Mh. Balozi Mithupu,
Mie bwana kwanza kabisa naomba usiminye komenti yangu, maana umekuwa mkali kama mwalimu wetu wa hesabu darasa la nne.
Baada ya hapo naomba kuwauliza wabongo; hivi jamani kifanyike nini hadi turidhike? Nataka kutoa mfano wa Mh. wetu laazizi JK a.k.a 'Smiling Boy'.
Yaani tuhuma za sijui EPA na mazagazaga kibao zilipoumuka na yeye (JK) kuonekana kutochukua hatua, kila mtu alikuwa anapiga kelele na kuna hata wengine waliodai ameshuka chati.
Haya, leo hatua kadhaa zimechukuliwa na watuhumiwa kibao, ikiwa ni pamoja na kina mramba na yona wake leo, wameonja joto la jiwe lakini makelele bado yapo pale pale. Tena wengine bila aibu wameanza kusema ooooh changa la macho, hakuna kitachoendelea utadhani JK ndiye hakimu.
Hivi mnaoosha vinywa mnafahamu maana ya utawala wa sheria? Mnajua kwamba ili kumfikisha mtu mahakamani inabidi ujiandae kwa ushahidi tosha? Najua mtanigombea kama mpira wa kona, lakini sijali ila nataka kuanzisha mjadala kwa kuuliza tufanyiwe kitu gani turidhike????
Mdau wa Mikindani
(Email kapuni pliiiizzzz)
Mheshimiwa nadhanikunakitu unamiss. kwa kizungu tungeweza sema ''you have not reached both political and academic maturity'' in this case we need to send you back to school. Kimsingi kuwapeleka mahakamani watuhumiwa walioshindwa kulipa pesa za EPA kwanza ni kinyume cha utawala wa sheria. Kwani kinawagawa watu na niuonevu. hawa watu wote walifanya kosa moja la wizi wa kughushi. sheria ipo wazi walitakiwa wote wafikishwe mahakamani na pili warudishe pesa zetu. Hivyo kuwapa nafasi warudishe na kuwafikisha mahakamani walioshindwa kurudisha kimsingi naweza sema hii ni planned deal kwa JK akitaka kutoa sadaka kwa watu wachache na kuwalinda wengine. Hapa kuna mambo mengi sana mi yanantibua sana ngoja niishie hapa nsije hama key bure!
ReplyDeleteYOU JUST HIT THE POINT: Wa Bongo, ndiyo maana kuendelea inakua ngumu, maana kulalamika kila kukicha hatuachi...utakuta watu wamekaa vijiweni wanalalamika serikali haiwapi maisha bora kama ilvyoahidi...MAISHA BORA HAYAJI KWA KUKAA VIJIWENI NA KUPIGA DOMO
ReplyDeleteHIVI KUNASHERIA YA NCHI YA TANZANIA INAYORUHUSU MTU KUIBA PESA KWA KUGUSHI KUZITUMIA NA BAAADAE KUZIRUDISHA BILA KUSHITAKIWA! HAPO MSANII SMAILING BOI AMECHEMSHA KABISA.
ReplyDeleteUKWELI NI KWAMBA UKIFUATILIA HATA YEYE AMEHUSIKA KUZIIBA HIZO PESA, NDIO MAANA AMETOA AMNESTI AU KAMSAMAHA KWAKE MWENYEWE NA MAFISADI WENGINE.KAMA KESI IKIENDA BILA UPENDELEO YATAFICHULIWA MENGI.
PILI BUNGE LA TANZANIA LINABIDI LIMUMWADHIBU RAHISI WA NCHI KWA KUKIUKA KIFUNGU CHA KATIBA YA NCHI KWA KUKIUKA MAADILI YA UONGOZI NA DHAMANA ALIOPEWA NA WANANCHI HAPO ANAPOTOA MSAMAHA KWA WAHALIFU WALIOIBA PESA ZA NCHI NA IKIDAIWA KUZIRUDISHA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
Haaminiki kwa sababu hajiamini. Watanzania hawana tatizo la kuelewa wala kuamini, viongozi wametumia uelewa wa haki wa Watanzania kuwaibia, kuwadanganya na mbaya zaidi kuwaona mabwege. 'Watanzania sio mabwege tena' Dr. H. Mwakyembe
ReplyDeleteKwani kuna mtu kasema kuna ambao hawatafikishwa mahakamani? na hata hao wakifikishwa haitatosha kwa sababu hata sisi watoa mada humu ni wezi, kwani hiyo ni moja ya sifa ya mafanikio.
