MAREHEMU SAID ALLY MUYONGO ABAD
Baba ni miaka ishirini leo(20) tangu ulipotangulia mbele za haki mnamo tarehe 04/12/1988. Sikujua kama nitafika hapa leo bila wewe lakini kwa uwezo wake maulana nashukuru ninaweza kufanya kisoma kukuombea dua kwa mwenyezi mungu akupumzishe kwa amani mpendwa baba yangu.

Mjukuu wako Steve iii alinitia uchungu sana kila alipotaka kujua baba yangu uko wapi. Bali kwa rehema za mwenyezi mungu ametambua na amepokea kwa masikitiko pumziko lako kila siku hukuombea dua kila anapolala.
Pumzika mpendwa baba yangu Asante kwa upendo, busara, ucheshi na ukarimu uliotuachia.

Baba na Mama ulioniachia Mzee Said Nawawi na Mama Mwanaidi Zuberi nao wametangulia mbele za haki. Yote Nashukuru Asante. Wapumzike kwa aman. Amen

Kutakuwa na dua ya kuombea marehemu wote,; Said Ally, Said Omary, Said Mohamed, Said Ahmed, Said Nawawi, Mama Mwanaidi Zuberi, Mzee Bakari Muyogo, Nyanya Asia Bure, Nyanya Hindu Bure, Nyanya, Rukia Bure, Shariff Ally, Zubeda Shariff, Nyanya Zubeda Shariff na marehemu wote.
Dua itafanyika tarehe 06/12/2008 Mwananyamala Koma koma saa tisa alasiri nyumbani kwa Mzee Mohamed Rashid (Msegeju) Wamoa na watu wote mnakaribishwa kushiriki dua hii.

WABILAH TAWFIQ.
INNA LILLAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN.
AMEN
Ni mimi mwanao mpendwa
Beatrice Muyongo Abad
na
Mjukuu wako Steve III.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Marehemu apumzike kwa amani. Amen

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa moyo wa subira.
    Are you related to the Kotta's?

    ReplyDelete
  3. Kwa hakika ni siku nyingi zimepita. Marehemu Abad Sharif kama sisi tulivyozoea kumuita, nilikuwa nae tullivyokuwa wote Iringa miaka ya 1976 hadi 1979. Wakati huo yeye akiwa Chuo cha Benki na mimi nikiwa Afisa Mipango wilaya ya Iringa. We used to socialise a lot. Sisi tukimuita yeye Kaka kwa sababu alituzidi umri. Lakini alikuwa mtu mwema na mkarimu sana. Miaka ile ilikuwa ya mfumo wa chama kimoja na mara nyingi tukikutana hoteli ya Cats ambapo tukibooze sana na kupeana michapo ya kila aina. I recall tulikuwa na akina Benjamin Rugumyamheto ambae sasa anafanya kazi Botswana University. Mimi wakati huo kipato changu cha kiserikali na nikikatwa mshahar ukienda JKT, kaka Abad used to rescue me kwa kutununulia round. Anyway hayo ndiyo maisha ambayo lazima ikifika siku basi yanafikia ukomo. Inna Lilahi wa inna Ilahi Rajioon.Mola apumzishe peponi. Amen.

    ReplyDelete
  4. Those words are so powerful that they almost made me cry. Tt shows just how much you loved and still love your father. May the almighty G-D rest your father's sould in eternal peace.

    ReplyDelete
  5. kweli zamani aiseee!!!! manaake picha inajieleza

    ReplyDelete
  6. Nahisi ni BEATRICE ABAD nimjuwae, mama mweupe hivi, MTANASHATI MPENDA WATU, ASIYE NA MARINGO anafanana sana na huyu mzee marehemu, ni mtu wakaribu sana kwangu kama ndo yeye, na nahisi ni yeye, kwa vile niko mbali sana huku sitoweza kuhudhururia hii shughuli, nakutakia kila la kheri na muikamilishe shughuli salama salimini, na nisaalimia STEVE na anasalimiwa na MICHAEL MKWELELE, yupo hapa kwa likizo, atarudi Nairobi January 2009. AMIN, MUNGU AKUBARIKI NA AKULINDE.

    ReplyDelete
  7. Rest in Peace mr good friend Abad. Mtoto Beatrice alichosema ni kweli. Abad alikuwa Rafiki yangu sana. Said Nawawi nilimfahamu pia na mara zote alikuwa haishi kimzungumzia mtoto wa nduguye. Alilia kwa uchungu mkubwa kila alipomwona na ALIMWITA NI MWANAE WA MWISHO ALYEACHIWA NA MDOGO WAKE ABAD.Tutakuwa pamoja kwenye dua kwa Bro. Mohamed Rashid. Yote ni kazi ya mungu tulipokea

    ReplyDelete
  8. Tuje na tasbihi au rozari?

    ReplyDelete
  9. Haya jamani ni muda mfupi tu umebakia kuanza kwa dua hii kubwa katika wakati mwafaka wa kurehemu mararehemu wote. Kama jadi yetu popote ulipo ndani na nje ya Tanzania tumia japo takika 5 kutoa dua yako kwa marehemu wetu. Siyo mpaka ufike kwenye shughuli yenyewe. Popote ulipo unasoma dua yako. Asanteni. Mwinyijuma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...