SINA NIA YA KUWAHARIBIA SHEREHE KWA KUTUNGIKA PICHA HII YA KUSIKITISHA MMOJA WA ALBINO ALIYEKATWA MIKONO NA WATU WASIOJULIKANA WANAOSADIKIWA WANAFANYA HIVYO KWA IMANI ZA GIZA.
HII NI MCHANGO WA GLOBU YA JAMII KATIKA KUTAKA KUPATA UFUMBUZI WA JANGA HILI LA TAIFA KWA NJIA YA KUPATA KUPATA MAONI YA WADAU.
WAKATI GLOBU HII YA JAMII INALAANI VITENDO HIVYO VYA KINYAMA, INAULIZA JE KIFANYIKE NINI ILI KUKOMESHA UKATILI NA MAUAJI DHIDI YA ALBINO WASIO NA HATIA?



KWA MAONI YANGU MIMI NAONA KWA ATAKAE KAMATWA NA HATIA HIYO NI BORA KWANZA ACHANJE MWILI MZIMA NA VIWEMBE KISHA APAKWE PILIPILI KICHAA AU MBUZI KISHA AKATWE NA YEYE MIKONO KISHA MIGUU NA MWISHO KICHWA CHAKE AONE UTAMU ULIVYO
ReplyDeleteKuna mapungufu kwenye intellegence ya Taifa....Yanahitajika mabadiliko makubwa kwenye uongozi, mbinu na mikakati ya kiusalama wa Taifa kwa kushindwa kujua ni akina wanahusika na mauaji haya. Kama Wizara ya mambo ya ndani imeshindwa kupata ufumbuzi wa hili basi ni bora waziri awajibike ikiwemo kujiuzulu...
ReplyDeleteJamani, I think sisi as a society tunalifumbia macho hili jambo ambalo ni aibu kwa Taifa as far as I am concerned. Our fat leaders need to get of their lazy backsides and sit down as a Cabinet to seek a solution to this crisis. I would like to apologize to our Albino brethren for us as a nation not doing enough to address this matter. Shame on us!!
ReplyDeleteMdau, Boston, US.
Inabidi Serikali ya Tanzania iwatenge albino wote waweze kuishi sehemu moja na pia wapatiwe ulinzi
ReplyDeletehawa ni watu kama watu wengine.
bro michuzi kweli hili swali nalo sheria zipo wazi,mtu anaeua inajulikana adhabu yake akithibitika kaua,sasa maswali ya nini kifanyike yametoka wapi tena? au kwa kua ni albino ndio hatujui nini kifanyike.
ReplyDeleteHERI YA KRISMAS MR. MICHUZI NA WADAU WOTE WA GLOBU HII..
ReplyDeleteKwanza kabisa haina ya kutuomba msamaha kwa kutuharibia sikukuu kwa sababu umeweka hii picha.. Sisi ni binadamu na uchungu hauna sikukuu wala siku maalumu. At anytime, mtu unapatwa na hisia huzuni ukiona unyama wa aina yoyote unatendwa kwa binadamu anayestahili haki zote kama Binadamu wengine. Hawa ALBINO ni Binadamu kama sisi wa ngozi nyeusi. Haki zetu ndio haki zao!
Pili, Ni vizuri kabisa umetuwekea picha hii ya kuhuzunisha wakati kama huu ili tuweze kufungua mioyo yetu na kuona jinsi tunaweza kuishi bila ubinafsi tuliozoea.. Ni wakati wa kuwafikiria wenzetu ambao hata kwa mapungufu yao lakini bado ni BINADAMU.
Tatu, Serikali inavyochelewa kuwachukulia hatua hao wanaosababisha mauaji ya ALBINO na mateso mengine yasiyosimulika, JE ingependeza kama wananchi wangechukua sheria mikononi na kuanza kuwaadhibu wauaji hawa? Na wao wachinjwe, wakatwe viungo vya miili, wauzwe kwa waganga etc...?
HALI INASIKITISHA SANA MR. MICHUZI...
Haya yanatokea katika nchi ambamo watu tunajifanya tuna dini sana, nchi ambamo mikutano, mihadhara, nyimbo, ngoma, maandamano na shuhguli za kidini zinaendelea usiku na mchana na zinazidi kupamba moto. Hapo hapo, ufisadi, uvunjwaji wa haki za binadamu, na ukatili kama huu wa kuwaua watu au kuwakata viungo unashamiri muda wote. Ni nchi ambamo elimu inazidi kudidimia na ujinga unazidi kuenea na kuota mizizi kila siku.
ReplyDeleteJe, ni nani aliyetufundisha Watanzania kuwa ili tufanikiwe katika biashara, ni lazima tumchune mtu ngozi au kumkata viungo?
Huku Marekani kuna vitabu vya kila aina vinavyotoa elimu kuhusu biashara. Kuna semina, warsha, na makongamano kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa biashara na huduma mbali mbali. Watu wanatumia hela nyingi kununua vitabu hivyo na kulipia semina hizo. Nami, kwa kujiongezea elimu, huwa nanunua vitabu vya aina hiyo, na nimewahi kutumia hela nyingi kulipia semina, kwa vile nijikongoja katika kuunda taasisi ya kutoa ushauri na elimu ("consultancy.")
Ninajifunza mengi kutokana na hivi vitabu na semina. Kitu kimoja ambacho nimejifunza ni kuwa ukiwa na biashara, kampuni, au taasisi, umjali sana mteja. Ukimridhisha mteja akafurahi, ujue kuwa huyu ataenda kuwa mpiga debe wako mkubwa. Atakutangazia biashara au huduma yako na kukuletea wateja bila wewe kuingia gharama ya utangazaji. Na ukimridha na kumfurahisha kila mmoja wa hao wateja, nao watakutangaza kwa wengine na kukuletea wateja zaidi. Biashara au huduma yako itastawi kwa namna hiyo.
Hili somo linaonekana kuwa si la ajabu, lakini kwetu Tanzania wengi au hawalielewi au hawalizingatii. Wanaanzisha biashara au huduma, na hawajali kama mhudumu wanayemweka hapo ana tabia njema ya kuhudumia vizuri wateja, au kama ana ufahamu wa saikolojia ya wateja.
Kitu ambacho nimejifunza kwenye hivi vitabu na semina nilizotaja ni kuwa ukimwudhi mteja, ataenda kueneza habari mbaya juu ya biashara au huduma yako. Wewe mwenyewe utakuwa umeihujumu biashara yako. Na kila mteja mwingine atakayekuja na kukosa huduma nzuri ataenda naye kueneza habari mbaya juu ya biashara au huduma yako. Ndio maana unatakiwa uwe mwangalifu sana unapompata mteja.
