HAYATI HERRY MAKANGE

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA NA MSHTUKO HABARI KWAMBA HERRY MAKANGE, MPIGANAJI WA CHANNEL TEN NA DTV, HATUNAYE TENA BAADA YA KUFARIKI KATIKA AJALI HAPA DAR JANA MCHANA.

HABARI ZILIZOPATIKANA JANA USIKU NA KUTHIBITISHWA ASUBUHI HII NI KWAMBA HERRY ALIKUTWA NA MAUTI AKIELEKEA MJINI KUTOKEA KAWO KIBAHA AKIWA ANAENDESHA PIKIPIKI. ALIKUWA NDIO KWANZA AMEREJEA TOKA TABORA KIKAZI NA ALIKUWA AKIENDA KURIPOTI KAZINI.
IKUMBUKWE KWAMBA HERRY ALIKUWA MMOJA WA WAPIGANAJI WALIONUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI HUKO KIBITI ILIYOMHUSISHA PIA MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI AMBAYE HADI LEO YUKO SAUZI AKITIBIWA SHINGO NA MGONGO. KURASA YA AJALI HIYO YA KIBITI BOFYA HAPA
TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA KILA KINACHOJIRI BAADAYE IKIWA NI OAMOJA NA MIPANGO YA MAZISHI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MPIGANAJI MWENZETU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, bwana alitoa na bwana ametwaa. Amen.

    ReplyDelete
  2. Marehemu alikuwa mchapakazi hodari,mnyenyekevu,poleni wafiwa.Innalilah wainah illaih rajuun.

    ReplyDelete
  3. Dah...Rest In Peace My Friend, Tutakufuata.

    BooSt3D.

    ReplyDelete
  4. Maskini huyu kaka enzi hizo naanza upaparazi nilikuwa namuonaga mdogo wake Athumani Hamis nilikuwa naona wanafanana....ajali nayo wakapata pamoja ye akapona...leo hii ...Hatunae...Rest In Peace.

    ReplyDelete
  5. MMH..si nimesoma usiku huu huu habari nyninge nikaona ili jina bado nabrowse habari tofauti narudi nakutana na haya tena. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peoponi bwana alitoa bwana alitwaa. Jina la bwana litukuzwe...

    ReplyDelete
  6. KWANI HUYU KAKA SI ALIFARIKI KWENYE ILE AJALI AMBAYO KAKA MMOJA HAMIS YEYE ALIPONA? SASA HII NI IPI TENA AMA MICHUZI UMETURUDISHA NYUMA KUTUKUMBUSHA KAMA KIFO KINA KUJA? UNANI CONFUSE WEWE MICHUZI MIMI HATA HUWA SIELEWI MESSAGE ZAKO ZINA MAFUMBO MENGI WEWE.SASA NASHINDWA AMEKUFA LINI TENA KWENYE GARI AKIWA NA HAMISI AMA KWENYE PIKIPIKI NA NI LINI TENA HIYO MAANA MIMI NILIJUA NI SIKU NNYINGI HII STORY IMETOKEA SASA TENA IMERUDI VIPI?

    ReplyDelete
  7. Jamani! Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amina. FK

    ReplyDelete
  8. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi

    ReplyDelete
  9. Ohhh jamani poleni sana wafiwa, REST IN PEACE BRO!yaani alivyokuwa handsome mwenyewe anyway kila nasfi itaonja mauti hiyo imeandikwa!

    ReplyDelete
  10. Kazi ya mungu haina makosa. Pole nyingi kwa familia na tunamuomba mwenyezi mungu aifariji familia na kuwapa uvumilivu katika hiki kipindi kigumu.

    Bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

    Rest in Peace

    ReplyDelete
  11. Life is one big road with alots of signs,jamaa aliskip kifo cha ajari...anyway inaonesha ndivyo alivyoandikiwa, mwenyezi amrehemu.
    R.I.P Bro Henrico

    ReplyDelete
  12. MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI. JAMAN KWELI UKIITWA UMEITWA TU ALIMUITA NA SASA YUKO NAYE TUMUUOMBEE KWA MUNGU.

    ReplyDelete
  13. Kaka Michu, huyu ndugu yetu si ndiye alioa hivi karibuni? nadhani na fungate amerudi hivi majuzi tuu. aisee kweli mipango ya Mungu, katika suala la kifo katufumba.Pole sana mke wa marehemu, poleni ndugu na jamaa wa marehemu, Mungu awajalie moyo wa matumaini katika kipindi hiki kigumu. May Almighty God rest his soul in peace. AMEN

    ReplyDelete
  14. Poleni wafiwa, kazi ya mungu haina makosa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
    Tangulia nasi twaja kwani hakuna ataeishi milele hapa duniani. Kifo ni kwa wote

    ReplyDelete
  15. Hapo wabongo tunasema kuna namna sio bure!

    ReplyDelete
  16. wewe cynthia masasi embu tuliza munkari na kusoma habari,maswali mengi matupu hayasaidii umma..huu ni wakati wa majonzi. i cannot believe this,he was from his honeymoon after he got married..REST IN PEACE!!

    halafu bwana michuzi naomba nikupe somo kidogo..huyu sio hayati,ni marehemu. hayati ni mtu aliekufa kuanzia miezi 12 iliyopita..any how than that its marehemu

    ReplyDelete
  17. poleni sana familia yote ya marehemu.Bro alikuwa mtu mtaratibu sana na mchapa kazi sana.nimesikitishwa na habari za msiba wake.inanillahi waina illah rajiyunna.

