Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. KP you made my day, jamaa anajitahidi kusahulisha deal lakini haoni msumeno uko maeneno mabaya, yeye aweke tu shingo asilete longolongo nyingi. Thanks KP you are a star.

    ReplyDelete
  2. acha kupotezea weka shingooooozzzzzz msumeno unakuhusu

    ReplyDelete
  3. Paschally Mayega




    RAIS wangu umesafiri kwenda Inyala, mkoani Mbeya kumzika mpendwa wetu, ndugu yetu Richard Nyaulawa. Umeshuhudia jeneza lililokuwa na mwili wake likiteremshwa chini ardhini.

    Kuthibitisha yametimia kuwa mwanadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi, mlichukua udongo katika mikono yenu na kumtupia Richard kule chini kaburini kwake alikolala.

    Apumzike kwa amani kwa maana imeandikwa, umetoka kwa udongo na utarudi kwa udongo.

    Huu ndiyo mwisho wa safari yake mwanadamu hapa duniani. Mwisho wa kila mmoja wetu. Ndivyo itavyokuwa kwangu mimi mtumishi wako nisiyestahili, na ndivyo itakavyokuwa kwako wewe rais wangu, maana imeandikwa ‘kila nafsi itaonja mauti.’

    Ni hali yetu ya ubinadamu kuwa kila tunaposhiriki mazishi ya wenzetu tunapata fursa ya kukumbuka na sisi siku yetu itakapofika.

    Mtu hushindwa kujizuia kuwakumbuka ndugu, jamaa na wapendwa wake waliotangulia kuiaga dunia.

    Katika hali kama hii ndiyo nakuuliza ndugu yangu rais, ungependa ukumbukwe kwa lipi?

    Wakati tukimwombea ndugu yetu apate mapumziko mema peponi, mema mengi yalisemwa juu yake. Kuanzia kanisani Masaki, misa yake ilihudhuriwa na watu wengi akiwemo mkuu wa nchi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

    Hii ilitosha kuthibitisha kwamba taifa limempoteza mmoja wa wana wake wema.

    Duniani tunapita tu, makazi yetu ya kudumu yako mbele ya safari, kwake aliye juu.

    Mwenzetu anakumbukwa kwa mema yake, ndugu rais ungependa wewe ukumbukwe kwa lipi?

    Siku yetu sisi itakapofika tutakumbukwa kwa lipi? Mimi nitakumbukwa. Watu wema watasema huyu alikuwa anaandika makala ya Rais wangu Kikwete.

    Rais wangu zamani ilikuwa ukimwambia mtu aandike wosia ilionekana ni uchuro.

    Unamtaka uchusa. Jirani zetu walikwenda mbali zaidi katika hili. Walitaka itungwe sheria kuwa mtu yeyote atayefikiria tu kuwa rais anaweza kufa awe tayari ni mhaini.

    Adhabu ya mhaini ni kunyongwa mpaka kufa. Dunia yetu ni mviringo inaendelea kuzunguka.

    Leo ni kitu cha kawaida kabisa mtu akishajenga nyumba yake nzuri anawaonyesha wanafamilia yake sehemu atakayotaka azikwe baada ya kufa. Hapo haumwi na wakati mwingine ni kijana tu.

    Kukuuliza unataka ukumbukwe kwa lipi sikuchurii. Ukomo wa maisha yako hapa duniani, ajuaye ni Mwenyezi Mungu peke yake.

    Siku hiyo ikifika mwili wa mwanadamu hutengana na roho yake.

    Roho imtokapo mtu huashiria matendo yake aliyoyatenda wakati wa uhai wake. Kwa mtu mnyang’anyi, mtenda dhuluma, mwovu au mtawala asiyehaki roho yake humtoka kwa taabu na mahangaiko makubwa. Mwenye haki hujinyosha na kuitikia wito wa Muumba wake kwa amani kabisa.

    Wakati mwingine watu hushindwa hata kutambua ni saa ngapi hasa roho ya marehemu iliutoka mwili wake. Waadilifu huomba siku zote Mwenyezi Mungu awajalie kifo chema.

    Roho yako itauma utakapokumbuka kuwa hukuwatendea haki waja wa Mwenyezi Mungu.

    Roho yako itauma kama waja wake walipodhulumiwa rasilimali walizopewa na Mwenyezi Mungu wewe ukiwa na uwezo na mamlaka hukuzuia.

    Roho yako itauma kama ulishirikiana na mafisadi. Roho yako itauma kama utawalinda mafisadi kwa namna yoyote ile.

    Mtu atahukumiwa kufuatana na uzito wa mamlaka aliyokuwa nayo, maana kila mamlaka yanatoka kwa Mungu.

    Utatapatapa na kuhangaika. Utakuwa peke yako. Familia yako italia sana lakini hawatakwenda na wewe.

    Utaacha majumba yako, magari ya kifahari, mashamba na pesa zako nyingi. Watoto wako pia utawaacha na utajiri wao.

    Walinzi wako wote watabaki duniani na silaha zao zote. Na kwa imani yako utarudi kwa muumba wako ukiwa mtupu kwa maana ulikuja kutoka kwake ukiwa mtupu.

    Kwa nini basi kuisumbukia dunia? Ndugu rais, mali itokanayo na ufisadi ya nini ikiwa hutaondika nayo?

    Rais wangu, urais katika nchi yetu una ukomo. Sijui utaondoka lini, leo, kesho au 2010, lakini kama katiba yetu haikubadilishwa 2015 urais wako lazima utakoma. Kwa mapenzi tu, natahadharisha, baada ya hapo ungependa ukumbukwe kwa lipi? Ukumbukwe kama Mwalimu Nyerere au au mzee Nelson Mandela?

    Ukumbukwe kama kina Chiluba kutwa mahakamani? Au ukumbukwe kama Thabo Mbeki? Kusoma alama za nyakati ni muhimu sana kwa kumbukumbu njema ya baadaye.

    Thabo Mbeki alisoma alama za nyakati. Achana na ushauri wa watu wa mshahara. Ushauri wao kwako ni kwa ajili ya matumbo yao, nao watakujazia wapiga ramli wengi na kukuvisha hirizi.

    Nakaa najiuliza, kwa nini Mwenyezi Mungu aliuweka Mlima Kilimanjaro Tanzania? Huu ni mwinuko wa dunia mrefu kabisa kushinda mwinuko wowote katika Bara la Afrika.

    Je, alitaka nchi yetu ikae juu kabisa kuliko nchi zote za Afrika? Je, ni kwa kutambua hilo ndiyo maana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliamua kuwasha Mwenge na kuuweka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro?

    Umulike hata nje ya mipaka ya nchi yetu ili ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini! Ulete upendo pale ambapo pana chuki! Ulete heshima pale ambapo pamejaa dharau!

    Mama yangu Tanzania, hayo ndiyo maziwa yako uliyotakiwa kuwanyonyesha wana wa mataifa baada ya kuwa wanao wamekwisha shiba.

    Rais wangu, ulipokuja uliwajaza wananchi matumaini makubwa sana. Matumaini ambayo sasa yamefifia kabisa. Ukawaahidi maisha bora kwa kila Mtanzania.

    Ahadi hii kama hukuitimiza, nayo ikakugeuka, ina ncha kali kuliko makali ya upanga. Kama watawala wetu watakuwa ndio haohao Deep Green, ndio haohao Kagoda Agriculture Ltd, ndio haohao Tangold, Meremeta na wenzao, Tanzania yenye neema itawezekana vipi?

    Mlichokifanya sasa ni kuuondoa upendo uliokuwapo na kupanda chuki kali kati ya wananchi na Deep Green, Kagoda Agriculture Ltd Meremeta, Tangold na hasa na watawala ambao wanaonekana kuwa sehemu yao au kuwabeba na kuwahifadhi. Siku ya siku wote ‘manzi ga nyanza’, kasema Mwalimu Nyerere. Wote watapata msukosuko. Watawala ambao hawana aibu. Wanaosema uongo hadharani.

    Wengine wanawadhalilisha wananchi kwa kuwafanya hawana akili, eti wezi wakipelekwa mahakamani nchi itayumba. Hawatetei wezi peke yao, wanajitetea na wao wenyewe.

    Sasa hivi nchi inayumba kwa wizi, rushwa na uongo wao, yeye kwake ni sawa tu.

    Namhurumia mwenye mamlaka ya kumfukuza kazi ambaye hadi leo hajatimiza wajibu wake wa kumfukuza. Siku ya siku wote manzi ga nyanza.