Wakati wenzetu wanatafuta elimu na ujuzi wa namna hiyo, sisi Tanzania tukianzisha biashara au huduma, tunatafuta ngozi au viungo vya binadamu. Inashangaza kuwa hatuelewi jambo hili la msingi: kwamba siri ya mafanikio ni ubora wa bidhaa, ubora wa huduma, kumridhisha na kumfurahisha mteja.
Je, wakati mataifa mengine yanajizatiti kwa elimu na ujuzi, ili kushindana katika dunia ya leo ya utandawazi, sisi tutaweza kweli kushindana kwa kutumia mizizi, ngozi, au viungo vya binadamu?
Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya, pamoja na kuwa picha hii inasikitisha sana, umefanya jambo jema kuiweka hapo. Tunatoa pole kwa hao binadamu wenzetu waliofanyiwa ukatili huu, lakini pole haitawarudishia uhai wale waliouawa, wala haitawarudishia viungo mwilini wale waliokatwa viungo. Tunachotakiwa kufanya kuutafuta mzizi wa matatizo hayo na kuutokomeza. Nategemea picha hii itachangia kuamsha hisia na fikra zitakazotusaidia kutokomeza ujinga na ukatili huu, kutokomeza huu ukiukaji wa amri za Mungu na haki za binadamu.
Mkuu wa Wilaya ya naniino! Hiyo picha inaweza kusema mengi sana kuhusu nchi yetu; lakini sidhani kama wadau wanaweza kujadili uzito wa jambo hili. Haya mambo ya siasa ni ya sisi wanakijiji, wadau hapa waendelee kujadili "leboozzz"!!
ReplyDeleteMambo mazito ya kitaifa yana mahala pake!!
Mi nadhani aulizwe waziri Masha anayesema hili suala si kubwa kama linavyotangazwa.
ReplyDeleteMaana serikali ndiyo yenye dhamana ya kuwalinda raia wake,sasa kama inaliona ni suala dogo inashangaza.
Mimi nadhani umefika wakati itungwe sheria haraka dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivi,kwamba atakayekamatwa kwa kosa la kuua albino au kumkata viuongo basi naye afanywe vile vile kama alivyomfanya albino,kama alimkata kwa panga naye akatwe vile vile na kesi zao zipewe kipaumbele kuliko kesi zingine ,zisikilizwe haraka na kutolewa hukumu ndani ya kipindi kifupi .
Ni habari za kusikitisha sana ila kwa upande mmoja mimi naona pia viongozi wa serikali wanahusika na hili swala zima la kuwaandama na kuwafupishia maisha ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi (albino) nasema hivyo maana mpaka sasa ni matukio mengi yamefanyika lkn cha kushangaza hakuna hatua yoyote ya kuridhisha ambayo mpaka sasa imeshachukuliwa.
ReplyDeleteIkiwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge kukaa kimya kama habari hizi haziwahusu kwani wao ndio wanaohusika na kutunga sheria za nchi. Ninaimani kama wangekaa siku moja na kutunga sheria ya kuwa atakayehusika na mauaji ua albino basi na yeye auawe. Kwa maana kuwa hukumu yake iwe ni KIFO ninaimani mauaji haya yangepungua kama si kwisha kabisa. Inawezekana hata hawa wabunge nao wanatumia viungo vya albino kwenda kwa waganga wa kienyeji ili waweze kupandishwa vyeo au washinde katika chaguzi zao wanazofanya.
Mimi binafsi nasema kwa sauti kubwa kabisa kuwa WAHESHIMIWA WA NCHI HII WANAHUSIKA NA HILO.
Kwanza serikali inabidi iingilie kati na ichukue hatua kupitia vyombo vyake vya sheria. Kama mimi ningekuwa Serikali ningejaribu kuchukua njia mbali mbali za kuwanasa hao waovu wanaowafanyia ndugu zetu mambo mabaya. Kwani tunajua siku zote panya hunaswa na mtego na nyama. Sasa kama tuta weka dolia kubwa sana mahala popote tunapopaisi halafu tuweka kamtego kadogo na tuweke mmoja ya hao ndugu zetu natumaini haita fika mwezi tuta kamata mhalifu wetu, na atataja wenzake waliomtuma na teyari ameshafanya mara ngapi na maswali mwengi tu ataulizwa au wataulizwa halafu ndio wachukuliwe hatua kali ya kisheria. Najua hatunyongi Tanzania ila wafungwe maisha, wasihesabike kwenye msamaa wa rais wa mwesho wa mwaka.
ReplyDeleteBwana mi naona usinizuie comments zangu, please...Im about to explode now. I'm furious!. See inaudhi, sikitisha na kuchanganya akili haswa ukizingitia wengine tuko mbali na hatuna cha kufanya. Walau Blog hii inasaidia ku release our toxic emotions (rage). Being born an Albino is already a borden...haswa kwa maisha ya Africa na jua lote kali...sasa b ado tena these cruel MFs wanawafanya maisha yazidi kuwa magumu. Are these people humans, or just greedy murderous beasts!!. Do they believe in God, and the hereafter?. Hizi ndio sababu zinazotufanya tusitake kurudi nyumbani Tanzania, I am ashamed of some of my own people. Uchawi, wivu, tamaa na ukatili. I do not want my kids to grow in that environment...Is the government doing enough to protect its citizens??. My suggestion probably won't help but I say serikali ikabidhi kila Albino a gun for self defence...and give them licence to kill when they are threatened/attacked. Whatever it takes...ikibidi wananchi wengine waongezewe tax sawa tu...ili mradi kila Albino aweze kuwa na gun kuweza kujitetea (especially wanawake). In the meantime, to all of you Albinos who might be reading this, our prayers are with you...please don't walk alone, don't live alone, have company around you at all times, carry a serious weapon with you at all times. What's the matter with us?? Mara kuchuna watu ngozi, mara kuua Albino. Naona suala hili halijawekwa mkazo na serikali. I cannot imagine having to live in fear at all times, just because of your skin condition. Mwenyezi mungu awalaani kabisa woote wanaoshambulia hawa wenzetu, shetani wakubwa. Ipitishwe sheria ya kuruhusu Albinos kubeba guns...ikibidi watu wa nje kuunda umoja wa kusaidia kununua bunduki za maalbino...I'll be the first one.
