Kaka Michu,
Bongo raha saaana, ona Hammer na mkokoteni bumper to bumper kwenye foleni, weweeeeeeee
Leo jioni pale Mikocheni mbele ya ofisi za TANESCO jamaa mmoja kaunguliwa na gari. Nilisnepu picha hii wakati ndio kwaaaanza gari la zimamoto linafika. Kama unavyoona moto ulishazimwa na gari la zimamoto limekuja kushangaa tu na kupiga kelele nyingi saaana njiani.
SIKUKUU NJEMA
MDAU



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi , mpiga picha alitegemea gari la zimamoto, au helikopta ya zima moto?

    ReplyDelete
  2. Ninampa pole huyo ndugu aliyepoteza mali yake kwa kuunguliwa na moto.

    Kwa hakika mimi binafsi sipendi uzembe wa aina yeyote ile, lakini kwa hali ya jiji la Dar es Salaam huduma ya zimamoto inabidi iangaliwe upya. Jiji la Dar es Salaam lina kituo kimoja cha zimamoto pale Faya (Fire) kwenye makutano ya United Nations na Morogoro road. Kituo kile kilijengwa wakati wa enzi hizo kukidhi mahitaji ya jiji kwa wakati huo na kwa maana hiyo mabadiliko ambayo yamejitokeza tangu miaka hiyo hadi leo ni wazi kuwa shughuli za zimamoto katika jiji la Dar es Salaam haziwezi kabisa kukidhi hali iliyopo sasa hivi.
    Leo hii moto ukitokea Mbezi Beach tunataka zimamoto ifike kwenye eneo la tukio kabla ya madhara makubwa hayajatokea, inawezekana kweli? Hata kama zimamoto watafika huko na maji yaliyopo kwenye gari (ambayo ninavyojua mimi ni kuwa kutokana msukumo mkubwa wakati wa kuzimamoto huwa yanakwisha haraka), je tunapata wapi maji yaliyo karibu na eneo la moto. Sidhani kama maeneo mengi (kama siyo yote) yanahuduma ya maji kwa ajili ya zimamoto.
    Tusitegeme hata siku moja kupata ufanisi kwenye eneo hili la zimamoto kama miundo mbinu yake haipo kabisa. Kuwa na magari ya kisasa ya kuzimia moto ni sehemu tu ya kukabiliana na moto na kuwa na miundo mbinu thabiti ni jambo litakalo rahisisha utoaji wa huduma kwa ufanisi.
    hayumkini kila siku tutaendelea kuwalaumu wafanyakazi wa zimamoto kuwa ni wazembe wamefika baada ya moto kumalizika lakini je tunajiuliza kuwa huduma hii na miundo mbinu yake iko sawasawa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...