kivuko kipya cha mv magogoni kitaanza libeneke la kusafirisha watu, magari na mizigo kwenda na kutoka kigamboni hivi karibuni. kina uwezo wa kubeba abiria 1,000 na magari zaidi ya 50

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. sasa kitabeba watu 2000 waweke watu kwa hesabu angalau wafanye watu 800 na magari 40 sababu zisije kuingia gari nzito iwe angalau na kila mwisho wa mwezi iwe inachunguzwa uzima sio mpaka ije kusimama katikati ndio mjue kamba mbovu, mungu amzidishie aliyeleta hiyo MV na zitokee na zingine na Usafiri wa ma UDA makubwa yarudi sasa Dar-es-salaam.

    ReplyDelete
  2. michuzi naomba uwe unachanganuamambo unayoyasema,ukisema watu 1000 sawa sasa hayo magarini 50 ni ya aina gani na uzito gani,wengine wanafikiri ni magari ya aina yeyote?sasa subiri watapakia watu 1000 na scania zakuvutana 50.balaa aa!

    ReplyDelete
  3. Kaka Michu, nipo nje ya nchi kwa hizi sasa, ila kama my memory saves me right, "Mv Magogoni" si tulikuwa nayo (as a matter of fact, this one appears very similar in shape/design). Nimeona nuuliza maana para yako inasomeka "kivuko kipya....": Nakumbuka vivuko vingine vilikuwa na Mv Alina (kadogo hivi, nafikiri kilikuwa na rangi ya Chungwa), Mv Usiwe Kupe. Naomba ufafanuzi. Mr GM

    ReplyDelete
  4. tupanuwe ubongo tuondokane na usingizi! sisi tunataka daraja! mambo ya felna viunginevo vyote ni rushwa tu! jenga DAraja watu wapite mda wote wawezavyo, si leo fel mbovu, isotoshe ni mbovu na ni rangi tu imepakwa! subiri abiria mtakapo zama ndo mtajua!! kazanieni daraja! amka mwananchi acha piga usingizi! jaribu kuona mbali!

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi

    Napongeza hatu hii madhubuti. Serikali imejitutumua katika hili. Sasa kigamboni angalau hapo ferry tutakuwa tunateleza.

    Mtazamo wa pili ni kwenye taswira: Nimevutiwa sana na uhai uliopo katika taswira. Hao watoto wametokea vyema na kuipamba taswira vyema.

    Wasalaam

    ReplyDelete
  6. Wadau samahani naomba kuhama kwenye mada husika nihamie kwenye ishu ya hukohuko Kigamboni. hivi karibuni Serikali ilitoa tangazo kuwa shughuli zote za ujenzi zimesimamishwa,upimaji na utoaji hati Kigamboni zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa madai kuwa inataka kuigeuza kigamboni kuwa mji wa kisasa unaojitegemea!!!

    Wadau hii inakera na imetibua mipango ya watu wengi sana tuliowekeza huko, inakera zaidi kwa sababu wengi wetu hatukukurupuka na kuanza tu kujenga bali tulipia taratibu zote za kiserikali na tumejenga kwenye maeneo ambayo yapo planned as residential area. Serikali kwa miaka mingi sasa haswa DSM imekuwa ikidhulumu ardhi za watu na kuziuza kwa watu wengine kama viwanja vilivyopimwa huku wamiliki wa awali bila kujali ardhi zao walinunua kwa pesa ngapi wakilipwa pesa ndogo kupita kiasi na kwa staili ya dhulma dhulma. Wadau mnazungumziaje dhulma hii inayofanywa kila kukicha na serikali yetu kwa uongo wa kuboresha mipango miji? nafikiri imefika wakati tuanze kupinga hii sera ya ardhi ni mali ya serikali hii ndio wanayotumia kutudhulumu ardhi kwa kutlipa mazao peke yake bila kujali tumenunua ardhi hiyo kwa pesa ngapi

    ReplyDelete
  7. DU HIYO PICHA, KUMBUKUMBU NZURI SANA KWA WATOTO HAO.

    ITAKUJA KUWA KUWAKUMBUSHA BAADAYE MAISHA YA UTOTONI.

    KAMA WATAKUWA NA SHIDA AU RAHA HIYO PICHA ITAKUWA INAWAPELEKA MBALI SANA NA KUTAMANI ENZI HIZO AMBAZO WAKO SASA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...