ReplyDeleteKaka Michuzi asante sana kwa kuliweka hili suala zito litape mjadala. Mimi binafsi linanitia kichefuchefu. Not only ni aibu kubwa sana kwa taifa letu, pia ni inatudhalilisha watanzania pote duniani kwa ujumla. Hivi karibuni niliona kipindi cha BBC world wakitoa taarifa toka Mwanza, mahali mambako unyama huu unafanyika kwa wingi. Ilinisikitisha sana, na watu wengi walioona hii taarifa wanaweza kueleza jinsi ilivyotutia aibu kama taifa.
ReplyDeleteJambo la kufanya kwa mawazo yangu binafsi:
1. Wananchi wote tusimame kidete kwa pamoja kukemea huu unyama. Watu wanaoufnaya huu unyama ni watu waishio kwenye jamii zetu, tukishirikiana, itakuwa rahisi sana kuwatambua na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
2.Wakuu wa dini zote wanaweza kusaidia sana kwenye hili. Mara nyingi viongozi wetu wa dini zote wanakemea maovu mengi na inasaidia sana jamii kusimama imara.
3. Serekali itafute njia kabambe za kupambana na waganga wanahusiana na haya majanga. Hawa watu ni hatari kuliko majambazi, lazima serekali kwa kutumia uwezo wake ifanye kila linalowezekana kutokomeza hii aibu kwa taifa.
4. Wale wanye jamii (communities) zenye maalbino, wawe ndio vinara wa kuwalinda kwa pamoja. Ifanyike kama sungu sungu, watu wajitahidi kadri ya uwezo wao kusimama nao na kuwawekea mazingira ya usalama.
Hayo ni mawazo yangu tu, Naomba sana Mung atusaidie sana ili hili suala liweze kutokomezwa kwa haraka sana.
naomba niwakilishe!
mdau wa huku ughaibuni Bukoba.
`Nashauri wale wanaokamatwa na kutiwa hatiani mbele ya mahakama za sheria wanyongwe hadharani huku wale ambao bado kesi zao zikisubiri hukumu washuhudie.
ReplyDeletePia kuna haja ya kuteua albino wawili watatu wenye elimu ya sheria wawe majaji wa mahakama kuu ili wasaidiane na majaji waliopo kutoa hukumu zinazofaa kwa madhalimu hao wenye tamaa za utajiri wa giza.
Kwanza na anza kwa kumpa pole sana dada yetu kwa yaliyemukuta.Mungu atamjalia atapona na kuendelea na shughuli zake.
ReplyDeletekwa hao watu wanaofanya unyama kama huu kwa binadamu wenzio inabidi serikali kuwakata na kunyong'a kwa kifo ambacho wengine watapata fundisho.Sio kuwafunga haitasaidia kitu.kwani wanachukua nafsi za watu na zakwao zabidi zichukuliwe.
pili serikali inabidi kuwakamata waganga wote wa kienyeji bila kujali ni mganga wa aina gani.hapa na maanisha waganga hawa wanaojiita wa kuagua na wanaotoa majini au kukupa dawa za kimazingara.kwani imani zao ndio zimefikisha watu kuwa hivi.Na baadae hadujui wataanza kuwauwa wakina nani.
Hapa ni kukomesha uganga wa kienyeji kwanza ndo unasababisha umasikini since watu wanazidi kuwa ignorance
Vile vile tunaomba raisi JK aingilie kati na kuwapa fundisho wote wenye kuwauwa au kuchukua viungo vya ALBINO.
Na uwakika wanaofanya hivi tunawajua na nindugu na jamaa zetu.Ila kesho atakapo kuulia mwanao au ndugu yako ndo utaona uchungu au watakapo kuuwa wewe
Tuwe na upendo na umoja na uchungu wa maendeleo.Tusikubali kunyanyaswa hata kama ni jamaa zetu.Tuwa fichue hao wote wanao fanya vitendo vya kinyama namna hii
Asanteni
Mdau Edinburgh from Heriot watt University,Computer Science
Asante Michuzi kwa kuchochea mchango wa mawazo kuhusu suala hili.
ReplyDeleteTuanze kwa kuiwajibisha serikali yetu. Serikali kupitia vyombo husika inatakiwa kulinda wananchi wake wote. Hili ni muhimu jamani, kweli mpaka sasa hakuna aliyejiuzulu kutokana na mauaji haya yanayoendelea. Mzee Ally Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzulu alivyokuwa waziri mambo ya ndani!!
Nina wasiwasi, isije kuwa baadhi ya viongozi (inajulikana walivyo washirikina)wanahusika katika hili maana kwa sasa wengi wanatumia imani za kichawi kujilinda nyadhifa zao au kuogopa kwenda kwenye sheria kutokana na wizi!
Jamani tunakuwa na wakuu wa usalama ili walinde raia wote.
Michuzi,kwanza kabisa heri ya x-mass...,pili ni kweli kbs picha hii ni ya simanzi sn, lakini waelewa twaelewa sii nia yako kutupa simanzi bali kutushirikisha juu ya uchungu huu wa jamii na kuona tunaweza tukatatuaje kero hii mbaya sana ya jamii yetu.
ReplyDeleteBila kupoteza wkt, nina mitazamo kadhaa juu ya swala hili
1.Kisiasa.
Swala hili inabidi litazamwe katika mtazamo chanya wa kisiasa, hapa namaanisha
(i)Zitungwe sheria au (kama zipo) zitekelezwe kwa vitendo SHERIA KALI za kuwaadhibu wanaojishirikisha na vitendo hivi, na tuhakikishe hata viongozi wanaoongoza taasisi au idara au wizara zinazoweza kupelekea haya kufanyika wanalitambua hilo na wanaumizwa na hilo, tofauti na ilivyokuwa siku za hivi karibuni kiongozi wetu mmoja KIJANA alisema HILI NI JAMBO DOGO TU.....kwahiyo hii inaonyesha bado kuna tatizo hata katika ngazi kuu za uongozi na serikali kwa ujumla.
(ii)Serikali iwe makini na mikataba ya madini, maana tangia mikataba ya madini ianzwe kuwa inafanyika kiholela na mingine kusainiwa mahotelini na vichochoroni, kumekuwepo na mfumuko wa uvamizi wa wachimbaji hawa toka ng'ambo, na hivyo kuwakosesha wazawa ajira kisa hawana nyenzo, sasa kwakuwa wanajua kuwa madini ni yao nao wanatafuta kila hali ilimradi wapate madini hayo na katika hilo ndio shetani anaingiza idea zake kwamba hadi utumie ushirikina wa ngozi za albino nk ndio utapata madini....so tuangalie zaidi viini vya yote haya.
