mdau wa peramiho katuletea hii kuonesha twin towers za huko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hivi twin towers kwa kiswahili sanifu nini jamani?
    M3

    ReplyDelete
  2. twin tower zimetulia, wajerumani wamepafanya vizuri sana

    ReplyDelete
  3. twin towers=matawi yanayotoka tumbo moja

    ReplyDelete
  4. Hapa kuna printing press na duka la vitabu ambapo vile vitabu adhimu na adimu kama "Someni Bila Shida Book 1 na 2, Hekaya za Abunuwas, Machimbo ya Mfalme Suleiman, Hadithi za Inkubu, Nyleptha, Umslopagaas vinapatikana na vinginevyo vingi, kuna hospital maarufu ya peramiho, kuna tailors wazuri ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa akishonewa nguo zake na mpaka sasa kuna baadhi ya waheshimiwa wanapatumia, kuna butchery, bakery n.k Wanajitegemea kwa umeme na maji, Wajerumani walipajenga na nafikiri hawakutegemea kuondoka, inasemekana kuna madini kwa kuwa haikufikirika walifuata nini miaka hiyo ya 1900's. Twin Towers ni Minara Pacha

    ReplyDelete
  5. Asante kwa kunikumbusha nyumbani.
    Salaam kutoka Njambe..

    ReplyDelete
  6. Twin towers MINARA MAPACHA

    ReplyDelete
  7. Hapo panaonekana kama jela la alkatrazi...duh bora kwetu Mbeya!!!

    ReplyDelete
  8. umenikumbusha mbali sanaaakipindi kle cha kumzika fr Gottard OSB kwenye makaburi ya "kizungu" kwenye fensi inayoonekana kona ya chini kushoto.

    ReplyDelete
  9. Penyewe umekumbusha mbali sana mwenzako.Wangoni oyeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. Peramiho ile ya zamani enzi za Askofu Komba achaa bwana. Palikuwa panatisha kwa vile ilikuwa ni kitovu muhimu kwa mikoa ya kusini katika nyanja za tiba (hospitali), Ufundi sanifu ( trade school),ufundi magari( machenical school),uuguzi ( nursing school), elimu ya sekondari kwa wasichana, uchapishaji, kwa kutaja machache. watu walikuwa wakisafiri kutoka mikoa ya mbali kufuata huduma za kisasa za tiba kwa madaktari wa kijerumani km Dr Ansgar, na waswahili wachache. Lakini hivi sasa hali imekuwa mbaya.Sababu zitolewazo ni kuwa kiongozi wa sasa anaihujumu, kutokana na uelekeo wake wa kuendekeza ukabila.Hata major seminar ya muda mrefu hapo inasemekana ni choka mbaya, hasa baada ya mpango wa awali wa kuifanya chuo kikuu cha katoliki, kuhamishiwa Iringa kwa kiongozi huyo. naambiwa madaktari bingwa wote wamekimbilia Ndanda hospital wilayani masasi ambako kiongozi huyo, ambaye wakati wa harakati za uchaguzi mkuu wa 2005 alijiingiza matatani na waumini wake kwa kumpigia debe kanisani mgombea wa kabila lake, jambo ambalo lilimfedhehesha sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...