Jamani mnasemaje kuhusu watoto kunyonya vidole? Mtoto aachwe aje kuacha tabia hiyo akikua au awe anakatazwa? na nipeni ushauri, akatazwe kwa njia gani, maana mi mwanangu ananipa tabu tabia hiyo.
- Jiang Alipo
-------------------------------------------------------------
Wadau, Mambozzzzzz
Naomba nirushe blog yangu mpya ya
kama jina linavyojionyesha ni blog ya kujipendelea watoto tu!
so wadau nitumieni picha za sherehe mbalimbali za watoto wenu kama b'day, kipaimara, maulidi, ubatizo, hata mtoto akizaliwa namrusha saa hiyohiyo.
tuma picha hizo kwenye:
pia soma upate alimu kuhusu mambo mbalimbali kuhusu watoto na malezihalafu shiriki mijadala na polls mbalimbali: mdahalo wa sasa ni kuhusu watoto kunyonya vidole, na poll ni lini mtoto wa kiume atahiriwe?
karibu u-enjoy!
Love,
Jiang.
----------------------------------
Jiang!
Hongera kwa kujitosa kwenye libeneke la globu. Hakika nimefurahishwa sana kwa uamuzi wako huo wa kuja kivyakovyako, tena kwa mada nyeti ya mama na mwana. Nina imani kabisa kwamba utapata wadau wengi tu, kwani mada na midahalo unayoendesha yanagusa jamii yote.
Karibu sana kilingeni. Natumai hatua hii ya kuigwa italeta changamoto kwa wadau wengine kuanzisha libeneke itayolenga mambo mengine ya maana kama hayo, kuliko wote kuelekeza nguvu kwa habari na matukio.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Huyo dogo amerithi kutoka kwa baba yake SIXTUS hakuna jinsi akikua ataacha!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kule Iringa wanasema mtoto akinyonya kidole akikua anakuwa hawezekani kwa ulanzi na kihambule kwa hiyo jitahidi kumzuia. Finally, with all due respect, your name sounds Chinese - or is it only me?

    ReplyDelete
  3. heeeeee JIANG ALIPO????
    siamini weee binti
    hongera sana kwa kijamaa icho vere cute na baba yake ni SIXTUS???yule tumjuaye au???
    hahahahahaaaaaa
    ningejitambulisha umu bt waosha vinywa na wabeba box watanchanganya
    bt fresh saaaaana kwa libeneke hili bab'kubwa la mama na mwana.
    uo ni kama kilema fulani yan vinaishaga venyewe tu,,usimuwekee pilipili

    ReplyDelete
  4. hamna umuhimu sana katika swala la mtoto kutahiriwa kwa nionavyo mm japo nimetahiriwa pia lkn sioni kama ni muhimu kumtahiri mtoto..najua wadau wapo watakaonimeza lkn watupe sababu za kufanya hadi iwe ni lazima kutahiriwa na athari ambazo mtu asipotahiriwa atazipata.kuna watu ktk dunia hii ambao tunawaona kama ni wenye uelewa au hadhi au ujuaji wa mambo mengi makubwa duniani lkn hawajatahiriwa na watu hawajalijua hilo.so kutahiriwa sio big deal

    ReplyDelete
  5. My son started sucking one of his fingers at 3 months.... a medical Pediatrician told us not to interfere with that as it is a mean of consoling himself

    ajabu aliacha chini ya mwezi mmoja,ila ushauri wa dr ni kuwa mwache tu most of them wanataka kujibembeleza na hupoteza quality times wakifikiria ya dunia... akikua kidogo akiwa na akili unaweza kumwelewesha sababu za kuacha ni zipi na ataacha... but at young age (below 1) let him enjoy his time

    ReplyDelete
  6. Ushuri wangu ni kwamba shusha kijast bikozi chako toa chuchu mpe mtoto. Kila akitaka kunyonya kidole fanya hivyo ataona afadhali aache. Ila halahala ziwa likinyonywa sana wana sema likuwa ndala haraka hasa kama mama ni kimbao mbao.

    ReplyDelete
  7. PACIFIER NDIO KIBOKO YAKE

    ReplyDelete
  8. Pole sana mama. Mtoto huyo amefanana na baba yake. Baba yake alikuwa na tabia ya kunyonya sana vidole lakini alipokuwa mkubwa akaacha. Hivyo na huyo atakuja kuacha tu hiyo tabia mbaya.

