Mungu si asumani leo nimetua dar salama salimini
napokelewa hoteli ya la kairo
hatimaye nimetua salama bandari ya libeneke na mambo yote nimekuta mswano, sema madimbwi kibao ambayo nimeambiwa ilinyesha sana ijumaa na jumamosi wakati niko vijijini kanda ya ziwa katika kuchaji upya betri. si unajua tena mwaka umeisha huu....
kwa kweli sina mengi ya kusema zaidi ya kushukuru shirika la nanihii ambalo baada ya kunilaza mwanza jana bila kupenda (bonge la hoteli inaambiwa, kiyoyozi na dstv ndani. nani alale?), hatimaye leo nilikuja kuchukuliwa asubuhi na wenzangu niliokwama nao na kupelekwa eapoti kama walivyoahidi.
sina cha kuripoti zaidi ya kwamba kwa sasa usafiri wa anga ni mgumu kiasi sehemu kubwa kama mwanza, ukizingatia msimu ya krisimasi na mwaka mpya umewadia, ukiambatana na watoto kufunga shule. inakuwa balaa tupu.
nawashukru precision air kwa huduma bomba, japo sijawasamehe kwa kusema pale hotelini nile tani yangu na kusaini, ila vikali (hata mie wa soda) juu yangu. ah jamani!
lingine ni zogo nililolikuta eapoti ya dar ambapo madereva taxi wa yanga na simba waliokuwa wakipopoana macho kwa kila mmoja kudai mchezaji wao ndiye aliyesababisha stars iwalambe sudan 3-1.
Yanga walikuwa wamekazania kwamba magoli yote yamefungwa na 'kijana' wao na simba walikuwa wanabisha kwamba endapo krosi zisingetoka mtaa wa msimbazi mfungaji asingepata fursa ya kucheka na nyavu...
-michuzi






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mvua ikinyesha basi vumbi angani lakua tope na ndege huwa zagoma kwenda! tumeshazoea mkuu.......... karibu tena kwa wenyewe

    ReplyDelete
  2. Here we go again!!
    Simba,Yanga....zzzzzzzz
    I'm tired of this crap!!

    ReplyDelete
  3. yaaani mburaah!!!me too!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...