Mjadala huu wa Afrika Mashariki hatuwezi kuufunga ama kuuhairisha bila ya kufanya maamuzi yenye manufaa kwa Taifa letu.
Baadhi ya wananchi wenzangu wametoa ushauri na maoni yao juu ya mjadala wawa jumuiya ya Afrika Mashariki. Mjadala huu umepamba moto kwa kasi sana hivi karibuni. Na kumekuwa na kutoelewana katika kufikia muafaka haraka.
Mpinzani wetu mkubwa Kenya, analalamika sana eti kwamba Tanzania tumekuwa kikwazo kwa jumuiya hiyo kufikia makubaliano haraka tusaini mkataba. Hawa Wakenya mbali na kutulaumu kuwa tunachelewesha jumuiya hiyo, utakumbuka kwamba hawa hawa Wakenya ndio waliovunja agano la kwanza, na sasa wanatulazimisha tuingie katika agano jipya bila kufikiria, yaani watuburuze tu!. Haiwezekani hata kidogo.
Hivyo basi, napenda kuchukua nafasi hii kupata maoni ya wazalendo wenzangu, kwani natarajia kutoa kitabu hivi punde Kitakachoitwa MJADAL A WA AFRIKA MASHARIKIHATIMA YA ARDHI YA TANZANIA NA USALAMANimeamua kujitosa katika changamoto hii baada ya kuona kuwa ni sehemu ndogo kati ya watanzania, walio bahatika kutoa maoni yao ama kusoma maoni ya wengine kuhusiana na mjadala huu.
Hivyo basi kudumisha harakati hizi nakusudia kutumia maoni mbalimbali ya wazalendo waliochangia.Katika kuendeleza jitihada za kuilinda Tanzania, nimeazimia kufuta usemi wa jirani zetu kwamba ,eti sisi Watanzania ni watu wa kulalamika tu na hatufanyi chochote cha maana. Hivyo basi, imenilazimu nichukue hatua muafaka kwa wakati muafaka kufuta usemi wao.
Halikadhalika, ninataka kuwatahadharisha umma wa wana wa Afrika Mashariki wajue kuwa, sisi ni kizazi kipya na si cha kudharauliwa, na vile vile kuwahakikishia kuwa hakuna mtu aliyelala usingizi tena hapa Tanzania. Tumesoma, tuna uwezo, upeo na tuko tayari kulinda maslahi yetu na hatima ya taifa letu kwa ajili yetu na vizazi vyetu vijavyo. Kwa hiyo hatuko tayari kukubaliana na masharti haya katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nanukuu, kama ilivyoandikwa kiingereza
Chapter One: common standard travel document" means a passport or any other valid travel document establishing the identity of the holder, issued by or on behalf of the Partner State of which he or she is a citizen and shall also include inter-state passes;
Chapter Seventeen: Free Movement Of Persons, Labour, Services, Right Of Establishment And Residence
Mwisho wa kunukuu
Nisingependa tena kurudia maoni tuliokwisha changia. Kwa kifupi tu wenzetu hasa Kenya na Uganda wana matatizo makubwa sana ya ardhi. Tanzania ndio nchi pekee iliyobaki yenye ardhi kubwa kwa ajili yake na wananchi wake. Daima tunakataa, kwa Tanzania haiwezekani ardhi yetu iporwe.
Kamwe hatuta ruhusu ardhi yetu iporwe,
