KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania Limited leo imemchagua, Sweetbert Damian Taga mwenye umri wa miaka 41, aliyebahatika kuibuka mshindi wa kumi wa zawadi ya gari jipya aina ya RAV 4 jijini Dar es Salaam.
Sweetbert, mkazi wa Sumbawanga ambaye ni askari polisi, aliibuka mshindi katika bahati nasibu iliyoendeshwa Dar es Salaam leo kwenye ofisi za makao makuu ya Zain.
Gari hilo ni moja kati ya magari 11 yanayotolewa na kampuni namba moja nchini ya simu za mkononi ya Zain Tanzania katika promosheni yake kubwa kuliko zote ya Endesha Ndoto 2.
“Kama mnavyofahamu Zain Tanzania bado inaendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika.
“Zain, kampuni namba moja ya simu za mkononi nchini inaendesha promosheni ya Endesha Ndoto 2, tutakabidhi jumla ya magari 11 mapya kwa Watanzania wenye bahati likiwemo jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer. Leo tumemchagua mshindi wa kumi aliyenyakua gari aina ya Toyota RAV 4,” alisema Kelvin Twissa, Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania.
Promosheni ya Endesha Ndoto ni sehemu ya programu endelevu ya Zain Tanzania. “Lengo letu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwafanya waishi kwa raha zaidi kwa kuzingatia kauli mbiu yetu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa),” alisema Twissa. Katika mahojiano na Twissa badaa ya kuibuka mshindi, Sweetbert alisema amefurahi kuibuka mshindi na akabainisha yuko tayari hata kutembea kwa miguu kutoka Sumbawanga ili kufuata gari hilo ofisi za Zain Dar es Salaam.
Mpaka sasa droo ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain imekwishawawezesha watu tisa kuibuka washindi wa magari aina ya RAV 4.
Mshindi wa kwanza alitoka Dar es Salaam, wa pili alitoka mkoani Mbeya, wa tatu Iringa, wa nne Pwani, wa tano Tanga, wa sita Dar es Salaam, wa saba Tabora, wa nane Dar es Salaam na wa tisa Mwanza.
Mbali na mshindi huyo wa RAV 4 jana, pia mkulima ambaye pia ni fundi seremala wa Nyamuswa wilayani Bunda, Petro Samaku (32) aliibuka mshindi wa sh. milioni 1 katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 kwenye droo iliyofanyika Dar eS Salaam.
Samaku aliibuka mshindi wa nne katika bahati nasibu iliyosimamiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh.
Ili kushiriki katika promosheni ya Endesha Ndaoto 2, mteja anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda nambari 100 na atakuwa ameingia rasmi kwenye promosheni hiyo ambayo zawadi kubwa ya mwisho iliyobaki ni Toyota Land Cruiser.
Mbali ya zawadi ya magari, Zain pia inatoa zawadi nyingine anuwai kupitia Ndoto Pointi. Kila mara mteja wa Zain anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto Pointi. Kwa kila Tsh 500 anayozungumza anajipatia ndoto pointi moja.
“Mteja akifika kati ya Ndoto Pointi 1,000 hadi 3,000 anajishindia kufurishi cha zawadi kutoka Zain, akifika Ndoto Pointi 3,001 hadi 5,000, anajishindia simu mpya aina ya Nokia 1110i. Mteja akifika pointi 5,001 hadi 7,001 anajishindia simu aina ya Nokia 1650 wakati pointi 7,001 hadi 9,000 anajinyakulia Nokia 5310 au Ipod. Pointi 9,001 na kuendelea mteja anajishindia simu ya kisasa ya Blackberry bure,” alisema Twissa.
Twissa aliwatahadharisha Watanzania kuwa makini na jinsi taarifa za matapeli wanaowalaghai watoe pesa, na akabainisha kwamba pale mshindi anapopatikana, Zain Tanzania haitumi sms, bali hupiga simu na mshindi hahitaji kulipia gharama zozote.
baba sio njago ni njagu.
ReplyDelete