bango
ubwabwa
ubwabwa
nyama rosti
andazi
kwa ndani
chiken
pametulia tuliiiii
pasafi ile mbaya
bufee
Ndugu Muhidin Issa Michuzi,
Salamu toka Kijiweni Restaurant.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha waTanzania wote kwenye Restaurant ya Kitanzania hapa jijini Dallas, Texas.
Maanjumati ya aina mbali mbali ya Kitanzania na ya Afrika Mashariki yanapatikana hapa kwa bei chee.
Wote mnakaribishwa.
Management,
Kijiweni Swahili Restaurant
125 SOUTH CENTRAL EXPRESSWAY RICHARDSON,
TX 75080
PHONE #S: 972-836-2282
972-310-9701
214-709-4423
HOURS: MON-FRI. 11.00 a.m. - 10.00 p.m.
Weekends: 8.00 a.m. - 11.00 p.m.
KARIBUNI WADAU TUJICHANE KWA MISOSI YA HOMU
hongera jamani kina rose,sheila,zainabu,habiba,edda, june na wengine Restaurant imetulia haya basi naona hakuna mteja mbona mimi ninatafuta part time job huko dallas simtanipatia jamani.
ReplyDeletemichuzi na wewe bwana eti chiken ni kicheni au umeona andazi akili imekuruka kidogo, heeeeeee
ReplyDeleteHONGERA SANA MFANO WA "KUIGWA"
ReplyDeleteNimefurahi kusikia kuwa mmefungua Kijiweni-I hope mtafanikiwa sana na biashara yenu na tena nitakuja kuwa support as soon as possible.
ReplyDeleteimetulia sana hiyo..namissi sana vyakula vya home..mtaniona soon
ReplyDeleteHÄ°LO NÄ° WAZO ZURÄ° NATAMANÄ° KATÄ°KA NCHÄ° NYÄ°NGÄ°NE Ä°NGEKUWA KAMA HÄ°VÄ°
ReplyDeleteEvarist Mwakasula hongera sana kwa kufanya mambo haya Mungu akuzidishie na akufanikishe zaidi na zaidi Big up Brother!!
ReplyDeletewakuu nikishuka huko south south lazima niwatembelee maana mimate hapa yanidondoka,ushauri wa bure naomba usafi na quality ya msosi viwe number one bila hivyo mtafunga virago mapema...napenda kuona homeboys mkifanikiwa,narudia tena usafi usafi usafi sana sana bathroom...nimeongea kama mtu ninayeelewa hiyo industry kwa saaaaana,good lucky na msituangushe!
ReplyDeletewabongo wa dallas mi nawapa hongera sana,i wish we have one like that here in washington dc,huo ni mfano wa kuigwa naamini watanzania watawapa support ya nguvu.
ReplyDeleteHongera sana what an accomplishement!!!!!!
ReplyDeleteAt least mtaajiri wabongo wakiingia tu mjini...Tuliajiriwa na wahindi na wajewish tulipoingia tu huku.....saa hivi ni raha kuona mbongo naye kafanya mavitu yake
MUNGU AWABARIKI
YAANI WEWE ACHA TU HAPO NDOO MAHALI PA KUWEPO.LAZIMA NISHUKE HAPO TX KIDOGO NIPATE JIBWABWA LA NYUMBANI
ReplyDeleteMBOLLO FEZA
KOLUMBUSI
OHIO
HONGERA TENA SANA SANA...NI MFANO KWELI WA KUIGWA...MIMI NITAMAKE A SPECIAL VISIT SIYO KAMA NAMISS VYAKULA VYA HOME ILA KUWASUPPORT WATZ WENZANGU JAMANI TUUUNGANIKE KUMSUPPORT HUYU MDAU WATU WA TX NA MIJI MINGINE MAMBO YA KILA SIKU KULA KWA WACHINA (WAHOOHIO) NA WAMAREKANI TUYAACHE IT'S TIME TO SUPPORT OUR OWN ROOTS...
ReplyDeleteBig up, Dallas! So I guess the saying that everything is big in Texas is proving to be correct!
ReplyDeleteHopefully mtajaribu kuweka vitu fulanifulani vya kiTanzania such as Chai na Kahawa, korosho etc.
Dallas, making Tanzania proud!
Pametulia.. hongera sana
ReplyDelete....eeehe bwana eehe!!msisahau wali wa nazi,maharahage ya nazi,njegere za nazi,bamia,misumari aka anchovy aka dagaa ,ugali na n.k lazima nishuke dirty south kUwapa support mdau hapa JERSEY CITY.tumechoka kupigwa bao na wakenya hapa state.
ReplyDeleteHii ingekuwa bongo mambo yangeenda mswano. Hapo bongo hakuna self-service katika migahawa.
ReplyDeletem3
Safi sana hii. Natumaini huu mfano utaigwa katika miji mingine yenye wabongo wengi.
ReplyDeletebig up guyz. mnaweza omba ushauri wa customer service kwa mzee gado 79 london road. juu huwa anatufikisha saana. kuanzia ksport channels, fruit shoot kwa watoto, pool table, red wine ugali amarula, na promotion za hapa na pale like happy hour juu wabeba box huwa wanaanza kutoka out kunzia saa tano usiku. unless kuna mpira or... kama nilivosema mtafuteni mzee gado atawapa marizi yote ya kuvuta wateja.chooni usiajiri safisha mwenyewe. ndo siri ya mgahawa good luck guyz
ReplyDeletendugu zangu mnakumbuka ile story ya "cat cat cat" sasa mleta habari za hapa anatupa nyengine chiken badala ya kitchen. safi sana!
