDeletekuna kitu kipya kimeanzishwa Tanzania kinaitwa UNIT TRUST OF TANZANIA, wenyewe wanauza VIPANDE (its like shares ila kuna tofauti kidogo) taasisi hii ni mwanzilishi wa mifuko mbalimbali ya uwekezaji kama mfuko wa umoja, wekeza maisha, mfuko wa watoto na jikimu fund. Hii ni sehemu mbadala ya benki, sifa kubwa ya mifuko hii waweza ukaingia na kutoka muda wowote ule kama ifanyavyo benki ila faida iliyopo hapa ni kwamba unajiwekea akiba at the same time unapata faida za uwekezaji. Hii ni mutual fund ambayo ni tax free, kama unataka uwe na fixed deposit under your own conrol, this is your best place now. Wengi hawajiligundua hili ila it help a lot my friends,nenda kwenye website yao hawa jamaa utapata contact zao zote www.utt-tz.org.
ReplyDeleteMfukuampunga kalambamaji Labda USA nimeishi england for 6 years hela yako uliyonayo kwenya acc inakuja hivyo hivyo ho hidden charges kama hizo za bongo yaani kinachouzi thye use our money kwa investiment ya benki na faida zao still they rob our pockets kila transcation na monthly charges doesnt make sense nilienda home nikaweka hela nimerudi tena eti hela hakuna na still nadaiwa kulipa charges outstanding nikirudi home nitakuwa na kisanduku changau
ReplyDeleteTatizo kubwa benki za bongo ni ukiritimba uliokubuhu na umasikini uliokidhiri. Bado mabenki ya bongo yanaamini kuwa mtu ukiweka hela benki
ReplyDeletebasi wewe ni tajiri, kumbe ni kwa sababu za kiusalama tu. Nchi zote za Ulaya no charges on serving accounts.
Aisee huyo anaesema hawacharge chochote mzushi,au labda sijui ni nchi gani alipo lakini sio ya umoja wa Ulaya. Mimi binafsi niko Ulaya (Belgium) na nimeshakaa nchi 4 tofauti. Kinachofanyika ni kwamba wanakata flat rate kwa ajili ya huduma zote za benki, ikiwa ni pamoja na kuweka, kutoa, kuhamisha, nk..Labda huyo jamaa hajasoma vizuri contract yake na benki, maana waswahili wengi hua tunasign tu bila kucheki. Mimi mwenyewe mwanzoni nilijua ni bure lakini mwisho wa mwaka nilipokatwa hela ndiyo nikagundua.
ReplyDeleteJama kwanza kabla ya kulalamika inabidi muangalie jinsi mabenki yanavyotumia pesa zinazotunzwa na wateja wake.
ReplyDeleteHuku nje mabenki yana invest hizo pesa kwenye stock markets na wanatengeneza faida kubwa sana... kwahiyo wanaweza kutomtoza mteja kwa kuweka pesa zake na pia ukija kwenye savings account wanaweza kumpa kiasi cha faida.
Sasa bongo na nchi nyingi za Africa mambo sio hivyo.. labda tungepata mtu atuambie mabenki yana invest vipi pesa za wateja wao.. baada ya hapo ndio tuweze kulinganisha.
Freddy bank gani hiyo?uliza vizuri wanakuwaga annual fees japo sio nyingi. Swedebank, nordea?
ReplyDeleteHizo monthly charges na Interset charges on accounts ndizo zinazowalipa mishahara wafanyakazi na kuiletea bank profits, wasipocharge watapata wapi pesa?
ReplyDeleteWakitoa charges ktk savings accounts kila mtu atafungua savings accounts na current/cheque accounts zitakuwa hazina wateja, then, hakutakuwa na mishahara wala faida, matokeo yake unakuta benki imefilisika..acha wakate hayo makato, kama unaoperate your account chini ya kiwango kilichowekwa (minimum balance charges) kwa nini usikatwe?, kama unaoperate account at a debit balance (account inakuwa iko chini ya zero is negative) kwa nini usikatwe, acheni hizo bwana, majuu wanakata ili wapate faida iwe bongo
Mfukuampunga Kalambamaji, hapa uk hakuna hilo, infact kila mwezi wewe ndio unaepewa interest kutegemea na kuasi gani umeweka na kutowa kwa kila mwezi. charge hata za kutumia atm hakuna kwa atm za benki zote kubwa, unapigwa charge ukiwa umekwenda overdraft bila ya makubaliano, cheque iki bounce, pia kuna interest ndogo kama umetumia overdraft yako within the limit waliyokupa. ukizidisha pia unakula charge. ikiwa account yako ina pesa au haina hakuna charge zozote za kila mwezi.
