wakazi wa nyangoto katika maeneo ya mgodi huko tarime
sehemu ya umati mgodini hapo
umati katibu na mgodi

mgodi
magari ya askari yakiwa mgodini
ffu wakiwasili kutuliza ghasia hizo

trekta likiteketea baada ya kupgwa moto
Na Makubo Haruni, Tarime
POLISI wa Kituo cha Nyangoto Kata ya Matongo wilayani Tarime wamempiga risasi na kumuua mkazi wa Kijiji cha Kewanja, Hezron Mwita Magwena (35) ambaye anadaiwa kuwa ni mmojawapo wa watu zaidi ya 200 ambao walivamia mgodi wa Nyabirama unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick.

Katika uvamizi huo magari na mashine za kuchimba dhahabu zenye thamani ya Sh bilioni 16.6 vilichomwa moto na wavamizi hao.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Deus Katto alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11 jioni. Alisema wavamizi hao wanadaiwa kutoka katika vijiji mbalimbali na walikuwa na silaha, mbalimbali za jadi.

Katto ambaye ni Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa ameeleza kuwa, watu hao walifanya uvamizi huo baada ya kupata taarifa kwamba, Kampuni ya Barrick ilikuwa imejiandaa kulipua kwa baruti mawe ya dhahabu na kupeleka kiwandani kwa ajili ya kuyasaga.

Alisema watu hao waliwatimua walinzi wa mgodi na kuzamia machimbo hayo ya Nyabirama, Nyamongo na kusababisha kampuni hiyo kuomba msaada wa polisi ambao licha ya kuwataka waondoke kwa amani na baadaye kupiga risasi hewani, wananchi hao waliwashambulia kwa mawe na kujeruhi askari wanne.

Moja ya risasi hiyo ilimpiga tumboni marehemu na kufariki papo hapo. Kamanda huyo alisema polisi waliofika awali walizidiwa kabla ya kuitwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia.

Hata hivyo Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Barrick, Tewel Tewel akizungumza kwa njia ya simu, alisema kuwa, watu hao wameharibu na kuiba vifaa mbalimbali vya mashine ya kuchimba dhahabu iitwayo Loda, mashine mbili aina ya shavo RH 70 na RH 120, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto mashine nyingine ya kuchimba dhahabu uharibifu ambao umeitia hasara Kampuni ya Barrick dola za Marekani milioni 16.6.

Kwa mujibu wa Tewel, uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na baadhi ya watu hao wengi wao wakiwa vijana, wakiwa na kila aina ya silaha za jadi umefanya mgodi wa North Mara kufanya kazi katika mazingira magumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. hawa watu wanavijiji sio wendawazimu. Lazma kuna sababu hivyo kwa maoni yangu inabidi kupata ushauri kutoka kwao. Sio haki kwa askari mwenye silaha kumwuua mtu/mwananchi asiye na silaha hivyo kwa maoni yangu huyu askari lazma achukuliwe hatua na afikishwe mahakamani. Hii si kama yaliyotokea huko Ugiriki hivi karibuni???

    Malisa BG

    ReplyDelete
  2. Mie sioni tatizo mtu anapodai chake, haya madini yapo mara lakini watu wake ni masikini wa kutupwa. mi nashauri wazawa wanaokutwa eneo la mgodi wakihamishwa wapewe share ya kumiliki mgodi.

    ReplyDelete
  3. bwana malisa wewe hawa waliyanchoka huwajui wewe
    akili hawana hawa panga njenje tu
    wanadhani wanavyopiga wake zao ndio hivyo hivyo watapiga na kuchoma moto mali za watu
    hawa wawekezeji japo wanatudhulumu lakini wapo kihalali na wanalipa kodi , ngoja watandikwe risasi na ualiyanchoka wao

    ReplyDelete
  4. There are some reasons behind that faracas, they are not just bunch of crazy people, the government must do deep reasearch on that. One of things could be a reason for that is, as people of that area they don't see the advantage of that investment, the profit,commission/tax government gets from that ends to the central cofer of the government and building Osterbay Roads only insted of giving back to them, not all of the money but even some of it by improving their ways of living such as health, roads, education, water, agriculture improvements, fishing improvement, modern housing even by loans/mortgages. So the government as well as the Company/Barrick have social responsibilty on the people around.

    ReplyDelete
  5. Usitutolee mifano ya wagiriki kwa wavuta unga na wadandia meli huko,japo zoezi la uvamizi nimelikubali

    ReplyDelete
  6. Hii na bado Yatatokea mengi kama haya, Wakurya Hawawezi angalia mali yao inachukuliwa hivi hivi tena na watu ambao wanasafilisha hadi Michanga kwenda kwao , hawatoi hata ajira kwa wazawa wa eneo husika, hii ni mwanzo tu, Bado Wasukuma, Na huyo asikari lazima sheria ichukue mkondo wake, nini maana ya asikari na kwenda mafunzo , kuna njia nyingi za kutumia kuzibiti fujo siyo kuua, Wakurya kweli Mwisho endeleza mwende huohuo .

