Sema Michu,Natumai ni mzima wa afya na unaendelea vyema ktk shughuli zako za kila siku. ebwana naomba utoe issue ya moja ktk blog, ambayo ni kuhusu bei kubwa za Internet ambazo zinazotolewa na Internet Providers wa Kitanzania.
Kwa mfano tu angalia bei za Vodacom
ambazo ni kubwa sana kulinganisha na soko la dunia, pia angalia TTCL http://www.ttcl.co.tz/Broadband_Pricing.asp#How
ambazo ni karibia mamilioni ya pesa kulinganisha na soko la dunia. angalia sasa na UK virgin media wanatoza si zaidi ya paund 20 ktk packages zao http://allyours.virginmedia.com/websales/service.do?id=2
au angalia BT
bei ni ndogo sana tena sana. Mkuu naomba fuatilia hili swali kwa nguvu zako zote ili Watanzania nao wapate benefit ya kuwa na cheap internet na kwenda na wakati.
Pia kama ikiwezekana uongozi wa hivi vyombo na vinginevyo viweze kutoa kauli kamili kuhusu bei zao zinazo tesa watanzania na kuwafanya kutokwenda na wakati na kupata faida kubwa ambapo ata Serikali hawaliangalii hili swala.
Mdau UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Kabla hujamtuma Michuzi kufanya kazi kwanza wewe ndio ufanye studies. Pigia simu Telecomunication consultant na uwaulize kwa nini Tanzania cost ya Internet ni higher?

    Reason ni old technology ambayo Tanzania wanatumia. That is the reason, sio unaamka kama chizi na kuanza kulinganisha bei kisha unatusumbua hapa.

    NEXT TIME DO UR HOMEWORK.
    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  2. kwahio we mdau unataka wabongo waje kuchukua internet na contract phones UK for use in DAR??? au unataka nini maana sijaelewa point yako
    those prices za bongo they are pathetic wataendelea kuibiwa tu

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni ukritimba wa biashara.Watoa huduma wa Internet ni wachache tofauti na uingereza na marekani hivyo wanajenga jeuri ya kuweka bei kubwa watakavyo.

    Soko ni huria.Dawa ya bei kushuka ni wadau wengi kuingia.Internet providers wakiwa wengi bei itashuka tu hata chini ya hiyo iliyoko kwenye soko la dunia.

    Kwa sasa bado wateja wataendelea kukoma ubishi.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau uliyetuma hii taarifa inaoneka huna data za kutosha, umekurupuka.

    Nadhani kifuatacho kwenye tutaz utasema kuwa watoto wadogo wa hapo Uingerezani wanajua kuongea kiinglishi.

    ReplyDelete
  5. wabeba boski fungeni mabakuli yenu bwana na nyie jamaa ana nia nzuri tu swala ´kama mnajua nn chanzo cha kufanya bei kuwa juu mtueleze sio mnaanza kupayuka tu kama mahayawani vile,asante sana mdau hata mm na wabongo tulio wengi hizi bei zinatuumiza sana na ndio maana hadi leo bongo net ni anasa wakati ilitakiwa iwe easy tu

    ReplyDelete
  6. Watanzania wengi hawafahamu ni kwa nini,ila kama alivyosema mdau wa kwanza ni technology ambayo Tanzania inatumia(setelite) hii ni gharama na vile vile si speed yake ni ndogo ukilinganisha na fiber optics ambayo wanatumia nchi nyingi zilizoendelea,ila nimesikia kuna mradi umeanza wa kupitisha cables chini ya bahari ,na Tanzania ni nchi mojawapo itakayo faidika na mradi huu mkubwa.hebu tuvute subira huenda mambo yakawa safi .

    ReplyDelete
  7. Mdau uliyetoa hii post:
    Tatizo siyo kwamba hao ISP wa Tanzania wanapenda kuchaji hizo bei ila tatizo liko katika gharama za bandwidth siyo tu Tanzania bali bara zima la Africa. Ukifanya research yako next time, utagundua kwamba serikali za Africa kwa sasa zinajaribu kutatua hili suala na kufikia June 2009, gharama zitapungua sana ukilinganisha na sasa kwani kuna Broadband network ambayo itakuwa imekamilika itakayounganisha bara la africa na europe hivyo kupunguza gharama. Kwa miaka mingi sana bara la africa lilikuwa halijaunganishwa na global fiber network ambayo nchi za asia na ulaya wanatumia na kufanya gharama ziwe chini sana. Please jenga tabia ya kufanya research yako kabla hujaanza kufananisha Tanzania na mataifa ya ulaya na kumbuka Tanzania ina miaka 46 tu na kidogo tokea imepata uhuru.

    ReplyDelete
  8. Washikaji msimlaumu pengine anahitaji kuleta kampuni yake ambayo ni rahisi, lakini aangalie, kuna tume zinaishi kwa kutegemea makampuni hayo kulipa ada ya uendeshaji.Zina mashangingi na viyoyozi na wanajenga magorofa ya kupangisha!! mathalani kuna tume ina mgao katika kila lita ya mafuta na katika kila galoni ya maji na katika kila unit ya umeme unategemea nini Bongoland? mjomba?

    By chakupewa

    Chakupewa

    ReplyDelete
  9. ah watu wengine bwana mnajifanya mnajua sana, hivi unafahamu kwamba serikali yako ni kati ya serikali zinazotoza kodi kubwa sana hapa duniani?? sasa kwa nini internet isiwe bei km kila kukicha kodi zinapanda? iulize Serikali kwanza usianze kulaumu mitandao halafu eti unafananisha na mitandao ya mbele kijana kwenda ulaya kusikufanye uwe limbukeni baba hii ni third world na technolojia yetu nadhani waifahamu kwa hiyo soma kwa bidii uje utukomboe

    ReplyDelete
  10. Tanzania ni bei sana kwa sababu bado tunatumia Satelite kwa internet, ambayo kusafirisha data ni slow na ghali sana.Lakini kuna mkonga wa mawasiliano unatoka South Africa hadi UAE na kupitia hapo kwetu na sisi tutaunganishwa nao.Baada ya hapo bei itashuka kwa asilimia 80 !!

    ReplyDelete
  11. huu ni ushenzi hata fumo boi, mkali wa IT IFM anaikataa

    ReplyDelete
  12. mdau wa UK, a,ewasilisha jambo la maana sana hapa hila ndio hivyo tumeshidwa kumpa ushirikiano,maana wengi wenu mlio toa comment hapa mnaonekana mna viji-cent hivyo ampati shida na gharama zinazo tozwa na internet provider wa hapa bongo,ila napenda kumwambia mda wa yuke kuwa hapa tz wapo internet provider ambao charger zao ni sawa na za huko UK ila kasheshe ni speed yake ukitaka kulipa tsh 40,000 speed yake ni 12 kbps, kwa hiyo ni we mwenyewe tu na mahitaji yako.

    ReplyDelete
  13. Kazi ya watanzania kila siku kulalamika tu bila kufanya utafiti wa kile anachokilalamikia. Wengi wanafikiri technologia inatoka hewani, hivi ungefanya utafiti ukajua ni technologia gani inatumika huko TZ kisha ukalinganisha na ya huko UK ndio ungeleta hapa kwenye blogu ya jamii kitu kilichokamilika na sio kulinganisha bei tu, linganisha mpaka na technologia zenyewe! Jamani mwe, mitandao mnayo lakini hata habari muhimu hamusomi kwenye hiyo mitandao yenu? Kazi kutafuta blogu za utamu na kutumia dakika mbili tatu kwenye blogu za jamii basi.

    Sasa nenda katafute kwenye internet huko mradi wa kutandaza nyaza baharini kuanzia South Africa mpaka Egypt (Fibre optic cable?), halafu utapata habari zote huko ambazo zitakuleza mabadiliko ya technologia yaliyo njiani kuja Afrika, huo mradi ukikamilika na jinsi ambavyo itakuwa nafuu au cheap kwa watumiaji kulinganisha na sasa!

    Ujanja wa buree! kwanza hata hushangai jinsi hata speed zilivyo tofauti?

    ReplyDelete
  14. Sema kama unataka internet ya bure ukirudi bongo kama uko huko ukerewe inaelekea hujakusanya vipound vya kutosha unafikiri hizi ni kampuni za baba yako mramba.

