Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inapenda kuchukuwa fursa hii kuwatangazia Watanzania wote wa maeneo ya Kanto na maeneo ya jirani na wale watakaokuwa wanatembelea Kanto wakati huu wa kipindi cha mwaka mpya kuwa kutakuwa na sherehe kabambe ya kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka mpya 2009 siku ya tarehe 3/1/2009 huko Mkoani Kanagawa.
Maelezo kamili ya shughuli hiyo ni kama ifuatavyo:-
Siku: 3/1/2009 (Jumamosi)
Muda: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo
Kiingilio: Yeni 3000 (utapata chakula na vinywaji viwili)
Ukumbi: Club intercontinental (karibu na station ya Sobudae mae (Odakyu line))
Mengineyo: Muziki wa nguvu, mashindano ya kumtafuta mrembo na mtanashati wa siku hiyo, mashindano ya kucheza muziki pamoja na bahati nasibu.
Zawadi mbalimbali nono zitatolewa kwa washindi. Kwa ufafanuzi na maelekezo ya ziada tafadhali piga simu zifuatazo
Katibu Mwenezi (Daddy): 080-3532-4043
Mwenyekiti Kamati ya Starehe(Pembe): 080-3458-8786
Simu ya Ukumbi:046-238-0721
Uongozi wa Jumuiya unawaomba Watanzania pamoja na marafiki zao wa mataifa mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha sherehe hii.
Ahsante
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani


yeni 3000 ni sawa na usd ngapi wadau?
ReplyDeleteTumia hiyo hiyo internet unayotumia kuuuliza YEN 3000 NI SAWA NA USD NGAPI, hata ukitumia google.com unapata. Just ask like this:- convert 3000 japanese yen into USA dollar intakuja website itakuelekeza namna nya kubadilisha. internet inajibu kila swali hapa duniani, ni kitu nzuri hata ukiuliza juu ya kijiji chochote cha Tanzania utapata maelezo yake na google settelite map hata nyumba yanu utaiona.
ReplyDelete3000 ni kama dola za kimarekani 30. Wadau, tupe tena hio stesheni maana siioni hyperdia, haiikubali. Najua Odakyu ipo shinjuku lakini Sobudae mae ni hola. Ni JR au Tokyo subway?
ReplyDeleteDola 29.99 ni sawa na Yen 3000
ReplyDeleteMdau, Yen 3000 ni kama US $32
ReplyDeleteasante sana kwa majibu yenu swadakta,kweli sikuhizi internet imeondoa lile gape kubwa lililokuwepo baina ya wasomi na wasomile maana hawawezi tena kutubabaisha kama hapo bosi yaani hapo zamani kilakitu wakijuacho wao sie pia tukikitaka twakijua in a second tu
ReplyDeleteWabongo hatueleweki. Yaani hamna kiongozi yoyote anayofatilia hapa, kama wadau wamepotea au wanahitaji msaada. Kupiga simu ni kupoteza pesa tu. Niliuliza jinsi ya kuja huko kwa kuwa hio stesheni haipo katika ramani ya treni (hyperdia), labda mumekosea jina? Nilikuwa na nia ya kuja huko lakini naona bora nitumie Yen 3000 zangu katika baa yangu ya karibu na nyumbani, hasa nikizingatia kuwa nitafunga magoli sana. Kaeni na kijipati chenu.
ReplyDeleteKwa Anonymous wa December 30, 2008 6:49 AM. Acha uvivu bwana, kama unakaa Japani na unaijuwa Odakyu line uwezi kupotea hiko kituo. Kama unaogopa gharama za simu nina wasiwasi uenda hata kiingilio huna, gharama za simu sio kubwa kiasi hiko. Hata ku-beep uwezi?
ReplyDeleteAnony 12:50 juu, mimi mvivu lakini Yen 3000 nnazo, si unajua ukidunda na PR gaijin card huwezi kurosti.
ReplyDeleteTatizo nina mademu watatu sasa na wote wanataka kula New Year pamoja, si unajua Wajepu wanavyopenda maraha?
Sasa wadau nisaidieni, niende kwa wabeba maboxi wenzangu katika kijipati chao au niende kwa mademu bomba watatu wa Kijepu kufunga magoli?