Michuzi,
Salaam. Pokea kikwangua anga kingine hicho kilichojengwa enzi za mkoloni wa Kijerumani kijijini Singa, Moshi Vijijini, Kilimanjaro. Ni Kanisa Katoliki la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, lililopo karibu na Hospitali Teule ya Kibosho (Kibosho Designated Hospital).
Pembeni ni nyumba ya Mapadre na hapo kuna Mlima Kilimanjaro kama ulivyonaswa hivi karibuni.
Mdau Deus Ngowi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. DEUS, THANK YOU FOR SHOWING THE WORLD THIS BEAUTIFUL PLACE, WHERE SOME OF US WERE BORN AND RAISED UP.

    IT IS A WONDERFUL SCENE. I MISS IT DEARLY. DO GERMAN TOURISTS KNOW THERE IS SUCH A GOOD ATTRACTION IN MOSHI? CUDOS DEUS. LONG LIVE KIBOSHO SINGA... Deo Mushi

    ReplyDelete
  2. Mandhari nzuri sana!Aishiye hapo anafaidi .

    ReplyDelete
  3. Asante sana Deous!! hizi zinaweza kuwa best pictures za mwaka huu...ubarikiwe Mangi!! Aikambe!!!

    ReplyDelete
  4. Jamani Kibosho kuzuri,aah yaani unaamka unasalimiana na mlima Kilimanjaro? Mdau Deus Ngowi umenikumbusha mbali saaaaaaaana

    ReplyDelete
  5. kwa ndani altare kuna art moja babu kubwa ni mchoro wa bila kukosea moyo mt wa yesu. ni image taswira nilonayo kichwani mpaka leo. naomba wadau watakapo enda hapo ku hiji this x mas watuletee tafadhali. duh memory are made of this. pia nina fobia ya mlio wa kengele za kanisa!¬! na hii itilafu ilianziaga hapa nikiwa na miaka 12 nililazwa hapo kwa matibabu. duh michu wee kiboko.

    ReplyDelete
  6. braza michuzi umenikumbusha mbaliii.....kibosho nyumbani

    ReplyDelete
  7. Asante sana kwa picha.

    Hii ni kazi ya wamisionari wa shirika la roho mtakatifu ambao wengi walikuwa waamerika (In fact wa irish wa philadephia)na wafaransa ile ya kule peramiho ilikuwa wamisionari ya Benedictino (wajeremani).

    Kwa historia hilo ni kanisa la parokia ya pili (1893)ya jimbo la moshi baada ya ile la Kilema(1890)na baadae Nkuu Rombo (1896) , Uru (1913) na kadhalika

    Nawakilisha

    Mdau Kiwoso

    ReplyDelete
  8. Inasikitisha mimi nilikuwa naamka na kuona kibo nyeupeee sasa barafu imekwenda wapi?? Inabidi tutunze mazingira tulikuwa tunaona malori yanakuja kuchukua magogo/miti kwa ajili ya mbao ni matumaini yangu sasa ilishapigwa vita. Mlima kilimanjaro ndio chanzo cha maji kwa maeneneo mengi ya Kilimanjaro hivyo inabidi Serekali ya mkoa wa kilimanjaro ipige vita aina yoyote ya uharibifu wa mazingira kuzunguka mlima huu

    ReplyDelete
  9. Nafurahi kuona picha hizi za Maputo na watu wake. Kuhusu Rais Armando Guebuza, nakumbuka kuwa wakati nasoma idara ya "Literature" pale Chuo Kikuu Dar, 1973-76, tulikuwa tunamfahamu kama mshairi maarufu. Tulisoma baadhi ya mashairi yake, yaliyotafsiriwa na Margaret Dickinson, na kuchapishwa katika kitabu kiitwacho "When Bullets Begin to Flower," kilichochapishwa na Tanzania Publishing House. Viongozi kadhaa wa Msumbiji, na wanaharakati katika vita vya ukombozi, tuliwafahamu kwa mchango wao katika fasihi, wakiwemo Marcelino Dos Santos, ambaye ni mshairi, na Louis Bernardo Honwana, mwandishi maarufu wa hadithi. Kitabu cha hadithi zake zilizotafsiriwa, "We Killed Mangy Dog," nilikuwa nakipenda sana.