    ReplyDelete
  18. Ilibidi nifanye Take Two ndo niamini. Si alipona katika ile ajali nyingine? Jamani. Kweli kama umeandikiwa umeandikiwa.

    Mola ailaze roho yake mahala pema. Peponi. Amin.

    ReplyDelete
  19. Naomba kuungana na wanajumuia wengine kutoa pole kwa wafiwa. Vifo vya ajali barabarani vinasikitisha sana kwasababu ni vya ghafla na mtu alikuwa mzima wa afya. Mungu aipe familia yake nguvu katika kipindi hiki kigumu.
    Naomba pia kutumia nafasi hii kumtumia ndugu yangu Pascal Mayalla hongera kwa kuacha kuendesha pikipiki. Hiki ni chombo cha moto kosa kidogo tu unajikuta unacheka na lami.

    ReplyDelete
  20. May he Rest In Peace ,
    Kazi ya Mungu haina Makosa

    ReplyDelete
  21. kweli si rahisi kuzoea kifo, kifo kimeumbwa, nakukumbuka sana Heri, tumefanya kazi wote kwa muda pale DTV ingawa idara tofauti. Tulikuwa tunagombania wote usafiri wa kwenda kazini pale vingunguti, au wakati mwengine tukitegea gari ya DTV likitoka kumchukua boss na sisi tunapata lift, leo hii Heri haupo tena, inauma, inasikitisha sana, M/Mungu anajua zaidi,Hakika sisi ni wa M/Mungu na kwake tutarejea. Poleni wote, familia na DTV kwa ujuma, Tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  22. WEWE MASASI CYNTHIA KWANZA WEWE MWENYEWE NI COMFUSE.COM,hahaha!!!!!! soma uelewe tena Mkuu wa wilaya kaandika kwa lugha yetu ya taifa kila mtu anasoma na kuielewa sasa hapo wewe kipi hukielewi ingekuwa kaandika kiinglish tungesema wewe not.....ble kuwa Marekani sio kila mtu anakijua bwana.

    Poleni sana wafiwa na mungu ailaze pema roho ya marehemu ampumzishe kwa amani.

    ReplyDelete
  23. UYU KAKA ALIMUA JANE MPONZI MDOGO WAKE GRACE MPONZI

    ReplyDelete
  24. Du! Jane Mponzi ni mapema mno kuwa mjane...Henrico amefariki baada ya mwezi mmoja wa ndoa yake...damn R.I.P Henry

    ReplyDelete
  25. Kaka Kheri ni vigumu kupata tabasamu lako.Kwakweli si mimi tu nahisi ni wengi watalikosa.

    Mpendwa wifi yetu MUNGU hata siku moja hachukui kitu kibaya. Mshukuru tu kwakua anamipango na kila aliye wake. Sema asante naye atakufariji.Pole sana mama.

    ReplyDelete
  26. wewe anon hapo juu, marehem alikua amemuoa jane mponzi, dada yake grace mponzi, sio mdogo wa grace mponzi.. and yes wamefunga ndoa a month ago.. na wewe cynthia, marehem hakufa ktk ajali unayoisema, soma kiswahili uelewe.. michuzi hawezi kukurupuka tu kutuma habari ya kifo mara mbili..
    dada jane, pole sana kwa kumpoteza mwenzi wako.. mungu akae nawe na akutie nguvu na faraja ktk kipindi hiki kigumu.. we love you so much sister..
    R.I.P SHEM

    ReplyDelete
  27. Anon Dec 18,11:16, chunga sana silabi zako asipochunga utamaanisha tofauti na ulivyotaka kuelezea, HUYU KAKA ALIMUUA JANE MPONZI MDOGO WAKE GRACE MPONZI. hii ndo maana ya sentensi uliyoandika hapa au ALIMUOA?

    ReplyDelete
  28. its a big loss anyway may God rest him in peace.. Loh kweli kila kiumbe kitaonja mauti.

    ReplyDelete
  29. Huyu kaka alikua charming sana, nakumbuka likua ananitania sana wakati mjamzito, na hakukosa kuniachia siti nipimzishe tumbo langu enzi hizo. Ntakukumbuka daima.
    Mungu ampe nguvu na ujasiri Jane Mponzi akabiliane na hali hii aweze kuyarudia maisha salama as yote ni mipango ya Mungu.
    Mungu alilaze roho ya marehemu Hery Makange mahali pema peponi.
    Amen.

    ReplyDelete
  30. sasa we michu umebana nini kwani huyo annoy hukuona alicho andika kama kamuua jane mpozi? tulitaka tusikiee na aombe msamaha kwa typing error yake si kubanacomment aha hizo

    ReplyDelete
  31. huyu marehemu nilisoma nae Kibaha (Tumbi Primary School) its so sad alikuwa mpole na mpenda maendeleo
    RIP Henry wote tutakufuata

    Funzadume

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...