
JK akiongea na Emir wa f Qatar sheikh Hamad bin Khalifa al Thani hoteli ya Four Seasons jijini Doha leo. JK yuko huko kuhudhuria mkutano wa fedha na maendeleo.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Tafuteni mitaji kwetu – Mtawala wa Qatar
Na Mwandishi Maalum,
Na Mwandishi Maalum,
Doha, Qatar
Mtawala wa Qatar, The Emir His Highness Sheikh Hamad bin Khalifa al Thani amesema kuwa wakati umefika kwa nchi za Afrika kubadilisha mawazo kwa kutafuta mitaji ya uwekezaji katika nchi tajiri za Kiarabu, badala ya kuendelea na jadi ya kusaka raslimali za maendeleo katika nchi za Magharibi.
Mtawala wa Qatar, The Emir His Highness Sheikh Hamad bin Khalifa al Thani amesema kuwa wakati umefika kwa nchi za Afrika kubadilisha mawazo kwa kutafuta mitaji ya uwekezaji katika nchi tajiri za Kiarabu, badala ya kuendelea na jadi ya kusaka raslimali za maendeleo katika nchi za Magharibi.
Mtawala huyo wa Qatar pia ametaka hatua zaidi kuchukuliwa ili kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya nchi yake na Tanzania, akisisitiza kuwa hata muziki, jadi na utamaduni wa nchi hizo mbili vinafanana.
Mtawala huyo ameeleza hayo wakati alipomkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye yuko Qatar kuhudhuria mkutano wa kimataifa unaojadili jinsi ya kusaka fedha za kugharimia maendeleo na jinsi ya kukabiliana na matatizo ya sasa katika mfumo wa fedha duniani.
“Mnaweza nyie katika Afrika mkaona ni jambo la lazima kuanza kusaka mitaji ya uwekezaji katika nchi zenu kutoka kwenye nchi za Kiarabu sasa. Sisi wenyewe tunatafuta nafasi ya kuwekeza katika Afrika, na nyie katika Afrika mnahitaji kuanza kutuangalia sisi kama chimbuko la mitaji,” amesema mtawala huyo, Sheikh al Thani.
Mtawala huyo amemwambia Rais Kikwete katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya Four Seasons mjini Doha: “Kwa upande wetu tumedhamiria kuwekeza katika Afrika. Mataifa makubwa sasa yako katika matatizo makubwa. Kwa sasa mataifa hayo yanataka kukubatia na kubakia na fedha zao.”
Ameongeza Mtawala huyo: “Tunataka kufufua uhusiano wetu wa kihistoria na kijadi. Tunazo sababu za kuhistoria kufanya hivyo, hasa hasa kwa Tanzania ambayo watu wake wengi wamehamia hapa, na ambayo hata muziki na utamaduni wake vinafanana sana na vile vya Qatar.”
Naye Rais Kikwete mbali na kusifia uhusiano wa miaka mingi kati ya Tanzania na nchi za Kiarabu amempongeza Mtawala huyo kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo ambao muhimu na ambao umefanyika wakati mwafaka.
Rais kikwete pia amempongeza Mtawala huyo kwa jinsi alivyosimamia maendeleo ya nchi yake ambayo imebadilika mno katika kipindi kifupi tokea Mtawala wa sasa kushika madaraka mwaka 1995.
“Tumefanyia mkutano wetu katika huduma bora na za kisasa kabisa. Mahoteli yetu ni mazuri mno.”
Rais pia amesema kuwa Tanzania inahitaji mitaji mikubwa ya uwekezaji kutoka Qatar na akamwalika Mtawala huyo kutembelea Tanzania.
Mtawala huyo pamoja na kukubali kuwa atatemblea Tanzania, ameomba kwanza mawaziri wa nchi hizo mbili kukutana mara moja, ili kukubaliana ni maeneo gani hasa nchi hizo zinaweza kushirikiana, ili “nikija mimi iwe ni kutiliana saini tu mikataba iliyokamilika.”
Mara baada ya mkutano huo na Mtawala huyo, Rais Kikwete amewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi, Mustafa Mkulllo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Qatar, Dk. Khalid Al Hatia.
Baadaye Sheikh Al Thani amekula chakula cha mchana na Rais Kikwete ambako wameendeleza majadiliano yao kuhusu jinsi ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Qatar.
Rais Kikwete pia ameendelea na mikutano mbali mbali na wakuu wa nchi, serikali na mashirika ya kimataifa ambayo yako Doha kwa ajili ya mkutano huo.
Pia ameshiriki katika mkutano wa kujadili mpango maalum wa jinsi gani ya kuzipa nchi vivutio katika kufanikisha sekta ya elimu. Mpango huo unajulikana kama Cash-for-Delivery, na Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza duniani kujaribiwa kutekelezwa kwa mpango huo.
Hee! Umeshatoroka tena nchini kwako upooo!!!! Kwa kweli we ni waziri wa mambo ya nje! Majukumu ya uraisi kila siku safari, kazi zitaenda kweli?
ReplyDeleteNi kweli asemayo kiongozi mkuu wa Qatar kuwa tuanze kuchangamkia mikopo toka Uarabuni maana labda itakuwa nafuu kwa kutotoza riba (interest) kama vyombo vya fedha vya ulaya na marekani.
ReplyDeletePia tufanye juhudi za makusudi kuhakikisha watanzania wengi wanapata ajira mashariki ya kati kwa kujifunza lugha ya kiarabu ktk shule za msingi na sekondari. Tusisahau kuwa lugha ya kiswahili ina maneno mengi ya kiarabu hivyo haitakuwa taabu kama kujifunza kifaransa. Hivyo tusisahau uhusiano (special relatonship) kati ya Arabuni na afrika mashariki.
Watanzania wakiwa na uwezo wa kutumia kiingereza na kiarabu tutapata ajira nyingi Uarabuni.