ReplyDeleteKama sheria ikufuata mkondo wake keko hapatoshi! kumbuka neno Bongo!
Wanaosema changa la macho ndugu yangu hawajakosea. To know the history is to predict future.
ReplyDeleteTumewaona wengi tu wakiingizwa mahakamani na mwisho kuachiwa bila hata kuadhibiwa. Eg marehemu mkuu wa mkoa ......sasa watu wakilalamika sio waosha vivywa bali wanajua fika nini kinachoendelea.
Kwani kama serikali inafanya kazi yao kwanini ingojee watu walalamike au isikilize hata hao wanaolalamika. Kama sheria ni moja isingekua na go turn around ambazo kila siku tunaziona
Sasa nyinyi kelele za nini na mambo yako jikoni yanaiva nyie mwalalama chakula hakitoshi ngojeni kiive?
ReplyDeleteMdau wa Mikindani,
ReplyDeleteMimi simlaumu Presida kwa chochote lakini naomba wewe unayefahamu utawala wa sheria juu ya habari hii ya wizi uliotokea na kulipotiwa siku nyingi kupitia wakaguzi unisaidie mimi mjiga.
Ebu eleza kutoka rohoni kwa utaalamu wako kwa busara yako,
1. Je unafikiri aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu hakuwa anajua kilichotokea?
2. Kwa nini hakuulizwa chochote umma ukijue.
3. Kwa nini hakurejeshwa mara moja hata wakati ubalozi wa USA ulisema wao hawajaombwa arejeshwe
Sasa ushahidi wa huyu mheshimiwa marehemu (RIP) na yote aliyoyajua na yeye alichokifanya na alivyomdanganya Mh. Meghji au ambavyo hakumdanganya kamwe utapatikana wapi???????
Usiniambie mambo ya kuumwa kwake maana taarifa ya ugakuzi ilitolewa siku nyingi kabla hata ya kusafiri.
Utawala wa sheria mimi unaniambia kuwa ukikutwa na na loss ya namna hiyo na utoaji wa fedha kwa njia za udanganyifu wakati wewe ndiye ulikuwa Mtendaji Mkuu hapo hapo unasimamishwa, unatoka ofisini na kuacha nafasi ya uchunguzi na wapelelezi kuja na taarifa yao. Bila shaka angefikishwa mahakamani kabla ya 'kuugua' na lazima angesema analojua tu!
Unajua in the absence of information, lazima rumours zistawi kama uyoga.
Mdau wa Mikindani tuambie kwa nini ilikuwa hata haieleweki huyu Mh. kalazwa wapi, anaumwa nini anaendeleaje na ghafla baadaye unaambia kafa na kazikwa huko! Loh hata kama wewe ndie mwanzilishi wa maneno hayo ya 'utawala wa sheria' lazima unakuwa na kiwingu kikubwa sana moyoni na katika ubongo!
Zaidi ya yote sasa waliorudisha fedha wanaitwaje katika utawala wa sheria; ni waliokuwa wakopaji? au ni waliokuwa wamepitiwa na kupewa fedha wasizostahili na mpenzi jini? au ni waliokuwa wametutunzia fedha zetu bila riba?
Tena utaamuaje fedha iliyokuwa imeibiwa iende akaunti gani kabla ya Hakimu kusema juu ya hiyo fedha?
Wa ikindani, utawala wa sheria bado unazihesabu hizo fedha zilizorudishwa kuwa ni vielelezo fulani vya ushahidi.
Kama vile haijatosha wanasheria wachumi watakwambia kuwa haiwezekani kamwe fedha iliyochukuliwa enzi hizo irudishe hiyo hiyo, utawala wa sheria hujali thamani ya fedha leo na kesho na kuitofautisha kama inavyobidi.
Niseme kuwa kazi inayoendelea ni kututoa jasho maana tumetanguliza mkokoteni mbele na punda wako nyuma!
Michuzi hii haiminywi huyu jamaa kama amejitumwa kupima wananchi wanafikiri nini habari ndiyo hiyo.
I'm gonna be straight with you. Dont you think Wananchi are foolish by playing with them like a ping pong ball. Its obvious all the financial scandals are the ultimate failure of the goverment when it comes to the fact that even ministers are directly involved. Just look at the mere fact when all these dubious transactions took place. You would see how long it took to reach this point. I applaude wanannchi and other political parties tireless efforts in combating corruption, without them nothing would have been done. Beleive me it took pressure for the goverment to start cleaning its mess. We have witnessed commissions, appointed by JK, which lied to wananchi at the first place.
