Michuzi,
Hebu cheki Shemeji langu la nguvu pamoja na mama mzazi wa my wife wangu ni jana katika tafrija ya kumpongeza Anna(Nankondo) baada ya kukamata nondozzz lake la kwanza chuo kikuu cha Mzumbe siku ya ijumaa .Alikula nondozzz ya uhasibu na uchumi (BAF) Ila mimi kama shemeji mtu nimemuonya asije akathubutu ku-EPAlaizi.

Mdau Julius

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera shemeji

    ReplyDelete
  2. Bratha Misupu mbona unatunchanganya weye! wewe si unadai my wife wako anatoka Uganda? ama ndo familia yao isha hamia Bongo kuomba ASYLUM?

    ReplyDelete
  3. Mdau Julius natangaza ndoa kwa shem wako.

    Wasifu wangu:
    Umri 29
    Elimu Msc kazi nzuri malipo mazuri
    Mrefu 6"3 maji ya kunde
    Mpole sina makuu nina tabia nzuri
    Mdau marekani

    ReplyDelete
  4. http://www.youtube.com/watch?v=p95zWsAmTyw

    ReplyDelete
  5. Mzumbe hakuna degree ya uhasibu na uchumi. Hiyo BAF ni Business Accounting and Finance. Kwa kifupi ni B.ACC (BAF), yaani Bachelor of Accountancy in Business Accounting and Finance.
    Mpe hongera shemeji yako kwa kuikwaa hiyo nondo.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana dadangu..

    Lakini hivi ni kwanini sisi wabongo huwa hatu-smailigi (smile) kwenye picha ili angalau picha zinoge? Graduu ni kitu cha ku-celebrate, na si kitu cha kuhuzunikia.

    Hilo ni wazo tu..

    ReplyDelete
  7. Kaka Julzz tupeane madijiti basi hayo ya shem au kashachukuliwa?...au inakuwaje-kuwaje. Mdau uzalendo ushanishinda tayari...

    ReplyDelete
  8. Kaka Jully, chunga sana huyo anyeomba uchumba kwa shemeji, anadai na tabia nzuri sijui hamna lolote, kwanza kujisifia mwenyewe hana makuu na tabia nzuri tayari keshajichanganya, hana heshima hata kidogo.

    hongera Nankondo kuikwaa nondozzz!! ila uwage unachekaga kidogo ukiwa unapiga pichaaaaazzz.

    ReplyDelete
  9. Ha ha haaa, nimefurahi sana kwa ujumbe bwana Julius.Asante kwa picha na hongera sana kwa shemeji.Pls fanya kazi kwa bidii, sisi walipa kodi wote wa Tanzania tumechangia elimu yako , NO EPA-LISATION, Please.

    ReplyDelete
  10. kumbe kweli nilifikiri utani!naskia sikuiz wanaume wanapenda wanawake wasomi nimehakikisha usemi huu,maana tayari watu washaanza kuuza sura kwa dada yetu hapo.Siri kwakina dada kazaneni mmalize shule mtaolewa kirahisi sana.

    ReplyDelete
  11. UMECHAPIA MZUMBE HATUNA NONDO YA UHASIBU NA UCHUMI USIRUDIE TENA.

    ReplyDelete
  12. makubwa
    ila duh wanaume wa siku izi mwanamke msomi dili ile mbaya mana weshagutuka zile mambo oooo sijui asiyesoma katulia ana adabu waaaapi nyinyi???
    wanaume weshaona ugumu wa kula kulala wataka mteremko hahahahahaha

    aaaaa kwa sana tu buku na vijisenti kina dada,yan dume aja akukuta una house,usafiri nk nk basi penzi lashamili mana nooo kuombana weee mana ndo ugomvi wapoanzia

    ReplyDelete
  13. KAKA MICHUZI, SIJUI HATA NIKWAMBIE NINI ILA KWA UFUPI HIYO PICHA TU INATOSHA KUMTOA NYOKA PANGONI. MTOTO ANAVUTIA SIO MCHEZO. KAMA VIPI MIMI NIKO SINGO, SIJAPLAN KUOA LKN KWA SHEMEJI YAKO NITABADILISHA UAMUZI MARA MOJA. ELIMU YANGU CHEKECHEA LKN MAMBO YANGU SAFI. ASITIE SHAKA ATAKULA BATA MPAKA ASHANGAE NA MOYO WAKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...