    ReplyDelete
  15. ila kweli jamani internet bongo ni gharama..hata kama ndio huduma inaanza inaumiza sana...mimi nina connection na TTCL na sio siri...its too expensive..wakiboresha gharama watumiaj watakuwa wengi na watapata faida zaidi....sasa hivi ilivyo gharama mtu hata hujisumbui unless una shida sana ya kutumia internet...sasa hapo wanakosa mapato..TTCL wakipunguza bei na wengine watafuata. mfano rahisi ni huduma ya simu za mkononi , mmoja alianza sijui extreme na wengine wote wakafuata na matokeo yake wanapata faida sana kutokana na idadi ya watu wanaotumia hiyo huduma

    ReplyDelete
  16. Kuna issue pia ya supply and demand. Demand ni pamoja na soko liko tayari kiasi gani kugharamia huduma au bidhaa. Ndio maana Hummer inauzwa USD 30K Marekani na gari hilo hilo linauzwa Tshs. zaidi ya 300M Dar es Salaam.

    Swala la bei kubwa na mfumko wa bei Tanzania linaongezewa pia na lack of control. Sio ujinga. Hatuna vyombo makini vya kudhibiti bei kama huko unakolinganisha bwana, eeh. Bei ya mafuta ilivyopanda duniani, Tanzania ilikuwa inapanda sambamba nao. Sasa "barel" ya mafuta imeporoka kutoka karibu dola 200 iliyowahi kufika na kurudi mpaka kwenye dola 50. Tanzania haiporomoki kama hivyo na watu wanaumia tu.
    Mimi nadhani swala hapa ni udhubiti zaidi kuliko ujinga. Ukiwa UK au USA unaweza kugoma na kusikilizwa. Ukigoma Tanzania unakutana na FFU mara moja bila kujali unagomea nini. Tutafika tu huko na sisi bwana. Sio wajinga kiasi hicho

    ReplyDelete
  17. Nafikiri hapa hawa wadau wanaopingana na hoja hii ya bei kubwa za internet ni kwa sababu jamaa katoa hoja hii akiwa UK, so kama kawaida yetu wabongo ni wazee wa kupondea tu.Hali hii inatufanya kufikia kiwango cha kuona aibu hata kudai mambo yetu ya msingi. Ukitazama viwango vya gharama za internet per 1MB pindi TTCL wanaingiza bidhaa yao ya Broadband kwenye soko walikua wanacharge Tsh.40 per 1MB,kwa sasa ni Tsh.95 hivi,na kwa wireless inafikia Tsh.250 per 1MB baada ya kuona wamevuta wateja wengi kiasi walichojiwekea malengo. Ukitazama Zain na Vodacom bei zao zote aibu! Cha ajabu mbona Zantel wanacharge bei fair tu angalau Tsh.56 per 1MB tena wireless dial up connection kama ya TTCL na wanapata faida?
    Hoja aliyoileta mdau ni ya msingi sana ili tuweze kurekebishana hii tabia yetu ya kujifanya sie ndio waelewa,wenye uwezo sana kifedha,tunaojua kila kitu,hali inayotufanya tushindwe kudai hata haki zetu za msingi kwa kuona haya eti utaonekana wavivu wa kufanya reserch,au kuonekana hatujasoma,masikini na kila kitu,na hii ni kwa sababu jamii kubwa ya watanzania ni kweli hatujasoma,ni masikini,na wavivu wa kupambanua mambo ili kujua ukweli,hali inayosababisha kutoona umuhimu wa kudai haki zetu za msingi.
    Mfano kwa sasa mafuta yameshuka bei katika soko la dunia je ni nani kati yetu aliyehamasisha jamii kuandamana au kudai serikari kupitia vyombo vyake kudai bei za mafuta zishuke? achana tu na dizeli au petroli, mafuta yanayotumiwa na jamii kubwa ya watanzania mafuta ya taa ukienda kwenye maduka ya rejareja wanauza hadi sh.1800 kwa lita1 wakati kwenye baadhi ya maduka ya jumla yanauzwa hadi sh 900 kwa lita 1 na muuzaji huyo anapata faida!
    Ninachotaka kuwashauri Watanzania wenzangu ni maisha bora yanatokana na jitihada za wananchi wenyewe kudai haki zao na sumu inayotukwamisha ni kauli zetu za kudhalilishana kama walizoleta wadau wenzangu,maana kama tungekuwa na ujasiri bila kuwa na aibu vyombo vys kudhibiti bei vingekua na nguvu,kwa sasa havina ubavu kwa sababu sisi wenyewe hatuoneshi jitihada za kutaka kusaidiwa