    ReplyDelete
  10. he jamani thanks wanikumbusha mabali nilisoma Kibosho Girls Sec wakati huo ilikuwa hapo mlimani. Kanisa hilo lilinikomesha (utoto) kila asubui kabla kwenda breakfast lazima kwenda kanisani na kuoga maji yanayotoka mlimani wow.... Siyo home town lakini beautiful area. Its only now (adult) una realize the beauty of the place. Thanks for the memories.

    ReplyDelete
  11. da hapo naona coment za wachaga tu wajeruman walikuja kaka ulieuliza hapo juu wakachukua chao waka waacha na hizo fantas za kuzuri mara hii ndio taswira ya mwana
    anyway taswila imetulia na wakibosho nao wangetulia kama taswila tanzania ingekua mbali sana polotical social na economcal
    thanx.

    ReplyDelete
  12. NDUGU ZANGU KUNA SIKU NILIKUWA LIBRARY KATIKATI YA JIJI LA LONDON CHUONI "UEL" NAPERUZI,NIKAKUTANA NA KITABU KINAZUNGUMZIA KUUSU MAMBO YA "EAST AFRICA" NIKAWA VERY INTERESTED KUKIPEKUWA,KINAONGELEA KUUSU CHIMBUKO LA KISWAHILI NI KUTOKA KENYA,NA KUWA MLIMA KILIMANJALO UPO KENYA,NIKASEMA KWELI WAKENYA WAMETUZIDI UJANJA LONG TIME,YANI HICHO KITABU NI CHA LONG TIME,KWELI TULIKUWA TUMELALA NDUGU ZANGU,TWENDENI SHULE ILI HAWA WAKENYA WAACHE KUTUCHEZEA NA KUTUDHALAU,ELIMU TUU NDO ITAWEZA KUTUPA CONFIDENCE!HAKUNA MKENYA ATAKAE KUDHALAU KAMA UPO GRADUATED,NADHANI SISI NDO TUTAANZA KUWADHALAU WAO!

    ReplyDelete
  13. Michu umechokoza nyuki...!! Ngoja wale wabeba maboksi waliosomeshwa na hilo kanisa na sasa hivi wapo Newala ama Ukerewe waanze kuongea ..!! Mbona tutakoma!! Au wale wa mahujaji wa Dar - Moshi kila krismasi na pasaka!! Comment zao hazikosekani humu..!! Ipe kama muda tu utaona mwenyewe Michu..!!

    ReplyDelete
  14. Duh...Kenya kweli tambarare,yaani mlima wetu Kilimanjaro kunapendeza...naam...Harambeeee!!!!

    ReplyDelete
  15. Mdau Anony hapo juu 9:22 PM, sasa wewe unalalamikia habari hizo potofu wakati wewe mwenyewe kiswahili sahihi kinakushinda. Mtu atakayekutana na wewe lazima aamini kiswahili kilianzia Kenya. Maneno kama "Kuusu", "Kilimanjalo", "Kuwadhalau", "kukipekuwa" kama ulivyoandika yote ni makosa kitahajia. Maneno sahihi ni "Kuhusu","Kilimanjaro","Kuwadharau", na "kukipekua." Nakushauri urekebishe lugha yako kwanza kabla ya kutoa hoja.

    ReplyDelete
  16. Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya na pia wadau, samahani. Ujumbe wangu hapo juu unaohusu masuala ya Msumbiji, nilipangia niuweke kwenye ile sehemu inayohusu ziara ya JK Msumbiji, lakini nikafanya kosa kiutendaji. Samahani sana. Hata hivyo, naungana na wadau katika kumshukuru huyu ndugu aliyetuletea picha za Kibosho. Ni nzuri sana.

    ReplyDelete
  17. KIBOSHO TAMBARARE!!! MBONA JAMAA ZETU WAMEJAZANA HAPO MANZESE??? DAR TU NDO TAMBARARE, SI UNAONA WATU WOTE WANAVYOKIMBILIA.