ReplyDeleteI dont applaude JK team or even him because nothing yet has been done.
Mindless people just jump to conclusion bacause of just arraingment. What if the DPP fail to prosecute them because of the pressures he faces from the goverment because of his title being part of exucutive wing instead of operating indipendently as judiciary wing.
Wake up fool and see the reality. CCM is facing a hard time right now because the elections are too close and they look nasty infront of wananchi eyes
Hata afanyeje wala haturidhiki kwa sababu wengi wetu tunapenda dezo, wezi, wala rushwa yote ni sababu ya dezo na kutaka utajiri wa haraka bila kufanya kazi. Labda alete hizo extreeme kama za kina Tigo, atoe mapesa ya bure kama Zain kwa kisingizio cha promotion! Ooh nimekumbuka neno muafaka linalotufaa watanzania 'PROMOTION'. Hatutaki kufanya kazi kwa bidii tunasubiri promotion, sasa sijui JK aje na promotion gani, maana watu walivyosikia maisha bora kwa kila mtanzania wengine wamekaa wanasubiri bahati nasibu na promotions uchwara ziwatajirishe. Wakati ukilima hoho mabondeni huko nusu eka tu unapata tumilioni twako sasa sijui mungu atupe nini magunia ya chawa!
ReplyDeleteWazee wa promotions lazima tuendelee kulalamika kwa sababu kuna mwimbaji aliimba kuwa
'binadamu hatosheki hata umpe nini milele hataridhika!'
Haya wanapromotions msinimeze namie nasubiria promotions ya Zantel sasa hivi nipate vocha za bure au promotions za vinywaji sijui promotions za elimu ya bure itakuja lini?
Kweli binadamu hatosheki,
ReplyDeleteAtatosheka na nini eehee ikiwa apatacho hakitoshi, awe ni mwenye mali ataka tena nyingi, kulalamika hachoki eehe!
Mdau wa Mikindani:
ReplyDeleteKwanza ungetuambia kwamba Rais JMK kafanya nini bora mpaka sasa hivi ili tumsifie.
Tunachojua ni kuwa.
Moja: Ameingilia kazi ya Polisi.
Utawala wa sheria uko hivi: Pale uvunjaji wa sheria unapotokea mfano wizi ni kazi ya Polisi kuchunguza na sio Rais. Kitendo tu cha kuunda tume ile ya EPA ya watu watatu kilikuwa ni kuingilia kazi ya polisi. Na kama unafuatilia mambo kuna maamuzi yaliyotolewa juzi tu hapo kwa watani Kenya ambapo majaji wamewaachia huru watuhumiwa kwa kuwa tume iliingilia kazi ya polisi kwa hivyo kieleweke kuwa Tume ya Rais haibatilishi mamlaka ya kikatiba ya Polisi ya kufanya uchunguzi.
2. Kazi ya kuendesha mashtaka ni kazi ya DPP baada ya kupokea jalada kutoka kwa Polisi na kuridhika upo ushahidi wa kutosha kumfungulia mtu mashtaka:
Sasa hili swala la Jalada kupitia kwa Raisi aone alafu aseme fungu hili wapelekwe kwa DPP na hili nawasamehe, anawasamehe kwa kosa lipi????!!! Maana anaeamua kuwa umefanya kosa si Raisi bali ni Mahakama. Baada ya mahakama kuamua ndio Rais kwa kutumia mamlaka tuliyompa basi anaweza kutoa msamaha. Vinginevyo ni kinyume cha Sheria.
Hivyo Mdau wa mikindani inabidi ufugue macho na masikio yako uelewe kuwa wabongo si mabwege tena hivyo hakuna wa kushangilia wakati mfalme yuko Uchi!! Tunahitaji kumfunika mfalme.
Tutamshangilia Rais kama atavipa nguvu na uhuru vyombo vya Dola Polisi, Mahakama, nk kufanya kazi yake yeye anatakiwa ahakikishe viko imara.
Nafikiri juzi tumesikia malalamiko ya mahakimu kuhusu hali zao kimaslahi na kiusalama je haki itapatikana vipi??? Hakimu anapanda daladala, anaishi manzese na huku anatakiwa akamhukumu mtu kwenda jela mwenye bilioni kadhaa mmmh inakuja kweli hapo?????!!!!