Sisi ni watanzania halisi,
Raia wa Tanzania,
Watoto wa Tanzania,
Tanzania ndio kwetu.
Baba yetu wa Taifa, MWL. JULIAS K. NYERERE alituambia
Nanukuu
In a country such as this,"... where, generally speaking the Africans are poor and the foreigners are rich, it is quite possible that, within eighty or a hundred years, if the poor African were allowed to sell his land, all the land in Tanganyika would belong to wealthy immigrants, and the local people would be tenants. … but even if there were no rich foreigners in this country, there would emerge rich and clever Tanganyikans. If we allow land to be sold like a robe, within a short period, there would only be a few Africans possessing land in Tanganyika and all the others would be tenants"Mwl. Julius K. Nyerere, 1958
Mwisho wa kunukuu
Ndugu zangu, watanzania tuamke tembeleeni hii website ya Jumuiya hii, na mchimbe kwa makini,
Mwisho, nawapongeza sana viongozi wetu wa sasa, wakiongozwa na Rais wetu, Mh. Jakaya M. Kiwete kwa msimamo waliouonesha kutetea maslahi ya nchi katika mjadala huu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Na pia nawaomba wakumbuke kwamba NGUVU YA UMMA NI KUU, haswa linapokuja suala la kudai haki.
Mungu Ibariki Tanzania
Mwana harakati
Mzalendo halisi
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. EAC ni bora tu iharakishwe!
    miungano daima...na kwa kusisitiza tu kama tanzania bara inavoifanyia zanzibar ndani ya tanzania ndivo kenya itakavoifanyia tanzania kwa ufupi...mi nahisi baada ya EAC kuundwa balozi zote za nchi za nje iwe haina haja tena ya kukuwepo TZ na badala yake zikuwepo tu kenya!
    raisi wa EAC awe direct anapatikana kutoka katika uchaguzi wa kenya..na awe anaishi kenya!japo wa tanzania awepoila yule wa EAC awe ndio amiri jeshi mkuu..mitihani yote ya taifa la EAC iwe inatungwa na kusahihishwa kenya...na tuwe tunatumia sarafu moja ila viwango vya mishahara vya wafanyakazi wa serikali ya kenya viwepo juu zaidi ya vya wale wa tanzania bara wakifuatiwa na kule visiwani..mawaziri wote wa wizara za EAC wawe wanaishi zao kenya..raisi wa tanzania awe anachaguliwa kupitia vikao vya chama tawala cha EAC vinavofanyika kenya...uwanja wa ndege wa jomo kenyata ndio uwe uwanja wa ndege mkuu wa east africa..i mean ndege zote zinazotoka nje kuja tanzania ziwe direct zinatua kenya..jina la east africa liwe ni KENYUGATANBURWANDA linalotokana na maneno ya mwanzo ya nchi zenyewe nchi zenyewe lakini kwa kuzingatia ipi bora ndio inaanza mwanzo.... na mengi mengineyo !
    then kwa yule mkaazi wa tanzania bara atakaeona mabaya ya mambo haya asiwalaumu sana wazanzibar wanapolalamikia mapungufu ya kutokuwepo kwa usawa wa muungano wa tanzania.

