KAMATI YA RUFAA YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU (TFF) LEO IMETUPILIA MBALI RUFAA YA MICHAEL RICHARD WAMBURA (PICHANI SHOTO AKISALIMIANA NA MH. PROFESA KAPUYA) ANAYEWANIA NAFASI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA CHAMA HICHO. UCHAGUZI WA TFF UNAFANYIKA KESHO KWENYE UKUMBI WA NSSF WATERFRONT.


KWA MUJIBU WA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO, JAJI JOHN MKWAWA, IBARA YA 12 (6) YA KANUNI ZA TFF HAZITOI FURSA YA RUFAA, AMBAPO NDIO KUSEMA WAMBURA SASA AMETOLEWA RASMI KATIKA MTANAGE HUO.


KAMATI YA UCHAGUZI ILIKUWA IMEMUWEKEA KWA SABABU KUU ZA MSINGI MBILI.


1. KUSHINDWA KUKABIDHI OFISI MPAKA LEO HII AKIWA KAMA KATIBU MKIUU WA FAT KWA KIPINDI KILICHOMALIZIKIA MWAKA 2004.


2. KUTOTOA MAELEZO KWA BAADHI YA MAMBO YA MSINGI KATIKA RIPOTI ZA MAHESABU ZINAZOHUSU MWAKA 2002, 2003 NA 2004.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Uongozi hauwezi huyo. Toka 2004 hujakabidhi office ya watu. Alizania ni permanent secretary?

    ReplyDelete
  2. Jamani hapo mimi ndipo ninapochoka na viongozi wa Tanzania.Iwe wa ngazi ya chini au ya juu. Mtu hajatoa taarifa inayoeleweka, miaka mitano imepita hakuna hatua zinazochukuliwa. Na taarifa yenyewe ni ya michuzi. mnamngojea kwenye uchaguzi ili mumuengue. Kwanini taratibu za kisheria zisifuatwe huyo mtu akafikishwa kwa Pilato ili akatolee maelezo yake huko?. Haya mpaka leo mnasema ameshindwa kukabidhi ofisi ina maana ninyi mliingia ofisini kwa kuvunja mlango au dirisha sio!. Watanzania tuache kulindana. Au mnajilinda ili na nyie mtakapokuwa mnaachia ngazi msisumbuliwe? Tusipoangalia tutaangamizwa kama wafuasi wa Kibwetele.

    ReplyDelete
  3. Hivi we mtoa maoni ya pili, unadhani kukabidhi ofisi maana yake kukabidhi funguo?! Mbona kazi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...