Watu kadhaa wamepokea ujumbe kwenye inbox zao unaoashiria kuwa umetoka kwangu. Tafadhali usifungue ujumbe wowote wenye maneno ya picha za ngono kama vile sex, nude, porn nk. unaoashiria kutoka kwenye anwani yangu.
UJUMBE kama huo hautakuwa umetoka kwangu ASILANI!
Kwa bahati mbaya anwani yangu imepokwa na kutumika vibaya bila mimi kufahamu na bado sijang'amua chanzo, kwa sasa ninakagua na kusafisha kompyuta yangu.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.
Shukrani Deo K, Dk. Mwiru R na Tom L kwa kunistua!

Katika juhudi za kusaka chanzo cha wizi na utumiaji wa anwani yangu kutuma ujumbe wenye maneno yasiyoeleweka kama vile FW, Funny, eBook.pdf,.mpg, Re nk na attachment ambazo huenda ni virusi, nimegundua imefanyika Tanzania.Mimi sipo nchini Tanzania kwa sasa hivyo sijaweza ku-access kompyuta yoyote yenye IP address iliyotumika kwenye ujumbe huo mchafu.
Kwa umbali wa mahali nilipo kutoka Tanzania, haiwezekani nikawa natumia TTCL kama ISP. Kwa bahati mbaya, ifahamu kati ya maeneo yanayohudumiwa na TTCL kama ISP mwenye anwani hiyo, ni nani atakuwa amechafua habari. Unaweza kujionea nilichokuwa natafuta na matokeo niliyoyapata ni kama inavyoonesha hapo chini.
Subi
----------------------------------------------------------------------------------
1. Received: by 10.90.67.10 with SMTP id p10mr77463aga.14.1230072401215; Tue, 23 Dec 2008 14:46:41 -0800 (PST) Return-Path: <subi.nukt...@gmail.com> Received: from acct3 ([196.43.83.236]) by mx.google.com with SMTP id 39si5110672yxd.15.2008.12.23.14.46.16; Tue, 23 Dec 2008 14:46:41 -0800 (PST) Received-SPF: neutral (google.com: 196.43.83.236 is neither permitted nor denied by domain of subi.nukt...@gmail.com) client-ip=196.43.83.236; Authentication-Results: mx.google.com; spf=neutral (google.com: 196.43.83.236 is neither permitted nor denied by domain of subi.nukt...@gmail.com) smtp.mail=subi.nukt...@gmail.com Date: Tue, 23 Dec 2008 14:46:41 -0800 (PST) Message-Id: 49516a51.e701be0a.1b83.ffffe703SMTPIN_ADDED@mx.google.com> From: "subi.nukta77" <subi.nukt...@gmail.com> To: <muXalumni@googlegroups.com> Subject: Fw: Real show MIME-Version: 1.0 Content-Type: multipart/mixed; boundary="----=_NextPart_8.29104721546173E-02" This is a multi-part message in MIME format.
2. Your IP Address: 196.43.83.236IP
Address Hostname: 236.83-43-196.
Admin.morogoro.ttcldata.netIP
Country: Tanzania, United Republic of IP Country Code: TZAIP
Continent: Africa
IP Region: Dar es Salaam
Guessed City: Dar Es Salaam
IP Latitude: -6.8IP
Longitude: 39.2833ISP
Provider: TANZANIA TELECOMMUNICATIONS CO. LTD
IP Address Tracking Program
This program performs an IP address lookup and finds the ISP and country of origin
Enter IP Address to Trace
Results of IP Tracking for 196.43.83.236
IP address196.43.83.236
Hostname236.83-43-196.
Admin.morogoro.ttcldata.net
ISPTTCL1-20051207,
TANZANIA TELECOMMUNICATIONS CO. LTD
CountryTanzania

How to handle an abusive or fraud mail
If you are tracking an abusive or fraud mail here is a possible list of email addresses to complain to.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Da Subi,
    Pole sana na swaibu hilo kubwa sana, Mungu yu pamoja nawe.Naamini kabisa kwa yoyote yule aliyepokea ujumbe huo, na pia anakufahamu, au amebahatika kupitia blog yako na kujua nini unafanya...hakika naamini hakuna anayeweza kuamini huo ujumbe umetoka kwako.

    Mdau
    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  2. NO NEWS!!!!

    hiyo ni kitu cha kawaida tu, unashtuka nini ??

    umeclick spam mails, na kucopy address book yako, na kusambaza kwa wenzio, ambayo wameshtuka hawajaclick..

    nani wa kulaumiwa

    WEWE MWENYEWE

    ReplyDelete
  3. kujituma kwa vitu hivyo ni kutokana na computer yako kuwa na virus i had the same problem from my frnd nikapokea kumbe ilikua ni viru na comp yangu ilikua inatuma endapo utapokea tu na wewe kwako itaanza kujituma u have to clean ur comp again thanks

    ReplyDelete
  4. POLE SANAAAAAAAAAAA DADA SUBI.YANI KATIKA WATU WOTE WAMEONA WEWE NDIO WAKUKUFANYIA HIVI.NAKUPA POLE SANA NA ENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWAIDA.
    BY MZAWA

    ReplyDelete
  5. Pole sana kaka Michuzi. Huyo mtu kama anasoma hili oni inabidi aache mara moja hiyo tabia kwani siyo kitu kizuri.

