


Balozi wa Zain;
Asalaam Aleikum!
Juzi watanzania waishio Marekani walijumuika na wenzao katika sherehe za "Thanksgiving" ambako hapa Houston, Texas, ambapo mwamba wa kutunisha misuli katika miziki ya zamani old school Bonny love hakuwaangusha mashabiki wake kwa kuwapa vitu adimu vilivyowakumbusha bongo miaka ya nyuma. Shughuli hii ya kufana ilifanyika katika ukumbi unaotamba mjini humo wa Huston Safari Hall.
Mbali na Bonny Love walikuwepo MaDJ wengine akina Dj Rex, Dj Issa, Dj Rich"Maka" ambao ni mahiri katika fani ya miziki ya kizazi kipya,hip hop, raggae na bolingo ambapo kama kawaida waliweza kukonga nyoyo za mashabiki wao.
Watanzania waishio Texas wanaungana na wenzao walioweza kuja hapa kusherehekea Thanksgiving weekend ambayo ni taratibu iliyodumu kwa takriban miaka kadhaa sasa. Kwa mgeni ambaye amefika hapa kwa mara ya kwanza kama mimi nimefurahishwa mno na ucheshi na ukarimu wa wenyeji wetu.
Karibu kila mtu alikuwa anaongea kiswahili na kuonyesha moyo wa upendo. Shughuli hizo kwa ijumaa kulikuwa na michezo ya BasketBall na pool na pia Disco la kukata na shoka la bure mpaka asubuhi katika ukumbi wa Celebration Party Hall.
Jana Jumamosi kulikuwa na michezo mbali mbali ukiwemo na mchezo wa mpira wa miguu, volleyball na michezo kwa watoto ikifuatiwa na nyama choma. shughuli hizi zinamalizika leo Jumapili kwa party ya kuagana katika ukumbi wa Belvedere Lounge.
Napenda kuwakilisha,
Mdau Isaac A. Kibodya
Midlife crisis
ReplyDeleteI second you... Anonymous.. December 01, 2008 4:34 AM
ReplyDeletewatu wengine hawajui kwamba time imefika !!
ReplyDeleteNilidhani salaam ni za Thanksgiving na jinsi watanzania walivyosherehekea kumbe ufinyu umepelekea shambulizi kwa mtu binafsi..basi kazi...
ReplyDeletei second anonymous wa December 01, 2008 4:34 AM
ReplyDeletekwa haraka ukiangalia kwa undani indeed ni midlife crisis
michuzi mdaku umemtoa wapi, mpoki aisee mpoki michuzi namuona kwenye kona kule.
ReplyDeletemichuzi namjua yule jamaa kwenye kona kule, alikuaga mshikaji high school.
ReplyDeletedj bon luv naona mambo poa kabisa, mpoki namuona lete more snaps basi michuzi.
ReplyDelete