Michuzi,
pole kwa vacation na pia kwa kukosa ndege.
Nipe nafasi kidogo niongelee wizi mdogo mdogo hatimae mkubwa katika Julius Nyerere International Airport maana inakera na inauma ile mbaya
Ni kwamba kuna utaratibu kwenye viwanja vya ndege kuzuia abiria kubeba vichupa vyenye vimiminika zaidi ya ml100. Kwa hiyo inalazimu abiria kulazimisha kupima mzigo hata kama una 6kg ili mradi kusalimisha mafuta na vi-manukato kwa namna moja ama nyingine.
Kitu kilichojitokeza pale ni kwamba kampuni ya kupakia na kupakua mizigo ya Swiss port imeshindwa kudhibiti wafanyakazi wake na hivyo kupoteza hadhi ya kuchukua dhamana ya mizigo ya abiria. Nilichokiona mimi ni kwamba wale jamaa wanaobeba mizigo hufungua zipu na kukagua kilichomo ndani. Wakiona kitu cha thamani wanaweka mifukoni mwao.
Na kinachoumiza ni kwamba kama kuna vitu vilikuwa kwenye mifuko midogo ndani ya begi ambavyo labda ulitaka visigusane na vingine basi utavikuta tofauti, maana wanachana vimifuko ili kutafuta wanachokitafuta wao (WIZI MTUPU), ustaarabu hakuna hata kidogo.
Sasa nataka kuuliza kuna usalama gani kama mtuu amepima mzigo ili kufuata sheria za usalama wa usafiri wa anga na hatimae wajinga wachache wapitie vitu vya thamani kwenye mizigo yake? Na je, hii itatoa picha gani kwa abiria wapendao kutumia viwanja vyetu kusafiri kwa kuchukulia kuwa ni salama kwa kwa mali na mizigo yao.
MIMI NI MDAU NA NIKO AIRPORT.
Naomba kuuongezea machache.Ni kweli kabisa,ni kweli tupu kuhusu huo wizi hapa Uwanja wa DIA...
Kweli huwa mabegi yanafunguliwa tena wana utaalamu kuliko unavyodhani wanafungua zipu bila kuiharibu,na wanatoa vile wanavyovitaka wao kama Camera,Simu ,I-pod ,Laptop... na biashara kubwa ya kuviuza inafanyika huko NJIA PANDA sehemu ya kwenye Bar na Makazi ya watu....na huwa wanajisifu sana, na isitoshe ni kweli wana maisha mazuri sana LOADER AMA PORTER WA BONGO NI SAWA NA PORTER AMA LOADER WA ULAYA nikiwa namaana ya kwamba maisha yao yako juuu na ni matawi kuliko hata Maboss wao waliopo maofisini ,maana wao hupata Pesa kila aingiapo Shift.
Kulikuwa na utaratibu wa kuwapekua wakati wakitoka kazini,lakini sasa hakuna ila hata hivyo ni wajanja sana mara nyingine wanauza humu humu jengoni.na tunapata sana malalamiko mengi kutoka kwa wageni wetu watakao na kuingia nchini.Binafsi inaniuma sana maana ni juzi tu nilitumiwa na ndugu yangu mzigo wa Camera na wakailamba.
Na Juzi kuna wawili walijaribu kuiba mzigo wa mama mmoja Mmalawi waliushusha kwenye Air Malawi wakadai kuwa unaenda na Precision Air lakini Askari aliwashuku na kuwakamata sasa sijui kesi imeendaje.... WIZI WIZI WIZI KILA KONA......
Nini kwenye mabegi ya abiria, na wizi wa mafuta ya ndege je??? tena hiii ni issue sana kubwa maana hadi baadhi ya watu ambao hawastahili kuwepo wanashiriki kwenye hiii....jaribuni kufuatilia.
USHAURI WANGU kwa TAA na SWISSPORT wangetengeneza bango kubwa kuwasaidia wageni wanaondoka Departure liwekwe Getini pale nje kabla ya security liandikwe kwa kiingereza na kiswahili hata french kuwa ABIRIA ASIWEKE CAMERA, SIMU, LAPTOP AMA HELA MAANA NASIKIA KUNA WATU HUWA WANAWEKA HELA KWENYE MABEGI...PLEASEACHENI AIRPORT IMEKUWA MBAYA..
NA ABIRIA WA KUTOKA NJE WATAJUA HILI SUALA TARATIBU TUWASAIDIE HAWA WAONDOKAO....
mheshimiwa, habari hii imenigusa kwa sababu yalinikuta na ningependa shauri hili uliweke front page.
ReplyDeleteNimekuja kugundua kuwa katika kuimairisha ulinzi viwanja vya ndege kumefanyika kaufisadi ka kuwapa kampuni binafsi ambazo nazo zimeweka walinzi ninaohisi hawana hekima wala uzoefu wa huduma kwa abiria ikiwemo mambo ya anga. Nilitokea kusafiri kivakesheni huko kusini nikiwa na zana kwa ajili ya shughuli za uzinduzi wa miradi kwa hiyo nilipaswa kuchukua mikasi maalum (rangi ya dhahabu)kwa ajili ya kukata utepe, bendera ndogo za mezani za nchi kadhaa ambazo vitako vyake ni vya crystal na bendera kubwa mbali za sherehe za kitaifa.
