Hello kaka Michuzi,
Akhsante sana kwa kutu-update na mambo mbalimbali kuhusu jamii yetu. Mimi leo ningependelea kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kutumia CONDOMS ili kujiepusha na magonjwa ya zinaa haswa UKIMWI.
Hii ni kwa sababu leo ni siku ya ukimwi duniani na ningependa wote tuungane na watu wote duniani kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki waliokufa kutokana na gonjwa hili ambalo bado halijatafutiwa ufumbuzi. Kumbukumbu hii ituelimishe na kutupa tahadhari juu ya ukimwi.
UNAIDS inakadilia kwamba mpaka sasa kuna watu milioni 33.2 duniani wanaoishi na virusi vya ukimwi, kati ya hao milioni 2.5 ni watoto. Pia wanakadilia watu milioni 2.5 wameathirika kwa kipindi cha mwaka 2007 tuu. Nusu ya watu wanaoishi na ukimwi duniani ni vijana waliopata maambukizo hayo wakiwa chini ya miaka 25, na hufa kabla ya kufikia miaka 35.
Karibu asilimia 95 ya watu wenye ugonjwa wa ukimwi/virusi vya ukimwi wanaishi kwenye mataifa ya kimasikini duniani, lakini virusi vya ukimwi leo ni tishio kwa watu wa jinsia zote na watoto duniani kote.
Siku ya ukimwi duniani ilianza tarehe 01/12/1988, naomba watanzania wenzangu tuelimike kuhusu ukimwi na tujue kwamba ukimwi bado upo na unaweza kunipata mimi, wewe na yule. Watanzania safari bado ni ndefu.
Ni mimi,
Mdau Mrs K

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nafurahi kuona hii post. Nilitegemea zitakua picha nyingi sana leo humu ukizingatia huu ugonjwa umegusa kila mtanzania. Sidhani kama kuna mtanzania yeyote ambaye hana ndugu au rafiki wa karibu aliyepoteza maisha kutokana na huu ugonjwa.

    Tunahitaji kukumbushana kila siku jamani kuwa huu ugonjwa bado upo. Na pia ni muhimu kujua status yako kama wewe unabadili wapenzi kila mara hii itakusaidia usitambae kwa wengine au kama umeupata ni rahisi kupata matibabu na ukaengeza muda wa kuishi.

    Leo NY City kila unapopita kuna ribon nyekundu. Hata kama hutaki kujua leo ni siku ya nini utaelewa tu. Kwenye TV stations nyingi wanaonyesha jinsi watu walioathirika na huu ugonjwa wanavyoishi. Hii inakuzidishia kukukumbusha kuwa huu ugonjwa bado upo.

    Na pia ingawaje wanasema huu ugonjwa 95% ya watu walionao wako kwenye nchi zinazoendelea lakini ukweli ni kuwa hiyo 5% iliobaki wako kwenye nchi zilizoendelea na majority ya watu wenye ukimwi ni wanawake, senior citizens na wahamiaji....it is sad kusikia wahamiaji nao communities zao zina data kubwa lakini ukweli ndio huo.

    Hivi tunavyoishi kwenye communities zetu na kupenda kuoa na kuolewa na watu wa kwetu au kwenda kwetu kuoa/kuolewa inachangia sana hii. Watu wakija kutoka nchi zetu na rushwa iliyobobea nyumbani inakua rahisi sana kwa watu kupata cheti kutoka kwa dr bila hata kupimwa na wengine hata hawapimi. Tunaona kila siku huku mgeni akija kila mtu anataka kuwa mwenyeji wake once wakishamfahamu basi ujue wenyeji umeisha na wengine tena nao wanakimbilia hapo hapo kua wenyeji basi ndio hiyo triangle inavyoanza ndio maana wahamiaji tumeshaingizwa kwenye status.

    Awareness muhimu iwe unaishi bongo au nje ya nchi. Ukimwi ni ukimwi hauchagui wapi unaishi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...