    ReplyDelete
  2. Thanks men, umesema siyo Mashaka kazi kutukana kwa Kiingereza tu lakini hana reference yoyote, badala yake anazungumzia NAFTA.

    Safi, safi sana. Okoa jahazi.

    ReplyDelete
  3. Mzalendo Halisi umesema cha maana! We cannot take it anymore insults from some people in Kenya as our fathers used to! There is NO WAY! We Tanzanians treat people with respect including foreigners!Now some guy, Warigi stands there and throw anything on the face of Tanzanians just because he can speak English! No Way this Time!It's a matter of time, JUSTICE will take its course!
    Chakubanga

    ReplyDelete
  4. Ahsante Mzalendo kwa kunifumbua macho kuhusu Website hii ya Wizara ya Afrika Mashariki, ambapo naona Mwenyekiti wa Kamati Profesa Wangwe anapokea maoni kutoka kwa watu wanaotaka kuchangia. Naomba wale mlioweza kupangilia pointi zenu vizuri msichoke, mzitume tena huko kwa Wangwe.

    Bwana Michuzi Ahsante sana kwa blogi yako hii. Kupitia blogi yako Watanzania wenye upeo mkubwa wa kuangalia mambo kwa undani, lakini hawana pa kuzungumzia, wameweza kutoa maoni yao bila woga, na nadhani kwamba mengi yatakuwa yamefika sehemu husika, na viongozi wetu, pamoja na wale waliokabidhiwa dhamana na Watanzania wataweza kufikiri kwa mapana zaidi na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

    ReplyDelete
  5. Fikiria kuwa ulikuwa unaoga kwenye bafu ya makuti, ghafla kichaa kaja kachukua nguo zako ulizokuwa umezitundika mlangoni na kuanza kukimbia nazo barabarani. Je ipi busara kwako, kumfukuza huyo kichaa ukiwa uchi huku ukimtupia matusi ya nguoni AU kutafuta namna ya wewe kwanza kujisetiri upate nguo ya kuvaa, kisha utengeneze hiyo bafu iwe nzuri ya kisasa na imara ili siku nyingine huyo kichaa asiweze kukudhalilisha tena? I COULD SAY, ALUTA CONTINUE, BUT WITH CONSTRUCTIVE AND POSITIVE IDEA. TUSIPOTEZE MUDA.WENYE UPEO MZURI WATUSAIDIE TUTAFUTE MAJIBU YA MATATIZO YETU

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  6. I think these Kenyans and Ugandans are confused, and I don't know their ways of thinking, still yet they think we are the same of 1947, no way, now we are more educated than they think. You know what they want? 1. TAX FREE FOR THEIR PRODUCTS FOR FIVE YEARS, 2. FREE MOVEMENT OF LABOUR, 3.LAND OWNERSHIP, 3.SAME PASSPORT,
    4.FOREIGN DONORS TO DONATE UNDER FEDERATION NOT INDIVIDUAL COUNTRIES AND MANY MORE, PLEASE TANZANIANS AND OUR LEADERS let us read between the lines of the so called the fedaration document itself before we give our final judgement.Please take time and read what KAMALA said below:


    "Many obstacles to EA Federation, says Kamala

    2008-12-08 11:24:46
    By Hellen Nachilongo


    The Minister for East African Cooperation, Dr Diodorus Kamala has said there are many obstacles that each EAC member state faces that hinder the creation of a political federation.

    The minister was officiating during a ceremony held at Genius King`s Nursery School over the weekend in Dar es Salaam,``Saying that Tanzania has to leave the rest of the EAC countries to proceed with the Federation does not sound good for our regional political and economic undertakings,`` Kamala said.

    The minister`s comments were prompted by school proprietor Julius Rutumbanja, who said his institution was facing a shortage of teachers who could teach in English.

    Rutumbanja told the minister that it was quite hard to get English teachers from neighbouring countries because it was taking too long for them to secure working permits.

    Dr Kamala said establishment of the East African Federation would not come soon, given the obstacles each EAC member state was facing.

    ``They (other EAC member states) are complaining that we are taking too long to sign the common market protocol, but both Kenya and Uganda have demanded that they should be given five years tax relief for their products. These ``five years`` also serve as obstacles to the proposed East African federation,`` he said.

    The minister said: ``Allegations that we are stalling the unification process do not make sense to us because you cannot just build a house without building a foundation first.``

    He said some of the EAC states didn�t have abundant arable land compared to Tanzania. ``They think that they would get land from Tanzania after joining the federation, but we cannot do that. We cannot simply give it to them.

    We can only allow them if they want to invest, but not to use it as their property after joining the federation,`` he said.

    He said Tanzania`s land had been preserved for future generations and conservation of the country\'s natural resources.

    Kamala said Tanzania could not simply jump into the Common Market without first applying concrete solutions to the problems it was still facing.

    In August Kamala addressed representatives from Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi and Rwanda the five countries that make the EAC.

    The minister was quoted as telling delegates that although the country was committed to East African cooperation, it was still skeptical on provisions of the treaty concerning land.

    He said Tanzania would press on the omission of acquisition of land by non-citizens under the East African Common Market protocols.

    The Right of Residence � one of the major items under the Common Market protocol �does not automatically give a non-citizen from the East African Community states access to land.