Walionihudumia JK airport Bongo walinielewa na kuahidi kuutunza mzigo huo(security check)lakini vijana waliotajwa kwenye taarifa yako walivutiwa sana na mng'ao wa mikasi na crystals zilizokuwa zinawaka kwenye x-ray checking machine. Wakafungua na kusambaratika box langu, na hamadi walipoona hamna kitu kinachowafaa na kutishika na mabendera pia tepu iliyofunga mzigo huo,ilikuwa haiwezi kufungika iliwapa wakati mgumu sana. Fikiria, nikapaswa kupokea mzigo uliosambaratika pale Mtwara pamoja na mizigo ya viongozi wakuu kwa aibu sana. Ina maana ingekuwa ni vitu vinavyouzika nisingepata kitu. nililalamika na kwa mara ya kwanza nilibembelezwa sana sijapata kuona, wakaniomba nisiandike kwenye gazeti maana niliahidi kufanya hivyo. Mheshimiwa Mithupu, tafadhali jambo hili litafutiwe njia ya kudhibitiwa kabla halijatuharibia heshima ya nchi. Udokozi umezidi. Huduma ya viwanja kubinafsishwa isitoletee aibu. Kemea jambo hili.Pole kwa kubadilishiwa eropleni lakini ulipata fursa ya kuziaga balimi maana ni marufuku kutoka nazo stone town.afadhali ya pombe haramu unaweza kutorosha.
by Chakupewa
Michuzi sasa ushahidi kamili nitakutumia kuonyesha jinsi hao KLM na SwissPort walivyomliza Mama mmoja na mtoto wake wa miaka sita. Nitakupa na majina ya wahusika wote kwenye hiyo dili maana ni aibu tu. Begi la mtoto wake lilichanwa kabisa na kuibiwa vitu kibao na hapo eti alisafiri na KLM kutoka Copenhagen kuja Dar es Salaam. Tena maskini mama wa watu alikuwa anarudi kuwahi mazishi ya baba yake mzazi. Can you imagine? Baadaye narudi natafuta data zote.
ReplyDeletehalafu cha ajabu Michuzi huyo mama aliyeibiwa na kuchaniwa begi yake akitokea Copenhagen kuja Bongo hakulipwa hata senti tano wahuni wa KLM walikuwa wanampiga dana dana hadi muda wake wakurudi ulipofika akaondoka mtupu. Mimi ni shahidi kabisa ninafanya kazi hapa Airport. HUU NI WIZI WIZI MTUPU.
ReplyDeleteNimesoma hii story na kwa kweli nashangaa. Nasafiri saaana mara moja at least kila wiki saba nakwenda nje nchi mbali mbali na huwa nina mizigo haswa. Kama msafiri Mtanzania nahakikisha mizigo yangu ina kufuli kwenye hand luggage nabeba necessities zangu zikiwemo expensive perfumes. kwa kifupi sijawahi kukumbana na tatizo kama hili analozungumzia mdau huyu. Inasikitisha kusikia haya lakini siyo representative ya hali iliyopo hapo JK airport. Kitu ambacho nimekishuhudia wakati wa kucheck inn ni kwamba iwapo mtu ana dawa ya meno au perfume chupa kubwa na kadhalika hao wanaocheckin kwenye final gate huwa hawaruhusu vipite na huwa wanafanya hivi wazi kabisa. Na hii siyo tu kwa Tanzania bali duniani kote sasa hivi Heathrow is even worse!!! Swali la kujiuliza nikwamba wanapochukua hivyo vidawa vya mswaki wanavipeleka wapi? huenda airport management ingeweka mpango wa kugawa kwa yatima vitu hivi kwani kwa sasa ni wazi wale vijana huwa wanavichukua na huu sio wizi ni kwamba hakuna airways inayokubali vitu hivi. Mara nyingi wanafungua pochi langu lenye vito vingi vya dhahabu na navimwaga mezani but I never ever lost a thing. Wangekuwa wezi waliokithiri basi ningeingizwa mkenge kila mara but hata kwenye mizigo ya cargo sijawahi kupata hili tatizo-tatizo lililopo ni la rushwa kwa mfano wakiona umetoka nje watatamani wakugonge au uwatulize. Unaposafiri kutoka nje ya nchi na waTZ wanaosachi wakiona hela za kitanzania wanakuuliza kiutani je hela za Tanzania hutumika huko nje in essence wanachotaka hapa uwape tip ambayo ni rushwa of some sort-Hii siyo rahisi iishe kwani sasa hivi pamoja na udhibiti mkali uliopo ni jambo ambalo linaendelea na si rahisi kunote kwani hakuna njia ya kudhibiti maongezi kani ya anayesachi msafiri. Kikubwa ninachokiona hapo JK airport ni vyoo kuwa vichafu saaaaana!! Duh wanahitaji kubadili bathrooms na toilets kuzifanya ziwe comfortable environs. kuweka wasichana pale haitoshi iwapo vyoo haviflushiwi na kusuguliwa ipasavyo. Otherwise wakiimprove viti vya kukalia upande wa kuondokea itakuwa bomba zaidi. Ninafurahishwa sana na duty free shop hapo airport pamoja na restaurant ile-safi sana but please serve drinks like Konyagi na d tanznaian beer. Na ile elavator vipi ipo kimapambo au? Muwe mnawaambia wadau wachange vitu vingine kama serikali imeshindwa kumaintain. Katika upande wa kutoka pale JK kuna maofsa wa TRA wakorofi sana wanajidai kubishana hata na madiplomat!!! Huwa nawashangaa sana baadhi yao ambao wametoka shule juzi juzi na wanataka utajiri wa haraka haraka just because wako TRA?? kauli zao ni mbovu za kibabe na wakivaliwa njuga na wWHOEVER is in charge Tanzania inaweza ikapendeza zaidi. Otherwise mie naona ni matatizo madogo yanayoweza kurekebishwa hapo airport-Mandhari so far kwa mbele ni safi kwa nyuma sijui serikali ina mpango gani nyumba zimejengwa kiholela hazina hata show??? tunapitwa na nchi ndogo kama Uganda airport yao ya Entebbe iko makini kabisaaa!!!
