


kwa kweli sina mengi ya kusema zaidi ya kushukuru shirika la nanihii ambalo baada ya kunilaza mwanza jana bila kupenda (bonge la hoteli inaambiwa, kiyoyozi na dstv ndani. nani alale?), hatimaye leo nilikuja kuchukuliwa asubuhi na wenzangu niliokwama nao na kupelekwa eapoti kama walivyoahidi.
sina cha kuripoti zaidi ya kwamba kwa sasa usafiri wa anga ni mgumu kiasi sehemu kubwa kama mwanza, ukizingatia msimu ya krisimasi na mwaka mpya umewadia, ukiambatana na watoto kufunga shule. inakuwa balaa tupu.
nawashukru precision air kwa huduma bomba, japo sijawasamehe kwa kusema pale hotelini nile tani yangu na kusaini, ila vikali (hata mie wa soda) juu yangu. ah jamani!
lingine ni zogo nililolikuta eapoti ya dar ambapo madereva taxi wa yanga na simba waliokuwa wakipopoana macho kwa kila mmoja kudai mchezaji wao ndiye aliyesababisha stars iwalambe sudan 3-1.
Yanga walikuwa wamekazania kwamba magoli yote yamefungwa na 'kijana' wao na simba walikuwa wanabisha kwamba endapo krosi zisingetoka mtaa wa msimbazi mfungaji asingepata fursa ya kucheka na nyavu...
-michuzi
mvua ikinyesha basi vumbi angani lakua tope na ndege huwa zagoma kwenda! tumeshazoea mkuu.......... karibu tena kwa wenyewe
ReplyDeleteHere we go again!!
ReplyDeleteSimba,Yanga....zzzzzzzz
I'm tired of this crap!!
yaaani mburaah!!!me too!!
ReplyDelete