Kwa unyenyekevu tunatoa Tribute’ za Mpendwa wetu Salome Phillemon (Original Chaoo), aliefariki tarehe 07/11/2008, huko Kisarawe Mkoa wa Pwani na kuzikwa tarehe 09/11/2008, huko huko Kisarawe.
Salome Phillemon alizaliwa tarehe 15/05/1918, na kupata elimu ya msingi na za Chama na Jumuiya ya Chama cha CCM kwa vipindi mbali mbali na sehemu mbali mbali za nchi yetu. Alikuwa kiongozi wa Jumuiya ya Wanawake enzi za Tanu na mama Maendeleo wa Kisarawe kwa muda mrefu. Alishawahi kugombea Ubunge wa Kisarawe na alikuwa ni muumini mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi.
Aliolewa 1936 na Bwana Johannes Marko Kuga (Marehemu tangu 1987) na kujaliwa kupata watoto 11 (7 wakike na 4 wakiume) . Mume wake(baba yetu) alikuwa mfanyakazi wa Kanisa hivyo waliishi sehemu nyingi hapa Tanzania.Watoto wa kike ni; (Mrs Teuka Mwombela, Mrs Monica Sozigwa, Ms Maud Kuga, Mrs Veronica Opanga, Mrs Agnes Muganda , Mrs Beatrice Makani na Mrs Martha Kayige(Marehemu), watoto wa kiume (Mr Daniel Kuga, Mr Thomas Kuga(Marehemu) Mr Jacob Kuga na Mr Yosia Kuga (Marehemu)
Watoto hao walijaliwa watoto 68, (wajukuu ) wakike na wakiume, ambao nao pia wamejaliwa watoto 83 (vitukuu), baadhi wameshapata watoto 7(vilembwe). Mnaweza kunisahihisha; kama ni wajukuu wanazaa vitukuu na vitukuu wanazaa vilembwe.
Ni jinsi gani tunadaiwa shukrani kwa wote walioshiriki kumuuguza, kutusaidia kwa hali na mali, kutuma salamu za rambi rambi, kutuma maua, hadi kumlaza pale Kisarawe Mama yetu Bibi yetu huyu.
Pia kwa Umati wa watu wanaohusika kwa kila alietajwa hapo juu, pamoja na familia za wakwe zao na waume na wake wa wajukuu na vituu wake na rafiki zao wote, Majirani tunashukuru kwa uvumilivu wenu, Madaktari asanteni kwa kumpa msaada.
Viongozi wa dini mbali mbali hususani Kanisa la Anglican kwa kumpa msaada wa Kiroho hadi saa ile anakata roho mkimpaka mafuta ya Wagonjwa … Mbarikiwe sana.
Ushuhuda mkubwa ni wingi wa watu walijitokeza Kisarawe tangu tarehe 7th November hadi siku ya mazishi…
Mwenyezi Mungu asiwapungukie, awabarikie na waume/wake zenu watoto wenu, kazi za mikono yenu na roho zenu.
Alipenda kila alieletwa na watoto na wajukuu zake pale kwake, alipenda kusaidia na kumtolea Mungu fungu lake la kumi katika kanisa lake hata kama alipewa za chakula chake. Basi Mwenyezi Mungu tunakuomba uzikumbuke kazi za Mjakazi wako huyu na Umlaze Mahala pema Peponi.
Kutakuwa na sala ya Kumshukuru Mungu kwa maisha yoofu ya Mama huyu siku ya tarehe 13/12/2008 hapo hapo Kisarawe. Mnakaribishwa sana wote. Watakao weza kukesha nasi siku ya Ijumaa tarehe 12/12/2008 hadi tupate chakula cha mchana siku ya tarehe 13/12/2008 mikono miwili tunawakaribisha.
Ni mimi kwa niaba ya Ndugu zangu,
Beatrice Makani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kuishi maisha marefu ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Upumzike peponi bibi yetu

    ReplyDelete
  2. We are going to miss ever sooooo much bibi. We wouldnt be here without you. May God grant you Eternal Rest and Peace!!!

    ReplyDelete
  3. R.I.P. bibi Sally.

    ReplyDelete
  4. We love you Bibi Salome and we ALL are going to miss you. May you rest in peace. Thank you for everything Bibi we are luck people to have you as our angel lady.

    ReplyDelete
  5. Mai Waifu. Rest in Peace. To All Mama Bigs and Mama Smalls Poleni!

    Bibi I hope mtaendeleza libeneke na Mama Juma. Miss you All!!! (LOL)

    UncleMGEE

    ReplyDelete
  6. RIP Bibi Salome, We will surely miss you.

    From Reena, Nicola and Natasha

    ReplyDelete
  7. POLE SANA AUNT YANDU MPENDWA EGNES NIPIE POLE MA-AUNT WOTE NA WAJUKUU NA NGUNGU WA MAREHEMU. NAJUA MMEPATA PIGO KUBWA LA KUMPOTEZA KIPENZI WENU NA PIA MMEMLILIA NA MTAENDELEA KUMLILIA HAPO NAPENDA KUWAKUMBUSHA TU ENDELEENI KUMLILIA NA PIA KUMFANYIA IBADA PALE MNAPOMTAJA HAU MNAPOONA MMEMKUMBUKA KWANI IBADA YETU NDIO NJIA PEKEE ITAKAYOMFANYA MPENDWA WETU BI SALOME APUMZIKE KWA AMANI MIMI HUWA NAAMINI MTU YEYOTE MZURI ANAPOTUTOKA HUWA HANATUTOKA MWILI LAKINI KIROHO BADO TUPO NAE SASA TUAMINI KUWA BIBI AMETUTOKA MWILI LAKINI KIROHO TUKO NAE.SINA MENGI MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA PENDWA WETU BI SALOME MAHALI PEMA PEPONI AMEN QUEEN KOMANYA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...