ReplyDeleteLakini wizi kama huo ukitokea,ni nani anabeba mzigo. Kwasababu umeshawakabidhi wao begi lako, kwahiyo kikiibiwa kitu ni wao wanatakiwa walipe?
ReplyDeleteM3
MImi nionavyo, kama ni kukaguliwa hakuna shida yoyote. Shida iliyopo ni watu kutokuwa waaminifu. Kama wanaiba mali za watu si halali na si kwamba ndio maadili na mwongozo wa kazi yao. Kukaguliwa kutaendelea na hakuna nchi yoyote ambapo unapita hivihivi bila kukaguliwa. Nimepita viwanja vikubwa kama ST.PAUL Minnesota, J.F.K-New York, SANFRANSISCO(California), Seattle (Washington) nk. nikitokea Bongo na siku zote mabegi huwa yameshakaguliwa kabla hata ya kuingia ndani ya nchi kwenye viwanja hivo nilivyotaja. Na kama hawatakagua, jua walishapikisha wakati wewe hupo. Na huwa hawaibi.
ReplyDeleteKitu kingine ni kuwa kama unasema watu wasikaguliwe kwa kigezo cha mali za thamani, je, thamani gani unaizungumzia? Watu kama Bilgates wanakaguliwa na kuvuliwa mkanda kwa swala la usalama, acha mapato. Je, waachwe kisa sababu wana hadhi? Hadhi has nothing to do with security. The same way, thamani ya mizigo yako haina uhusiano na swala la watu kukwepa kodi, kuingiza vitu vya hatar nchini nk. Tena wabongo huwa wanakagua zaidi vitu vya thamani, maana ndio nyie mnaokwepa ushuru wa kingiza bidhaa. Mtaipata, nchi ya kanuni hiyo mzee. siyo mambo kiholela!!!
Mdau,
Kwa OBM.
Mleta hoja asante sana kwa hili.
ReplyDeleteTutakua macho sasa hii ni aibu kubwa sana kwa watumishi wa uwanja wa ndege na mabosi wao.
Tafadhali sana hata tutumie blogu na vyombo vyote vya habari kuwataja kwa majina wenye mchezo huo. Shame on them! Ngoja tu kuna siku mtu ataingiza mkono sehemu anatoka na nyoka isiyoachia kidole mpaka kieleweke!
Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa na watu wote kwa ujumla, yaani inaweza kushusha hata utalii wa nchi kama watu wakijua kuwa hakuna usalama wa mali zao. Kama mtalii anakuja na camera yake ya maana halafu inaibiwa hiyo ni dissapointment kubwa kwani ni extra expense kwa upande wake. Na kwa sisi wenyewe kama umesave vijisenti vyako ukanunua kamera ya maana halafu mtu anaiba ni kutiana umasikini. Kwakweli ni muhimu hili swala liangaliwe kwa umakini. Zamani watu walikuwa wanasema kuwa kenya watu ni wezi lakini amini usiamini kuna wakati nilitumia kenya airways kutokea ughaibuni na nilisahau kamera yangu kwenye mkanda wakati wa kubadilisha ndege, yani wale vijana wa airport waliitangaza mpaka nikapatikana mwenyewe na mimi wala sikuwa najua kama nimeisahau. Kwahiyo tujitahidi kudumisha uungwana na si kuharibu jina la nchi na watu wake. Miss Mdau
ReplyDeleteKama hujawahi kukutwa na adha ya kuibiwa airport basi shukuru mungu, kwani wizi (is udokozi a proper word?) upo sana. Cha msingi, kama una kitu chochote cha thamani ni bora ukiweke kwenye mzigo wa mkononi (hand luggage) kuliko kukiacha kiende na mzigo wako mkubwa kwenye sehemu ya mizigo, kwani huko utaibiwa!
ReplyDeletekwakweli hii ni tabia mbaya kabisa, mimi yalishanikuta na mpaka leo roho inaniuma, nilikuwa nasafiri kwenda South Africa,nilipofika airport ya johanesburg nikakuta begi langu limefunguliwa (tena wamevunja kofuli) na vitu vyangu vya thamani vimeibiwa. yani kwakweli hawa watu inabidi wachunguzwe na wachukuliwe hatua kali kwasababu wanaitia haibu nchi kuwaibia wageni vitu nyao.
ReplyDeleteNamshukuru mdau alieandika hii mada na mimi nitoe dukuduku langu, mimi naishi huku uaghaibuni january 2005 nikiwa natokea Tz nakuja huku na ndege ya emaret hapo jk airport waliniambia bag langu limezid weght nikapunguza uzito hadi wakaridhika matokeo yake nikawa mtu wamwisho kuingia ktk ndege, sikomplain hilo tatizo nikuwa lile bag sikulipata tena kabisa hadi hii leo nasikulipwa chochote nafikiri halikuingizwa ktk ndege na mulikuwa na vitu vya thamani pamoja na dhahabu za mke wangu na nyingine zilikuwa amana za watu nilipewa niwafikishie wenyewe huku pia mulikuwa na my weding video na zawadi nyingi za waif nilikuwa ndio kwanza nimeowa lile bag limeniuma sana hadi hii leo nasikia uchungu, lakini namuachia muumba hakipotei kitu kwake atalipa tu.
ReplyDeleteYALABI,,NIMEHISI ATA KULIA
ReplyDeleteWEE annon apo km hujaibiwa usitupe mifano yako ovyo,,,nje ya mada
YAN ME NDO ILIKUA WORSE ILE HAKUNA,YAN NATUA MWANZA TOKA DIA NILIKUTA MY SAFAR AG LIKO UCHI KABISAAAA WAAAZI YAN WALIFUNGUA ZIPU SASA IKAWASINDA KUFUNGA WAKABANDIKA NA MIGUNDI YAO,,SIJUI WALIFIKIRI NIMEBEBA DHAHABU???YAN MAHARAGE,MKUNUNGU WOOTE NJE,,NILIKUA NIMEBEBA NEW SHOES,NA VITU VIDOGO IVI UZURI NILIVIKUTA BAADA YA KUPEKUANAO OFISINI KWAO,,,NILICHOWAAMBIA YAN BEGI SIWADAI VITU VYOTE VIPO ILA MNA BAHATI SAAANA MNGEKOMA WENYEWE IYO KASHFA YAKE YAN MNGENILIPA MAMILIONI NA PRESS ADI NJE,,NYAMAFU SANA WALE
TAREHE 9 FEBRUARY 2008 WALIIBA PETE YA HARUSI YA MAREHEMU MAMA YANGU AMBAYO NILIWEKA KWENYE BAG KATIKATI YA NGUO KENYE SANDUKU. NILIFIKA LONDON NIKAKUTA KUFULI LIMEVUNJWA NA PETE IMECHUKULIWA AMBAYO ALIACHIWA MDOGO WANGU KAMA URITHI KATIKA KUGAWA VITU VYA MAREHEMU NA NILIKUWA NAMPELEKEA. NATUMAINI MAREHEMU HUWA ANAMJIA HUYU MWIZI NAKUMSUTA!!! NA ATASHIKWA SIKU MOJA. SOMETHING HAS TO BE DONE MAANA IT IS A SHAME TO THE NATION!!! I HATE GOING THROUGH THAT AIRPORT NAFUU KIA. SHAME ON JK AIRPORT SECURITY. I SAY AGAIN SHAME ON THE WHOLE MANAGEMENT!! INA JINA LA BABA WA TAIFA NA INAENDELEZA UPPUZI WA NAMNA HII. I SAY SHAME AGAIN AND AGAIN. MICHUZI WAFIKISHIE HUU UJUMBE PLEASE.
ReplyDeleteAIBU SANAAA HATA SINA CHA KUSEMA.
ReplyDeleteYAANI NAMPANGO WAKUJA BONGO MWAKANI SASA NTAKUWA MAKINI. UNAJUA BWANA MTU UKIKAA HUKU ULAYA HIVYO VITU VYA UWIZI NA UDOKOZI UNASAHAU KABISA LAKINI KUMBE MHHH KWINGINE NDO KUMEKUCHA.
MUNGU SAIDIA TANZANIA YETU
Nimefurahi sana kwa aliyeanzisha mada hii,kwani mimi yaliyonikuta wakati natoka tz naelekea u.k mara niliambiwa mzigo umezidi,kwani ndege ya british airways hawaruhusu uwe na hand luggage na ukiangalia kwenye foleni wenzangu wote wana hand luggage,na nilipotoka u.k kwenda t.z nilikuwa na hand luggage,mara tuachie vichenjichenji.mara ya mwisho kuna dada akanifata na bila ya aibu akaniambia nikitaka hand luggage yangu iende inanibidi niwape kitu kidogo.Mradi aibu tupu
ReplyDeleteMSEMA UKWELI NI MPENZI WA MUNGU. MCHEZO WA KUIBIWA VITU KWENYE MABEGI TZ HAUKUWEPO. ILA KENYA AIRWAYS WALIKUA NAO SANA. KWA MARA YA KWANZA NILISHITUKA KUSIKIA MTOTO WA KIKWETE KAIBIWA SIMU DAR AIRPORT. TOKA SIKU HIYO NIKABADILI NJIA NA KUA NATELEMKIA KIA KWANZA NI RAHISI UNAWEZA KUPONYA SIO CHINI YA LAKI TANO ZA KITANZAMIA. PILI WATU SIO WENGI HIVYO UWEZEKANO WA KUIBIWA NI FINYU (KWA MAWAZO NYANGU). JARIBUNI KIA HII NI BIASHARA MTEJA NI MFALME KAMA HUPATI HUDUMA INAYOSTAHILI KWANINI UTESEKE. KWA WALE MNAOTOKEA EU JARIBUNI CONDOR AIRLINE HAIPITII DAR. YENYEWE NI FRANKFURT MOMBASA NA NI CHEAP SANA UKILINGANISHA NA KLM AU SWISS TOFAUTI YA LAKI TANO MPAKA SABA KAJAMBANAINI NI KUBWA SANA KWA HUKO HOME. KWANI NDEGE ZIKIKOSA WATEJA SI WATAFUKUZA TUU HAO WEZI?.
ReplyDeleteWizi upo sana hapo Airport pamoja na wafanyakazi wa baadhi ya ndege pia. Nimeshaibiwa mara mbili video camera na pochi ndogo yenye fedha nyingi za kigeni pamoja na vitambulisho vyangu. Nasikia uchungu kuzungumzia hili na yote namwachia Mungu! Ipo siku watajulikana tu na kuumbuka. Hata sielewi hizo camera zao zinasaidiaje kukamata wezi!Kwakuwa vitu hivyo nilivipata kihalali sikuiba wala sikufisadi naamini Mungu anajua cha kuwafanya na si mimi binadamu!Na hilo shirika lina jina kubwa lakini usimamizi hafifu!
ReplyDeleteUMENIUDHI SANA WE ANOY HAPO JUU UNAOWAFAGILIA ETI HAWAIBI ,WEEWE HUWA UNAMWAGA MIDHAHABU JUU YAMEZA.
ReplyDeleteSASA KWA TAARIFA YAKO NI MUNGU TU ANA KUSAIDIA ILA NAKUPA MUDA PELELEZA HASWA ABIRIA WANAOPANDA ETHIOPIAN,KLM,BA, KQ WATAKUPA HABARI YAKO,NA MOST OF THEM NI WAGENI WETU NDIO WANALIZWA SANA SASA FANYA RESEARCH UJUE,
ILA HAKUNA WA KULETA MAJUNGU HAPA KWANI HUSHANGAI MBONA SIKU ZOTE MICHUZI YUPO NA STORY HAIANDIKWI SASA WEEE LETA ZAKO ZA KUWAPA BIG UP HALAFU WAWEKEE MADHAHABU YAKO THEN SIKU WAKULIZE NDIO UTALIJUA JIJI...
WIZI UPO NA HATA UKITAKA MAJINA WTU WANAYAFAHAMU NA UWEZEKANO WA KUWEKWA HADHARANI UPO..WAMEWEKWA HADHARANI WATU WA EPA NA RICHMOND SEMBUSE WAO VIDAGAAA...WEEE VIPI ANGALIA SANA ,NA SIO KWAMBA KATIKA NDEGE YOTE YA ABIRIA 350 BASI WATAIBIWA WOTE NO WAY UNAWEKA KUKUTA NO ABIRIA 50 TU AMA 80-100 NDIO WANAIBIWA NA KWA MUDA TOFAUTI ZITUAPO NDEGE MAANA RAHA ZAIDI WANASHIRIKIANA MASECURITY, SWISS LOADER NA WENGINEO ,LOADER ANACHUKUA ANAMPASIA SECURITY WANAWEKA KWENYE VIFUKO VYAO VYA NDEGE NA MAGAZETI YAO...NA KUMBUKA KWAMBA WALE WANA MASURUALI MAKUBWA YANA MIFUGO UTADHANI WANAZIMA MOTO ...USHAURI WA BURE HAPA WAPEWE UNIFORM ZISIZO NA MIFUKO ZIWE PLAIN NA WASIINGIE NA MIFUKO KAZINI NA IWE SHERIA HATAKI MTU BASI AACHE KAZI WAKO WENGI WANATAKA KAZI NA UKIZINGATIA VYUO VIMEGOMA ....MR. TEMU NA MR.MSANGI MKO WAPI AMKENI PLEASE MSAIDIE AIRPORT INANUKA KWA WIZI ...JUZI KAIBIWA PADRE MIZIGO YA BAHASHA SABA KULIKUWA NA HELA NDANI INAVYOSEMEKANA ALIPEWA ALETE DAR KWENYE FAMILIA ZA WATU ,WANATIA WATU MAJARIBUNI HAWA NA KUNA WATU WAKO SPECIALIZED KUIBA PESA TU ,NA RAHA ZAIDI WANATUMIA KARUMANZILA ILI WASIKAMATWE HIII NI NOMA NA HAITOISHA HIII.....SI UNAJUA HATA MAJAMBAZI BAADHI WANATUMIA NDUMA..KARUMANZIRA ILI WAFANIKIWE WASIKAMATWE SASA NA HAWA LOADEARS NA SECURITY NAO TUNASIKIA WANAFANYA MAMBO HAYO,...KUMBUKA KUWA DUNIANI HAKUNA SIRI NA WAO WENYEWE NDIO WANATOLEANA SIRI BAADA YA KUDHULUMIANA MAPATO KATIKA BIASHARA YAO YA MALI ZA WATU ...