ReplyDeleteNakubaliana na Freddy. Kina kera sana. Kwani zamani mbona kulikuwa hakuna makato kama hayo na mabenki yetu yakipata faida nyingi tu. Wanakata halafu utasikia mara wamefadhili hiki na kile. Kwani wale wanaochukua mikopo si ina maana wana uwezo zaidi na ndipo wachajiwe interest? na mapato ndiyo yapatikane kwa njia hii? Wangekuwa wanalegeza masharti ya mikopo nafikiri wengi wangeweza kukopa na ndipo kungekuwa na unafuu kwa wale wanaowekeza kwenye savings a/c na ndiyo maana na savings ili upate ongezeko kwa kuwekeza pesa katika benki
ReplyDeleteNi kweli kaka, Benki za hapa kwetu zinamakato mengi sana kulinganisha na Benkihizo hizo US na UK. Mimi nimekaa UK, na kwakweli wenzetu hawana hizo monthly service charges na kwamba kila unapo withdraw wanakata. Jamani ninachoshangaa ni kwamba Benki ni zile zile sio za Bongo, lakini iki operate Tanzania tu basi operations services zao zinakuwa tofautu kwanini?. Kama Bank ya Barclays naona ndio kabisa wanatoa huduma tofauti na hapa bongo ukilinganisha na UK. Kwanini kuna makato makato hayo jamani mara unapotoa hela unaambiwa kuna badilio la kima cha chini kinakuja. Kweli inauma sana hizi charges kama alivyosema msemaji mwingine mara nyingine wanakata mara mbili. Nashauri kaka Issa kwa nchi kama yetu inayoendelea, benki hizi ziachane na mambo ya kukatakata wateja kwa nini kule kwao hawakati kama huku bongo?
ReplyDeleteAcha fix wewe. Wewe uko nchi mpaka usikatwe hizo monthly charges. Inawekana hujui lugha yao wewe. hakuna bank haij-charge mtu humu duniani. Inategemeana charges ziko wapi. Hivyo ndivyo banks zina-operate duniani. uliza kwanza upate jibu na usijipe jibu juuu kwa juu.
ReplyDeleteJAMANI HABARI ZA ASYBUHI MBONA TUNADANGANYANA SANA ULAYA MAREKANI, KATIKA DUNIA HII HATA SCHOOL TUMESOMA SAVING ACC UNA PATA FAIDA WALA HUTOZWI KODI LAKINI HAPA ULAY KUANA ACC AMBAYO SIO SAVING KWA HIYO UTA PATA BANK CHARGE KILA BAADA YA MIEZI MITATU AU NINA TEGEMEA NA BANKI YAKO, KUHUSU HUKO KWETU KAMA SAVING ACC UNAKUCHARJI HUO NI WIZI WAKIMACHO MACHO TENA UNASHINDA EPA BABA KIKWETE TUWAOKE
ReplyDeleteUSA zipobank ambazo kuna waiver ya monthly charge iwapo utafanya direct deposit toka kwa employer wako.
ReplyDelete...kwa ufupi, zipo bank ambazo haina monthly charges .
monthly charges sawa naelewa.. but charges when withdrawing money?mmh..hiyo kali sasa. sasa hela mnataka niwaachie nyie benki au?si zangu bwana,kwanini mnichaji nikitoa hela zangu..si bora kuzifungia kwenye sanduku nyumbani..piggy bank teh teh
ReplyDeletemi nipo england,and i get charged monthly.. yawezekana wewe una student account au ya under-19s ndio mara nyingi inakua free
Somo la soko huru au Free Market limewapitia mbali Watanzania wenzangu wengi. Ni hivi; Mfanyabishara yoyote yuko tayari kulinda maslahi yake kwa gharama yoyote ile ili mradi ana uhakika wa kupata faida zaidi na zaidi.
ReplyDeleteKinachotokea Tanzania, sio kwenye sekta ya mabenki peke yake bali hata kwenye sekta za mawasiliano, nishati n.k ni kwamba wafanyabiashara wana uhuru na nguvu ya kuamua watakavyo.
Ni mpaka siku Tanzania itakuwa na "Umoja au Jumuiya HURU za Wateja" zenye malengo ya kutetea maslahi ya wateja kwenye sekta mbalimbali ndipo nguvu hiyo ya Wafanyabishara itapunguzwa kwa kiasi kikubwa ua hata kumalizwa kabisa..!!