    Mtoa maoni

    ReplyDelete
  7. lazima kuna jambo hapo.na haiwezekani wananchi wakaaribu mali ya thamani kiasi hicho bilion dollar?hat siamini ni utata mtupu.

    ReplyDelete
  8. nawaunga mkono hao waliovamia mgomo,na siungi mkono mtanzania kiumuua mtanznia mwenzake kwa mali za wazungu,polisi wanatukumbusha askari wa afrika kusini kipinde kile walivyoua waafrika wenzao.nashauri wote waliokaribu namigodi kufanya hivyo wanpopata taarifa za mawe yenye mali.pole kwa wafiwa ,huyo kafia nchi.

    ReplyDelete
  9. Liwe somo, hakuna haja ya kufanya 'research' kila kitu kinajulikana. Nani asiyejua Serikali yetu haijawa makini kuhakikisha "win-win situation" ktk raslimali ya madini? Wameamua kujinufaisha wachache na sasa haya ndio matokeo. Watu wamelia mikataba ipitiwe na bado viongozi wameziba masikio. Hebu tusikie N/Waziri Malima atasema nini kuhusu hili maana wamazoea kuropoka hata pale wananchi wanapolalamika mambo muhimu.

    Libeneke lililoanzia Mara litaendelea sehemu nyingine za migodi mpaka hapo hao wawekezaji watakapohacha kutumia wanasiasa kuchota mali pasipo kunufaisha waTanzania.

    ReplyDelete
  10. Hata kama kuna watu wasiotaka kusikia kuhusu ugiriki kwakuwa ni kwa wavuta unga na wadandia meli lakini hii issue haina tofauti.

    Mimi nimetokea kijijini na tofauti yake ni kuwa huko kuna wadandia mabasi na malori na wavuta bangi basi.Lakini haki ya mtu haingalii huyu nani ni nani.

    Na haya yote ndio matokeo ya ufisadi wa viongozi wetu.Itafika wakati watu wakichoka zaidi wataziingilia familia za hao mafisadi na huu ndio ukweli wenyewe.

    Michuzi usibanie ujumbe huu kwakuwa si wa uchochezi.

    ReplyDelete
  11. Mmeng'enyo wa hayo yote: Wadau sikilizeni:

    1. Uwekezaji ni kuchuma, huku ukisaidia panapowezekana kimakubaliano a sio kubeba majukumu ya KIJINGA unayoyakuta hapo:

    Mimi naishi eneo hili, na machungu yake nayaona: Najua ni thamani kiasi gani migodi inawekeza kwenye maeneo husika. (Uwekezaji unaweza usiwe mkubwa sana wa kuonekana kwa macho kama jengo la ghorofa, lakini kusaidia jamiii kunaendana na makubaliano ki-mkataba,na mahusiano kati ya jamii na kampuni yanayoendelea kuwepo tangu kampuni inavyoanza uzalishaji. Jamii inaweza kupata usaidizi katika elimu, vijihospitali, maji, mifumo ya barabara, uokoaji wakati wa majanga, kusomeshwa wazawa, vijikodi, harambee na kulinda amani. Hapa huwa ni mapanga, mishale, kug'echa na kukomoana)

    2. Mbuzi kajibana machinjioni kwa pembe zake, kamba ya nini?

    - hawa wawekezaji walikuta mali zetu tunauza kama hivyo. hakuna cha mrahaba, wala cha ardhi mraba. Tukakubali - "Hewala mabwana, chukueni tu asilimia 100"! Iweje baada ya miaka zaidi ya 10, tuanze kusema wawekezaji hawatoi maeneo kwa wachimbaji wadogo? inaingia akilini kweli eti ukienda kununua shamba la mzaramo pale Kitunda, (ashakum si matusi),mkakubaliana bei , halafu uje kulaumiwa kuwa hukumwachia eneo la yeye kulima bustani!! Mbona watu tunaacha kuzungumza ukweli kuwa SERIKALI HAINA MIPANGO ENDELEVU KWA WATU WAKE. HAIKUPANGA KWAMBA WANANCHI WATAHAMIA WAPI, WATAKULA WAPI, WATAVUNA NINI.

    Serikali haijui kama watoto wa sehemu hizi watasoma, hakuna ajira mbadala zilizokuwa "created" ilik wakati madini yanaisha, basi vijana wawe wameibuka na SIDO, ujuzi wa VETA, biashara, Kilimo au Uvuvi. Tupo tupo tu!!

    3. Mtoto umleavyo... na utawala wa kanuni na sheria

    Tarime, kihistoria na kimapokeo, ni sehemu inayojulikana "eti ina wakorofi, eti inawatu hatari". Utwala wa sheria , utendaji wa mahakama na polisi ni mdogo, ISIPOKUWA wakati watawala wakiona kuwa karibia wananyamg'anywa ubunge au Udiwani. Simaanishi maaskari hawapo, lakini sehemu sugu kama hizi zinahitaji ulinzi, udhibiti mkali. Nakumbuka kwetu ilikuwa sheria
    a)- hakuna vijana kuonekeana ovyoovyo masaa ya kazi (1-8 mchana)
    b) - sensa ya mashamba inapitishwa na katibu kata, wenyeviti wa vijj -kila kijana aonyeshe mashamba aliyonayo, mifugo aliyonayo, biashara alizonazo na kodi alizolipa alipochuuza
    c) - mabaa, kumbi za disko au starehe hazifunguliwi hadi saa 11 jioni
    d) - anayekutwa tofauti na hayo - ni mboko na mijeledi, na kufikishwa kituoni kujibu au kufungwa uzurulaji, uzembe