ILA JASHO LA MTU HALIENDI JOSHI,NA MALIPO DUNIAN NDUGU ZANGU ,UTAKULA LEO CHA MWENZIO HUKU UNAKENUA LAKINI KITAKUJA KUKUTESA KWA STYLE YOYOTE ILE NA UKAJUTA.
MAJINA YAPO TUTAWEKA HADHARANI TU.NA RUSHWA HAPA NI KAMA KIFUNGO NA SHATI JINSI VINAVYOPENDANA/VINAVYPATANA,.BEBA VITU VYAKO VYA THANMANI KWENYE HAND LUGGAGE PLEASE PLEASE.
ASANTE.
na wanajua,maana siku wakilipitia la mkuu wa wilaya ya nanihii,ambaye ni mzee kule zain ndio watajua kilichomfanya jaluo asipige mluzi.washenzi sana wanatutia aibu si tanzania tu,kwa mwafrika yeyote.
ReplyDeletechondechonde mzee misupu lifanyie kazi tafadhali.
Jamani, katika nchi nyingine aibu kama hii ya wizi wa mali za wadau linapotokea wahusika wakuu uwajibishwa. KWANINI BWANA TEMU (mkuu wa SwissPort TZ) ASIJIELEZE ANACHOKIFANYA? LA SIVYO AWAJIBISHWE.!! huu ni uonevyu kwa wadau sio sawa.
ReplyDeleteMdau,
TZ
Tatizo ni 'ratio' kubwa ya wapagazi JKairport kulingana na abiria wanaotumia uwanja huo.
ReplyDeleteAirport za ulaya kila abiria anavuta,kusukuma au kubeba mzigo wake, labda abiria awe anahitaji msaada akiwa mgonjwa au mlemavu au mzee wa siku nyingi sana.
Hivyo ratio ya wapagazi airport za ulaya kulingana na abiria ni ndogo sana, hii inawezesha uadilifu na uwajibikaji mzuri wa wafanyakazi wa airport.
Ili kuondoa tatizo la wizi JKNairport DSM, hiki 'kiwingu' cha wafanyakazi wa TAA na wapagazi wa Swissport na wafanyakazi mashirika ya ndege kipunguzwe kwa sana hapo JKairport DSM.
Pia sisi abiria tutumiao JKairport tukuze utamaduni wa kutotegemea wapagazi kutubebea mizigo yetu, hii itafanya 'kiwingu wa watu wasio abiria kupungua airport na kuwezesha kuwajibisha wafanyakazi wasio waadilifu, kwani itakuwa rahisi kujua ni mfanyakazi yupi wa TAA/swissport alikuwa eneo gani na alikuwa anafanya nini. Pia CCTV camera ziwekwe kila mahala kufuatilia mienendo ya watu wenye nia mbaya ya kuibia abiria.
Mdau
Rocy
Jijini London.
mie ni anon wa tarehe 2 saa 11:20. Naandika tena kumaintain jamani mnaosafiri mara kwa mara kupitia JK ni wapi pale mnapowapa watu wawabebee mizigo? Mbona mie sioni? Kama ni kwenye xray na umecheck in mapema siyo ziro minute una every right kumfahamisha huyo anayetaka kufungua mizigo asubiri uwepo wakati anasachi infact labda wananiheshimu for who I am but mara zote huwa wananieleza kabisa tunahitaji kuangalia pochi yako uangalie usije ukasema tumekuchukulia chochote.
ReplyDeleteKwa kweli namaintain situation imebadilika sana sasa hivi. Sina share airline lakini naona kabisa wanajitahidi hapo kwenye X-ray labda wizi unapotokea ni kwamba wewe kama msafiri haupo attentive/makini kuhakiki mizigo yako inakwendaje. Wanaponitolea dhahamu zangu all eyes on them!! na naongea nao-they are just human!!
Lakini kwa kuwa wadau wengi wanalalamika naona Huenda hali ni tofauti mnaposafiri kwenda mikoani na hapa inabidi niulize je mnazungumzia old airport ambapo biashara ni survival for the fittest au JK? Katika JK ushauri wangu kwa msafiri yeyote yole ni kwamba vitu kama ipods, video camera's laptops na mobile phones havipaswi kwenda kwenye buti la ndege unaingia navyo kama hand luggage. Of course ukiviweka wazi ukidhania third world country yetu ni kama huko ulaya ambapo almost everyone can afford-mnawashawishi vijana.
