mshtakiwa sophia joseph toka benki kuu akiwa chini ya ulinzi mahakamani kisutu leo

kaimu mkurugenzi wa idara ya madai wa benki kuu esther komu akiaga wakati akipelekwa segera leo

washtakiwa wa kesi ya epa toka benki kuu toka shoto bosco kimela, esther komu na imani mwakosaya


washtakiwa wa epa walofikishwa mahakamani kisutu kwa mara ya kwanza jana toka shoto farijala shaaban husseinj, rajabu maranda na japhet lema wakiwa mahakamani




mshtakiwa edda mwakale akiingizwa kwenye karandinga leo baada ya kushindwa mashart ya dhamana



mshtakiwa jeetu patel akirejeshwa segerea baada ya kushindwa masharti ya dhamana leo




mshtakiwa devendra vinodbhai patel akirejea rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana leo




mshtakiwa manase mwakale akirejeshwa rumande baada ya kushindwa dhamana leo.
ni washtakiwa wawili tu ambao hadi sasa wameweza kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa leo. hao ni godfrey mosha na davies kamungu. wengine wote mambo bado ni magumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Jamani jamani mambo kweli, hapo ni mahakamani badala ya kulindwa na polisi panalindwa na jeshi tena yuko full nondo kama yuko vitani.

    ReplyDelete
  2. mbona lukaza simuoni kuingia garini? mhaya amezichota sana yule.

    ReplyDelete
  3. isije ikawa ni mchezo wa kuigiza hapa. tunataka wananchi waridhike kwamba haki imetendeka.

    ReplyDelete
  4. Uandishi uchwara MASHARTI GANI WAMESHINDWA nyie waandhishi vipi

    ReplyDelete
  5. hayo masharti ni yapi sasa?

    ReplyDelete
  6. tatizo ma anonym wa 8.11 na yule wa 8.41 huwa hamsomi habari ndani ya blog yetu, kazi kung'ang'ania kusoma habari za mamodo. hebu pitieni habari ya awali kabisa kuhusu hawa jamaa mtayaelewa masharti. @@@~~~~~##?????xcchwiii.

    Nkonolungulungu.

    ReplyDelete
  7. Naona hizo hela zikirudishwa basi zisaidie na kujenga au kukarab jiji. Mbona inatudhalilisha?

    Na hao walioweza kuweka dhamana tunataka tuone hizo hela zilitoka wapi? Au waliwagawiaga ndugu zao miaka ya uizi wao.

    Nakumbuka sharti moja uliandikaga ni kuwa walipe half of the money mtu anayokisiwa kaiba. sasa hao hiyo half of the money ilitoka kwa nana?

    Je huyo mwenye hiyo hela ameipataje? Au bongo hela ni hela tu. Haman cha kuonyesha umeipataje au umeilipia vipi kodi ya mapato

    Kussurender passiport sio big deal manake nawajua watu wenye hela sana hapo bongo lakini hata Kenya hawajafika.

    Je majumba yao na mabiashara yao yameshikiliwa au wakirudisha hela (faida) mtaji wana keep? Hiyo itakua mbaya sana. kwa vile watu wengi watafuata mfano huu. Kama ukiiba unatakiwa urudishe ile hela bila kujali ulikaa nayo muda gani, thamani ya hela hiyo ulivyoiiba ilikua ipi na uliyorudisha hela value yake ni ipi.

    lesson kama walirudisha some of the money means they are all guilty. Hao waliorudisha hamna hata ccha kusikiliza kesi. Peleka jela msipoteze hela za walipa kodi kusikiliza wameshajifunga wenyewe

    Utarudishaje hela kama hujaiba au hujakubali kuwa you were wrong

    ReplyDelete
  8. Kumbe ziliibiwa billion 207 na zimerudi shwa so far billion 19 tu? This is so silly. Kwanini wasifilisiwe kila kitu. Yaani kurudisha hizo ndio basi au watafungwa wakitoka jela wanakuta hela zao zipo na maisha yanaendelea kama kawaida

    ReplyDelete
  9. unaetaka masharti waliopewa njoo Kisutu, daftari la kesi lipo wazi kwa kila mtu kusoma.

    Nyie mnaolalamika kaeni kimya, mnatuchefua.

    dawa ya mafisadi hawa hizi hindizzzzzzz

    ni kuwapeleka lupango bila kujalia utajiri wao.

    JK TAKE MY BIG THUMB UP & HAT OFF.

    2010..Njia nyeupeeeeee

    wenye wivu wajinyonge na kamba ya kiatu!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Jamani sio uandishi Uchwara, ni matter yakuwa updated jamani..yaani mnamenyewa tunda then mnataka mliswe? moja ya masharti ni kwamba watoe nusu ya hela wanazodaiwa kuiba kama dhamana..kitu ambacho ni kigumu kulingana na kuwa ni hela nyingi sana especially kama hawajaiba, plus kutotoka nje ya mji wa Dar/es/salaam na nje nchi bila ruhusa ya Judge. so yawabidi pia kukabidhi passport zao.hope ni bit clear sasa!!!