ReplyDeleteDah!mi nataka ugali na matembeleee vipo hivyooo.
ReplyDeleteuji jamani upo
ReplyDeleteSafi sana, pametulia mwanangu, je? kuna ugali, ngogwe na bamia la kupwaza. Nitatia timu washikaji.
ReplyDeleteKijiweni big up sana kama wadau waliopita naomba tuwasupport sana hawa kijiweni waweze endelea hasa kwa sasa kwani ndio kwanza wamefungua hii sehemu Pls let surpport our brothers & sisters
ReplyDeletehongera sana.
ReplyDeletewe anony wa saa10:02 unanishangaza
ReplyDeletekwani uko bongo ipi jamani mbona sasa bongo mambo tambarare hebu nenda hapo nyumba ya sanaa au we ndo wale wabeba mabox mlio bobea huko tangu mtoke huku nineteen kweusi unafikiri bado tuko nyuma masehemu kibao kwa kwenda mbele hebu rudi home . na kama uko dar hebu uwe mtokaji during week ends ujionee mwe . no hard feelings
wewe cynthia hao kina rose zainabu eda n.k hawaishi dallas wako houston, usidakiye issue za watu kama hujui
ReplyDeleteCongratulations!! Sasa basi Waswahili lets make sure tunawasupport wenzetu kwa kwenda na kujichana kwa nguvu. Hope business is good and wishing you luck and much success.
ReplyDeleteAkilimali.
Hongera! Umeleta nyumbani karibu.Tutakuja kula nyma ya ku Choma! Ashante.
ReplyDeleteNoman Kassam,
Lewisville, Texas
Hingereni sana na nawatakia kila la heri
ReplyDeleteswali moja-nyama munazotumia ni za halali ama za inakuwaje?
Ambassador
IMETULIA LAKINI UGALI WA MUHOGO NA MCHUNGA UPO PIA MSISAHU KUTUWEKEA MLENDA NA NGURU/PAPA MKAVU NA MAJI YA MADAFU, MIE NAOMBENI TENDA YA KUTENGENEZA TOGWA!!!
ReplyDeleteHii ipo shwari si utani.Na inasaidia si tu kwa sisi sote tuliopo maeneo ya karibu (kwa Obama), bali pia kuitangaza nchi yetu kwa vyakula vyetu asilia!!!. Lazima nishuke hapo walau kwa andazi na chapati fulani za kaharage kanazi.
ReplyDeleteJuzi tu nilikua hapo DFW nikisubiria connection yangu nikaona tangazo la tourism in Tanzania, nilifurahi sana, hapo nilishaliona kama hilo pia kwenye TV.
Usikonde mdau, utapata wateja kwani mambo ni polepole tuu.
Tena ukiweza jitangaze kwenye vijitabu fulani vya mji wa Dallas kwa wageni wote.
Na ushauri wa bure ndo huu: hapo chini ya Swahili Restaurant Ongezea An East African or Tanzanian Flavor"
kama ndo moto of your business!!!
Mambo yako safi sana ndani ya Kijiweni. Sisi wakazi wa Dallas twanufaika na Menu hatari kweli kweli. Jana tuu nilitapa pilau kubwa lenye nyama kibao, ndizi za kupikwa, wali wa nazi & nyama rojo, mchicha na mihogo ya kukaanga (chips dume) bila kusahau chachandu. Yote hayo kwa $7 tuu. Hata Mc Donald's Menu got notin' on Kijiweni. Kula kubwa hadi nikasaza. Chapati na maandazi yametulia tuliiiiii. The ONLY challenge I have to all wabongo Dallas na maeneo ya karibu, please tujitokeza kuwasupport wenzetu basi ili nasi tuwe na kitu cha kujivunia. Cha ajabu ni kwamba Wakenya, Waburundi, Wazaire, na Waganda wanatuzidi kwa mahudhurio Kijiweni. Go support mtu wetu wa nyumbani people!
ReplyDeleteMerry Christmas and a joyful 2009 to all.
Nimefurahi sana kuona watanzania nasi tuna restaurant yetu.Kila nikipata kideti,nilikuwa nikielekea Ethiopian Restaurant badala ya kwetu Tanzania.Niko mbali na Texas,lakini nitatembelea kwa kupata msosi wa nyumbani sio burgerKing kila wakati.Ongeleeni saaana waanzilishi.Mimi nawa-support asilimia mia moja.
ReplyDeleteChakubanga
Mungu akupeni mafanikio mazuri lakini muandishi kuna kosa na uandikaji katika sehemu moja ya chakula ANDAZI NI MOJA yakiwa mwengi Huitwa MANDAZI huwa sio andazi tena tusaidiane lugha kubwa hii
ReplyDeleteBy yunus
Hii ni nzuri sana nawapongeza hao watanzania wa Dallas, wengine wafuate huo mfano.Watanzania tuachane na dhana ya kwenda Ulaya au Marekani kutafuta kazi tuende tukaanzishe kazi na kuajiri wengine, namna hiyo tutafanikiwa sana!
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania.