MH. BASIL MRAMBA NA MH. DANIEL YONA WAKISHUKA TOKA CHEMBA NAMBA MOJA YA MAHAKAMA YA KISUTU BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA MUDA MFUPI ULIOPITA.
MAWAZIRI HAO WA ZAMANI WANAOKABIRIWA NA MASHITAKA KADHAA, HATIMAYE LEO WAMEACHIWA HURU KWA DHAMANA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU.

DHAMANA HIYO IMETOKA BAADA YA MH. MRAMBA NA MH. YONA KUWA RUMANDE KWA SIKU KADHAA KWA KUSHINDWA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA AMBAPO WALITAKIWA KUTOA KILA MMOJA BILIONI 3.9 KESHI.
WASHTAKIWA HAO WAMEACHIWA BAADA YA KUWEKA DHAMANA YA HATI ZA NYUMBA ZENYE THAMANI INAYOZIDI BILIONI 2.9 KILA MMOJA
HABARI KAMILI BAADAYE....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. JANA WALIPELEKWA MAHAKAMANI BILA HATI INAYOWARUHUSU WATOLEWE LUPANGO...KWAHIYO MATOKEO YA LEO TULIYATEGEMEA, TUSUBIRI KAMA KWELI SHERIA MSUMENO TUONE UTAKAVYOKATA.

    ReplyDelete
  2. nafikiri tulishapoteza uelekeo kuwa tulitakiwa ku -concetrate kwenye isssue za EPA KWANZA na wala sio hawa watu ambao hawakuwajibika. Hivi mmesahau ni wangapi hawajawajibika nchi hii? Niwataje? Eh? Je aliyewaburuza mahakamani yuko tayari kukamilisha kazi hiyo kwa kuwaburuza waliobaki? Au na yeye atabaki?

    ReplyDelete
  3. Hili swala mbona tulilitegemea tangu zamani. Naona foleni yao ya hati inayowaruhusu watolewe lupango imepitia shortcut ya buguruni
    Haya ngoja tuone kama watarudishwa tena au ndo imetoka kama wakina patel

    ReplyDelete
  4. WAKOME NA WIZI HAO
    WAONE WALIVYOCHOKA HATA SIKU KUMI HAWAJAMALIZA,JE WANGEKAA KA-MWEZI SI INGEKUWA BALAA!!!!
    AIBU ZAO!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. OVYO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    WEZI HAO

    ReplyDelete
  6. Ayaaaaaaaaa,


    Dah!


    Why!!!!!!!!!!!!!!!

    Kwa niniiii!!!!!!!!!!!!!!!

    Huyo Hakimu na Sijamuelewa,

    Hao ilitakiwa wakae huko huko mpaka kesi yao itakapoisha.

    Huku Uraiani ni kuvurigiana Ushahidi tu,

    Mwankenja fikiria upya hii issue ya kuwaachia hao jamaa,

    Tutawapoteza hao pamoja na ushahidi muhimu

    ReplyDelete
  7. Ayaaaaaaaaa,


    Dah!


    Why!!!!!!!!!!!!!!!

    Kwa niniiii!!!!!!!!!!!!!!!

    Huyo Hakimu na Sijamuelewa,

    Hao ilitakiwa wakae huko huko mpaka kesi yao itakapoisha.

    Huku Uraiani ni kuvurigiana Ushahidi tu,

    Mwankenja fikiria upya hii issue ya kuwaachia hao jamaa,

    Tutawapoteza hao pamoja na ushahidi muhimu

    ReplyDelete
  8. Nini hasa masharti ya dhamana yao, this is a very high profile case, and I am telling you now, if the government failed to put them in jail for very extended period of time, then my trust of this country and many of the tanzanians will fade.

    It will have an historical impact for years to come, why we failed yet so close ! My suspicious are comming to life, JE NI CHANGA LA MACHO.

    The government should have right to monitor their movement, and find out who do they meet, and totally confined them to their houses, until we know the outcome and end result of their case. DHAMANA doesn't mean you are off the hook.

    No let off, if then the influence of others penetrate on their behalf then that is it, we are simply writing our destiny, being the nation of corrupts and tainted politicians for years to come. NEED TO BREAK LOOSE!

    ReplyDelete
  9. Hawa jamaa nijuavyo mimi, kama watafanikiwa kuchukua nchi 2010 au jamaa yao akachukua nchi 2010 au 2015, rais mtembezi wa tz na dr. hosia lazima walale segerea, wamedhalilishwa sanaaaaa. kulipa kisasi kutakuwepo... .... mbona dr hosia alisema hakua rushwa suala la richmond wakati tume inasema kulikuwa na rushwa na hajachukuliwa hatua...????

    ReplyDelete
  10. Duh Kumbe wana mali bwana...Houses worth 2.9 Bil ??!! Wakiambiwa wataje mali zao..Ohh ! mimi nina kibanda tu..mbavu za mbwa kimeezekwa kwa makuti...ooh mimi nimekopa hata deni halijaisha !! Tunazugana tu !!

    ReplyDelete
  11. mhh nauliza hivi Alhaj Mintanga yule Boss wa NGUMI ameshapata dhamana au ndio DANGANYIKA hiyo

    ReplyDelete
  12. Wakihusika wao,basi anatafutwa chambo na kuambiwa aseme kuwa amefariki magharibi ya bali.wakiona hawakuhusika moja kwa moja wanajifanya kuwa wanapeleka watu mahakamani wakati kila mdangayika anajua kuwa ni danganya toto.Hakuna serikali hapo,hakuna mahakama hapo na wala hakuna uhuru wa vyombo vya habari hapo.sasa nashangaa kwa nini wanapochota walio wanyonge wanaozea segerea?, halafu bongo bwana, hao watu inasadikiwa wanamaela mengi tu sasa mbona wanaoneka kama choka mbaya,au mimi macho yangu yana walakini? au ndiyo hela za madafu uwe nazo au usiwe nazo hakuna tofauti kwa kuwa bongo kila uendako vumbi kali? kilichobakia wewe ukiwekwa kwenye mfereji wa hela tafufa ndoo uchote.Wenye hiyo mchi walisha zikwa siku nyingi

    Mbega hapa

    ReplyDelete
  13. tupige mahesabu mishahara yao yote na marupurupu yao tuone kama ni kweli wanastahili kumiliki mijengo yenye thamani ya pesa hio kama sio kuibiana huko?imagine kuna hospitali hazijafikia hata thamani ya milioni 20 na ndizo zinazotegemewa kwa uhai wa watu tena wengi basi sio familia tu ya bwana yona au mramba,wajawazito na watoto wetu wanazitegemea hospitali hizo na kila kukicha wanaambiwa serikali haina uwezo kumbe kuna watu humohumo serikalini wana miliki mahekalu ya mabilioni howcomes????!!!!JK taifisha mali hizo kisha uza pesa ikanunuliwe mashine au vipimo muhimbili na hospitali vijijini

    ReplyDelete
  14. Nyumba ya bil 2.9. Bila kukopa benki wamekua masupastaa wa usa. Kabla ya yote watolee maelezo hizo mali zao.

    ReplyDelete
  15. 1. Hivi tukienda kwenye documents za kiofisi- utawala bora & Bunge hawa watu walikuwa wana nyumba zenye thamani hiyo? au ndo mahesabu ya exponential appreciation when you need to be bailed out!

    2. Hivi kwa nini tunaanza na kesi za kutoajibika wakati ziko charges zinazowahusu za wizi na pia wengine wengi ambao hawajakamatwa kwa ajili ya wizi. Usiniulize nilete ushahidi maana wakaguzi walishamaliza kazi yao siku kibao.

    3. Rais wetu Kikwete ukitaka hili jinamizi la wizi wa wazi la EPA litoke mikononi mwako acha Mwendesha mashitaka amsogeze Meghji na Lowasa mbele ya haki na kesi zao zifanyike haraka iwezekanavyo na kuisha kabla ya mei 2009 (na hii inawezekana maana umeshaunda tume kibao na wakaguzi wameandika na wapinzani wamesema mbona ushahidi uko wazi hata Meghji mwenyewe alisema kuwa alidanganywa kwa hiyo alishakiri makosa!!
    Kuna wakati wa kujali urafiki na wakati wa kujali kiapo cha kulinda katiba. Huna haja ya kuweka pamba masikioni juu ya Lowasa maana mengi yanamuhusu likiwamo la ulaghai na hasara iliyotokana na matapeli wachapishaji -Richmond!