MWISHO NATOA MAOMBI MAWILI:
1. UTARATIBU UFANYIKE ILI NAKALA YA HII BLOGU NA MAONI YAKE IWE INAPATIKANA SEGEREA WADAU WAMEONGEZEKA KULE.
2. SERIKALI ITANGAZE TENDA MPYA YA KUPELEKA NYASI SEGEREA KWA AJILI YA MTEJA MKUU WA NYASI.
Nadhani wewe unayesema watanzania hawaishi kulalamika hujasoma vya kutosha na Kutembea kuona nchi nyingine skendo kama hilo linashughulikiwa vipi? au una undugu na jamaa hao ndiyo maana unaumia saaana, natoa mfano unashilingi 200 kwa ajili ya familia yako mtu akakwapua 150 ukabaki na 50 watoto wako utawapa nini wale?
ReplyDeleteAcha habari zisizo kuwa na msingi na hayo yote yamefanyika baada ya kuwa na external pressure kutoka kwa mataifa tajiri yanayokuchangia wewe uishi na uone bongo kama ilivyo bila hivyo hakuna hatua yoyote ambayo ingechukuliwa.ngoja niishie hapa lakini nasema unahiji kuelimishwa kuhusu nchi yako.
nasema TANZANIA NI NCHI TAJIRI LAKINI SERA PAMOJA NA RUSHWA VINATUFANYA TUWE MASKINI WA MWISHO,URANIUM,GESI,DHAHABU,WANYAMA PORI,TANZANITE, MPAKA SASA NCHI ZINAFAHAMU TANZANITE MARI YA KENYA, UTAJIRI ULIOPO TANZANIA HUWEZI KULINGANISHA NA PHILIPENES LAKINI BADO SISI MASKINI
hayo huyaoni?
bado unasema kafanya kitu,
kitu gani hicho? au
kajitahidi kulinda UFISADI
Kama rasilimali za nchi hii zingesimamiwa vema,hii nchi ni paradiso!dhahabu,almasi,makaa,chuma tanzanite,ulanga,gesi,mafuta,mbuga,maziwa,misitu,rutuba nk umaskini huu ungepotea!
ReplyDeletekuhusu utawala wa sheria naunga mkono maoni chanya ya waliotangulia.hali ikiendelea hivi kura yangu 2010 ipo kwa slaa...
Unamisi vitu vingi sana,tuache sasa kuangalia sura!hela ya wazee wa EAC imeenda wapi?toka lini mtu akiiba pesa na akirudisha anasamehewa?na kwa nini aingilie uhuru wa mahakama kutoa msamaha kinyume na sheria?watanzania sio mabwege,wameamka!
ReplyDeleteKosa kubwa mi ninaloliona ni kuwa jamii sasa imesoma na wasomi tuko wengi tunaoweza kujiuliza!lakini viongozi watawala bado wanadhani bado wanaweza kuwatawala watu kama enzi zile watu hawajasoma!ni wakati sasa wa kuwa safi(kutofanya faulo)!Bado JK hajafanya juhudi yeye kama yeye katika haya mambo.hata yanayofanyika ni kwa sababu ya mashinikizo ya wananchi kufichua mambo kila kukicha...
Mheshimiwa,hoja yako haina msingi ndo maana unajua kwamba utashambuliwa kama mpira wa kona.
ReplyDeleteAnons 1:42AM na 5:04AM, wameongea ukweli mtupu (I applaud them). Mimi nahisi wewe u either need to go back and do ur homework, au una uhusiano wa karibu na mafisadi (no offense).
Watanzania tumezidi, yaani ni haibu tupu. Tumeweka matako chini tunategemea maendeleo yaje kupitia mashindano ya umiss, Zain na Buzz. Leo hii kuna mtu atakwambia JK ni rais bomba sana, bomba wakati gharama ya maisha inazidi kupanda kwa rate kubwa sana, kila mtu anajenga shule yake na curriculum yake, almost contract zote za serikali zina wizi ndani.
Then, unasema watanzania hawaridhiki? Just to help you. Hali ni ngumu saana, maisha yanazidi kuwa magumu kwasababu ya few greedy people ambao bila kukuficha JK anawajua ila anawalinda.
Na hata hao waliotolewa ni danganya toto. He knows the real deal
WAKE UP PEOPLE THE HOUSE IS BURNING REALLY BAD
unayeuliza hii issue labda hujaishi nje ya nchi na umekua polarized na maisha ya bongo
ReplyDeleteHii issue ingekua imetokea nchi nyingine ungeona jinsi inavyoshighulikiwa.