2.Jamii
Jamii ya watanzania hasa wanaojishirikisha na unyama huu popote walipo, lazima waelimike na watambue kuwa huo ni unyama wa hali ya juu, hapa
(i) makanisa
(ii)Misikiti
(iii)shule-Vyote hivi vishiriki katika kuielimisha jamii
NAWAKILISHA
Ban All Nigeria Films kuonyeshwa Tanzania
ReplyDeleteHuu ni Ugojwa wa akili. Serikali inapaswa itumie kila walichonacho kusaka hawa binaadamu wenye mawazo potofu na kuwachukulia hatua kali sana. Ninashangaa yote haya matendo ya kinyama yanaendelea, bunge na Waziri wa mambo ya ndani wako kimya. ALBINO'S TOO HAVE THE RIGHTS TO FREEDOM OF MOVEMENT AND LIVING IN PEACE LIKE ALL OTHERS....
ReplyDeletePlease uncle michuzi myself and others who condem this we have question to ower gorvement what they are doing to stop this. Becouse every time you read any news paper you see some albino have been murder. And thers no suspect, why they dont find those people who are resposeble with those murder. Im sorry we should open charity donate money and put some investigotor who can come up whith some answer.
ReplyDeleteINASIKITISHA SANA KWA WAZIRI MZIMA KUSEMA KUWA JAMBO HILI LINAKUZWA ILIHALI LIKO NA LINAONEKANA, KAMA MZEE MWINYI ALIJIUZURU NA KASHFA YA MAUAJI YA WACHAWI HUKO MASWA (MAREHEMU BABA YANGU ALIKUWA MKUU WA WILAYA HIYO WAKATI HUO-RIP) NA ILIKUWA MAUAJI YA VIKONGWE IWEJE WAZIRI HUYU ANAPATA WAPI GUTS ZA KUSEMA JAMBO LINAKUZWA ILIHALI WATU WANAKUFA?
ReplyDeleteNAFIKIRI SERIKALI MBALI NA KUTOA MATAMKO HAITOSHI HATUA ZICHUKULIWE, TUMEONA RAIS ALITOA TAMKO NA KESHO YAKE MTOTO WA MIAKA 6 AKAULIWA, KAMANDA MSIKA ALIPOULIZWA ALISEMA WATU 56 WAMEKAMATWA LAKINI WANATAFUTA WATAWASHTAKI KWA SHERIA GANI?
KAMA MDAU HAPO JUU ALIPOSEMA KUWA MTU KAUA ADHABU NA SHERIA NI ZILE ZILE KWA NINI UJIULIZE LEO SHERIA YA KUTUMIA AU KWA KUWA NI ALBINO?
NAFIKIRI KUNA HAJA YA KUWA NA SAUTI YA PAMOJA SIE WANAJAMII KUTOKA BLOG YA JAMII MHESHIMIWA SANA MICHUZI TUNAKUTUMA KWA MSEMAJI WA POLISI AU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI AKUPE MAJIBU NI HATUAGANI WAMECHUKUA MPAKA LEO KWA WALE WALIOKAMATWA NA KUKUTWA NA HATIA? NA UWAAMBIE NI SAUTI YA WANAJAMII
KWA WATUMIAJI WA FACE BOOK BADO TUNAKUSANYA SAINI TAFUTA KUNDI LINAITWA ALBINO TANZANIA UTAPATA NA JIUNGE HUMO.
Mwanakijiji unatukosea sana na naomba utuombe radhi kwa kusema kuwa
ReplyDelete"Hapa tunaweza kujadili Lebo tuu na si mambo mazito kama haya na ya siasa..."
Tafadhali kwa mdau mkubwa kama wewe n inayekuheshimu sikutegemea kauli ambayo mi naiita ya dharau kwa wadau humu kwenye blog ya jamii.
Mdau PM
Niliiona hiyo BBC WORLD DOCUMENTARY kuhusu mauaji ya malbino Tanzania, sasa dunia nzima inajuwa kuwa sisi ni wauwaji wa wenzetu hawa, si unajuwa wazungu wanavyojuwa kuongea walitupaka sana, kwa kweli inatia aibu, serikali inaliona hilo lakini naweza kusema haijali haifanyi chochote juu ya swala hilo, kinachotakiwa sasa ni sisi wananchi kuishinikiza ifanye inavyotakiwa kufanya, kulinda usalama wa watu na mali zao ndo maana tunalipa kodi, tumewaweka madarakani watulinde, tumeajili polisi na tunawalipa mishahara ili watulinde.WABUNGE MPO WAPO MBONA HILI HAMLISHIKII BANGO, HAMJALI, KWA VILE SISI nyinyi mnauliwa, ni aibu kubwa sana kwa taifa na ubinafsi.
ReplyDeleteHii yote inatokana na imani za Kishirikina. Sasa mnasema serikali ikaripie hii kitu. Hao mawaziri ndio wanashinda kutwa kwa waganga ili cheo kipande au wasifukuzwe, sasa wakifika huko wanaambiwa walete viungo vya mazeruzeru matokeo yake ndio haya. Watu inabidi kumrudia mungu. Wakuu wa dini wanajaribu kupinga ila bila serikali kukazia uzi ni kazi buree tu.
ReplyDeleteNDUGU MICHUZI KWANZA KABISA NATOA SHUKRANI KUBWA KWA KULIWEKA JAMBO HILI LA KISHENZI NA UNYAMA UNAOFANYWA NA SERIKALI YA CCM.
ReplyDeleteMAANA WAUAJI WOTE WANAJULIKANA VIZURI NA CCM SIYO SERIKALI MAANA TZ UKWELI CHAMA NDICHO KINACHOTAWALA JAPO WANAITA SERIKALI.
LEO INGALIKUWA WAKATI WA UKOLONI TUNGALIAMBIWA NI UBAGUZI.
CHA KUSHANGANZA NI KUWA WAKATI MAANDAMANO YANATAKA KUFANYIKA DHIDI YA CCM JAPO YA AMANI ULINZI HUWA HAUKOSAKANI NCHI NZIMA.
LEO NDUGU ZETU WANAUWA KUSHINDA WANYAMA NDIO KWANZA KIKWETE KATIKA HARAKATI ZA KUTEMBEA NA KULA MARAHA YAKE.
SHERIA IKO WAZI PINDI SERIKALI IKIWA ADILIFU.
