HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA MZEE GEORGE KRITSOS, YULE MWENYEKITI MSTAAFU WA KLABU YA GYMKHANA NA MMILIKI WA SHELI YA GAPCO ILIYOVAMIWA NA MAJAMBAZI LEO ASUBUHI PALE MAGOMENI MAPIPA HAJAMBO NA AMERUHUSIWA KWENDA NYUMBANI BAADA YA MADAKTARI KUMHUDUMIA MAJERAHA YA RISASI.
INASADIKIWA MZEE GEORGE ALIPIGWA JUMLA YA RISASI MBILI, MOJA ILIINGIA BEGANI NA KUTOKA UPANDE WA PILI, NA MOJA BADO IMEBAKI NDANI. INASEMEKANA WALILENGA USONI, AKANUSURIKA KIFO KWA KUDRA YA MWENYEZI MUNGU...
NIMEONGEA NA MTU ALIYE NAYE KARIBU MUDA HUU NA KANIHAKIKISHIA KWAMBA HAJAMBO NA ANAENDELEA VIZURI, ILA MOYO UNAMUUMA SANA KWA KIFO CHA MHASIBU WAKE AMBAYE ALIPIGWA RISASI NAYE WAKATI WA HUO UPORAJI.
MZEE GEORGE KRITSOS PIA AMETOA SALAMU ZA SHUKRANI KWA WADAU TOKA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI AMBAO WAMEKUWA WAKIMPIGIA SIMU KUMJUA HALI TOKA GLOBU YA JAMII ILIPOTOA BREKING NYUZZZ YA KUVAMIWA KWAKE.
ANASEMA INAGAWA ANAOMBOLEZA KIFO CHA MHASIBU WAKE, LAKINI ANAFARIJIKA KWA MOYO WA UPENDO AMBAO WADAU MMEMUONESHA KWAKE, NA ANAWAOMBEA AFYA NJEMA.
GLOBU HII YA JAMII INAMTAKIA MZEE GEORGE KRITSOS UNAFUU WA HARAKA NA KUMWIMBA MOLA AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU MHASIBU WAKE ALIYETANGULIA MBELE YA HAKI - AMINA
Kaka mpe Pole mzee George,mwambie nampa pole kwa Kigiriki,PERASTIKA..
ReplyDeleteMdau Ugiriki
KAKA MICHUZI USIOGOPE KUAMBIWA NA WEWE MICHUZI NI MBEYA HIYO LISASI YA BEGANI KUTOKEA UPANDE WA PILI UMEIONA? KAMA KUNA RISASI IMEBAKI NDANI KWA NINI KARUHUSIWA KWENDA NYUMBANI? HUYO MTU KWELI AMEJERUHIWA AMA NI UMBEYA WAKO TU? JUNOLISTI MZIMA UNATAKIWA KUTUPA VITU VYA UKWELI SIYO LONGOLONGO. HALAFU UTAIBANIA HII COMENTI ETI NIMEKUTUKANA? LA ASHA NIMEKUPA VIDONGE VYAKE!
ReplyDeletePoleni sana. Je tunaweza kupata jina la huyu mhasibu wake? maana ukisema mhasibu pake yake haitoshi kufahamu. Labda naye tunamfahamu au anatuhusu.
ReplyDeleteTunashukuru kwa updates za nyumbani.
Mdau
Mashariki ya mbali.
Pole sana
ReplyDeletemzee kristos,jamani ninaswali hivi huyo kristos
ndo baba yake na Evelyn kristos
kaka Michu tunaomba jina la Marehemu, mzee Kristos tunashukuru kapona lakini haitakuwa haki kama hatutamtaja marahemu kwa jina na kuishia kumuita tu mhasibu wake nadhani kama ambavyo tunalitaja jina la mwajiri wake na la marehemu ni rahisi kulipata pia. Asante mdau ughaibuni.
ReplyDeleteHuyo mzee yeye ni robot nini anaeweza kutembea na risasi ikiwa bado ipo mwilini mwake?acheni mzaha mie nahisi hata kuibiwa basi atakuwa labda hajaibiwa pia kwa style hii
ReplyDeleteNdugu Balozi Michuzi,
ReplyDeleteNakushukuru kwa kutupa habari za ndugu Kristos na tunampa pole sana.
Nasikitika kusema kuwa baadhi yetu bado hatuwezi kuandika maoni bila ya kutoa mtusi ya nguo na naomba urudie tena kubana maoni ya wadau kama hao.
Mimi nilikuwa mmoja wa wadau hapa waliokupinga ulipokuwa unabana maoni lakini sasa nitakuunga mkono kama ukibana maoni hasa yanayokukutukama wewe binafsi kama ya 4:02 hapo juu. Usilazimike kuchapisha maoni yanayokuita mmbeya. Tunakuunga mkono kama utawabana wadau kama hao wasiokuwa na shukurani na kazi unayoifanya hapa.
Aluta Kuntinua.
Hi Michuzi,
ReplyDeletePole kwa kazi.
Mimi napenda tu kukusahihisha. Nafikiri watu wengi sana hapa kwetu hawajui maana ya "shell" na badala yake wamekuwa wakilitumia hili neno (ikiwa ni pamoja na wewe) kumaanisha "kituo cha mafuta". Ninavyojua mimi vyote vinaitwa "vituo vya mafuta" lakini makampuni ni tofauti. Kwa mfano: Kituo cha mafuta cha Total, Kituo cha mafuta cha Oryx, Kituo cha mafuta cha BP nk. Hii kituo cha mafuta cha shell kilikuwepo zamani huku kwetu lakini kwa sasa hakuna tena, ila nchi nyingine kama vile Kenya na Uganda ambapo mimi niliwahi kuzitembelea bado zipo.
Ni hayo tu mzee.
Ila hakuna kitu kama "Shell ya Gapco".. Ahahahahhaa...
Kazi njema mzee na pole kwa wahanga wa tukio la jana la ujambazi.
wewe kabwe unadhani kila ukiongea utapata umaarufu? hii inaonesha hata huko bungeni hauko serious mimi nilikuwa nakuamini sana lakini hii coment uliyo weka inaniogopesha kabisa. sasa matusi ya nini humu unakuwa sawa na masha sasa. mimi nilikuona mwelevu lakini haya matusi nakuogopa sasa
ReplyDeletewatu kama KABWE ndiyo wale walio na roho za "KWA NINI!"
ReplyDeletetutafika kweli tukiwa na watu kama hawa?
He tayari mmeshajua ni Kabwe wa Bungeni? mmm...mapema mno jamani, embu muwe mnajaribu kuuliza basi ni kabwe gani sio tu kuponda, ooo kama masha, sijui nini huko. Mnaudhi kweli sometimes wadau wenzangu
ReplyDeleteHawa wezi yawezekana kuna mkono wa askari dezaini ya zombe .Sadi kazi kwako. Wameshajua hata zombe yawezekana akatoka, hivyo kuna uwezekano mkubwa akawa ni askari tu.
ReplyDelete