Halafu toka lini mwizi akiiba anarudisha hela tu halafu anasamehewa?
Too bad watu wengi siku hizi wamesoma na hawajasomea hapa bongo
Mwisho wa yote ni kuimpeach tu this smiling boy wako
yani ni vita kati ya kambi 2:former presidaa na smilliong boy,,manawajuaaaa????
ReplyDeleteyan nikiwaandika apa michu itaibana hii newz.dah basi tu!!!!
ila jamani bora atleast hivi kuliko kunyamaza kimya kbs,,,mambo taratibu tutafika tu justice will take place
ALUTA CONTINUA,,,ADI KIELEWEKE KDG
Jamani, wengine sisi hatuko sharp kama nyie wengine. Hivi haya 'madudu' yooote yalitokea kipindi gani? Awamu ya tatu yakakaliwa au Awamu ya nne yalipoibuliwa? Chunguzeni basi mtuambie na sisi .. mseme ukweli lakini
ReplyDeleteWatu bana hawana dogo,mdau umesema tena laivu kuwa wabongo hawatosheki, zaidi ni wale wasio na lakufanya ila kukuwadia habari.Presido kwa kuwapeleka vigogo mahakamani kaonyesha nia ya dhati kutatua ufisadi uliokithiri.Sijui mlitaka JK akalie benchi pale Kisutu au vipi, kama changa la macho iba na wewe halafu uende pale Kisutu na Keko/Segerea na ndo changa utaliona kama lipo.Kunyea ndoo kwa muheshimiwa si changa hilo ni soo
ReplyDeleteMi nakubaliana na mtu aliyepost hii mada,nafikiri watu wengi atuelewi sheria,mtu huesabiwa kosa mpaka mahakama umemkuta na kosa,kwa hiyo mda wote anakuwa mtuhumiwa.Na kitu kingine ieleweke Mahakamani hamna siasa,kama hakuna ushaidi wa kutosha obvious mtuhimiwa atashinda.Mi nafikiri wanasheria au ma lawyer wanaweza kutoa elimu nzuri zaidi ktk jambo hili la sheria.Kama kuna mtu mwenye taaluma hii tuelimishe zaidi watanzania...
ReplyDeleteKwani hizo pesa za EPA zimeanza kuchotwa 2006 baada ya JK kuingia madarakani? Mbona nyie walalamishi siwaelewi na ndicho hicho kinachomshangaza hata mdau wa Mikindani. Wizi wa EPA ulianza tangia 2000, je mbona hamkuwa mnadai huo utawala wa sheria wakati wezi wanaiba tokea 2000 mpaka 2005? Kwani nchi ilikuwa haina uongozi wakati ule? Ilikuwa haina serikali? Ilikuwa haina utawala wa sheria? Hamkujua kuwa kuna wizi hasa huo wa EPA, na hata IPTL ambayo bado inachota mapesa mpaka leo? Na Netgroup solutions waliokuja kuifilisi Tanesco pamoja na Simu Limited waliofilisi TTCL? Sasa niambieni mbona hamkuwa mnapiga kelele hizi wakati huo pengine hizo kelele zingenusuru baadhi ya mapesa na wizi mkubwa uliotokea? Sasa mnataka JK afenyeje? Anayesema polisi kwani kabla ya utawala wa JK polisi hawakuwepo? Au ofisi ya mwanasheria mkuu?
ReplyDeleteHuyo ambaye haya yote yalitendeka wakati wa utawala wake yuko kimya hata kumgusa mwamuogopa na bado alifanya mpaka biashara ikulu lakini kutwa mwaimba nyimbo za kumsifia. Na mie naungana na mdau wa Mikindani kuwaulizeni, NI NINI HASA TATIZO LENU? TATIZO NI JK kama JK? au Serikali yake au kuna watu wana allergy na kuongozwa na mtu wa aina fulani? Maana nashindwa kuelewa kama hali ngumu ya maisha lini tulikuwa na matajiri? Lini tulikuwa na hali nzuri? Kama hayo ma pesa ya EAC ni tangu enzi ya Nyerere alivyochukua pesa za watu akapeleka vitani Uganda, na watu tukafunga mikanda tukala dona la yanga na kisamvu na kuvaa madurufu, na kaniki, lakini mwaimba nyimbo na ngojera za kumsifu zile shida hamzioni.
Kabla ya JK watu walikuwa wanakula matunda mwitu porini, pesa hakuna mpaka tukaipa jina UKAPA, wanaffunzi ni hawa hawa na system ni ile ile, madai ya EAC na ya walimu yaliendelea kuwepo, na tena hao walimu hawakuthubutu hata kugoma kwani utawala wa Mkapa ulimaliza madeni yao? Kama yaliisha haya wanayodai yametokea wapi? Na kwa nini kipindi hiki ndio kila mtu anadai kwa bidii zote kuliko siku za nyuma, mshawasha na ushawishi unatokea upande gani hasa? Maana kipindi cha Mkapa walimu hata mishahara yao ilikuwa mbinde kuipata na hawakugoma iweje leo wagomee madai ya zamani na wala si ukosefu wa mishahara?
Kuna vitu vingi mtu mwenye kufikiri na kutafakari lazima atakuwa na maswali lukuki ya kujiuliza!
cha msingi tuelewe kuwa jambo lolote linataka moyo na mwanzo wa kuanzia..hivi awamu zote zilizopita kuna rais yoyote aliyewahi kuuvaa ujasiri aliouuvaa mawanajeshi kikwete...alifukuza waziri mkuu amabae ni sahiba yake kwa ufisadi..hawa watu walianza kuiba enzi za makapa na aliahidi kuwashughulikia na sasa ameanaza kufanya hivyo basi tumpe muda mambo ya sheria haya katika jamii ya leo iliyopstaarabika huwezi kuwa unaweka watu ndani kama enzi za nyerere tuwe waelewa.
ReplyDeletemi naona ni hatua nzuri..na tusidangaje kuwa maisha bora ni kwa serekali kugawa mahela kwa kila mwananchi bure hio haipo kokote tuchape kazi na tuache siasa za kinafiki...kwa taarifa tu wiki ijayo mbowe anapanda mahkamani kama dokta wa taasisi ya moyo nae anadaiwa na nssf...habari ndio hio vita haichagui....hongera luteni sisi WAPIGANAJI tupo nyuma yako..
YANI JAMANI JAMANI NI LINI TUTAELEWA RAISI NAE YUMO NAE KWENYE HAYA MADILI??????HAPA NI KULINDANA TU HAMNA LOLOTE
ReplyDeletexxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
ReplyDeletexxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Hajamaliza Afaghanistan(EPA), anakimbilia Iraq ...
=========
=========
=========
Kuna kitu kinafanyika chini kwa chini ili kuficha ukweli.
>>>>>>>>>>
>>>>>>>>>>
Hii kesi ya kina Mramba na Yona ina harufu ya usanii ...
Watanzania wa sasa ni tofauti na wale wa Enzi zileeeee!!!!
------------
Jamani kwanini watu wazima tunataka kuwageuza wenzetu mbumbumbu
////////////
///////////
Watanzania tusikubaliane na hizi trick za miaka hiyooooooo.
++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++
Kesi itakwenda kisanii sanii mpaka uchaguzi upite halafu then slowly mambo yatakuwa yanafutwa gradually
#############################
##########################
WA EPA WAMEJENGEWA SIX STAR RUMANDE NDANI YA GEREZA KWA KUWA WAO BADO NI WATUHUMIWA, MBONA WENYEJI WAO AMBAO WAMEISHI MIAKA NA MIAKA KAMA WATUHUMIWA KWANI KESI ZAO HAZIJAISHA WANAISHI KAMA WAFUNGWA? BASI NAO WAHAMISHIWE KWENYE HIZO SIX STAR RUMANDE.
ReplyDeleteACHENI UPUUZI WA KUTETEA VITU AMBAVYO SI SAHIHI, MWIZI NIMWIZI TU HATA AKIRUDISHA KITU ANAPASHWA KUSHITAKIWA, NA KAMA ANAONA NOMA KUWASHITAKI BASI HE SHOULD EVEN NAME AND SHAME THEM ILI WATU WAJUWE NI AKINA NANI, WENGINE NI MASWAHIBA WAKE NDO MAANA AKAWEKA KIPENGELE CHA KURUDISHA NA HAWATASHITAKIWA, KWA VILE ALIONGEA NAO NA KUWAAMBIA WARUDISHE, NA PENGINE DANGANYA TOTO TU TUNAJUWAJE KUWA WAMERUDISHA???
ReplyDelete