    ReplyDelete
  18. Uliyeleta huu mjadala atafute kitabu kinaitwa "the world is flat by Thomas Friedman" kitakupa mwanga kwa nini Ulaya na asia ya mashariki mtandao wa intaneti ni bei rahisi sana na kwanini makampuni mengi yamehamishia "back room office" huko India.

    ReplyDelete
  19. nyongeza, Ghana wana mtandao bei rahisi pia kwa sababu hiyo hiyo.

    ReplyDelete
  20. Kabla ya kuanza lawama; kwanza tafakari; tambua;changanua; utavumbua ya kwamba TZ intumia internet thru Satelite; na EUR, US na mataifa mengi yaliyoendelea yanatumia internet thru fiber backbone; sasa kweli unalalama nini au ni kutaka tu kuandika kwenye blog ya jamii kujizolea misifa?!

    ReplyDelete
  21. HUYU BWANA ALICHOULIZIA NI SAWA KABISA, HAPA WATU MNASEMA SWALA LA TECHNOLOGY,HIYO SI SAHIHI, TANZANIA WANAPATA WAPI HIYO TECHNOLOGY KAMA SI HUKO MNAKODHANI KUNA ZA KISASA!!! DEMAND AND SUPPLY, THIS IS ECONOMICS, KWENYE DEMAND KUBWA NA SUPPLY NDOGO BEI INAKUWA JUU. NA KWENYE SUPPLY KUBWA DEMAND NDOGO BEI INAKUWA NDOGO. SASA SINA UHAKIKA NA SWALA LA DEMAND NA SUPPLY TANZANIA,LAKINI NAHISI DEMAND NI NDOGO SANA HASA UPANDE WA HOME INTERNETS AS MOST PEOPLE DO NOT HAVE COMPUTERS AND LANDLINE PHONES, SO TUNGETEGEMEA BEI YA CHINI. SWALA HAPA NI CONTROL HAIPO YA SERIKALI, KWANI HATA HUKU ULAYA KWENYE UBEPARI SERIKALI INA CONTROL MASWALA YA WANANCHI, SERIKALI ZAO HUWA HAZIKAI KIMYA WAKIONA WANANCHI WANANYONYWA. KUHUSU FIBRE OPTIC CABLES HATA HUKU ULAYA NI ISP WACHACHE SANA WENYE HIZI HAPA UK NADHANI NI VIRGIN TU, NA HATA HIVYO HAIMAANISHI KUWA WANA HUDUMA SAFI HATA WAO PIA SOMETIMES INAENDA POLEPOLE NA HATA SOMETIMES HUZIMIKA, SOMETIES NI BORA HATA ISP WANAOTUMIA HAINA INGINE, NA HATA HIVYO FIBRE OPTIC BADO UNAHITAJI LANDLINE PHONE, NA ISP WOTE AWE WA AINA GANI SETTILE INATUMIKA, KWANI KUNA WATU HAPO WANASEMA UKITUMIA SETTILITE INTERNET INAKUWA POLEPOLE SI KWELI KWA VILE HAMNA HATA ISP MMOJA KATKA HUDUMA YAKE HAUSHISHI SATTELITE. JUST AN EXAMPLE UNAPATAJE INFORMATION SAY YA WEBSITE BASED IN CANADA IN UK KAMA SATTELITE HAITUMIKI KWA VILE HAMNA CABLE CONNECTION FROM UK TO CANADA, WITHOUT SATTELITE NO INTERNET, ISSUE NI CONTROL FOR CONSUMERS KAMA HUKO ULAYA SERIKALI ZINAVYOFANYA.