    ``An investor in Tanzania can access land without any problem. But land is not in the Right of Residence protocol,`` said the minister

    Last month, Tanzania openly gave its stand - that there would be no land deal in the East African Community (EAC).

    East African countries have failed to agree on how to handle three major pertinent issues: land ownership, free movement of people and permanent residence"

    KAMALA KAZI MZULI, UKILEGEA LAWAMA KWAKO HATUTOKUSAMEHE KAMWE.

    HIVI WANAJIONA WAJANJA NA SISI WAJINGA, BASI NA MUUNGANO WENYEWE BASI HATUTAKI.

    ReplyDelete
  7. HATUIITAJI MUUNGANO BWANA TUACHENI TUISHI KIVYETU NYIE WAKENYA.KWANZA MLITUINGIZA SHULE ULE WA KWANZA MKAKOMBA MALI ZOTE ULIVOVUNJIKA SASA HIVI MNATAKA KUTUSHIKA MASIKIO TENA AAAH WAPI. TUNA MIFANO HAI BADO INATUUMIZA MFANO MDOGO TU KILIMANJARO MNAITANGAZA KUA YA KWENU NA MNATUMIA MBUGA ZETU KUINGIZA WATALII MLIOWATAPELI ULAYA KUJA KUONA MBUGA ZENU KAVU HAZINA HATA MJUSI.NA NYIE VIONGOZI MNAOBABAIKA NA KUSIGN MIKATABA KWA MADAI MKIKAA KATIKA UONGOZI KIPINDI KIMOJA MNAJITENGENEZEA HELA ZA KULA MIAKA 100 SAFARI HII TUNACHOMA MOTO TU KAA KIBAKA ALIEIBA SAA YA ELFU KUMI TU ANAVOPOTEZA MAISHA . HUKO KENYA UKIULIZA NJIA WANAKUCHARGE SIE WATANZANIA HATUNA TABIA HIZO.DAHH TUKIJIPINDUA MANZESE ITAJAA CHOKORAA KUFA MTU

    ReplyDelete
  8. My fellow Tanzanians, It’s good to disagree without being disagreeable. Let’s not be a firewall towards regional trade. Global and regional trade is the norm of the 21 century. The fact of the matter is the whole world is moving toward global and regional trade liberalization.

    Mashaka made his opinion in the debate. None of us rule with our opinion in a debate. Mashaka himself knows well that US gave him that opportunity to advance and realize the American dream. This wouldn't be possible if US had its doors shut to foreigners. Mashaka opinion absurd and its like building a firewall towards international free market which put him in Wall Street at the first place. Misleading people by rationalizing the US recession and unemployment problems is a result of bad treaty such as NAFTA is a day break lie. Greed, mismanagement of corporate America and Wall Street in particular is to be blamed, and Mashaka you are a part of it. Brother, be honest with your facts while gaining your little fame back at home for your future endeavors. You and I, we both know what went wrong in the US. Let us be real about it.

    After taking a moment in scrutinizing the whole debate of East African federation, I can understand Warigi's point of view even though he had a negative delivery tone. His harsh words are a result of frustrations caused by Tanzania being a firewall in EA federation progression. Warigi even mentioned if we are not ready we can pull out and let other member countries proceed with the federation. I agree with him since Tanzania is putting other member countries in stagnation.

    On the other hand, I understand my fellow Tanzanians concerns and I strongly agree with them in issues related to land privatization to foreigners, employment, national security, mining industry, and tourism industry. I feel we should pull out of the federation and let other countries proceed while we take care of our own problems at home. By doing so, Tanzania will have a clear picture as we pay close attention of the federation’s progress before committing itself.

    The urgency of solving our own problems in the country overrides the significance of joining the confederation at this moment. Our priority right now should be: building our democracy; building our infrastructure; combating graft and corruption; fighting poverty and diseases; raising our economy with its people’s living standards; and educating our people.