    ReplyDelete
  18. AH bana !
    Mandhari ya mwambao ndio bora,hiyo picha nzuri kuweka ukutani tu.

    Ntaamini huko ni kuzuri siku woote mtakapo rudi kwenu badala ya kukimbilia mijini kuosha viatu.

    ...Au atleast mwende kufungia ndoa pembeni ya mlima badala ya ufukweni . LOL !

    ReplyDelete
  19. HE!we anon wa dec.16 @ 10:48
    kwani hakuna wakibosho walio ulaya? kama wapo kivipi hii picha inawachokoza ??
    Huupati uhalisi,Bado una mentality ya kusindana na Rwanda na kenya badala ya kuangalia nyumba yako .

    ReplyDelete
  20. So nice I love it!! Kwa ujumla sehemu nyingi huku uchagani zilizoachwa na wamisionari zinatunzwa

    ReplyDelete
  21. KIBOSHO INAVUTIA SANA LAKINI KUNA SEHEMU NYINGINE MKOANI KILIMANJARO NAZO NI BOMBA SABA. KULE KILEMA MAUA NA MACHAME NRONGA. HAYA MAENEO BOMBA SANA. KOTE UCHAGANI WATU WAMEENDELEA LAKINI, UKILINGANISHA NA MAENEO MENGINE NCHINI.

    ReplyDelete
  22. HOME SWEET HOME.... I love this place... I am proud of Kibosho and their people. Wakibosho bwana ni wahangaikaji..watafutaji to the maximum. Ukioa au kuolewa na mkibosho hufi njaa hata siku moja. Kingine kikubwa wakibosho wanapenda sana familia zao. I love Kibosho my home sweet home. Kibosho by the graces of God, i will see you sometimes next year. If any of you is going for Christmass Holidays, jamani Kisusio mniletee huku ukerewe basi au sio! Msininyime kitalolo...!!! Mtori...!!
    Mu-wadikire wooose pinyi!!
    Ruwa ngakuterewa baba mbe luakanye shiwana shafo!!

    ReplyDelete
  23. SOMENI HII HABARI TOKA KWA MTANZANIA MWENZETU MKALI


    East Africa Integration: Why Tanzania is Cautious


    There is great concern in Kenya and Rwanda in particular with regards to the stance Tanzania has taken reminiscent to the integration of East African states and free movement. The most recent evidence is an article that surfaced in Kenya’s Daily Nation newspaper accusing Tanzania of being a liability in the integration of the region. The said article accused Tanzania of being parochial with full view of rot and poverty!

    What brought all this kafuffles is the fact that Tanzania did not consent to free movement of East Africans. This is seen as curtailing the whole process of unifying the region! Full packed with salvos, dirty and unreasonable language, this, if anything, crossed the line so as to cause some brouhahas and bugaboos from the other side- the target. Let me not go the same evil way. Abusive language and threats won’t bring Tanzania into the fold but rather push her far away.

    But why, is Tanzania becoming an obstacle really? If reality is faced, there are strong reasons. The borders we’re taking pride in were demarcated by colonialists in order to weaken and divide us. Our people have always been one and we should strive for this in lieu of double standards and egoism.

    Needless to say, Tanzania is wary but not afraid. Many landless East Africans will invade her and grab her land. This will create animosity among Tanzanians, their government and East Africans from other countries. This stance is somewhat reasonable. Why should Kenya allow fertile land to be owned by a few rulers and white settlers without paying a damn to the majority landless? The family of the country's first president, Jomo Kenyatta, owns a chunk of land the size of Nyanza Province. His successor, Daniel arap Moi and Mwai Kibaki own big parcels of land, not to mention former British settlers. In May 2006 Cholmondeley, grandson of Lord Delamere, shot dead an innocent Kenyan for ‘trespassing’ on his Soysambu farm.

    If we sincerely mean business, Kenya should harmonize her notorious and nasty land policies whilst Uganda and Rwanda should embrace true democracy. Otherwise egoistic ‘ours is mine but mine is mine’ will never help. No fool at this time can subscribe to this bulimia. Kenyan authorities should be told to their face that without equal and fair re-distribution of land, the whole process will end up a cropper.

