JK akitoa heshima kwa mashujaa ya Msumbiji muda mfupi baada ya kuweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa hao vilivyopo jijini Maputo Msumbiji.Rais kikwete yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
JK akiweka shada la maua leo mchana katika viwanja vya kumbukumbu ya Mashujaa waliomwaga damu wakati wa vita vya ukombozi wa Msumbiji.
Askari wa kike wa jeshi la Msumbiji wakimsindikiza JK kwenda kuweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya Mashujaa mjini Maputo.

JK na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakitakiana heri kwa kugonganisha glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa katika ikulu ya Maputo ijulikanayo kama Ponta Vermelha jana usiku.

JK na ujumbe wake(kushoto) akiwa katika mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza mjini Maputo leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Msumbiji. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. PAMOJA NA KINA MGONJA NA MRAMBA TUNAWATAKA KWANZA AKINA EPA WOTE IKIWA NA DINGI KAGODA, MSITUVURUGE ILI TUWASAHAU EPA.

    ReplyDelete
  2. Alah! Nimependa hao askari(waliobeba shada) walivyo vaa viatu vya kawaida. Ina make-sense kwamba wako kwenye ceremonial dress. Sio kwetu hapa wanawapa viatu vya kiume!

    ReplyDelete
  3. ISSA JK HATUMII "TEMBO" WALA KINYWAJI "KINACHOASHIRIA TEMBO" HUMO NDANI YA GLASI INASEMEKANA KUNA "MAJI SAFI YAKUNYWA".

    ReplyDelete
  4. Bora tuungane na watu wa Msumbiji kuliko Kenya!

    ReplyDelete
  5. Cheers...very nice sherry!!!Duh msafiri anaonja maji ya mizabibu!!!

    ReplyDelete
  6. KWA MSWAHILI KILA SIKU ANAYEMSHINDA KUVAA HUMUONA MBAYA, MBONA WACHINA WANAOTULETEA BIDHAA MBOFUMBOFU TUNAWACHEKEA NA KUWAUZIA VIWANJA NA NYUMBA! UZALENDA WA NDUMILA KUWILI UMENISHINDA MIE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...