    Sikiliza tukusaidie jinsi ushindi wako wa sunami utakavyojirudia 2010mara dufu na hatimaye kupewa tuzo ya rais bora Afrika.

    Huitaji kuita wachumi wala washauri wako wa mambo ya kisiasa wakusaidie; Hapo ulipo sasa hivi ukisoma hii message Mlilie Allah na Mtume wake wakujaze nguvu, ushujaa na utuwema usimamie haki!

    Yaani baada ya rafikiyo Lowasa kutiwa hatiani (Watz hawana shaka na hilo), wewe kama kiongozi wa juu wa nchi usimame na kutamka waziwazi KUMFUKUZA KAZI LOWASA! Nasema sheria zote,taratibu za kazi, umma na Mola wetu watakuwa wanakulinda maana rejea itakuwa ni hukumu. Maamuzi huwa yanarejewa na kurekebiswa ipaswavyo.

    Akiwa huko Magereza waweza kumtembelea tu kama Kikwete maana hiyo ni haki yako na yake.

    Nakwambia kuwa hata kama nani angepelekwa rumande kabla umma haujamwona Lowasa na kundi lake mbona mnatwanga maji kwenye kinu? Halafu hasira zetu ni kuona eti mwizi wetu anaendelea kupata heshima na kupigiwa saluti kisa eti kwa sababu ana title ya ustaafu sijui wa nini?

    Wabunge nanyi mjiandae kupokea walichokipata Republicans hapa USA maana hamuezi kukumbatia sheria kama hizo ambazo zina encourage kauli mbiu: iba kwa nguvu ukibainika step down haraka kabla ya kufukuzwa ili ubaki na maslahi!)

    Lazima mtofautishe kati ya Waziri Mkuu aliyestaafu kwa heshima kwa matatizo ya ugonjwa au kwa kipindi chake kuisha na yule aliyelazimika kungátuka kwa maslahi ya umma na kwa aibu!

    Michuzi huu ndio 'mtihani wa national' utakaomvusha Mkuu wetu kuingia darasa litarajiwalo usipompa huu mtihani basi mtafutiwa matokeo wote.

    ReplyDelete
  16. Kweli Tanzania sio tofauti sana na nchi zingine za Afrika. Lini haya maswala yataisha au kuacha kabisa. Kunakitu sielewi hapa, ngoja niulize kwa watanzania wenzangu, kwa nini mtu anapewa dhamana na pesa hiyo hiyo inayodaiwa. Mimi sijaona kitu kama hiki, najua kila mtu anahaki ya kupata dhamana lakini kama hawa viongozi wanadaiwa pesa in billions then wanaweka dhamana hiyo hiyo pesa. Kwanza hizi pesa hawajarudisha na hawaonyeshi hudhuni yoyote. Hivi kuna mtanzania ananyumba yenye dhamani ya billions. Inaonekana mimi naishi kwa shida kweli. Hii ni kweli? Naomba mtu apige picha hizi nyumba na location zake. What hek is this. Something don't smell right here. I am sure these people have good lawyers and they are trying to get away or it's too hot to stay in prison. I am living in jail everyday because of their poor government decisions. Kenya has been voted as one of the corrupt nation in this world, where is Tanzania ranked? It's shame and this is stink stinkish! I real want to see the end of this crup. Then, these government officials have their kids and families misuse money oversea, buying expensive cars and live high life. Now, I know where this money comes from. Lets work up men!

    ReplyDelete
  17. JAMANI MIMI NADHANI KUNA WAKATI FULANI MABOKSI YALINIPOTEZA MWELEKEO. HIVI ZOMBE YUKO WAPI? AU NA YEYE ALISHAPATA DHAMANA? AU KESI ILISHAISHA? NAOMBA MNIJIBU, MSINIKAUSHIE

    ReplyDelete
  18. Mimi kidogo nimekwazika, hivi ukishatoa hiyo hela ya dhamana, utarejeshewa kesi ikiisha, au ndio imeliwa. Na kama imeliwa, ...du,mipesa yote hiyo itaingia serikalini?
    M3

    ReplyDelete
  19. Misupu,

    Mfikishie JK kwamba kwenye suala la dhamana ya hawa "wafujaji wa mali za umma" kunahitajika uchunguzi wa kina. Kuna kila dalili kwamba hakimu Mwankenja alishinikizwa na mahakama kuu kubadilisha masharti ya na baadae kutoa dhamana kwa hawa mabwana. Pili uthamini wa hizo mali umezidishwa ili kukidhi masharti ya dhamana (valuers na Ardhi) na tatu hizo mali za hawa wanyonyaji zilipatikana lini? Zipo kwenye rejista ya ofisi za maadali toka wakati wa uongozi wao? Kama sio, basi kuna kosa jingine la udanganyifu na ni ushahidi mzuri tu wa kugundua kwamba walikula kodi zetu.

