baada ya kazi nzito mdau Ibrahim (nyekundu, mmatumbi) akiwa anajidai baada ya kupokea Medali ya silver kwa kushika nafasi ya pili
hapo mdau akila timing kali ya kuongeza points

mdau katika harakati za ngumi jiwe. chini akipiga mawashi geri ambalo ndio teke lililompeleka fainali. hilo linapigwagwa kichwani kwenye upande wa sikio kama kelb vile ya mkono

Mdau IBRAHIM ELIAS anayesoma India huko Hyderabad Jumapili ilopita kafanikiwa kunyakua medali ya silver baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya karati ya DRAGON FIRST yaliyoandaliwa na MARTITAL ARTS ACADEMY OF INDIA.

Katika mpambano huo alishindania ubingwa wa mkanda wa kahawia na kujinyakulia nafasi ya pili na Silver medal. Mambo yalifanyika katika viwanja vya H B Colonya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera Ibrahim...kwa kunyanyua hadhi ya taifa langu kule India,hii ni medali ya halali kabisa...sio kama wale mabeba boksi waliodoea kule ulaya na marekani...wala hawanavipaji vyovyote bali kudoea vijizungu na vidola!!!aibu tu

    ReplyDelete
  2. Huyu ni Ibra wa ifunda tech ama siyo maana kwa mbani kama wamefanana jamaa alikuwa mnyonge kishenzi shule sasa kama anacheza karate kweli maisha yanabadilika

    ReplyDelete
  3. kabla sijakupa hongera zang.naomba nijibu hili kwanza
    Huko india umekwenda kusoma nini??
    umekwenda kusomea huo ugomvi (karate) au umekwenda kusoma masomo mengine lakini karate unacheza kama hobby??
    then mbona hao wapinzani wako wanaonekana MDONDO TU (WACHOVU)!!au macho yangu!!!maana naona wamekondeana kama mateja tu wa kinondoni!!!!
    ni hayo tu

    ReplyDelete
  4. ah hao ni watoto wadogo wacha maujiko tena age kati ya 15-19 yrs wakati ww una umri zaidi ya 30

    teh teh teh teh hah

    ReplyDelete
  5. Huyo ndiye yule wa ifunda tech.Wabongo achane nyodo ibra kafanya la maana sio sisi tunamfahau vizuri ni pamoja na masoma India ya sofware bado anajitahidi kufikia level hiyo nani mwenye ujasiri wa kuzipiga kama yeye ugenini? Tumpe shavu kijana aendeleze konfu yake na kututangazia jina la nchi yetu

    ReplyDelete
  6. Lazima wabongo tukubali Ibra katupaisha, hizo sio ngumi za mitaani jamani watu wanapangwa kwa level zao kuanzia uzito, miaka, na level zao za mikanda huwezi piganishwa na watoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...