    Ni upofu kufikiria kuwa kuna mtu kati ya hawa anaweza kupata heshima. Watajiita waheshimiwa mpaka midomo ipinde lakini heshima hawataipata kamwe.

    Dharau, tunaitengeneza wenyewe halafu tunawalaumu wengine wanapotumia haki yao ya kutudharau.

    Ndugu rais ungependa ukumbukwe kwa lipi? Mimi nitakumbukwa. watu wema watasema huyu alikuwa anaandika makala za Rais wangu.

    Kuwatamkia watu wazima, wasomi katika chuo kikuu kinachoheshimika kama St. Augustine kule Mwanza kuwa sera ya uchangiaji katika elimu haitaondolewa, kunataka umakini mkubwa sana zaidi ya kusoma hotuba iliyoandikwa kwa sababu sera hii itaondolewa tu.

    Suala hapa ni muda basi. Hata Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyayi Lowassa, aliwahi kutamka bungeni kuwa tunaelekea kwenye elimu ya bure.

    Ingekuwa ni heri kwako ikaondolewa wakati wa utawala wako. Ndugu yangu rais, ungependa ukumbukwe kwa lipi?

    Sijui ulienda na ndege ipi kule Mwanza kati ya ndege nyingi ulizo nazo. Lakini kama ulienda na lile dude lenye gharama kubwa, haikuwa sahihi hata kidogo kusema serikali haina uwezo wa kuwasomesha watoto wa taifa hili hata kwa mkopo tu wa asilimia mia moja.

    Safari moja kwa dege hili inatosha kusomesha wanafunzi wangapi? Elewa kuwa wale ni wasomi, tofauti na wananchi wa kule Nkanga. Wanaelewa kuwa pamoja na magari aghali aina ya Benz yanayotumika Ikulu sasa umeongeza magari ya bei mbaya zaidi ya BMW bila ulazima wowote.

    Gari moja ni kati ya shilingi 200-500 milioni. Haya yameagizwa kwa oda maalumu na kwa bei maalumu.

    Eti usalama. Nyerere kionambali alisema, “Mkiona tunjizidishia ulinzi mjue tunawaibia.” Mtu anasema Serikali haina uwezo hata wa kukopesha tu asilimia mia moja.

    Kwa ugumu wa maisha waliyonayo wananchi nalazimika kumheshimu sana ndugu Leonidas Gama, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye aliwaambia waziwazi watendaji waliopigwa mawe na kuporwa na wananchi wenye hasira kuwa wasishangae wanapoona wananchi wanajichulia sheria mkononi na kuwapiga mawe.

    Tuna wazazi wengi ambao wameendekeza anasa kuliko kusomesha watoto wao. Ndege na haya magari aghali ya BMW ni mfano mdogo tu kati ya mingi iliyofuja na inayoendelea kufuja utajiri mkubwa wa nchi hii ambao ungeweza siyo tu kuwasomesha watoto wote bila malipo ya ziada bali hata kutoa huduma zote za jamii kama afya na maji bila malipo ya ziada.

    Ni makosa na upofu kusema wananchi wanataka huduma hizi zitolewe bure, wanataka huduma hizi kwa gharama ya kodi zao. Si bure.

    Kuna busara gani kukusanya kodi karibu ya bilioni nne kwa mwezi kutoka kwa wananchi halafu ukamlipia Mhindi mishahara ya wafanyakazi wake kule Shirika la Reli?

    Kuna busara gani kuacha fedha zilizotokana na kodi za wananchi zizagae BoT mpaka mafisadi wakadhani hazina mwenyewe wakawa wanajichotea?

    Kuna busara gani kuachia vijisenti vya mabilioni vilivyokosa maelezo ya upatikanaji wake vikae nje ya nchi badala ya kusomeshea watoto wetu?

    Kwa mshahara wa mfanyakazi gani wa serikali, mtu aweze kulimbikiza mabilioni au kujidhamini kwa mamilioni ya shilingi mahakamani? Nchi maskini, maskini gani huyu anaibiwa mabilioni kila kukicha?

    Duniani kote mtawala aliyezungukwa na matajiri fisadi naye hunuka ufisadi.

    Leo hii mlofa mmoja kuhubiri kuwa nchi yetu ni maskini ni kudhalilisha upeo wake wa kufikiri.