    PCCB, DPP, Ofisi ya maadili jamani sikia kilio cha watanzania na chunguza haya mambo. JK imani yetu itazidi kama hizi ndoto zitakuwa za kweli na sio idadi ya watu wanaofikishwa mahakamani tu. Kura zetu za 2010 zitategemea prosecutions sio arraigments. Hapa namkumbuka Sokoine.

    ReplyDelete
  20. Nilisema awali kuwa swala la dhamana inamyima haki mwananchi wa kawaida. Wale washtakiwa wa EPA wamelazimishwa kutoa mabilioni ya fedha kama dhamana lakini mawaziri wamepunguziwa dhamana ili watoke rumande haraka. Inaonekana wazi wazi jinzi sheria inavyofanya kazi yake kwa mawaziri na kwa wananchi wa kawaida. Hapa wanaosema kuwa Tanzania kuna haki wafunge midomo yao. Mpaka hapo maofisa wa serikali watakapofungwa kwa wizi ndio tutaamini sheria ni sawa kwa wote. Raisi JK awadanganye wasiojua kusoma na kuandika.

    ReplyDelete
  21. Nilashasema wazi na siku za mwanzoni. Nchi za wenzetu ukishashtakiwa tu katika makosa ya jinai kama haya na kazi basi.
    Na ukiwa mbunge au waziri basi na ubunge wako au na uwaziri wako pia ndo umekwisha. Na kama hutaki kujiuzulu, waheshimiwa wenzako huwa wanakaa kikao chao na kukutoa ndani ya chama na ubunge kwa manufaa ya nchi.
    sisi TZ mtu wa chini anashtakiwa kwa kosa la kuiba kuku anafukuzwa kazi serikalini. lakini wakubwa wanashtakiwa na kupelekwa mahakamani hadi rumande kwa makosa ya jinai na bado wanaitwa wabunge.
    Tuache kuwapa watu nafasi namna hii ni kuchochea ujinga wa kisaikologia kwamba wamechaguliwa na wanachi ili kutuibia.

    ReplyDelete
  22. Inasikitisha saana kuona siku zote Africa kila kitu kinaenda kinyume na nchi nyingi za magharibi.

    Eti mtu kakuibia shamba lako, unampeleka mahakamani. Mahakama inamwambia "brother jiwekee dhamana na shamba uliloiba" hakuna shida....kweli??? only in Africa

    Eti ni mwizi anapelekwa mahakamani, then kesi zote zinasimamishwa serikali inalazimika kufanya kazi mpaka weekend ili mwizi atoke jela. Sheria zilizowekwa na serikali zinasema dhamana yake itakuwa sh 100...baada ya muda inabadilisha mawazo na kusema "kwa kuwa ni wewe mwizi mwenzetu basi dhamana yako itakuwa sh 10?..kweli??? Only in Africa

    ReplyDelete
  23. Kuleni kuku mayai mboga samaki maziwa. Afya bora. Wakimbizi tunasota ughaibuni lakini maisha ni bora sana. Bongo Kunakera uwe nancho usiwe nacho wote mnachoka tu! Ahha kama nchi haitajengwa na wenye nchi itajengwa na nan?i Tutakimbia nchi na kuwazomea wenzetu mpaka lini.?
    It is about time.President resign.