    ReplyDelete
  11. Michuzi umekosea

    huyo uliyosema Divendra ni Nandy.

    Divendra ni kale chembamba.

    ndugu zangu hao ndio maana nafahamu

    ReplyDelete
  12. Watu kama anon #1 huwa mnanishangaza sana.Hivi mlizaliwa na kukulia porini?Huyo sio mwanajeshi ni polisi-magereza toka jeshi la polisi kitengo cha magereza.

    ReplyDelete
  13. brother Michuzi, kwani hao waliotoa thamana walikuwa wanadaiwa ngapi? mana nilkuwa nimepitwa kidogo naomba nisamehewe kwa hilo. then kama mtu anakubali kulipa Nusu ya hela alizoiba means tayari amekiri kosa sasa sioni kama kuna haja ya kuchukua dhamani yake tena ni direct segerea..... au unlionaje hilo balozi wetu

    ReplyDelete
  14. Huyo Mwakosya mitaani tulikuwa tukimwita tajiri bill gate.Hana hiana kumwaga pombe kwa yeyote uliye karibu naye.Walevi tutamkosa Mwakosya.Kazi yetu ilikuwa kumzunguka na kumsifia tu basi ukimsifia mwenyewe anafurahi basi anakunywesha hadi ujinyee awe anakujua au hakujui.Ana roho nzuri mno kwa walevi wenzie.

    Pombe za bure tutatoa wapi Saidi Mwema mbona umetuweza walevi kutukamatia mshikaji wetu.

    Pesa za kumdhamini hatuna lakini tuna chupa tupu za konyagi nyingi tu tulizozinywa kwake tunazoweza kuzileta mahakamani kama mtakubali zitumike kama dhamana kwa rafiki yetu Mwakosya ili aachiwe.

    ReplyDelete
  15. wandugu...nadhani wengi wetu hapa hatu-deal na millions singali mabillioni kila siku. Naomba mnieleweshe kidogo...hiyo hela wanayotakiwa kutoa dhamana...wanatakiwa kuipeleka hapo mahakamani au wana-deal nayo namna gani?
    Pili...hao waliokuwa wanafanya kazi BOT...wameiba au wamesaidia kuiba? Na kama wamesaidia basi wataweza kweli kutoa hela wasio nayo?

    mtoto

    ReplyDelete
  16. KAMA KWELI HAO WAMEIBA BASI KWANINI WASITOLEWE NJE KISHA WAKAPIGIWA KELELE YA UWIZI WANANCHI WENYE HASIRA WAJE WAMALIZE MZOZO....

    ReplyDelete
  17. wakuu huyu ndie Jeetu Patel kweli? mbona kama sio yule niliwahi kuona picha yake miezi kadhaa huko nyuma?? isije ikawa tunachezeshewa picha la kihindi ikawa yale yale ya wachina mpira ukitoka anaenda kuokota mchezaji then anarudi nao mchezaji mwingine.

    ReplyDelete
  18. Anonym wa 5:52am sio "THAMANA" ni DHAMANA. Wewe mpare nini, mnasemaga thio thubu ni thupu!!! teh,teh heheheheeeeeeeeeeeeee!!!!!

    ReplyDelete
  19. Mithupu nasikia Johnson halali Segerea nasikia anatolewa saa nne usiku anaenda kulala kwake na kurudihswa alfajri hii imekaaje mr Mithupu!na ametamba kamwe harudishi hata cent tano na ansema siku akitoka atavurumisha VOGUE yake hapo kisutu mpaka mumtambue!Na amesema kesi hakuna kiini macho tu yeye best wa JK!

    ReplyDelete
  20. KAKA MICHUZI EMBU NAKUOMBA UMPE RAIS WETU USHAURI HUU!
    1-HIZO PESA ZILIZORUDISHWA AU SITAKAZORUDISHWA KWA NINI ZISIJENGEWE BARABARA ZETU MBOVUU NA NYINGI HAZINA MITAROO YA MAJI MACHAFUU?
    2-KWA NINI PESA HIZO ZISI JENGEWE MATAA YA BARABARANI HAPO MJINI MANAKE MITAA MINGI YA MJI WETU NI KIZA TUPUU WAKATII WATU WANACHEZEA MABILION YETUU KWA KUTUTESAA NA MA RANGE ROVERR LIVEE NA KUTUTEMEA MATE BARABARANIII??????
    3-KWA NINI HIZO PESA ZISIJENGEWE ZAHANATII NYINGII VIJIJINI NA MJINII?
    4-KWA NINI HIZO PESA ZISIJENGE PRIMARY SCHOOL KAMA 50 HIVII HAPO MJINI NA VIJIJINII ILI TAIFA LETUU LA BAADAE LIJEE KUNUFAIKAA?TUWE KAMA WENZETUUU WAKENYAAA NA MATAIFAA MENGINEE??
    5-KWA NINI KWA NINI WASITUJENGEE NATIONAL HOUSE ILI WANANCHI WAJE KUNUFAIKA NA WAWEZESHWE KUJA KUZINUNUA IN THE FUTURE?
    6-NA YA MWISHOO AHAKIKISHEE HIZOO RANGE ROVER ZAIDI YA TANOO AMBAZOO WANATUTESEA HAPO DAR NA YALE MAJUMBAA WALIYONUNUAA PALE MASAKII YAUZWEE NA WATUJENGEE BARABARAA ZETUUU HAPO MJINIII HARAKAA SANAA