HAPA SAUDIA MBONA HAKUNA HAO WAGANGA WAKISHENZI KWA VILE UKIUUA NAWE KISU SIKU YA IJUMAA.
YAANI UTAKALO MFANYIA MWEZIO NAWE UNAFANYWA HIVYO.
HAKIKA WAAFRIKA HATUNA MAPENZI TUNA MAPENZI YA KUWADANGANYA WANANCHI NA KUIBA PESA ZA WANANCHI.
ANGALIA SEHEMU ZOTE KARIBU ZINAZOTAWALIWA NA MWAFRIKA KATIKA AFRIKA SIFA KUBWA KUUANA, KUIBA, KUPINDUANA NA MAMBO YOTE MABAYA YA DUNIA YAKO AFRIKA.
SAMAHANI NDUGU ZANGU LAKINI NDIO UKWELI.
NAIMANI LEO TANZANIA INGALITAWALIWA NA MKOLONI BASI HAKI YA ALBINO ISINGALIPOTEA.
CHA KUFANYA NI WAANCHI KUWASAKA HAO WAGANGA WA KIENYEJI NA KUWACHULIA HATUA ZINAZOSTAHILI.
TUKITEGEMEA SERIKALI YA CCM BASI TUTABAKI UCHI LEO MIAKA 60 YA UHURU TANZANIA INAISHI KWA MISAADA YA NCHI YA NJE NA WAKATI HUO HUO MAFISADI WAMEJAA KIBAO KUANZIA RAISI MAANA KAINGIA KWA PESA ZA EPA NA KIGAONDA NDIYO KINARA ALIKUWA WAKUGAWA FEDHA.
WATANZANIA AMKENI SIYO KUDANGABYWA NA KANGA NA VITEGE.
TUGOMBANIA HAKI YA TAIFA NA SIYO YA MTU BINAFSI.
FIKRA NA VITENDO VYA BABA WA TAIFA TUKIZIFUATA TUTAFANIKISHA KWA MAANA ALIKUWA MTU WA HAKI NA UCHUNGU KWA WANANCHI MUNGU AMUWEKE MAHALA PEMA.
CCM YA ZAMANI NDIO ILIKUWA CCM AMA YA LEO NA KUIBA NA KUIFILISI NCHI.
LAKINI TUKUMBUKE KUWA MUNGU HUPOKEA DUA YA MZU;IMIWAJI MARA NA HAPO CCM WANAOJIFANYA NA UCHUNU WA NCHI MUNGU ATAWACHUKULIA HAKI NA KUWAPA ADHABU KUANZIA DUNIANI HADI AKHERI AMENI.
HAKIKA INANIUMA SANA KUONA WATANZANIA TUNAVYOJIUA HATA WANYAMA BORA.
WATANZANIA NI KUMUOMBA MUNGU ALIPE HAKI KWA WADULIMIWA NA AWEPE ADHABU KALI WOTE WENYE KUIBA NA KUTUMIA MADARAKA YA DHAMANI KWA AJILI YAO.
Kwanza kabisa naoenda kumpa pole huyo dada Albino aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama.
ReplyDeletePili, kujadili hili suala tufanyeje uli kukomesha hayo mauaji peke yake hakutoshi, maana wote humu ndani tumekazana kulaumu serikali, serikali haifanyi hivi serikali haifanyi vile, wakati sisi wenyewe ndio wahusika wakuu wa kuwa na imani potofu, imani inayoona watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali kuwa ni binadamu tofauti. Ntatoa mfani mmoja, ni nani kati yetu yukaribu na watu wenye ulemavu na kuwaona wako sawa na sie? Imani zetu tulizonazo ndio chanzo, wengi wetu hasa wanawake wakimuona albino ndio wa kwanza kutemea mate matumbo yao ili wasizae watoto Albino, utasikia mtu anamwambia mwenzie temea mate chini au temea mate tumbo lako ili usizae albino. Hapa namaanisha kuwa bado suala zima la kujua kwa nini watu wanazaliwa albino halipo, limejikita kwenye imani potofu.
Kwa hiyo jambo la msingi la kufanya sio kulaumu serikali, bali kwa kutumia vyombo vyote vya habari vilivopo pamoja na blogu zote kutoa elimu kwa watu wote (kwani wanaotafuta utajiri sio watu ambao hawajaenda shule peke yake, hata waliokwenda shule wako huko Mererani na kwingineko wakitafuta madini na kufanya biashara mbali mbali) kuwa suala la mtu kuzaliwa albino ni suala la kimaumbile si la kishirikina au halihusiani na nguvu za giza.
Tatu natoa ushauri upitishe mchango humu kwenye hii blogu yetu ya jamii, tuchangie kumtafutia huyo msichana viungo vya bandia, ili aweze kupata mikono mingine, hii itaonyesha jinsi tulivyoguswa na suala zima la ukatili unaofanywa kwa hawa watanzania wenzetu.
Mwisho kabisa kwa kuwa suala hili linahusisha imani za kishirikina natoa ushauri wa kiwendawazimu, si unajua jinsi washirikina wanavyoogopa 'Albadiri' basi isomwe Albadiri nchi nzima kwa ajili ya hawa wanaowakatili Albino, na ifanyike ibada maalumu nchi nzima kwa waumini wa dini zote kwa ajili ya kumuomba mungu kwa janga hili. Na vile vile viongozi wa dini wasidishe kutoa elimu kwa waumini wao kuhusu ukatili kwa binadamu wengine unavyomchukiza Mungu.
MDAU MWANAKIJIJI UMITUKOSEA MZEE
ReplyDeleteTUOMBE RADHI HARAKA LA SIVYO ITAKU COST HII UNAPOSEMA SIE WACHANGIA LEBEL? INAMAANA BLOG NZIMA YA JAMII? REKEBISHA MSEMO WAKO LA SIVYO NIONDOE KWE MAIL LIST YA CHECHE KAMA HATUWEZI KUHESHIMIANA.
XSAVIA-UK
Kwanza kabisa napenda kumdis value 08 8:24 PM, Mtoa Maoni: mwanakijiji...huyu jamaa elimu yake haimsaidii anadhani yeye anajua mambo mengi kuliko wengine, anasema blog ya michuzi iendelee kujadili mambo ya leboz na issue serious kama za maalbino tuwaachie wao wajuaji kuliko.