    ReplyDelete
  24. listen people.nyumba 20m gali tatu 90m.watoto wanasoma ulaya school fee/year $30.000 per person wanalipiwa lent za nyumba watoto 3 wote wana magali na hawafanyi kazi sisi tuna fanya kazi. tunatengeneza pesa zaidi ya wazili na tuna teseka kulinunua gari la mtoto huyo wa wazili tanzania inabidi tuanze kuambiana ukweli make watu wanaumia mikoani na mitaani wanakula mlo mmoja chai mara moja kwa week watu wakati wao ndi wanaolipa kodi za nchi yetu pia raia mnabidi mjue hao wafanyakazi TRA PESA WANAZO CHEZEA KUNUNULIA MAGARI 6 HADI MABASI TAX BUBU PESA WANAZITOA WAPI WAKATI WEWE MFANYA BIASHARA UNAYE RIPA HIYO KODI YA MAPATO UNASHINDWA ATA GARI MOJA NYUMBA ZA MBEZI ASILIMIA 90 ZA KWAO SERIKALI YA kikwete inabidi hilishugulikie hiyo place thanks

    ReplyDelete
  25. HAWA MAWAZIRI WAMETOA WAPI (BILLIONI TATU ?)

    UN, UINGEREZA WAZIDI KULIA NA MAFISADI

    2008-12-03 11:54:05
    Na Richard Makore


    Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Oscar Taranco, ameshauri serikali kuongeza juhudi za kufikisha mahakamani watuhumiwa mbalimbali wa rushwa na ufisadi.

    Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Uingereza, Gareth Thomas, kwenye ofisi za UN nchini.

    Taranco alisema juhudi mbalimbali za kupambana na ufisadi zilizoonyeshwa na serikali zinapaswa kuendelezwa.

    Kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Taranco alisema chombo hicho kinapaswa kufanya kazi yake vizuri kwa inapata fedha nyingi kutoka UN.

    Taranco alisema Takukuru lazima ifanye uchunguzi na kubaini watuhumiwa mbalimbali ili wafikishwe mahakamani.

    Mwakilishi huyo wa UN nchini, alitoa kauli hiyo huku watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi wakiendelea kufikishwa mahakamani.

    Baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani hivi karibuni ni waliokuwa mawaziri waandamizi katika serikali zilizopita.

    Akiunga mkono kauli ya Taranco, Waziri huyo wa Uingereza alisema lazima kuwepo na udhibiti wa fedha za umma.

    Kwa upande mwingine, alisema nchi yake imeongeza fedha kwa mashirika mbalimbali yaliyopo chini ya UN.

    Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia kuhudumia wananchi ili kupunguza umaskini, gharama za utawala, urasimu na kuongeza ufanisi wa wafanyakazi. Msaada huo unaofikia Paundi za Uingereza milioni 2.4.

    ReplyDelete
  26. MICHUZI NA WAPAMBE WAKE...

    KAZI KWENU WOTE MULIOSHABIKIA ISSUE YA BABANGU AMETOKA SASA KAZI KUFANYIZA KWA KILA MTU, AKIYA NANI MTAKOMA. HATA WEWE MICHUZI UMEMTOA SANA BABA MAPICHA MABAYA YANAMWONESHA NA KUMDHALILISHA BABANGU SASA KAZI INAANZA HII BLOG ITAFUNGWA KABLA YA JANUARY 09.

    ReplyDelete
  27. mali yote hiyo wameitoa wapi???????? ni'WIZI MTUPU'

    ReplyDelete
  28. i think we have to realise that this case is just a fraction or reality. Most Tanzanias (poor people) are facing bribery in each and every process they make. If its getting a form for housing needs, if they are registering children to school, or even medical needs. Lets see the bigger picture that is affecting most of us and not this case that actually is not affecting so much of us.

    By the way how about the INDIANS who have been taking and taking, bribing and slaving us for centrurys!

    ReplyDelete
  29. Ndugu Binti Pesambili. Katika miaka ya sasa, Watanzania wameamka na hatutatishwa na serikali wala wakubwa wowote, wawe mawaziri au wanajeshi au baba yako mzazi.

    Kila siku, Watanzania tunafungua macho na kuona jinsi haki zetu za binadamu zinavyodhalilishwa na serikali yetu. Blog hii na wadau wake hatuogopi baba yako, wewe binafsi, serikali au mkubwa yoyote. Sijui kama unajua, lakini siku hizi kuna kitu kinaitwa Uhuru wa mawazo, japokuwa bado serikali na watu kama wewe wanajaribu sana kuufunga mlango huu wa uhuru wa mawazo na vitisho vya kitoto na vya kweli.

    Aluta Kontinua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...