    Unatumia maneno yaleyale aliyokuwa anatumia Mwalimu Nyerere wakati nchi ilikuwa kweli maskini. Maisha ya Nyerere na viongozi wenzake yalifanana na umaskini wa nchi yetu na watu wake.

    Ukwasi wenu watawala wa leo ni kufuru mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yangu Rais ungependa ukumbukwe kwa lipi? Mimi nitakumbukwa.

    Watu wema watasema huyu alikuwa anaandika makala za Rais wangu Kikwete.

    Rais wangu wakati unaelezea serikali kukosa fedha za kusomeshea wanafunzi, wanafunzi hao hao walikuona ‘live’ ukipokea sh 400 milioni kutoka kwa mtu ambaye waliambiwa huko nyuma kuwa alihusika kuibia serikali mabilioni ya shilingi kutokana na udanganyifu katika mauzo ya rada.

    Sakata hili halijaisha. Wewe ni rais wa Watanzania wote. Kitendo hiki kimewasononesha kwa kiasi kikubwa Watanzania wote wenye kuchukia ufisadi na mafisadi, hasa walalahoi wanaoendelea kuteseka kwa sababu ya hawa mafisadi.

    Ni picha gani umejijengea kwa watu wako? Kwa nini kazi hiyo usingemwachia katibu mkuu, maana yeye amefaulu kukijengea chama taswira kuwa ndiyo hifadhi ya mafisadi.

    Kufikiria kuwa fedha ya mafisadi itaweza tena kuwanunua wananchi huko mbele ni kuota ndoto za mchana. Fedha za mafisadi zitamwagwa nyingi na wananchi watazipokea kwa furaha. Wamekwisha kutambua kuwa ni zao wanazoibiwa na mafisadi.

    Wanawarudishia japo kiduchu. Kura yao mafisadi wasahau. Wanajua kuwa ugumu wa maisha na umaskini mkubwa unaowakabili umetokana na ufisadi na mafisadi ambao leo wamekumbatiwa na chama chao.

    Ni masikitiko makubwa kwa Rais wangu kutumbukizwa katika picha mbaya kama hii. Unataka kuacha kumbukumbu gani?

    Rais aliyekumbatia mafisadi? Hapana!

    Ndugu yangu rais ungependa ukumbukwe kwa lipi? Mimi nitakumbukwa. Watu wema watasema huyu alikuwa anaandika makala za Rais wangu Kikwete.

    ReplyDelete
  4. UN, Uingereza wazidi `kulia` na mafisadi

    2008-12-03 11:54:05
    Na Richard Makore


    Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Oscar Taranco, ameshauri serikali kuongeza juhudi za kufikisha mahakamani watuhumiwa mbalimbali wa rushwa na ufisadi.

    Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Uingereza, Gareth Thomas, kwenye ofisi za UN nchini.

    Taranco alisema juhudi mbalimbali za kupambana na ufisadi zilizoonyeshwa na serikali zinapaswa kuendelezwa.

    Kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Taranco alisema chombo hicho kinapaswa kufanya kazi yake vizuri kwa inapata fedha nyingi kutoka UN.

    Taranco alisema Takukuru lazima ifanye uchunguzi na kubaini watuhumiwa mbalimbali ili wafikishwe mahakamani.

    Mwakilishi huyo wa UN nchini, alitoa kauli hiyo huku watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi wakiendelea kufikishwa mahakamani.

    Baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani hivi karibuni ni waliokuwa mawaziri waandamizi katika serikali zilizopita.

    Akiunga mkono kauli ya Taranco, Waziri huyo wa Uingereza alisema lazima kuwepo na udhibiti wa fedha za umma.

    Kwa upande mwingine, alisema nchi yake imeongeza fedha kwa mashirika mbalimbali yaliyopo chini ya UN.

    Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia kuhudumia wananchi ili kupunguza umaskini, gharama za utawala, urasimu na kuongeza ufanisi wa wafanyakazi. Msaada huo unaofikia Paundi za Uingereza milioni 2.4.

    ReplyDelete
  5. Hahahaaaaa..kwa kweli KP unatisha.
    Nimecheka sana...hahahaaaaa
    Mambo ya EPA ni changa la macho tu..hakatwi mtu shingo wala nini...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...