    SOUNDS FUNNY?
    Sasa unategemea nini kama vijana wamekua wakiona baba anakuwepo home toa asbh hadi uck? Unategemea nini kama vijana utaona wanafungua biashara, wanaoa, wanamiliki magari , pikipiki etc bila kuanza kidogokidogo, au bila hata mishahara kutokana na kuajiririwa baada ya shule. Unategemea kweli mtoto athamini kazi, athamini shule, athamini bidii ya jamii, na athamini maendeleo? NEVER!! Unategemea wazazi waliotokana na mfumo kama huu wawe na la usema kwa vijana wao hao? Unategemea wawafundishe kilimo, uvuvi, ulinzi wa mali, thamani ya utu na kuheshimiana?

    4. Walaumiwe Wananchi vilevile

    Tarime ni sehemu chache Tanzania zilizobarikiwa (bado) kuwa na mvua za kutegemewa sana. Wananchi wa maeneo ya migodi nawabebesha lawama kwa kutojitambua kwao:
    - kubweteka na madini, kama vile hayatakuja kuisha ardhinio
    - kuharibu mali za wenzao (ikiwamo uharibifu kwa mali na mifugo ya watanzania wenzao). Hawa watu wanaharibu hata mifumo ya maji safi inayotoka migodini kuelekea vijijini kwa, kwa ajili ya matumizi yao wenyewe!!
    - kujifanya sisi "wakurya" bwana, hatuguswi, polisi/wawekezaji hawana cha kutufanya: hii inajenga kiburi na ujinga. Hebu fikiria: hata vitoto vya miaka 3, 5 hadi wazee wanavamia migodi. Hivi ni picha gani hii!

    Na mimi nina hasira ati!

    Wa kutukana nitukaneni!

    Dr

    ReplyDelete
  12. watu wamara wananifurahisha sana kwa umoja wao hawa wawekezaji njiwa si ndo mnao wafungulia mashtaka sasa? kuna kampun moja iko ubungo ya wazungu walivyo chuma na kuona wamepata faida wakataka kuanza bila kulipa kodi jamaa wa jk wamewadandia sasa hawana issu. ha hawa ni haoa hao tunao wakataa wataiiba weeeee halafu wanatuacha uchi unafikiri kwanini wakenya wanalilia kuja huku si mambo kama hayo na siajabu wameajiriwa kwenye hiyo migodi wacha wachome paka kieleweke

    ReplyDelete
  13. Dr. umeongea lakini mwishoni sijafurahiswa nawe , unafikili kulinda mali yako kunahitaji kua kijana au MZEE.

    ReplyDelete
  14. Nabado Mura, hii nimwanzo wakirudi tena! nutachoma za dola milioni 80, wakachimbe kwawasukuma sio hapa.

    arafu wewe anon wa 9:58,umetahiriwa kweli? mbona unaongea maneno kama mrisya(mwanaume ambaye haja tahiriawa) au musaghane(mwanamke ambaye hajatahiriwa).

    SASA WAAMBIENI NA BADO MPAKA KIELEWEKE! HIINCHI NI YETU AU YAWAMAREKANI!

    ReplyDelete
  15. ahahaaaaaaa mrisya au musaghane???weee MURA hujatulia kabisa,,,
    yan unaendekeza ukeketaji wa mwanamke??kweli kwenu mwanamke ni kifaa km jembe,ng'ombe,kapeti nk wal'hali hii kali
    sasa izo hasira then what!!!mboni mtachapwa risasi adi muishe,,ishu apa awa wazungu apo wanamiliki kisheria kbs na serikali na mafisadi wasiosoma mikataba kwa kutumia wataalamu wamewapa,,,ishu vitu viwekwe mezani au mijadala ionekane waaazi jinsi awa wazungu wanavokula kilainiiiiiii
    MURA ACHENI TABIA YA KUUA NA KUCHAPANA MWISHO TUTAWARUDISHA BUREE KENYA TUKIFIKILI NI WAKIMBIZI WA KIJALUO aka washashi
    ila uwa mwaniacha hooooiii ile mbaya na tamaduni yenu

    ReplyDelete
  16. HAO BARRICK WAONGO, HIYO MITAMBO NA UHARIBIFU MWINGINE HAUWEZI KUFIKA USD 15M, WATUAMBIE NI MITAMBO MINGAPI NA KILA MMOJA NI KIASI GANI, TENA INA MISAMAHA YA KODI, TUNAWEZA HATA KUULIZA MANTRAC, WAMEPATA PA KUKWEPEA KODI AMBAYO HATA HAWALIPI.

    HII NDIO SPIRIT, WATU WASIPOPEWA CHAO HUKICHUKUA, ITAFIKA PAHALA HATA HAO ASKARI HAWATAKUJA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...