Kaka, Habari za safari?
Unapata internet wapi ukiwa vijijini? Au unatumia mitandao yetu ya simu? Natumia Zain nikiwa mikoani na inanisadia sana kitechnolojia. Niliahidi kutuma picha, nahisi hii ndio bora zaidi kutuma na sio zile nimepiga mbele ya Eiffel Tower. I feel this picture says something about France and Paris today.

Ukizoom, utaona kwamba ni picha hiyo hiyo moja, inayofanana na ya Obama wakati wa Uchaguzi US 08. Ila kila moja ina maandishi tofauti. Kauli mbiu ni YES WE CAN.

Maandishi yamenikumbusha matangazo ya shirika la HAKI ELIMU. Sijui kama ni chama chake kimeweka hizi poster mji mzima, lakini zinakumbushia ishu muhimu za kuzingatia kisiasa, kijamii, kiuchumi na fedha, kimazingira nk! Wanagusia AJIRA, RENEWABLE ENERGY, KODI KWA MAKAMPUNI YANAYOCHAFUA AU KULETA ATHARI YA MAZINGIRA nk.


Mwaka wa tatu ndani ya awamu ya 4, ni sahihi kiueledi kutathmini mwenendo wetu na sisi.

Katika vyombo vya habari, hapakosi kuwa na kipindi kuhusu nchi moja wapo za Afrika. Nchi hii bado ina ukaribu sana na yaliyokuwa makoloni yake. Hii ni kwasababu vijana wa sasa hawana uelewa mkubwa kuhusu watu weusi. Nao wamekua sehemu KAMILI ya jamii hii.

Watangazaji wa Kiafrika kwenye Tv ni wachache, au kwenye matangazo ya biashara, lakini timu yao ya mpira ni kielelezo kizuri cha DIVERSITE au mchanganyiko wa jamii ulaya leo!

Nilipostpone kutembelea Ubalozi hadi kesho asubuhi. Bado natafuta waungwana angalau niseme kiswahili kidogo kabla sijarudi Bongo wiki ijayo! Nawakilisha.
Safiri salama.
Taji Liundi
-------------------------
Taji!
Asante mdau kwa snepu na ujumbe mwanana. Naona Obama kakolea kila mahali. Ujumbe wake hata huku unatumika katika kuhamasisha mabadiliko katika jami. Kuhusu mtandao vijijini usikonde.
bongo siku hizi tambarare kwa jamu. Mtandao upo mradi tu kuwe na network ya nanihiii. Ah, si unajua tena. Mie bado nabangaiza vijijini. Raha kweli. Hakuna foleni ya magari wala nini.
Ukiazima injini kiuno kwa katibu kata wewe aaaaah unadunda tu. natamani kubaki huku wallahi. wenzetu hawana makuu, wanachapa sana kazi usiku na mchana. Halafu umoja ndio usiseme. Kila jambo linamhusu kila mtu.
Nakutakia ziara njema
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. Huyo sio Obama mzee! Angalia vizuri

  ReplyDelete
 2. KAKA MICHUZI HUYO NI NIKOLAS SARCOS WA FRANCE,SIO OBAMA KABISAAAA!AU TAJI ANATUTEGAAAA??????/

  ReplyDelete
 3. Sasa mtajuaje kama amegusa majuu?, lazima aonekane kwenye snow jamani. kila siku mnataka nyie tuu muwe Ulaya, nadhani ni matarajio yangu siu napanda Swiss air nitapiga picha ndani ya ndege kuja kuwaringishia humu kuwa nakwenda Kiwanja.

  ReplyDelete
 4. We Liundi acha mambo yako. Mitandao tele kila sehemu mpaka mpakani mwa Congo na Kigoma. Njii tambarare sana

  ReplyDelete
 5. we 5:22 pm hivi kuwa majuu ni big deal? Ngoja siku utakuja ndio uone kumbe sio chochote wala lolote. Hizi nchi ni nchi kama nyingine tu na kuishi huku sio privilege wala nini ni kama vile mtu anachagua kuishi arusha ama Tanga. Dar au Dodoma....Je utawaona wanaoishi au kutembelea tu Dar au Arusha kuwa ni big shot people? La ni watu wakawaida tu kama wewe. Maisha ni popote ni mipangilio yako tu

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...