Hali ya sasa ni kwamba makampuni ya simu yanaamua asubuhi kupandisha gharama ya kupiga simu, au Benki zinaamua kuchaji mteja anapotoa hela kwenye akauti yake; wananchi/ wateja wanachokifanya ni kulalamikia serikali. Enzi hizi zimepita kitambo, ni enzi za chama kushika hatamu; serikali ilikuwa inamiliki haya makampuni. Leo sivyo hivyo, Serikali haina sauti zaidi ya kudai kodi yake.
Watanzania, Vyama vya kutetea maslahi ya wateja ndio vinatakiwa Tanzania. Vyama hivi vikiwa na wanachama milioni moja na zaidi vitasikilizwa na haya makampuni bila ubishi wowote. Wakisema wanapinga ongezeko la gharama fulani Benki/Kampuni za Simu n.k wanajua hiyo ni sauti watu/ wateja wao milioni 1 au zaidi. Zaidi ya suala la bei, vyama hivi vitasadia sana kupiga vita uingizwaji wa bidhaa feki Tanzania.
Mhh kasheshe, sasa hiyo ulaya gani kila mtu anasema lake, huyu tunakatwa na huyu hatukatwi? Mimi nimeishi mashariki ya kati kwa miaka 12 sasa na mshahara wangu unapitia benki na hakuna hata mara moja wamenikata hata shilingi, isipokuwa pesa zinapozidi basi huniongezea... karibuni huku tuchimbe mafuta wadau :)... la kushangaza ndugu yangu yuko Tz na hata akitumiwa pesa kutoka bongo kwenda mkoani wanakata tena asilini 10, mfano atatumiwa laki atapata elfu 90, sasa si waseme tu kuwa kama nao wamekuwa kama western union? kuwa hiyo asilimia 10 ni charge yao ya kutumia? ni kweli kama mambo yenyewe ni hivyo nikirudi bongo pesa zangu nachenji naweka chini ya mto!..
ReplyDeletejiranimdaku
kaka john mashaka tunaomba ushauri wako kwenye hili swala. Au dokta shayo. Tunawaamimi mko wapi?
ReplyDeletemtu anajisifia eti kakaa nchi nne za ulaya halafu analeta utumbo mtupu! kama hamna la kusema sio lazima mseme.
ReplyDeletena hao wengie wanaosema hakuna benki nchi yeyote isiyokata pesa zako kama ilivyo tanzania nawaambia tembea uone mambo
Zipo benki zinakata pesa mwisho wa mwezi kwenye account za savings hata hapa UK, nipo hapa for nearly 10 years now and I had an account with RAYOL BANK OF SCOTLAND SAVINGS ACCOUNT walikuwa wanakata charge kila mwezi, nikafunga na kufungua Barclays Bank ambao hawakati lakini pia unatakiwa kuwaeleza wakati unafungua aina gani ya account unataka nao pia wana account wanazokata pesa mwisho wa mwezi kutokana na makubaliano yako na wao. Lakini kinachofanyika Tanzania ni usanii, kwani ukiweka pesa unakatwa, ukichukuwa unakatwa, ATM unalimwa, au hata usipochukuwa mwisho wa mwezi unakatwa pia, lakini ukiangalia kwa undani sana wako sahihi, sasa nani hapa duniani atakuwekea pesa yako bure bila malipo, utumie karatasi zao na kalamu zao wakati mwingine kuandika deposit or withdrawal slips, umetumia umeme wao kufanya transactions zako, and yet you wanna all of these to be free, sasa wao watapata wao pesa ya kulipia wafanyakazi, umeme, makaratasi na vingine kama hivyo? ndo maana wanakata hasa nchi za kimasikini za kiafrika ambako watu wengi wanaweka pesa tu na wakopaji wachache ambao watakatwa interest za kulipia gharama zote hizo na pia soko la mitaji la nchi za kiafrika si kama kama West kwenye NASDAQ, LSE, NYSE,DOW JONES na vitu kama hivyo ambako benki zinawekeza pesa yako na kujiandikisha na kupata faida kubwa kubwa pamoja na watu/invester wengine kununua shares za hizo benki na kukuza mitaji ya benki hizo kiasi kwamba hawaoni haja ya kukulima tena wewe.
ReplyDeletekuna benki kadhaa hapa US hazina monthly fees ktk Checkings wala Savings Accts endapo tu utakuwa na Direct Deposit.Personally nainjoi huduma hiyo kwa mwaka wa sita sasa.atleast kila mwezi wananipatia interest ya vijisenti kadhaaaaa...hahaha..kaaaazi kweli kweli.
ReplyDeleteUnayesema Marekani wanakata sio kweli labda inategemea bank yako. Yangu sikatwi hata cent kwenye both accounts. Saving account ina interest na checking account haina.....lakini ni free free free . Ila kama nikitumia atm card kutoa hela kwenye bank nyingine nikiwa nje ya state ndio nachargiwa $3 au nikitoa hela kwenye hizi quick mat lakini kama ni bank wala sichargiwi. Ila hawana tena overdraft protection for free. Hiyo unalipia...
ReplyDeleteKwanza sijaona bank hapa ambayo ukienda bank kutoa hela unachajiwa. najua kuna zinazocharge mwisho wa mwezi lakini ukishop arround na ukiwa a good customer...you score big
Jamani suala la kusema wasipoku- charge watatoa wapi mishahara halipo hapa.Wewe umeinvest kwao hivyo wanatakiwa kukulipa interest kama ambavyo wao wanavyotumia hiyo hela yako kuwakopesha wateja wao wanalipwa interest.kwa hiyo kama wadau wengine walivyokwisha sema these banks should revisit their strategies otherwise watu watakuwa wanawakimbia kila siku kwasababu thereis no point of having an account with the bank.Hizo pesa zako wao licha ya kuwapa watu mikopo, pia wana invest kwenye mabenki na makampuni mengine kwahiyo ni uonevu na wizi kutumia hela ya mtu bila kumlipa ujira wake.
ReplyDeleteNipo Bristol, nina akaunti ya Barclays. Mwanzoni walikuwa hawatukati monthly charge. Lakini sasa hivi wameanza, wanakata paundi tano.
ReplyDeleteNIPO HAPA UK MIAKA 18, NINA ACCOUNT ABBEY, HSBC, NATWEST NA NATIONWIDE, SIJAWAHI KUKATWA CHARGE YA AINA YOYOTE ZAIDI YA MIMI KUPEWA INTEREST...SASA NINA HSBC BUSINESS ACCOUNT HIYO NDIO NALIPA CHARGES NA NI FREE OF CHARGES FOR THE FIRST 18 MONTHS.
ReplyDeleteHapa UKEREWE huchajiwi anything iwe saving Ac au current Ac (cheque Ac) Also hakuna charge ukitumia ATM yoyote, iwe ya bank yako au sio. kuna la LINK ya bank zote.Nina Account na Abbey, mimi ndo huwa napata interest ingawa sio nyingi, ni kama 5p per montly statement.
ReplyDeletejamani jamani tuwe makini. kwanza SOAMES ahsante sana kwa undani wa maoni yako nadhani hilo ndoo watu wanatakiwa kufanya hapo bongo, kuwa na UNIONS za kutetea maslahi ya wateja.
ReplyDeletePili, popote duniani, inategemea na aina ya akaunti unayofungua na benki yenyewe. Benki zingine hazitozi, zingine zinatoza na hata hizo charges zinatofautiana na product yenyewe uliyopendelea.
Ila ukweli ni kwamba bongo wizi umezidi kwa sababu sisi wadau hatuongei. Nimefanya kazi benki hapo bongo na nilikuwa na-enjoy kwa sababu sitozwi charges (mi si mfanyakazi?) lakini it was too much. ATM charges, withdrawal charges, deposit charges, hadi kutuma hela kwa mtu mwingine hapo hapo bongo unachajiwakiasi kikubwa tu.
Benki zote hela wanazoingiza kwa charges hizo ni ndogo sana ndo maana huku ulaya they are able to impose no charges. Benki zinatengeneza hela kwenye investments za deposits za wateja (stock and bonds), na interest za mikopo. Hivyo vi-charges vina account for a small percentage ya income....
Bongo wezi jamani tuamke....
YAANI KAMA UKO ULAYA UNA-SAVE HELA BONGO ILI IWEJE? MIE BANK ZA BONGO SIZIAMINI HATA KIDOGO, UNAWEZA UKAAMKA UKAKUTA IMEFUNGWA NA MILANGO IMEGEUKA KUWA UKUTA! SAVINGS ACCOUNTS HAVE TO PAY DIVIDENDS, MONTHLY OR QUARTERLY. THE REASON BEING UKISAVE HELA BANK WANAITUMIA UWAPA WATU MIKOPO AMBAPO WANA-CHARGE INTEREST KUBWA KULIKO DIVIDEND. SO REGARDLESS, BANK WANATENGENEZA PROFITS THRU MIKOPO.
ReplyDeleteJAMANI TOENI MAONI YANAYOJENGA...SASA WATU MMEKAZANA KUSEMA USA HAWATOZI, UK WANATOZA N.K. TANZANIA SIO UK WALA USA, IWAPO WATEJA MNAONA HIZO HELA MNAZOKATWA NI SAWA NA WIZI KWA NINI MSIPENDEKEZE UFUMBUZI HAPA. MABENKI YANAENDELEA KUWAIBIA NINYI MTAENDELEA KULINGANISHA NA UK AU USA.
ReplyDeleteMabenki Tanzania yanawaibia wateja wake.
ReplyDeleteMabenki hupokea 'deposits' kwa kulipa riba na baadae yenyewe hutoa mikopo kwa kulipwa riba. Riba wanayolipwa kwa mikopo huitumia kuwalipa 'depositors', gaharma zao za unedeshaji, kodi, na kinachosalia ni faida gawio kwa wenye hisa zao katika benki hiyo.
Benki pia hutoa huduma ambazo ni bure au huwataka wateja wazilipie kwa mwezi. Benki nyingi duniani huwa na aina mbalimbali za akaunti. Sasa katika benki moja kuna akaunti 'basic' ambazo hulipishwi fedha kwa kuzitumia huduma hizo, ila huchagia kwa mapato yanayotokana na deposit zako.
Halikadhalika, kuna akaunti ambazo hulipii ilikwa salio lako halivuki kima fulani cha fedha kwa mwezi. Pia kuna akaunti ambazo hulipi kiasi chochote kile ila unapotumia huduma fulani.
Biashara ndani ya benki kiuendeshaji hugawanyika kwa msingi ya 'reja-reja' na 'jumla/kampuni' kufuatana na ukubwa na wingi wa fedha na matumizi ya akaunti hizo. kwa hiyo zile za reja reja ni matumizi ya mtu na iwe saving au current huwa hailipiwa ial unapotaka kuingia utaratibu wa kuzipata huduma fulani.
Benki za hapa Bongo zinacharge tu kwa kila mteja na kwa kila unachokifanya. Sababu zake ni kama ifuatavyo:
Kwanza ni kuwa katika nchi yetu 'Msimamizi udhibiti wa benki'(Benki-Kuu) hana uwezo kitaalamu. Huziangalia tarakimu zaidi badala ya kutathmini sera za kudhibiti risks, bei na gharama. Kwa hiyo mabenki yana uhuru mkubwa wa kufanya watakacho na watakavyo usiku na mchana.
Sababu ya pili ni kiburi cha mabenki kwa vile hakuna sehemu zingine za kuweka akiba kama vile soko la mitaji lililopana ambapo unaweza kununua hisa na dhamana mbalimbali, vyama vya kuweka na kukopa, hedge funds, mutual funds, na kadhalika.
Kadhia ingine ni kwamba idadi kubwa ya wawekaji sio kweli wawekaji akiba ila kwa sababu ya kipato kidogo hupitishia tu mshahara wao benki kwa vile muajiri amepanga hivyo. Mara mshahara ukiingia, basi hutolewa chap-chap. benki Haipati time ya kuweekeza ili ifidie garama za hudma zake. Kwa hiyo mabenki hujaribu namna ya kudhibiti tabia hii ya kuzifanya ni cashier tu wa wizara ua shirika la serikali. Huenda udogo wa vipato unaotokana na uchumi mchanga unawafanya depositors wadogo wazichukuwe fedha zao chap chap.
Sababu nyingine ni uvivu wa kujiwekea akiba. Mtu mwenye fedha yake huwa anawashwa mikono lazima akakae kwenye miamvuli pale Garden Rose au atanue kule uwanja wa Fujo - Gaza kwa kili na roast mpaka mshahara wake ukauke. Sasa ataweka akiba lini. Benki hazioni kuwa kundi hili linawaletea biashara ila ni bughdha tu. Maana mabenki tayari yana 'ukwasi' mkubwa wakati zenyewe hazina mianya mingi ya kuwekeza.
Kwa sababu za kukosekana udhibiti mzuri wa mabenki, uwekezaji finyu na ukwasi uliopo kwenye mabenki (liquidity) ya Bongo,benki za bongo zitaendelea kuwatoza na kuwaibia wateja wake kila kukicha. Ndio maana faida wanayoipata ni kubwa kuliko mabenki hayo hayo nje ya Bongo.
(idara ya utafiti, tabia za mabenki)
Annoy wa Tarehe November 11, 2008 3:33 PM.
ReplyDeleteMUNGU AKUBARIKI.