    ReplyDelete
  22. Tatizo ndugu zanguni baadhi ya wapiga box wenzangu wanaosha vinywa ili mradi tu amenena kilicho akilini mwake. Huyu mdau wa Uk kaleta mada ya maana sana. Naweza sema katika siku za karibuni, moja ya mada iliyonivutia na kunigusa sana ni hii. Watu mnalaumu bure, afanye utafiti, mnataka utafiti wa namna gani jamani??. Anonym wa 6.27 PM nadhani wewe ndo huelewi kitu na unatupa data mfu kabisa. Kama huna la kusema hapa, kaoge ulale @@@@@Xscschwiiii*****Unaongelea ati fibre cable, khaa, unatia hasira kwa kweli, hao TTCL wana fibre karibu nchi nzima, wana minara wanayomiliki karibu nchi nzima, na hata baadhi ya mashirika ya simu za mikononi yanayofanya vizur zaidi yao TTCL wanatumia mikonga yao lakini hebu angalia huduma za shirika letu hili, maskini!!!!!.

    Kama ni suala la internet, wanauwezo wa kufikisha mpaka Mpanda kama sio Nanjilinji ama kule Mlalo. Yaani wao ni kuamua tu, suala hapo ni RUSHWA!!!! Mimi nadhani kuna haja ya kuliangalia upya hili shirika, hasa uongozi wa ngazi za juu. Ukweli ni kwamba hili shirika rushwa ndio inalisigina hakuna kingine.

    Anonym wa 6.27 PM, kwa taarifa yako, TTCL hata wakiamua leo wanauwezo wa kurusha matangazo ya TV nchi nzima kwa kutumia FIBRE CABLE walizo nazo na ninavyoelewa mimi hizo cable zao zina ubora wa hali ya juu.Sasa jiulize, umeshasikia wana hata mpango wa namna hiyo?? Ambao ungeliendesha shirika kwa faida ya haali ya juu kabisa. La ajabu, kila kukicha migogoro ya kufukuza wafanya kazi, kubadilisha wabia nk. Hao wabia wenyewe wanaowekwa hamna kitu, RUSHWA tu. X~~~@@@&&&***|Zao@@@@@.

    Hebu tujiulize, ina maana hayo mashirika ya simu mnayotaka yaongezeke ili gharama za internet zipungue yana miundo mbinu zaidi ya TTCL???@@@~~Wapuuzi sana nyie@@@. Haya, TTCL wana huduma ya simu za mkononi, sijui ka anonym wa 6.27PM unalijua hilo. sasa kwa taarifa yako kanunue vilonga longa vyao halafu toka nje kidogo tu ya miji mikubwa halafu utatuambia hizo data zako za ajabu ajabu.Tujiulize, hayo mashirika ya simu binafsi kama Celtel, TIGO, VODACOM n.k yanaendeshwaje mpaka yamemudu kutanda nchi karibu nzima ili hali TTCL yenye miundombinu madhubuti inashindwa??

    Mwataka niambia, kweli TTCL wanashindwa kutoa huduma ya internet kwa bei nafuu Tanzania ati gharama za uendeshaji ni kubwa??? Hata kidogo!!! Bado narudi pale pale, RUSHWA. Nina hakika kabisaa, kama watapatikana viongozi wazuri ndani ya shirika letu ( ati changa, jamani) la TTCL gharama zaweza kuwa ndogo sana kuliko za mdau alotulete toka ughaibuni.

    Ati Tz kuna lack control ya mfumuko wa bei, Control ipi ndugu zanguni!! Msitake ncheke na hasira. Miundo mbinu ipo ya kutosha na madhubuti, hawataki kuitumia, halafu unatetea ati hakuna control ya bei!! Hata sikubaliani nanyi hata kidogo.mimi bado nalia na hayo mashirika mengine yaso ya kisirikali, yamewezaje kujitanua na kulifunika shirika la simu TZ (TTCL)??. Hili hakuna haja ya kufikiria mara mbili tatu, jibu tunalo, RUSHWA.