ReplyDeleteIssue ya maalbino inatokana na ufinyu wa ufahamu wa wananchi, tz ni miongoni mwa nchi watu wanakuwa matajiri kwa kutoa kafara mzazi wake, mtoto au mke/mme wengine wanajulikana kwa majina. kuna watu leo hii matajiri kufuru na hatujui shughuli zao wanaishi maisha ya kifahari kuliko jk mwenyewe, kutwa wanashinda kwenye mapub na tunawajua kwa majina...tunashindwa kujua tunahitaji elimu ya biashara ili tuendelee kama alivyosema prof mbele, watz tunapenda njia za panya...hatujishugulishi kupata kihalali ndo maana hata viongozi wakuu wa nchi uenda kwa waganga kwa kuhofia nafasi zao, kumbe anashindwa kujua utendaji wake kwa waliompa dhamana ndo kinga pekee na si mganga njaa...watz tuamke.
Nasapoti 100% na kusisitiza hoja za Mdau wa Bukoba (Dec 26/10:19pm) chini ya maoni yangu ya awali. This is the beginning on the net, wananchi waandamane kuonyesha muungano na ndugu zetu hawa, viongozi wa dini zote wakemee waziwazi, wanajamii wa sehemu ambazo zinahusika zaidi (haswa Mwanza) wachukue jukumu la kuwalinda ma Albino, na kuwa makini kupeleleza nani wahusika, na waganga gani wanahusika. Aliyetoa wazo la kuwakusanya maalbino sehemu moja na kuwalinda...hapana, wao ni wananchi wenye haki ya kuishi wanapotaka....na serikali na wananchi wanawajibu wa kuwalinda kama raia. Waelimishwe watu wanaokwenda kwa waganga kutafuta cheo, utajiri, ramli. Nashangazwa kusikia baadhi ya wasomi, na mawaziri nao huenda kuloga ili wapate vyeo n.k, na watu wengine wapate utajiri...kungekuwa na ukweli huo basi hao waganga wote wangekuwa matajiri na mawaziri...badala yake they are some of the poorest. Still, wazo la kuwapatia guns kila albino over 18 years of age, na kila mlezi wa albino mtoto ni zuri.
ReplyDeleteKwanza kabisa sipendi kutumia neno albino kwa sababu neno sahihi la kiswahili ni zeruzeru. Najua kuna watakaojifanya kuleta "too much of a PC"
ReplyDeletePili, katika nyakati hizi za "forensic medicine" sababu ya kutokamatwa hawa wauaji na wakeketaji wa mazeruzeru ni moja tuu, serikali haijali matatizo ya hawa raia. Binti ya Kikwete akibakwa, forensic knowledge itatumika na muhalifu atakamatwa. Zeruzeru akiuliwa, kikwete anatuma rambirambi mchezo umekwisha.
In my opinion,court of law and all legal firms should introduce and exercise public execution system against all those who are found guilty for being involved in this kind hostile attempts to try to harm or kill disabled people.
ReplyDeleteHeri ya Xmas wana blog wote.MICHUZI KWANINIUNASEMA MAALBINO WASIO NA HATIA?,MIMI NASEMA HATA WENYE HATIA WASUAWE WAPELEKWE MBELE YA DOLA.Nimejaribu kuzipitia comments zote.Asilimia 90 zimeelekeza lawama zote kwa serikali(Ni kweli),nyingine zimekuwa za kejeli kama hiyo ya Kwanza na baadhi.Nadhani kuna taasisi imemwomba Balozi wa Zain kuweka hii mada ili wachukue mawazo tofauti ya watu,so tuwe serious.
ReplyDeleteTwende kazi:
1:Hili suala limo ndani ya wizara ya mambo ya ndani,usalama wa tf umekufa.Dola ikaze buti wajameni hawa watu(wauaji) tunaishi nao.
2:Makanisa,misikiti wnaweza kutusaidia sana kukemea hili suala,serikali iwashirikishe.
3:Tuige ya Wilaya ya Kwimba,kwamba Albinos wote wawe registered,wanaojiita waganga wa kienyeji wawe registered likitokea janga la mauaji ya albino,waganga wote wa maeneo wawe wa kwanza,najua mwuuaji anaweza kuwa ameambiwa na mganga wa Mbali vile vilke
4:Elimu:Itolewe Elimu kwa hawa ndugu zetu,wachoji(artisan miners),wavuvi na wengineo walioko kwenye mazingira ya kupata vishawishi vya kuua albino.
5:Baadhi ya viongozi wetu na nyie mnajiusisha na mauaji ya albino??Nyie wengi mmneenda shule,jisikieni vibaya jamani ukiambiwa kakate mikono ya Albino mwambie huyo'daktari' akubadilishioe dozi iwe mikono ya kuku.kondoo,mbuzi n.k lakini siyo Binadamu.
Pole sana dada yangu kwa maswaibu yaliyokupata. Tunajua kuwa albino ni tatizo tosha lakini watu wenye uchu na utajiri wameamua kukuongezea matitizo.
ReplyDeleteBinafsi ushauri wangu ni kwa jamii kubadilika na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola. Nasema hivyo kwa sababu sisi ndiyo tunaoishi na waganga wa jadi (wengine baba/mama/ndugu zetu) pamoja na watu wanaokodiwa kufanya haya mambo ya kishenzi lakini mara nyingi tumekuwa kimya na badala yake tunapiga kelele za kuilamu serikali. Serikali haina polisi wa kutosha kuweka kila kona ya nchi na pia hata kama polisi wapo wa kutosha haitowezekana kila mwananchi kulindwa na polisi wakati wa mihangaiko yake ya kila siku, hivyo pindi wananchi wenyewe tutapoamua kujilinda kwa kutoa taarifa za uhalifu za watu ambazo tunawasiwasi nao nadhani polisi wataweza kusaidia sana kwa hili. Ndugu zangu inabidi tubadilike kwani mara nyingi matukio mengi ya mauji na ujambazi yanafanywa na watu ambao wengi wao wanafahamika lakini tunawaficha ama tunawaogopa kuwataja hadharani. Nawaomba viongozi wa dini pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya mtaa waanzishe kampeni itakayowezesha viongozi hao kupokea taarifa za siri za watu ambao tunawahisi ni wahalifu ili wazipeleke kunakohusika kwa hatua zaidi. BILA KILA M1 WETU KUWA MLINZI WA MAOVU, haya mambo hayataisha na yatazuka mengine
Albino watengewe vituo au makazi maalum. Wakusanywe maeneo hayo na pawekwe ulinzi wa kutosha.
ReplyDeleteNadhani kukianzishwa vituo kama hivyo kuna albino wengi tu ambao watakuwa tayari kuhamia.
Uwaweke albino kwenye kambi, jamani huo sio ubaguzi? hata kama wanalindwa maisha yao.