    Let’s look at another naked reality. Even if one compares the population of Tanzania and other East African countries, he’ll see why Tanzania is hesitating. Look at the reality in numbers: Burundi is 27,830 sq km with a population of 8,691,005 or 315 people concentrated in a square kilometre; Rwanda is 26,338 sq km with a population of 8.3 million that is set to double to 16 million by 2020. Its population density is the highest in Africa and has risen from 183 per sq km in 1981 to 345 per sq km in 2000. Rwanda’s rural population per square kilometre of arable land was around 901 in 1999 -- one of the highest in Africa. Kenya is 582,650 sq km with a population of over 30 million. Density is 2 settlers per sq. km, while in the rich and fertile western region, population density goes up to 120 settlers per sq. km. Uganda is 241,139 sq km with a population of at least 27.7 million and a density of 241 per sq km in 1999. Its population is projected to explode to approximately 66,305,000 by 2050. Tanzania is 945,100 sq km and, according to the United Nations, had an estimated population of 36,977,000 in 2003. The population density was then 39 per sq km.

    Demographic realities are not something to ignore. Even the superpower and richest country of the world, the US, is currently erecting a 3,200 kilometre fence on its border with Mexico to curb illegal immigrants. But Mexico like Kenya does not see this.

    Another point the detractors put forth is that Tanzania is afraid of Kenya’s vibrant economy. Let us face it. No African country can take pride when its economy run by corrupt officials in conjunction with foreigners. Who owns Kenya’s economy? Does the guy living in Kibera or Mathare associate himself with it? How can this “vibrant” economy become meaningful if the rulers do not even want to pay tax?

    The economy that does not serve the majority of the citizenry is as good as nothing. So instead of fearing each other, we need to put our houses in order so as to integrate our people who, in essence, have no obstacle to this integration and they are always ready.

    Another oft-ignored fact is that not all East African countries are under democratic rule. In Rwanda and Uganda, there are autocratic regimes- not to mention rebels fighting them and Kenya’s tribal animosity. So shall this be ignored, peaceful countries like Tanzania will nary blindly consent to this suttee. This is a challenge to other countries to cleanse their messes so as to forge ahead.

    Anybody doubting Tanzania’s commitment to the integration must go back to history which is a good judge. Shortly before attaining independence in 1961, Tanzania wanted to delay its autonomy until all colonies in East Africa were ready for the same status. What exemplary pan-African love and spirit! Tanzania still remembers the loss suffered from the 1977 debacle of the first East African Community as a result of megalomaniac rule in Kenya and Uganda spearheaded by Kenya’s former AG, Charles Njonjo.

    We must face all these realities before complaining or giving in. My belief is strong that East African countries will unite. But this should go tete a tete with putting our houses in order. If our rulers truly mean unification, let them form one country with everything instead of looking at their presidency. Failure to this Tanzania has all reasons to worry and curtail the integration. Shall we fairly and diligently treat ourselves; we’d dwell on our strength in lieu of weakness and egoism.




    By Nkwazi Mhango
    Mhango is a Tanzanian living in Canada. He is a Journalist, Teacher, Human Rights activist and member of the Writers' Association of New Foundland and Labrador (WANL)

    ReplyDelete
  24. Jamani hilo kanisa na mandhari yake yanafanana kabisa na kanisa lililoko Kilema Chini huko Moshi. Naomba mdau atakayefanikiwa kupata picha ya kanisa la kilema Chini RC aiweke humu ndani ya Michuzi. wajameni mtashangaa majengo hayo na mazingira yalivyofanana.

    ReplyDelete
  25. michuzi habari za kuaminika eti unavaa kiatu size number 6 je hii ni kweli? na kama ni kweli ukienda dukani unapo taka kununua kiatu unasema nataka size ya watoto ama unanunua vivyo hivyo? kaka michuzi nakuchemsha lakini post tu komenti naonaga miguu yako midogo sana nimeona nikutanie kidogo.

    ReplyDelete
  26. bwana michuzi asante sana kwa hizi picha za kibosho. kwa sisi wengine tulio mbali bring tears to our eyes. this is my best christmas present. keep it up

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...