Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. kikosi hicho kinanikumbusha enzi Tanzania ikipiga hatua kubwa kisoccer, hususan uzalendo katika kupigania maslahi ya timu na nchi, tofauti na hizi sasa ambapo ubabaishaji katika vilabu si kitu kigeni. nawaona akina Chitete, dilunga, sembuli, omar kapera, we acha tu

    ReplyDelete
  2. Cha kushangaza sana ni kuwa wachezaji wetu enzi hizo walikuwa wameshiba. Warefu na wenye nguvu waangalie hapo Yanga walivyokuwa wanatisha!

    Kuanzia kipa mpaka ma-forward wote wapekwenda juu na walikuwa wanauwezo wa kunfunga yoyote yule.

    Ninao wakumbuka hapo ni Omar Kapera (Center half wa nguvu enzi hizo). Kipa Muhidini, Chitete, Marehemu Sembuli, Dilunga,Kitwana Manara, Cach Prof. Victor, Abdulraman Juma... Wadau nisaidieni kumalizia.

    Hiyo yanga ilikuwa tishio sana, iliikuja cheza na timu kama Flumenence (Brzl), Aston Villa walikujaga TZ enzi hizo... Waliwatoa kamasi Asante Kotoko katika ubingwa wa Africa hawatasahau.

    Asante michuzi bahati mbaya nchi ilikuwa haijaendelea sana kama tungekuwa na kanda za video za wakati huo ndiyo watu wangeelewa naongelea nini lakini kiwango cha mpira wa Tanzania kilikuwa juu sana wakati huo.

    Wengi wa wachezaji wa kipindi hiko walikuwa size ya Drogba wa Chelsea ukitaka kuelewa naongelea nini.

    ReplyDelete
  3. MFANO HALISI WA KUSHUKA KWA LISHE TANZANIA....ONA JINSI WANAUME WA ENZI HIZO WALIVYOKUWA WAMESHIBA....FANANISHA NA HALI ILIVYO SASA....LISHE TU

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na walionitangulia hapo juu. Sasa hawa ndio wachezaji angalia maumbile yao, angalia walivyopanda kwakweli wanapendeza. hawa ndio celebreties and guess what mpira wao pia ulikuwa juu. Wachezaji wa siku hizi ni wamechoka na mpira pia hauendi. Timu ya mpira ndio inatakiwa iwe hivi kuanzia golikipa na wachezaji wengine. Hata timu kama Brazil, Argentina, Italy utakuta wachezaji kinaeleweka. Maradona alikuwa ni mfupi lakini mwenye nguvu za kutosha sana kiuchezaji.

    ReplyDelete
  5. Swala hapo waa siyo kushuka kwa lishe bali ni ula chakula likicho bora. Hawa wajomba walikuwa hawali chipsi mayai, kuku broiler na soda pop. Hawa walikuwa wanakula chakula cha kikweli kweli, mihogo, ugali, magimbi, samaki, (siyo wa kopo) na kadhalika. Eni hizo watu walikuwa hawaumwi kansa Afrika.

    ReplyDelete
  6. Dunia inabadilika, hata huku ULAYA unawaona watu wadowagodo, tufupi kama mbilikimo, wakati hawa jamaa walikuwa mabonge ya watu, hata TANZANIA siku hizi watu wengi ni vijitu tu, kuna mabadiliko fulani ya kidunia, pengine evolution is happening and we are towards the end of our species. Figure zetu zinazidi kuwa kiduchu, I guess somthing is happening, research on it is needed.

    ReplyDelete
  7. Jamani kuna mwenye kuwajua hawa wachezaji. Na wako wapi sasa

    ReplyDelete
  8. Wewe anonyDec 24th 2008, 12:47AM acha kufunga watu kamba kuwa watu ulaya walikuwa mabonge zamani.

    Angalia picha na video za 1980 kurudi nyuma, jamaa wa ulaya walikuwa sio vibonge kama sasa.

    Ndo maana hata Generali Idi Amin aliitisha mikutano ya harambee ya kupata mbuzi, magimbi,viazi mbatata awapelekee Waingereza waliokuwa wanakufa njaa miaka ya 1970, mwingereza kwa aibu kama ilivyo kawaida akakataa huo msaada kutokana na aibu.

    Ila sasa Waingereza ni vibonge kwa ajili ya chakula kisicho asilia-halisi yaani 'organic'. Sie sasa Tanzania tumedumaa kwa ajili wa umasikini kama ilivyokuwa Uingereza ya miaka hiyo '1947'.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...