ReplyDeleteUtakubali wewe mtoto uliyemzaa na unampenda akawekwe kwenye kambi?
Kitu ninachokiona hapa ni ubovu wa serikali tu,
Najua kama kweli JK anataka kuikomesha hii tabia ingekoma mara moja.
Tuna askari kanzu kibao Tanzania, kwanini wasipelekwe maeneo ya matukio nakuwatega hao wahalifu?
Kama mhalifu mmoja tu atakamatwa na askari kanzu basi wataambizana wote na wataogopa kufanya hivyo.
Anyway serikali yetu ina issue nyingi. Tunakokwenda ni safari ndefu.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
nina swali moja tu! KWANINI WEZI WAKIIBA HUWA WANAULIWA NA WANANCHI WENYE HASIRA?KWANINI HAWA MAFISADI WA MAALBINO WAKIKAMATWA HAWAFANYWI KITU?? kwanini tunakuwa na mioyo ya tamaa na ukatili?juzi kati huyu dada aliepo pichani alivokatwa mikono na mchizi ambaye ni jirani yake japo mchizi alikimbia kusipojulikana walishindwa kuwashikilia familia yao mpk waseme huyo mwenzao alipotokomea?au KUWAFILISISHA izi hilo hela ziweze kukimu mahitaji ya albino huyu ambaye ni MJAMZITO?watanzania tuache tabia ya wapopo hawa ndugu zetu uchawi upo kwenye damu wao ndo traders wakubwa wa hii biashara na wana tumanipulate na tuvihela twao na sie tusivo na akili tunaingia kichwa kichwa na wengine wanaventure kabisa. Ninajua kuna mmoja wa wamiliki wakubwa wa kampuni flani sitamtaja jina lake yeye kazika maalbino wazimaa kawazika ili afanikiwe!na hii ishu sio kwamba kafanya leo kafanya kitambo sana na ananunuaga uchawi wake nigeria. inasikitisha sana.
ReplyDeleteKAMA INGELIKUA MTOTO MMOJA TU WA MAFISADI ANGELIKUA NI ALBINO NA AMEPATA MAAFA NAMNA HII BASI HATUA ZA KISHERIA ZINGELICHUKULIWA KWA HARAKA
ReplyDeleteHali hii inasikitisha sana. Mara kwa mara, naulizwa hapa ughaibuni, kwa nini nchi kama Tanzanania yenye sifa nzuri duniani haiwezi kusimamisha hali ya kikatili dhidi ya Maalbino, huwa sina jibu ila machozi tu yananitoka. Pole dada na naomba msamaha kwa niaba ya Wananchi wenzangu. Naomba serikali iwasaidia Maalbino waweze kuishi kwa amani na usalama kama wananchi wengine.
ReplyDeleteKuna wadau hapo juu ambao wamekwazika na maneno yangu. Kama mwandishi na mjenga hoja kuna wakati tunatumia kejeli (sarcasm) kuonesha ukweli ulio wazi.
ReplyDeleteWakati wa mjadala wa Leboozzz nilitolea mfano kitu hiki hiki na suala hili hili la Maalbino. Majibu ya baadhi ya wadau (unaweza kuyasoma kwenye sehemu ile) mengi yake yalikuwa ni katika kujeli kutumia bulogu hii kuleta mjadala wa kitaifa kama wa mauaji ya Maalbino.
Wadau hao walipigia debe na msimamo kuwa bulogu hii ya jamii ni mahali pa kuburudika n.k
Niliandika hivi:
"Hivi kweli tunakerwa na vitu vidogo vidogo, na tukosoea na kujisokoa kwa vitu visivyo na msingi (trivial) kwani yote ni maisha lakini ni lazima tuweke kipaumbele cha kutovumilila kero kubwa kubwa au kuzifumbia macho kwa sababu zitafufanye tuonekane wanasiasa au watu wenye matamanio ya kisiasa au kuonekana tuna wivu kwa watu walioko madarakani!"
Mmoja wa wadau alinijibu hivi:
"Kuna blog elfu za mtazamo wako, pamoja na za kwako, hatuendi huko, pengie kwa sbabu ulizozisema lakini pia sio wajinga kiasi kuwa kila saa ni siasa tu za vyama au uadilifu wa serikali"
na mwingine akasema hivi:
"Fungua mijadala kwenye website zako juu ya kukosa chakula shuleni, usafiri wa wanafunzi, nauli za daladala, kukosekana maji, kufungwa kwa vyuo vikuu, kesi za Manji, Masha,Mengi, Yona, Mramba, Mgonja na ufisadi uliokithiri BOT, Madini, Ardhi, PSRC, nk
Yatajadiliwa huko. Heshimu watu."
na mwingine katika upotofu wa hoja zake akasema hivi:
"mwanakijiji mambo yako ya siasa unayaleta huku kutafuta nini. unatuharibia ladha sisi wapenda udaku."
na mwingine akasema hivi:
"moshi tech imeingiaje mwanakijiji mambo ya umbea tuachie wenyewe. siyo kila mtu anapenda stress za siasa. kwa nini unatulazimisha mambo hayo. wewe si una tovuti yako ya kupigia kampeni. acha kutuboa"
Sasa, si wote walionipinga hivyo. Wapo waliounga mkono kuleta hoja hizi kati ya Watanzania pasipo kujali forum. Hivyo jibu langu hapa lilikuwa linawalenga wale wanaotaka kushusha hadhi ya bulogu ya jamii kama hii na ambao wanabeza uwezo wa Watanzania kufikiri na kujadili mambo nyeti ya Taifa letu.
Kilichofanyika hadi sasa hapa kimethibitisha kuwa msimamo wangu ulikuwa sahihi; kwamba masuala ya kitaifa yawe juu ya mijadala ya labels, chupizz, na fulanazz! Kwamba kuna wakati tunafurahia udaku, tunachekeshana na kutaniana, lakini yanapokuja mambo ya msingi kusiwe na utata wowote.
Hicho ndicho nilichoandika.
Sasa kwa mtu ambaye anakwazika na kutishia kujiondoa kwenye mailing list, niandikie email nitakuondoa. Kama unataka maelezo ya nilichoandika unaweza kuuliza lakini hata mara moja siishi kwa kitisho cha mwanadamu yeyote.
Ni Mimi M. M. Mwanakijiji
wa http://www.mwanakijiji.com
Tatizo hili linahitaji hatua zifuatazo:
ReplyDelete1. Elimu kwa jamii kuhusu janga hili, kuacha ushirikina na tamaa ya utajiri.
