Alexander Gwebe Nyirenda, ni jina ambalo linakumbukwa na litaendelea kukumbukwa kutokana na mchango wake hususani wakati wa sherehe za uhuru.Nyirenda ndiye aliyeipandisha bendera ya uhuru kileleni katika Mlima Kilimanjaro na kuuwasha mwenge wa uhuru ili umulike mipaka yote ya Tanganyika.

Bongo Celebrity ilipata fursa ya kufanya mahojiano na Major Nyirenda ambaye bila kusita alikuwa mwepesi wa kutueleza historia ya maisha yake na zaidi juu ya utumishi wake jeshini na kumbukumbu yake kuhusiana na siku ile.
Kupata mahojiano hayo bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Watu kama hawa tunakutana nao mtaani tunawachukulia poa, tunapanda nao vidaladal tunawachukulia poatuuu!! Watu kama hawa inabidi wapewe matunzo muhimu na serikali kama US au nchi nyinginezi zifanyavyo kwa Senior Citizen wake au wastaafu wa jeshini!! Huyu (sijui cheo chake) Alexander Nyirenda awe mtu wa kukumbukwa na kuwekwa almost kwenye kila history book ila tunamsikia kwenye legends tu..!! Kana kwamba hana umuhimu!! Hawa ndio waanzilishi wa hii tunayoiita Independent Tanzania..

    ReplyDelete
  2. Major Nyirenda alistaafu utumishi uliotukuka Jeshini akiwa na cheo gani? na mwaka gani? Maana Bongocelebrity haikugusia hilo.

    Mdau
    Glasgow, Scotland.

    ReplyDelete
  3. oya nyirenda yani nyerere hata hakukulipa kamshahara kakununua buti la maana..jamani! buti hilo mbona limekwisha

    ReplyDelete
  4. INAPENDEZA KUONA NCHI YETU INAMCHANGANYIKO WA KILA AINA YA WATU SIKUJUA KAMA JAMAA NI WA MALAWI ORIGIN YAKE INAPENDEZA OYAH BRO MICHUZI EHE HII BLOG YAKO MAN NI FUNIKA BOVU TUNAOMBA TU MOLA AKUPE NGUVU KAKA MAANA DA KAZI UNAYOIFAYA SI MCEHZO HII NIKWA WOTE WANAOMILIKI VYOMBO VYA HABARI KWA KUTUPASHA WANANCHI NYETI MOTOMOTO SIO KUJINUFAISHA TU ILA KUNA NYETI ILE YA WIZI WA UWANJA WA NDEGE KUNA JAMAA NAKAA NAYE NA ANAFANYA KAZI UWANJA WA NDEGE AMENIAMBIA ATANIPA HABARI KAMILI OYAH HII KITU NI SERIOUS JAMANI NDUGU ZETU WENGI TOKA MAJUU WANALIZWA MAZAGAZAGA KIBAO HATA MIE NILISHAGA UZIWA ZAGAZAGA NA MTU WA UWANJA WA TAIFA SIKUJUA KUWA WANAYAIBA BAADA YA KUSOMA HAPA NDIO NIMEPATA MWANGA KUMBE HAYA MAZAGAZAGA WANAYAIBA MIE NILIJUA WANAYAAGIZA KWA KUWA WAPO PALE UWANJA WA NDEGE KUMBE LA HASHA PAMBAFU SANA HAWA MAJAMAA

    ReplyDelete
  5. Tunapenda sana sifa za mdomo, hizi ndizo hulka zetu wabongo.

    Wazee kama hawa ingetakiwa waenziwe, kwa mfano wenzetu wana utaratibu wa kuwasaidia wazee,angalau waishi kwa raha kipindi chao cha uzeeni, lakini Tanzania tuna sera za kuwatelekeza wazee,mfano kama wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki walivyofanyiwa, je kama wasingedai kwa mbinde unafikiri hizo haki zao zingeenda wapi? Na hawa kwasababu wana mwamko wa kudai, kuna wazee wamefanya kazi mbalimbali kwenye mashirika ya watu binafsi, haki yake ipo ndani ya mkataba uliotungwa na muajiri ili kumnyonya mfanyakazi, akilalamika anafukuzwa kazi.
    Mfano mwingine ni wakati wa kulipwa kiitwacho kiinua mgongo, NSSF NA NPF. Hiki kiinua mgongo kinakatwa kodi, kama sikosei, wakati huohuo huyu mzee alilipa kodi tangia anaajiriwa(PAYE),na kamshahara kake ka `mkono-hadi mdomoni-lakini hushibi.
    Hii hela anayolipwa kama kiinua mgongo inatokana na makato katika mshahara wake, ambao kila siku thamani ya hela hiyo inashuka. Kwahiyo thamani ya hela aliyokatwa enzi hizo hadi leo huwezi ukanunua kitu cha maana. Hela hiyo ilichukuliwa na NSSF NA NPF,Wakaizalishia kwa wakati muafaka,yeye anarejeshewa wakati thamani yake imekwisha, na sijui kama na yenyewe inakatwa kodi tena.
    Sasa jamani huyu mzee mnataka akafe au tunamjali vipi kama sio sifa za mdomoni ili tuonekane tunawajali. Tunasubiri wafe ili tuanzie kuwaimbia wimbo wa kuwakumbuka au kuwaenzi kama una sifa kidogo kama baba wa taifa, vinginevyo utasahauliwa kama choo.
    Mzee Nyirenda ameumwa na tunashukuru alipata matibabu, sijui alilipiwa na nani,nakama watoto wake wasingegangamala, tungeshamsahau shujaa huyu. Sasa huyu anajulikana kidogo, wapo wastaafu wa jeshi, wastaafu serikalini au hata mashirika ya wanyinyaji, hawa wote wamegeuka-ombaomba, wengine wagonjwa hawana wakuwapatia tiba.
    Jamani laana ya umasikini usidhani inakuja hivihivi, hata wazee wetu hawa wanachangia kutulaani kwa kuwaibia jasho lao na kuwatelekeza.
    m3

    ReplyDelete
  6. mh!!! malawi???

    WADAU AIR-TANZANIA NDEGE ZOOOOOTE HAZIRUSHWI TENA,,,CHEKSHIA BALAA LA USAFIRI SASA BONGO-MIKOANI

    ReplyDelete
  7. huyo anaye ongeleea buti anafikiri kalivaa jana . wajameni mbona midomo tu .

    the guy is from malawiiiiiiii, lakini wana adabu kuliko wakenya ila wana roho mbayaaaaa !we mubaya aaaaaaa akudo sound upooooooo

    baba yake suzyo nyirenda wa mac millan

    ReplyDelete
  8. It doesn't matter where the guy came from, the important thing is, he did what he did. Can we get his recent photograph?

    Happy Holidays Everyone :)

    ReplyDelete
  9. Michu fatilia hii,,,,
    gazeti la TANZANIA DAIMA tar 9Dec 08,,hii picha wameitoa na wameadnika ni jenerali mstaafu wa majeshi 2mrisho sarakikya2 na page ingine wamemtoa JK akiwa na mwamunyange ktk gari lile na wameandika miaka "462 ya uhuru wa tanganyika
    WHAT KIND OF EDITOR IS THAT??
    YANI KWA AKILI NDOGO TU UKO KUCOPY NA KUPASTE JAMANI GAZETI LALOSOMWA NA wa-Tz weeengi
    PPLE R NOT SERIOUS,,i was so shocked yan kusema historia ya tola darasa la 3 ni uongo??
    WHICH IS WHICH??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...