injini kiuno ni usafiri muhimu huku, na kinamama hawako nyuma katika libeneke hilo
shinyanga nako tambarare ati. kama kigali....
mohamed trans likiingia stendi kuu ya shinyanga
pembezoni mwa shinyanga hususan karibu na mgodi wa almasi wa mwadui na karibu kabisa na barabara kuu wachimbaji wadogowadogo wako kazini masaa 24 kwenye vitalu vyao




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Daah Michu!! UMENIKUMBUSHA mbali.. ungekuwa na muda ningeomba uende mji wa Mwadui mgodi maarufu wa Almasi Duniani. utupatie hata picha ...sijui kama mji huo bado upo au ndio ulishakula nyundo na wachimbaji..kwa wale waliobahatika kuisha hapo miaka ya Sabini mpaka mwanzoni mwa 80s MTAKUBALIANA NAMI, Mgodi huo ilikuwa Ulaya ndogo , kuanzia life style,public services mpaka mandhari ya mji. nakumbuka enzi hizo Mwadui walikuwa na ndege zao ..gharama ilikuwa shilingi 200 toka MWADIU MPAKA DAR kwa wafanyakazi ..

    ReplyDelete
  2. Hapo sawa misupu. Ukitoka hapo uende na kwenu upige picha utwekee tuone!!!

    ReplyDelete
  3. michuzi hapo ni maganzo umenikumbusha mbali saaaaana ndugu yangu mwishoni wa miaka ya 90 nilikua naenda mnadani kila jpili enzi hizo ndio maganzo imeanza kutema,,,tunakushukulu kwa kutukumbuka na huko kwetu..1

    ReplyDelete
  4. thanx for the memories.

    ReplyDelete
  5. Hivi jamani kitako cha baiskeli kinaweza kutia sugu nn....???. Nauliza tu naomba mnitoe tutani

    ReplyDelete
  6. Kwa picha hii Michu imetoa neno.
    Kumbe kweli mvumilivu hula mbivu. Ningekuwa nimeshalalamika zamaniii. Mbona kwetu huwa hupatoi. Safi sana mwanangu!
    Kula tano kabisa!!!
    Hapo ndi kwetu hivyo. Tunaanzaga kuendeshaga baiskeli ukiwa na miaka 5 na unaanzaga kabisa kusomba maji kutoka mtoni ukiwa mdogo, unabeba makorondo matatu. Hapo nakwambiaga na hata shule haipandi. Msichana au mwanamke kama hujui kuendesha baiskeli utajiju. Mwanaume haendagi kuchota maji au kusaga unga, maana mashine kwa kawaida ziko mbali-kwenye center tu. Sasa usipojua kunyonga kiuno ujalibeba debe na kuhesabu hatua hadi mashineni.
    Yaani natamani niendelee kuandikaga tu hapa.

    Misupu safi sana kakangu!

    ReplyDelete
  7. anon wa dec 01'6:56 kweli wewe ni msukuma UNAANZAGA,NAKWAMBIAGA,KUANDIKAGA.

    ReplyDelete
  8. Faida za madini hizo.
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    Wazushi mjinyonge.

    ReplyDelete
  9. Umenikumbusha enzi za Shycom & Shybush miaka ya 80s. Kulikuwa na group ya vijana wa kisukuma pale mjini walikuwa wanajifanya wanazo sana- Makunes etc. Dada zetu wengine walishindwa kuendelea na shule kwa kudanganywa na vijisenti vyao. Likizo walalahoi tukirudi kwa gogo 3rd class mpaka makwetu au Tanganyika bus, wenyewe walikuwa wanakatiwa tickets za pipa, lakini baada ya kuspend few days Shy. Lakini hizi shule zimetoa watu wenye kazi nzuri ktk mashirika mengi. ECA ilikuwa SHYCOM tuuuu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...