    ReplyDelete
  23. Tatizo ndugu zanguni baadhi ya wapiga box wenzangu wanaosha vinywa ili mradi tu amenena kilicho akilini mwake. Huyu mdau wa Uk kaleta mada ya maana sana. Naweza sema katika siku za karibuni, moja ya mada iliyonivutia na kunigusa sana ni hii. Watu mnalaumu bure, afanye utafiti, mnataka utafiti wa namna gani jamani??. Anonym wa 6.27 PM nadhani wewe ndo huelewi kitu na unatupa data mfu kabisa. Kama huna la kusema hapa, kaoge ulale @@@@@Xscschwiiii*****Unaongelea ati fibre cable, khaa, unatia hasira kwa kweli, hao TTCL wana fibre karibu nchi nzima, wana minara wanayomiliki karibu nchi nzima, na hata baadhi ya mashirika ya simu za mikononi yanayofanya vizur zaidi yao TTCL wanatumia mikonga yao lakini hebu angalia huduma za shirika letu hili, maskini!!!!!.

    Kama ni suala la internet, wanauwezo wa kufikisha mpaka Mpanda kama sio Nanjilinji ama kule Mlalo. Yaani wao ni kuamua tu, suala hapo ni RUSHWA!!!! Mimi nadhani kuna haja ya kuliangalia upya hili shirika, hasa uongozi wa ngazi za juu. Ukweli ni kwamba hili shirika rushwa ndio inalisigina hakuna kingine.

    Anonym wa 6.27 PM, kwa taarifa yako, TTCL hata wakiamua leo wanauwezo wa kurusha matangazo ya TV nchi nzima kwa kutumia FIBRE CABLE walizo nazo na ninavyoelewa mimi hizo cable zao zina ubora wa hali ya juu.Sasa jiulize, umeshasikia wana hata mpango wa namna hiyo?? Ambao ungeliendesha shirika kwa faida ya haali ya juu kabisa. La ajabu, kila kukicha migogoro ya kufukuza wafanya kazi, kubadilisha wabia nk. Hao wabia wenyewe wanaowekwa hamna kitu, RUSHWA tu. X~~~@@@&&&***|Zao@@@@@.

    Hebu tujiulize, ina maana hayo mashirika ya simu mnayotaka yaongezeke ili gharama za internet zipungue yana miundo mbinu zaidi ya TTCL???@@@~~Wapuuzi sana nyie@@@. Haya, TTCL wana huduma ya simu za mkononi, sijui ka anonym wa 6.27PM unalijua hilo. sasa kwa taarifa yako kanunue vilonga longa vyao halafu toka nje kidogo tu ya miji mikubwa halafu utatuambia hizo data zako za ajabu ajabu.Tujiulize, hayo mashirika ya simu binafsi kama Celtel, TIGO, VODACOM n.k yanaendeshwaje mpaka yamemudu kutanda nchi karibu nzima ili hali TTCL yenye miundombinu madhubuti inashindwa??

    Mwataka niambia, kweli TTCL wanashindwa kutoa huduma ya internet kwa bei nafuu Tanzania ati gharama za uendeshaji ni kubwa??? Hata kidogo!!! Bado narudi pale pale, RUSHWA. Nina hakika kabisaa, kama watapatikana viongozi wazuri ndani ya shirika letu ( ati changa, jamani) la TTCL gharama zaweza kuwa ndogo sana kuliko za mdau alotulete toka ughaibuni.

    Ati Tz kuna lack control ya mfumuko wa bei, Control ipi ndugu zanguni!! Msitake ncheke na hasira. Miundo mbinu ipo ya kutosha na madhubuti, hawataki kuitumia, halafu unatetea ati hakuna control ya bei!! Hata sikubaliani nanyi hata kidogo.mimi bado nalia na hayo mashirika mengine yaso ya kisirikali, yamewezaje kujitanua na kulifunika shirika la simu TZ (TTCL)??. Hili hakuna haja ya kufikiria mara mbili tatu, jibu tunalo, RUSHWA.

    ReplyDelete
  24. Ni ghali kwa vile wenzetu wanapeleka angani satelite zao sie tunategemea tutapata kwa the same price?