Tukiangalia ukweli halisi hata huko nje mnapojidai napo jamani store na sehemu za cashiers mnapofanya kazi si panahakikishiwa usalama? so what makes you think you should be more laxed in Tanzania? Kuna usemi abiria chunga mzigo wako!!
Kwa huyo kaka aneyesema kwamba alizidisha mizigo kwa kweli nashukuru Mungu I am a frequent traveller who knows the KG I am allowed to have. Unapopewa ticketi kwanini usisome unaruhusiwa kilo ngapi? halafu mnajidai mko nje mnashindwa kubadilika na sdevelopment kwa kununua weighing scale za kuwasaidia kupima mizigo yenu na kuenzure kilo ziko within the limits na kama zimezidi you have the money to pay for excess??? Last minute rushes hazitaacha kuwacost wala msilaumu vijana wa airport sana. Narudia tena nasafiri sana tena mara kwa mara. Tanzania haiwezi kulinganishwa na some West African countries-bado hamjaona kitu!!.
Kama umekabishi mzigo wako unatakiwa kuwa na kuzitunza vizuri kabisa luggage tags. With your luggage tags you can claim your luggage if it is lost through the main offices of the airlines. You are insured na so is your luggage. Nashangaa kuona watu wengine wanalia kabisa kana kwamba wamefiwa. All you need to do ukifikwa ni kuweka inventory yako na kuipeleka kwa main airlines. Nasema hivi kwa kuwa kuna Afsa mmoja alipoteza mzigo wake Cairo na aliweza kuclaim through the airlines alizotumia kwamba amefika na hauoni mzigo wake. Naamini kabisa mkiwa na muda wa kufuatilia mnalipwa-At least nafahamu Ethiopian,KLM, British Airways wanalipa in case of any thing including kama kuna cancellations.
Tatizo lingine ninaloliona la watanzania ni kubebana na mizigo-hata mimi hufanya hivi mara kwa mara kutokana na shughuli zangu lakini kadri miaka inavyokwenda naona vitu vingi kama electronics na vyakula vinapatikana kila mahali duniani including tanzania hivyo sioni haja ya kubebana. Vile vile kuna Cargo services kibao and again nikiangalia mabegi ya wasafiri wengi naona kabisa poverty inanukia. Jamani kama mnaearn madolla na maeuro na mayen hayo mabegi mazuri yapo!!! Make every effort kuzuia wizi on your own first kabla ya kulaumu wengine. Wewe unayejivunia kuchuma mali ulaya ili kuwekeza wherever- umeweza kununua ticket ya economy ya ndege-unashindwa nini kununua sanduku zuri secure kama samsonite cloth ambayo hayachaniki wala kuvunjwa zipu kirahisi? Stop being cheap you people and style up men!
Mjadala huu ni mzuri na najua fika kuna wengi wataoppose views zangu kuhusiana na wezi hapo airport. Chas msingi naona vijana hao wako GADO!!!Makini msiwaonee one experience should not overule over a thousand peoples experiences!!!
Mimi nionavyo kama msafiri wa mara kwa mara kwa miaka kumi sasa pamoja na watoto wangu kuwa careless wakisafiri hali ndivyo nilivyoeleza hapo juu!-JUST BE ORGANISED and stop shifting blame to other innocent vijana wanaofanya kazi badala ya kuiba mitaani!!
Wee mtoa commet wa 2:28 unaongea utumbo,kwa sababu hayajakufika kwa hiyo unawaona wenzio kama wajinga vile.
ReplyDeleteNi kwamba ishu iliopo sio wafanyakazi wa ukaguzi bali ni wale wa kupakua na kupakia mizigo. Nadhani yanayotokea mengi ni yale ya kupitisha mzigo chini (yaani upimwe)
ReplyDeleteKwa hiyo wizi hutokea pale mzigo unapokabidhiwa kwa wale jamaa wa SWISSPORT.
Nadhani kama kuna tukio jingine zaidi ya hilo litakuwa ni jipya kabisaa na la kipekee. Na watu watakaokuwa wanafanya hivyo hawafai hata kuonekana pale Airport.
Annon wa tarehe 2 bwana wewe wanakujua na hawawezi kukuibia. Inajulikana kuna wizi tena mkubwa sana hapo TZ sio Posta, Bandari na Airport. Kila mtu mwizi mtu maana wanaona kila mtu anaiba na hachukuliwi hatua basi kila mfanyakazi hapo TZ mwizi tu. Huwezi niambia mimi leo kwamba eti watu hawaibii TZ nitakushanga sana.
ReplyDeleteMshahara wa mfanyakzi kima cha chinina kati hakizidi laki mbili na nusu na ndio aslimia 70 ya wafanyakazi wote TZ. Kwa mwezi huo mshahara haumtoshi mtu yeyotye hapo TZ mwenye mke na watoto wawili sasa anaishi vipi kama sio kwa wizi.
