Asalaam aleikum kaka Michuzi,
naomba unisaidie kutangaza kwenye blog yako. NAMTAFUTA RAFIKI YANGU KIPENZI TULIYESOMA NAYE SHULE YA SEKONDARI AL-HARAMAIN MWAKA 1996-1999 ANAITWA MARIAM MBARUKU.
MARA YA MWISHO KUONANA NAYE ILIKUWA KWENYE MAHAFALI YA KUMALIZA KIDATO CHA NNE, MUDA MFUPI TU BAADA YA KUMALIZA SEKONDARI MIMI NILISAFIRI KUJA MAREKANI, NA YEYE AKAENDELEA NA MASOMO HAPO NCHINI, SASA NASIKIA YUKO BARA LA ULAYA.
KAMA ANASOMA BLOG HII YA JAMII AU KUNA MTU ANA ANA TAARIFA ZAKE NAOMBA ANITUMIE KWENYE EMAIL YANGU HII HAPA CHINI
Ndimi ,
Amina Salum,
Manhattan,NY.
-------------------------------------------------
Hi michuzi!
kwa mara nyingine naomba usinitupe kapuni.
Nina rafiki yangu mpendwa sana nimepotezana naye yapata miaka 15 iliyopita tangu tulipokuwa kibaha sekondari, nimefanya juhudi kumtafuta bila mafanikio, p'se, p'se naomba kupitia blog hii uniwezeshe kumpata huyu bwana. na kama kuna yeyote anayefahamu alipo naomba tuwasiliane.
jina lake ni JOHN PETER MACHA
ASANTE.
FRANK - MBEYA
email
chancefa@gmail.com
--------------------------------------------------------
Mimi Naitwa M Namtafuta rafiki yangu anaitwa JOYCE YACOB MSANGA ambaye tuliachana baada ya kumaliza shule ya msingi Mbuyuni.
Nilisikia mara ya mwisho alisoma Chuo Kikuu hapo Dar es salaam Tanzania na baadaye alisoma Chuo cha CBE naomba kama kuna mtu anamfahamu anitumie email au namba zake za simu kwa kutumia email yangu ya
vsltd@yahoo.com au masqtz@yahoo.com

Kwasasa nimeambiwa anaishi Temeke kwa wazazi wake kwani wazazi wake wamehamia Dar es salaam baada ya kutoka Tanga

Asante Issa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. MICHUZI NAONA MDAU WA 5,000,000 KARIBU ANAPATIKANA, MIMI NAINGIA KWENYE BLOG YAKO KILA SIKU KUTOKA ULAYA KWA JINA LA ANONY SASA UTANIJUWAJE KAMA NIKIWA WA MILIONI TANO, NA MKWANJA WANGU UTANIPATIAJE?

    ReplyDelete
  2. Hallow dada,eleza vizuri mimi maryam mbaruk ninaye mfahamu ana pacha wake anaitwa mwajuma sasa kama ni hao wako Japan sasa,eleza zizuri tukupe data

    ReplyDelete
  3. NNIO MIMI NA UNIKOME KABISA , KUNITAFUTA KWENYE MABLOGU . NINAMAISHA YANGU MOVE OWN . I NEED PRIVACY

    ReplyDelete
  4. Hahahahaha Manhattan, NY ...hehehhetttt.....wabongoooooooo

    kama ni wewe ninayekufahamu sina mbavu .......

    ReplyDelete
  5. Hii mambo ya kuwekana kwenye blog majina ya watu mweeee sio mazuri....Kwanini mtafutaji usijieleze tu wewe na useme unatafuta rafiki yako mlisoma naye shule fulani mwaka fulani na kuweka information zako tu....na kama she/he was your real friend ata kucontact....

    Watu wengine hupenda privacy....na rafiki wa miaka 15 iliyopita kama hamkukeep contact muda wote huo ....ni taabu tu....watu wamekua , maisha yamebadilika, majukumu yamebadilika....sana sana kumtaja yote mtu huku kwenye blog ukishampata itakua email au simu si zaidi ya nne na hata mkikutana ....ni tofauti sana...THINK ABOUT THIS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...