    ReplyDelete
  21. Viini macho tu mbona mambo ta richmond hayaletwa mahakamani? aletwe na mamvi mahakamani ndio tutaamini jk haagalii mtu usoni

    ReplyDelete
  22. watanzania masikini vipofu kazi kukupiga kelele za mbwa muoga.
    hii kesi siyo raisi aliyeshughulikia ni mataifa ya nje kama USA na ulaya magharibi.
    kikwete alikuwa kabana kimya akiwadanganya watanzania kwa nyimbo ya hotuba kila mwisho wa mwezi.

    hawa waliochukua pesa kwani walivunja bank la hasha ilikuwa ni mipango ya baadhi ya wana CCM katika uchaguzi.

    ingalikuwa siyo wazungu basi hata zaire tungalichana ziko wapi nchi za kiafrika wakati matatizo yanatokea.
    ingalikuwa siyo wazungu leo afrika inaglikuwa mwenye nguvu na jeshi liko kwake basi ndio mtawala.
    leo albino wanachinjwa kikwete kafanya nini zaidi ya kutaka kutokea picha zake kwenye magazeti na vyombo vya habari.

    2010 tuchague mtu wa kuleta maslahi kwa taifa na siyo drama ya ujanja ujanja kama alivyosema ikulu na mahala patakatif.
    watu wanagombenia kwenda ikulu huko hakuna biashara sasa ikiwa matajiri watakufanyia kampeni utawalipa nini kama siyo zaidi ya kuwaacha waibe pesa za EPA na richmond.

    watanzania tuamke jamani tusifanye masihara nchi inakwenda kubaya.
    mauaji ya albino
    ufisadi
    rushwa ya vizito
    majambazi
    uonezi kwa mlala hoi.
    na mengine mengi

    ReplyDelete
  23. Samahani kwa kuharibu hali ya hewa humu. Swali, hivi mafisadi waliozichota na kuzirudisha hizo pesa nao wako katika washtakiwa? Nilipitwa na habari, tafadhali naomba maelezo. Na kama la, inakuwaje hapo?

    ReplyDelete
  24. waliozirudisha ni "WATAKATIFU NA WATU WEMA SANA WANAHURUMA NA NCHI"so hashtakiwi kbsaaaa,,,yan kwa ufupi JK kawasamehe,,awa wengine walofikishwa mahakaman ni ni EPA ingine-watalipwa "KWA KUJITOKEZA HADHARAN KUPUNGUZA MUNKARI YA WA-Tz" ufupii kesi itaishia no ushahidi kbs
    ZINGAAA LA MUVI-superman movie

    ReplyDelete
  25. Mimi swali langu ni dodgo tuu, ina maana huku BOT ikipita idhini ya kulipa mabilioni ya pesa anaepiga sahihi ni karani tuu ?? Maana kutokana na amount ya pesa tunayoongelea hapa mimi hainiingii akili kuwa hawa makarani (kwangu mimi ni kama makarani kutokanan na nafasi zao) ndio waliopiga go ahead ya hii pesa yoote kutolewa. Hapa lazima vigogo wenye nyadhifa fulani serikalini walihusika kama vile waziri wa fedha wa wakati huo na Gavana na Wasaidizi wake wa karibu. Sasa sawa tumekubali Balali ndio huyo yeye kaanzishwa taratibu hao wengine wako wapi ?? Acheni kutuwekea listi ya makarani wa hali ya chini mkidai ndio walipiga sahihi hii mikatana ya EPA where are the big guns ?????? Hii yote ni kiini macho na kama listi haijakamilika basi hakuna haja hata ya kuwashutumu hao mafisadi wachache mliowapeleka mahakamani kwani ni sawa na wametoswa ..........

    ReplyDelete
  26. Kwa kweli wakamatwe samaki wa aina zote! Nyangumi hadi dagaa! Msituchezee picha halafu mkawaacha nyangumi wakiendelea kututimulia vumbi na ma-epa yao barabarani, na majumba ya mabilioni!Waliorudisha pia watajwe kama walivyofanyiwa hawa akina Manase!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...