Swiss port, Posta, Bandari , TRA,Mizani,Tscan, wote huko wezi tupu. Watu TZ wamefikia hatua ya kuiba hata simu za mkononi unasema sio wezi. Waliwahi iba blackberry ya mtoto wa Kikwete aliomletea baba yake wakati akitokea nje miaka mitatu imeshapita na wewe unawatetea hao wezi basi na wewe nae mwizi.
Nina wasiwasi na huyu mwandishi anyejiita annon wa tarehe 2 ninahisi ni bwana Issa Muhidin Michuzi mwenyewe kwani ndie anayewafanyia kazi hapo airport kama PR au spokesmana wao. Na inakuwa vigumu kumuibia yeye.
Kuna wezi sana hapo swiss port na ukitaka hata majina yao tutayaandika na sehemu vitu vyao vinapouzwa.
its soo simple,,
ReplyDeleteUTAWALA uwe na database inayoonyesha NANI anafanya kazi KITENGO FLANI?.. SIKU GANI na wakati GANI...?mteja akilalamika begi lake...liliibiwa then anataja tu siku aliyosafiri km ilikuwa alhamis tarehe 9..ndege ya saa tisa alasiri....ni kiasi tu cha kwenda kny computer na kujua nani alikuwepo kitengo cha kusachi siku hiyo,,,,,OF COZ huyo mtu ndie ATAKUWA RENSPOSIBLE!!!
na pia wote wanaofanya kazi hapo UWANJANI wavae BADGE yenye MAJINA yao!mtu akiomba rushwa,unamreport tuu...
mnaowatetea mie nawashangaa hii ni AIBU,imagine mtalii amekuja TZ ameridhika na kila kitu,amenjoy kila kila kitu wnkt wa kuondoka tuu ndio anapata hio dhahama!unadhani atarudi tena....nyie hapo UWANJANI...acheni hizo TABIA mara MOJA!!!
POLE weee uliyefikwa na dhahama ya kuibiwa mkanda wa harusi,na ww ulieibiwa pete ya marehemu mama yako...duh yaani nimeshangaa afu nikasikitika!...vitu vingine sio vya gharama sana but they WORTH a LOT!...
sasa km huo mkanda huyo mwanaharamu kaufanyia nini km hajautupa tu???unamkosesha mwenzio KUMBUKUMBU ya ku-last LIFETIME....SHAME ON YOU!MNAOFANYA HAPO UWANJANI......mnasema EPA this EPA that!,,,kumbe wengi wenu mna roho za ki-EPA EPA tuu...
NEY-BHAM
SECURITY CAMERAS ZIFUNGWE KILA KONA NA WAAMBIWE WANAREKODIWA 24 HRS TUTAONA WATAIBA VIPI...PUMBAVU KABISA!!!
ReplyDeleteHiyo MIJIZI ya airport nina hasira nayo sana. Nilikuja kwenye msiba wa mama yangu na nikaweka picha yake kubwa kwenye frame ili iwekwe kwenye jeneza, waliiba hiyo pamoja na vitu vingine. Nilikasirika sana maana niliwaambia ndugu zangu wasitengeneze picha mimi nitaileta nilkuja siku ya mazishi na hakukuwa na muda wa kutafuta picha!
ReplyDeleteKinachonikera mimi pale airport ni everytime ure checking out lazima mtu atakuomba hela "dada niachie basi ya soda"....jamani tipping is at my own discretion".Na ukiwa unarudi Tanzania sasa utajua tu umefika nyumbani hospitality ni 0,utaangaliwa vibaya na pale kwenye passport control mtu anatamani hata kukumeza kwa hasira.Ukijaribu kufikiria what did I do wrong huoni hata kosa ulilofanya.
ReplyDeleteO.R.Tambo airport pale Joburg wizi wanaucontrol and at least unaona hapa kuna hospitality...sitaki hata kuongelea JFK airport huku US.
Airport yetu ukifika tu inatia hasira,basi tujaribu kupunguza wizi labda tutakumbukwa kwa mema yetu na si kwa uzuri wa airport.
Ushauri wadngu mimi keep all ure expensive things with you,laptop,cellphone,ipod,cameras....kwenye bag inayocheck-in acha vitu ambavyo hata wakifungua na kuiba u won't incur a huge loss,thts what I always do.
Mdau
Connecticut,USA
nyie mnaosema ya kwamba ukiondaka unaangaliwa na jicho baya mara wanakuomba hela ya soda be proud where you came from do not complain so ever ina ndugu zenu wote ni BILLGATES OR OPRAH WINFERH.na kwanini ukatalie nchi za watu cos you like24/7video camera shame on you ndiyo maana mnapata green cards za fake I mean za kununua iliuwe U.S.A CITIZEN OR UEROPEAN CITIZEN HASA NYIE MLIOKO MICHIGAN STATE UNIVERSITY LANSING MICHIGAN WAZAZI WENU WAMEIBA FEDHA SERIKALINI ACHANI MASKINI NAO WANUFAIKE
ReplyDelete