    Gharama zao nani atazilipia

    ReplyDelete
  25. HATUNA TEKNOLOGIA YA KUWEZESHA INTERNET ISAMBAE NCHI NZIMA NA KWA BEI ZAIDI! WENZETU WANA MITAMBO CHINI YA ARDHI HAWATEGEMEI TU SATTELTITE SASA MPAKA NA SISI TUENDELEZE TEKNOLOJIA YETU BAS NA VITU KAMA HIVYO VITAKUA BEI RAHISI KWA KILA MTU!

    ReplyDelete
  26. naomba nimsaidie huyu mdau wa uk kama ni kweli! je anajua bei ya internet kutumia satellite? isp wote wana depend kuleta internet bongo kwa kutumia satellite. naomba aje afungue kampuni ya internet aweke hizo bei anazoona ni sawa. kaka beba box

    ReplyDelete
  27. HUYU JAMAA ALIYELETA HII ISSUE HAPASWI KUONEWA HURUMA WALA NINI, INABIDI AAMBIWE UKWELI KUWA HAKUFANYA RESEARCH YA KUTOSHA KABLA YA KUAMUA KUTUMA HII HABARI KWENYE BLOG. hII IWE FUNDISHO NEXT TIME KWA WALE WOTE WANAOPENDA KUKURUPUKA NA WAVIVU WA KUJITUMA. TUNAPOKUWA KATIKA VYUO MBALIMBALI TUNALAZIMIKA KUFANYA REASEARCH KAMA SEHEMU YA KUJIFUNZA KUJENGA DATA ZA UHAKIKA, SASA KAMA YEYE HAFANYI HIVYO BASI HANA HAKI YA KUTUMA KWENYE BLOG KAMA ALIVYOFANYA.

    USHAURI:SIKU NYINGINE WEKA HOJA YAKO KATIKA MFUMO WA SWALI, TUTAKUELEWA VIZURI KUWA HUJUI NA UTAELIMISHWA.

    ReplyDelete
  28. VodaCom Angalia wamefunga Hiyo Link ya Price zao hii kuzihilisha Wizi wao kwa watanzania Hawa jamaa wanao jifanya wanatoa huduma Bora ya Masiliano Bongo Ndiyo wezi wakubwa waangalie wenzao wa Extreme

    ReplyDelete
  29. Wote mliomshambulia mtoa hoja au aliyeuliza wote ni limbukeni, muulizaji au mtoa hoja hana matatizo, mlio na matatizo ni ninyi, nyie hamshangai kwa nini huo mradi wa Fibre optic cable kutoka South Africa haujafanikiwa hadi leo ni longo longo? wizi mtupu........hao TCRA unajua interest walizo nazo kwenye haya makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano? ufisadi tu.....bei haziwezi kupungua na wanajamii wataendelea kukamuliwa tu. hakuna cha kuregulate wala nini, hizi regulatory board zingefungwa tu, EWURA imefanya nini kuregulate bei za mafuta? haya TCRA imefanya nini ili kuhakikisha bei ya internet au simu za mkononi zinapungua? kama sio kukusanya fees tu kila kukicha, kwa hiyo ndugus tusimshambulie mtoa hoja tuangalie mzizi wa fitna uko wapi....ni serikali na vyombo vyake...na si demand and supply kama mtu mmoja aliyesema hapo juu, kama ni lwa ya demand and supply demand ipo juu tu hadi vijijini watu wanataka internet, matumizi ya simu Africa yako juu lakini bei bado ziko juu tu, Nawasilisha

    ReplyDelete
  30. kuna jamaa hapo anasema tanzania ina miaka 40 tu ya uhuru hivi kwanini tunasema hivyo, kwani dunia imeumbwa miaka 40 iliyopita,eneo la tanzania ilikuwepo tangu dunia imeumbwa na tulikuwa huru saana tukaapigana sana wenyewe kwa wenyewe wazungu wakaja tukauzana sana so kusema tuna miaka 40 ya uhuru ni exit excuse hazifai kwa dunia ya sasa
    tumelala tu kwanza miaka 40 ni mingi sana kama ni swala la maendeleo kama tungekuwa makini hayo ni mawazo yangu nipo positive hata 20 yrs ni nyingi snaa kwenye maendelea kizazi eg mtoto anayezaliwa leo ukianza kumulimisha uikampa elimu ktk kipindi cha 20 atakuwa yupo ofisini anaonyesha utaalamu wake so 40 sio mchezo ni mingi mno jamani

    ReplyDelete
  31. 1. Kwanza nasikitika kwa waliomponda muanzisha mada. Hiki ni Kijiwe anyone anaweza kuja na Mada yake, hukatazwi...Huna cha kuchangia Kaa KIMYA.