2. Ulinzi wa jamii, kuwalinda ndugu zentu hawa.
3. Kuwadhibiti waganga wote wa jadi, kuwatambua waohusika na wateja wao na kuwafungulia mashitaka ya mauji. Mahakama iendeshe kesi zao kwa speed.
4.Vyombo vya habari vionyeshe picha za wahalifu hawa: wanunuaji, waganga na wateja wao.
Nje ya mada:
Mwisho nimesikitishwa na maoni ya mtu aliejiita Mwanakijiji hapo kwa kukijeli wasomaji wa blog hii na kwadhihaki wasomaji kuwa (a) jambo hili ni la siasa, eti sio swala la jamii, (b) mumwachie yeye ajadili siasa, kwa sababu wadau humu ndani hamna uwezo wa kujadili kadhia kamaa hii.
Sijui ni kitu gani kinampa kichwa na ujeuri wa namna hii.
Mwinyi anasema kila mtu anataka kuwa tajiri!
ReplyDeleteKikwete ajiuzulu!
Kabineti yake ijiuzulu!
Waziri wa Mambo ya Ndani awekwe ndani!
Wananchi tufanye mchango wa pesa kupitia kwa Michuzi ili zimsaidie huyu dada kwani kwa kutokuwa na mikono + hali yake = matatizo+++.
ReplyDeleteMimi nadhani tukifanya hivyo tutakuwa tumeonyesha upendo wa dhati kwa dada yetu mpendwa na pia itaonyesha kwa namna gani tumeguswa na hali yake.
NB: Ni mawazo tu wadau, mnichafue hali ya hewa kama hamridhiki
inauma sana jamani serikali ipo wapi mpaka aya mambo yanazidi kuwa ivyo.wapo radhi kula mabilioni ya ela kujinufaisha wenyewe wanashindwa kuunda kabinet ya kuchunguza swala ili.kama kweli nyie watu mnaoua maalibino ni imani za kishilikina basi muuwe wazungu kwani hawana rangi tofauti na hao.mnawaonea hao maalibino. sababu hawana support eheeeeeeee nasema za mwizi arobaini.
ReplyDeleteNimesoma mchango wa mtu aliyejiita mwanakijiji. Amejaribu kuuita uefedhuli kuwa ni umahiri wa uandishi yaani sarcasm. Chama cha mafedhuli wanasema katika web site yao
ReplyDeletehttp://www.sarcasmsociety.com/
There is nothing more beautiful than sarcasm. That is definitely an overstatement but it should balance the moronic comment which says that sarcasm is the lowest form of humor. Now, whoever made that statement was desperately in need of a rectal broomstick extraction procedure.
Sarcasm usually requires a quick wit, and the ability to extract the minutest points of weakness in a conversation. So it is quite unlikely that it is the lowest form of humor as some would like to call it. Perhaps not being able to enjoy sarcasm is directly related to not having the ability to come up with sarcastic comments, which in turn creates a feeling of inadequacy, which in turn can spawn a Napoleon complex, that can cause someone to logicise that sarcasm is the humor of the stupid.
Kwa muhatsari wanasema ufedhuli ndio ucheshi wa mtu mjinga.
ALBINO NI ENGLISH NA ZERUZERU NI KISWAHILI, PIA SINA AHAKIKA KAMA KUNA KITU KINAITWA FORENSIC MEDICINE, HAKUNA KITU KAMA HICHO, ILA KUNA UTAALAMU WA FORENSIC UNATUMIKA KUKUSANYA USHAHIDI JUU YA TUKIO FULANI, IKIWA PAMOJA KUTAMBUA FINGER PRINTS, DNA NA VITU KAMA HIVYO, MEDICINE NI MASWALA YA DAWA INAYOTIBU UGONJWA FULANI, FORENSIC SI DAWA
ReplyDeletewhat a shame what people will do to another human being....what is our govermrnt doing?wanatembea na vitambi in the latest model cars wakati wengine hatuwezi toka ndani.....wewe unayesena albinos watengwe why? they have nothiong to be ashamed of. kama ni kutngwa basi na walio na ukimwi nao watengwe? there is no need for them to be isolated at all....people needs to understand this is as simple as kuzaliwa maji ya kunde or mweusi as mkaa and let them live their lives as free as we have been since 1961...as for those guys doing all these killing they belong gerezani for life... if the overment do do anything to help thats when people will take power in their own hands... vita ndio zinaanza hivi hivi see our majirani around us....i dont think this affects only albinos but families and friends as well worring kama leo will be the day... i cant belive watanzanioa tumekuwa wanyama ....have we forgotten our God and turned evil completely? if you know your jirani is doing this evil stuff report them for crying out loud....what if your son was zeruzeru ungekaa tu usubiri akatwe viungo?
ReplyDeleteKwanza kabisa naanza kwa kuwalaani watu wote wanaohusika na unyama huu. Kuanzia hao washenzi waganga washirikina wakubwa, binadamu wanyama wanaokata hivyo viungo vya binadamu wenzao na hao mahayawani wanaonunua viungo vya binadamu wenzao. MUNGU awalaani kwa kuwaua na kuwakata viungo viumbe wake!!!! Kwakweli dawa yake ni ndogo. Namuomba Raisi Jakaya Kikwete aanzishe utaratibu kama unaofanyika uarabuni kila ijumaa mwizi yoyote anakatwa mkono hadharani, akiiba tena mkono wa pili. Ndugu Raisi Kikwete kila Jumamosi uwanja wa zamani wa taifa watanzania wote tutakuwepo kushuhudia wakataji viungo wa albino wanavyokatwa mikono hadharani. Hata kwenye Biblia enzi hizo watu wakosaji waliadhibiwa kwa kupigwa mawe mpaka wafe!!!! Sababu hii mambo ya sheria itachukua mkondo wake. mtu akamatwe. awekwe ndani. apate mdhamana. uchunguzi bado unaendelea.ushahidi haujakamilika. Mara mtuhumiwa yuko huru. TUMECHOKA.TUNATAKA NDUGU ZETU ALBINO WAWE HURU KAMA WATANZANIA WOTE WALIVYO HURU. Serikali ikiendelea kuwa kimya wananchi tujipange tuchukue sheria mkononi kuwachoma moto watakao thubutu kuwagusa ndugu zetu Albino. Kweli duniani kuna watu wengi sana lakini Binadamu wachache. Mtu yeyote anayefanya unyama huu sio Binadamu ni MNYAMA!!!!
ReplyDelete