    ReplyDelete
  6. Hamna hiyo! Kuna wakati mtu anakuwa na ma-files kibao kwenye inbox yake. Sasa inapotokea virus kavamia kwenye pc yake, yale files na mengine yanarushwa kwenye addresses zote alizonazo.

    Sasa huyu ndicho kilichotokea. Anataka tuelewe kuwa amepokwa email yake lakini si kweli. Alikuwa amerundika mafiles kibao mengi yakiwa ya ngono. Immeshatokea kwa wengi sana hii. Asijifunike vidole kuficha macho

    ReplyDelete
  7. Anon December 24, 2008 12:40 PM,
    Nimetuma ujumbe huu kwa watu kwa tahadhari na si kuwa watu wote kwenye address book yangu walipata ujumbe huo. Aliyefanya hivi ametuma kwenye kundi pepe moja tu kati ya 6 niliyomwanachama na hakuna anwani yoyote ya mtu binafsi iliyopokea ujumbe wowote wa kipuuzi toka kwa aliyetumia anwani yangu. Hivyo si kweli kwamba amekopi address book yangu na kuanza ku-spam watu.

    Hata na hivyo, mimi ni mojawapo wa waratibu wa kundi allilotuma ujumbe huo kwa hivi mara moja nilikwenda kui-block anwani yangu mwenyewe na ku-redirect message zote kwenye anwani nyingine. Tokea kufanya hivyo, ametuma message nne tu zilizorudisha 'banned message to the sender', ni saa kumi sasa zimepita na hakuna ujumbe uliotumwa.

    Anon December 24, 2008 2:44 PM,
    Computer yangu haina virus hata mmoja. Nimechunguza na kusafisha mara tatu!

    Wadau mlionipa pole, ninashukuru sana na kama nilivyosema awali, nilituma tangazo hili kwa ajili ya tahadhari kwa watu wengi na kaka Michuzi aliamua kuiweka hewani kwa manufaa ya wengine!

    ReplyDelete
  8. Pole sana kaka. Hayo ni mambo ya kawaida. Ila umefanya jambo la maana kuwataarifu watu ambao hawafahau kitu kilichokutokea.

    Lakini kuna kitu kingine kimenishtua kuhusu mtu mmoja Emmanuel Nnko. Ninavyojua nnko yupo TRA kwa sasa. Sasa inaonyesha hizo tools za TTCL hawajachange data zao za watu gani wa kuwasiliana nao kama wakipata matatizo? Anyway, may be watakuwa wameweka aliases ambapo email zinaweza kuwa fowarded to some body else.

    Emmanuel (Mimi sio Emmanuel Nnko but nimetokea kufanya naye kazi somewhere)

    ReplyDelete
  9. Mtoa Maoni wa Tarehe December 24, 2008 10:39 PM:
    Ikiwa unazungumza uwe na hakina na unachokizungumza na si kusema alimradi unasema bila uthibitisho wowote hata ule wa kuthubutu kuandika jina lako halisi au anwani yako ili uthibitishe maneno yako. Na ikiwa unamheshimu aliyekuumba, usiwe unazungumza uongo. Yote uliyonisemea ni ya KUBUNI na UONGO, pengine imekutokea wewe ama mtu unayemfahamu.

    Uwe na soni!

    ReplyDelete
  10. Hata kama ukisema umtafute mtu alietuma itakuwa ngumu sana sana utakuta hiyo computer ni ya kwenye internet cafe za bongo manake Dar 90% ya cafe ISP wake ni TTCL. Inawezekana uliingia cafe ukasahau kusign out au ulitumia computer ya mtu ambayo imeweka Key logger, hiyo ni program ambayo kila kitu unachotype hata kama ni password inabaki kwenye computer uliyotumia mi mwenyewe nimezidaka password za gals niliotoka nao kwa style hiyo.

    Anyways, pole sana bibie.
    Hiyo ndo Darisalamu, kila kitu chawezekana.

    ReplyDelete
  11. Subi!
    Mimi nikiwa mmoja wa wasomaji wako wakubwa, sipendi kuona unabishana na watu humu.Watu watasema lo lote kukupandisha hasira.The best thing to do ni kutowajibu watu.Ukibishana na mpumbavu 'we might not notice the difference'

    ReplyDelete
  12. Mtoa Maoni wa Tarehe December 26, 2008 7:09 PM,
    Shukrani!
    Naahidi utii.

    ReplyDelete
  13. mdau hapo juu naweza vipi kupata hiyo program ya Key logger,nimejaribu ku-google ila sijaweza kuona pakuipata.tafadhali sana naomba jibu.


    bro! michuzi naomba usibane comment hii pls.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...