    ReplyDelete
  9. kwako anony,, hapo juu swala la kutahiriwa kwa wanaume ni mila na desturi za barani Afrika, na sababu mojawapo ni usafi na kuepukana na maambukizo ya magonjwa ya mbalimabali,,,
    Hebu kumbuka siku ya kwanza ulipomwona mwanaume mtu mzima akiwa hajatahiriwa, ulishangaa na uliona kinyaa takaka usitake ndo ukweli wenyewe,

    Kuna mataifa mbalimbali kama scadinavia hawatairiwi tena ni kesi ukimtahiri mtoto wa kiume na dr akajua..

    mila zetu zina baki pale pale, mwanao mwache na govi lake kama baba yake, huna ujanja.

    ReplyDelete
  10. Kuhusu kidole nadhani ni njia ya mtoto kujiliwaza, na kwa kuwa bado ni mdogo usihofu ila atakapoendelea after one unaweza tatufa njia sahihi without abusing him za kumwachisha,,,sio kutia pilipili kama walivyokuwa wanafanya zamani. Kuhusu "PACIFIER or DUMMY" sidhani kama ni good idea, wataalam wanasema kuwa zina disadvantage nyingi kwa development za watoto kuanzia speech, nk!

    Kutahiriwa ni mila na desturi ya tanzania sio africa maana nchi nyingi sana hazitairi..e.g. south africa, zimbwabwe nk. Na hapo bongo kuna makabila yalikuwa hayatahiri watoto..e.g. wahaya nk. So ni maamuzi ya kifamilia. However as a medical dr myself sioni any medical reason ya kufanya hivyo it is more of cosmetic... lakini kwa kuwa nimekuta wameshanikata sina ujanja, ila sitawatahiri wanangu...

    ReplyDelete
  11. 1. Jina la mwanao linapronounce waje?

    2. US kuna dawa unanunua ukiweka kwenye kidole mara mbili tatu anaacha. Lakini mimi naona ni bora mtoto anayenyonya kidole anakua mpole na ni wachache wanapitisha miaka 4.

    3. Pacifier sidhani kama ni nzuri kabisa. Mimi naona ni heri mtoto anyonye kidole kuliko kuwa na pacifier.

    ReplyDelete
  12. it normal for some kids to suck vidole but you can help him/her stop by giving her something else kama pacifier then akishaanza kuacha vidole anza kumwachisha pacifer as well....akiendelea kunyonya vidole ataanza pia kuaribu meno yake yatakavyotoka...yakakuwa yako mbele mwenyewe utakoma..... again you can keep explaining to her and distructing her....they are little but they do undestand things .....good luck

    ReplyDelete
  13. SWALI...JE KUNA ULAZIMA WA KUTAHIRI?

    ReplyDelete
  14. Huyo anon wa kusuggest pacifier anamshauri mwenzake vibaya. Pacifier zikitumika sana huleta ugonjwa wa masikio kujaa usaha na matatizo ya koo. Inaweza kutumiaka mda mfupi lakini siyo suluhisho. ukizidisha tu matumizi mtoto anakuwa na homa zisizoisha na ugonjwa wa masikio. Nimeshuhudia kwa dada yangu ambaye alimzoesha mwanae pacifier akawa anaumwa umwa na alipompeleka mwanae kwa mtaalamu wa watoto huko Oslo kashauriwa hivyo kuhusu pacifier. ushauri wa bure na lady s

    ReplyDelete
  15. Asanteni wote kwa comment zenu,
    Baba yake kakataa, kasema yeye hakuwa na tabia ya kunyonya vidole, sasa sijui huyu kaitoa wapi. mi sikumbuki kama nilikua nanyonya au la...
    comment za kutahiri na mijadala mingine, naomba mkazipost kwa mama na mwana, ili wadau wa kule pia wapate maoni yenu.
    Yap, mimi ni JIANG ALIPO, na ndio, ni Sixtus huyohuyo unayemjua.
    Ndio jina langu ni la KICHINA, ukitaka story ndefu kuhusu hilo itabidi tutafutane one- on - one.
    Jina la mwanangu linatamkwa 'sikaila' yani kama unasema skyler, so sio gumu kulitamka, kuandika tu ndio gumu.
    narudia tena asanteni wote for your support.

    Jiang.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...