    2. Wale wanaodhani Research hadi paper aiandike MTU, they are wrong...kwa Huu mjadala tu...yatosha kuwa Reseach. Kwa Namna ya wadau wanavyochangia, Muanzisha mada atakuwa ametafiti vya kutosha.

    3. Kwa elimu yangu ningependa nitoe ufafanuzi kiasi juu ya Hili...Japo ntakubaliana na baadhi ya wachangiaji ktk Hili...

    a) Walio ongelea Fibre Optic...hapa inategemea. Ikiwa unataka kuwasiliana na DSM-Mwanza au DSM-UK/US....Njia za Mawasiliano either cable, Wireless,au Satellite(Wireless over large distance)
    Kwanza TZ...Mradi wa Fibre to South or Dubai naona haujakamilika...Wenzetu wa Kenya huenda wakatuzidi...Rushwa ipo Kenya,lkn wanajitahidi kuwa serious ktk Utendaji...

    Pia sina Hakika kama Fibre tunayo locally TZ nzima thru TTCL, na Kama IPO basi tukubali kuwa TZ bado RUSHWA au USALITI ni wa Kiwango cha KUTISHA. Kwani TTCL wangeweza kuleta ushindani mkubwa kwa infrastructure walizonazo...

    b) Gharama za Internet ni kubwa kwa Mashirika ya simu kwasababu PATH yao primarily ni ya kupitisha VOICE Calls...na si DATA na ndio Maana charge zao zipo per MB. na si transfer speed. na Ndio maana internet ya aina hii ni ya kuangalia mambo muhimu tu, otherwise utajikuta unapay price kubwa.

    c) Kuwepo Fibre Optic baharini to SOuth or Middle east kutarahisisha sana International Calls na Internet( Hasa TTCL maana Tayari ana cables majumbani...)...Mobile Provider..wanaweza kuwa na Cheap international Calls, lkn price ya Internet yaweza isipungue na kama ikipungua basi si sana.

    d) Satellite bado nayo ina challenge kubwa na itachukua muda wa Mrefu kwani kwa infrastructure tulizonazo, tutaendelea kuitumia. Speed ya Satellite si Ndogo inategemea na matumizi yako.

    e) Kwa Bandwidth ya TTCL ya Satellite ni kubwa na sijui kama kuna Provider mwingine ambae anaweza kumfikia TTCL kwa capacity yake...Tuombe M/Mungu tumpate Kiongozi anaeipenda nchi yake...basi alau tupate alau kashika Kamoja kanachofanya Vizuri....nina Mengi lkn naishia Hapo

    ReplyDelete
  32. WACHUMI HEBU NIAMBIENI KWA VIPI KAMPUNI INAYOFANYA KAZI KWA GHARAMA HALALAI INAWEZA KUTOA ZAWADI ZA MAGARI KILA MWEZI MWAKA MZIMA, PIA INAWEZA KUTOA ZAWADI ZA MUDA WA MAONGEZI BURE, PESA TASLIMU NA MISAADA KWA JAMII? NA BADO IKABAKI NA FAIDA NA KUGHARAMIA UENDESHAJI WA KAMPUNI. TUNAHITAJI TUPATE UKWELI KUHUSU GHARAMA HALISI SI KWA MAKAMPUNI YA SIMU TUU BALI PIA GHARAMA TUNAZOLIPA KWA HUDUMA ZA KIBENKI IKIWA PAMOJA NA RIBA ZITOLEWAZO KWA MIKOPO MIDOGO.

    ReplyDelete
  33. Mtimkavu, wewe una akili. Naungana na wale walionena, mti mkavu hauchimbwi dawa. Ume summerize hii issue ninavyotaka, bila jazba, bila upoendeleo na point ni kali. Keep it up!!


    MBXc

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...