    ReplyDelete
  9. Issa Michuzi,please,please save everything from Warigi's COMMENT! I mean everything! Na yoyote ambaye haja-copy maneno ya Warigi,it is time now to save them!.Save everything from what there so called media said.

    Warigi:-
    You are insulting your neighbors with impunity protected by Nairobi;
    Descrate our traditional values,gladily;
    You make nonsence our deliberations,happily;
    Sometimes I wonder how you wound up in this council of media with your DIRTY COMMENT!With No Respect at All!

    We are going to show Nairobi and Warigi that Tanzanians can't be insulted so easily as used to,just because of EAC! We Tanzanians are known NOT TO FORGET at all! Hatusahau sisi hata siku moja! We are holding Warigi and Nairobi RESPONSIBLE for demeaning our Motherland till JUSTICE is DONE!It's serious,and it will remain serious! We cannot take it anymore Tanzanians, from some funny african from Kibera slum insulting us as though we are trash! NO WAY this time!NO WAY! Sisi hatusahau hata kidogo bwana! Msuya alisema: "kila mtu atabeba mzigo wake",akiwa waziri wa fedha;halipotoka baada ya miaka mingi,tulimweka hadharani atueleze kwa nini anaongea hivyo,wakati sisi ndio tulimweka kwenye Uwaziri huo.Mramba naye,tumemkumbusha hilo kwamba,kwa nini tule nyasi bwana,kwani sisi ni ng'ombe au mbuzi!We are also waiting,any violence,any chaos in Kenya;watanzania tutasambaza comments za WARIGI with capital letters to all the TVs,chatrooms,e-mails,magazetini, hata ya Nipashe na Udaku,so that NO kenyan should step near our dirty,poor borders running for safety! They should go to a clean and rich Uganda,Somali,Sudan,Ethiopia or other neighbors NOT Tanzania,the Warigi cursed,insulted and demeaned land!No way! We are NOT gonna allow Kenyans to the land they INSULTED just because they desperate need the EAC!Time will Tell!There will be another definition for Tanzania this time! Look! "People are respected by the wealth of their Virtue NOT by Virtue of their wealth"
    Chakubanga

    ReplyDelete
  10. hatutaki eac basi

    ReplyDelete
  11. HADI KIELEWEKE HII EAC YANI VITU VIWEKWE WAAAAZI NA KM KITU WANANCHI HATUKITAKI BASI STOOOOOP KBS KM ITATUGHARIMU TUVUNJE NA IWE IVO
    ARDHI
    ID
    JOB OPPORTUNITY
    YAN NYAN'GAU ATAEKIMBILIA KUSAINI MKATABA HUU BILA KUUSOMA NA KUUELEWA KITAALAMU,,,LZM AFE NA ASAFE YEYE NA KIZAZI CHAKE FOREVER
    EAC TWAITAKA SANA ILA VIPENGELE VILIVYOPO LZM VIWE WAAAZI NA TUCHAMBUE PUMBA NA MCHELE FULU-STOP
    mdau toa icho kitabu tukinunue safi sana yan tutakipigia debe weee acha asa sie tulio na ifluence ktk community ya church
    ALUTA KONTINUA

    ReplyDelete
  12. Huyu Mzalendo Halisi nampongeza sana. Ameamua kupeleka harakati kwenye kitabu ambacho kitasomwa na watu wengi. Yaani mpaka wale mama, wajomba, bibi na babu zetu walioko vijijini watasoma na kuona mustkabali mzima wa nchi yao.

    Tunahitaji watanzania wenye akili safi zinazofikiria kama Mzalendo halisi, sio kupiga domo tu na hakuna lolote la maana linalofanywa. Hakika hiki ni kizazi kipya. Tutakuunga mkono kwa kununua kitabu
    Big up

    ReplyDelete
  13. haki ya nani
    watakizuia icho kitabu,,,vibaraka na mafisadi wa nchi hii,,,nyie wait n see

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...