katuni za king kinya zikitamba ujerumani

King Kinya akiwa mzigoni
Ndugu yangu Michuzi,
habari za kazi ngumu za kila siku kutupa habari nyingi za hapo nyumbani. Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Blog yako, nafurahishwa sana na kazi zako. Hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya kutupa habari ndugu zako.

Siku ya Tarehe 2-11-2008, hapa Berlin, kwenye treni za chini ya ardhi nilipata bahati ya kuona katuni ya Mtanzania mwenzetu King Kinya ndani ya treni, kila alieiona alifurahishwa na katuni hii.
Nimeona nimpongeze King Kinya kupitia Blog yako, ajue na pia kuwapa moyo wachoraji katuni wote Tanzania wajue kazi zao nzuri huwa zinaonyeshwa hapa Berlin. Ongezeni bidii wachoraji wote ili mjulikane kimataifa, hii ni kazi ya pili sasa ya Mtanzania kuiona katika treni hizi.
Hapo mwanzo niliona kazi ya Ally Masoud (Kipanya) Bahati mbaya sikupata picha yake. Nawatakia afya njema na kila la kheri wote.
ni mimi mpenda maendeleo ya Watanzania wote.
Mdau ujerumani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mimi pia nachukua fursa hii kumpongeza lakini nina swali, Je mchoraji anafaidika vipi na jinsi kazi yake inavyokuwa displayed kwa matajiri? Pili, katika hilo vigezo vya International patent and copyright vimezingatiwa?

    ReplyDelete
  2. weeeeee king kinya jamani wee ni mzuri jamani heeeeeeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...