Home
Unlabelled
harrier for sale
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mdau naomba nikupongeze kwa kuweka bei wazi.
ReplyDeleteUmeonesha mfano wa kuigwa... mambo ya "Kupata bei piga simu namba xxxxx" huwa yanakosesha watu wengi biashara bila kujua na yanaleta usmbufu usio wa lazima kwa wateja na kwa muuzaji.
Ila kwa kuweka bei umepunguza usumbufu maana mtu ambaye $20,000 ni parefu wala hasumbuki tena kupiga piga simu.
Siku njema,
Fred
its 2.1 litres
ReplyDeleteHarrier hazina deal siku hizi. Zimeshuka sana bei. Unapata kwa Milioni 7 tu za kibongo. Kwa kuwa ni biashara, nakutakia mafanikio.
ReplyDeletendugu yangu, samahani kwa kukukatisha tamaa. lakini hiyo gari inapatikana kwa bei ya chini ya hapo. kwa hiyo labda upate mtu kutoka shinyanga au mwanza ambaye ameshauza ng'ombe zake na hajui bei za magari. angalia bei autorec, au japanesevehicles.com, au avongroup.com, utajua kuwa umechemsha kwa hiyo bei.
ReplyDeleteitabidi upunguze mpaka nusu ya hiyo bei uliyotaja.
Kila la kheri
Hii kweli kali! Ina vifaa km ile ya Obama nini? US$ 20,000 = TZS 20,000x1,400 = 28,000,000! Wee hii ni ya kununulia shangingi la mwaka huo huo!
ReplyDeleteHizo ndiyo za watanzania, wakati mwingine huwa nashangaa kama kweli wanamaanisha hizo bei au wanasema tu? Mfano mwingine ni wa kwenye matangazo ya kuuza nyumba au viwanja, utakuta mtu anaongelea $100000 kiwanja ambacho kiko sehemu za ajabu ajabu je ni mtazania gani mwenye uwezo wa pesa kiasi hicho kama siyo mafisadi na wauza maunga?
ReplyDeleteHizo ndiyo za watanzania, wakati mwingine huwa nashangaa kama kweli wanamaanisha hizo bei au wanasema tu? Mfano mwingine ni wa kwenye matangazo ya kuuza nyumba au viwanja, utakuta mtu anaongelea $100000 kiwanja ambacho kiko sehemu za ajabu ajabu je ni mtazania gani mwenye uwezo wa pesa kiasi hicho kama siyo mafisadi na wauza maunga?
ReplyDeleteHivi huyu jamaa anauza hili gari kinachomfanya ana overstate price ni hilo body au, hizi gari mbona cheap sana yaani FOB $4,578 unapata kitu kama hiki ongeza na kodi haifikia hata $10,000 mwambie aache utani acheki hapa kwanza kabla ya kutangaza fanyeni market survey siyo kulipuka na bei za Manzese tena unatangazia kwenye Net bora ataa angetungika kwenye nguzo ya umeme mtu hawezi cheki real market price in the work.
ReplyDeleteHebu cheki hii link hii halafu ufikirie bei upya kama muuzaji.
http://www.tradecarview.com/used_car/japan_car/toyota/harrier/1659174/
Oya wadau sio busara kutoa comment za aina hiyo, wewe km unajua pa kuzipata si ukanunue. Ila hupaswi kumkatisha tamaa mfanaya biashara km wewe ni maskini. Ila im sure atauza tena bila kupunguza sh. 1
ReplyDeleteSasa wewe michuzi unamwekea blogger Tangazo lake la biashara halafu hapo hapo unaruhusu comments za kumwaribia biashara yake.Sipati picha.Wewe mwenye gari usipanic utauza tu(Huo ni 'usenene')
ReplyDeleteWadau,
ReplyDeleteKwenye biashara kuna kitu kinaitwa "asking price".
Alichotaja muuzaji ni "asking price", kwa hiyo kama wewe ni mnunuzi at least una pa kuanzia katika negotiation.
Kwamba hilo gari linauzwa Japan kwa $4,578 hadi $8,000 sio ishu maana mteja anayelengwa hapa ni yule anayetaka gari SASA HIVI, na anataka alione kwa macho yake, alitest, etc.
Sio kila mtu ana muda wa kusubiri miwezi miwili mitatu gari ije toka Japan.
Kwa Mdau wangu unayeuza gari kikubwa fahamu kwamba wadau tunaocomment hapa sio wanunuzi.
Wanaohitaji hilo gari watakupigia simu muongee.
Siku njema,
Fred
wabongo bwana kwa kuongea ameweka bei wazi kwa maana ya kwamba hataki usumbufu wa kupigiwa na wasumbufu kama unajua pa kununua yanini kupiga kelele
ReplyDeletewabongo bwana mwennyewe nimenunua juzi tena six cyl kwa 26m, hii 4 cyl itakuwa ghali kushinda mi siyoni ajabu kwa bei hii kwanza yen ipo strong kwa dola kwa hiyo hata magari jap yamepanda ila watu wengi hawaelewi wanaongea tu,lakini waswahili kawaida yao kuongea,nakushauri stick to your price its worth it,tena na ma tv umemwekea
ReplyDeleteMbona wanakusakama sana? Nafikiri ulisahau kumalizia na trade mark phrase ya machinga "...pungufu unaongea...". Halafu wewe unayekandia watu wa Shinyanga na Mwanza ukome kwa sababu walijua bei za magari kabla ya wengi wenu. Unawajua wewe Idukilo au Lupondije na Banabakwe?
ReplyDeletemnaojua pakuzipata gari za bei rahisi kanunueni,kama lngo ni kuwasaidia wateja kwa ujumla basi tumieni lugha nzuri kufikisha ujumbe.
ReplyDeleteAcheni kejeli za kitoto,maisha haya !
wewe Kipili kazi yako ni kukaa kwenye computer na kuangalia bei ya magari. Inaonekana umepunguzwa kubeba boxi....
ReplyDeletewewe SENENE unachonga sana, benzi AMG la J.Mashaka lilipowekwa ukasema linanunuliwa FOB &,7,000
Leo hii harrier ni FOB $4,578 babu umechemsha, nenda ukanywe kwanza ndo urudi kutumwagia pumba. Kwanza harrier yenyewe hauna ubavu wa kuupanda hacha kununua
Au tumia huo muda kutafuta kazi siku hizi wanaweka applications online. Fala weye, au ukishindwa kauze kopo lako linalokufa njiani mara 4 ukienda kwenye ubeba boxi
Mwenye Harrier
We muuzaji anony wa January 26, 2009 1:49 PM
ReplyDeleteOya vipi, mbvona unajifagilia kwa kujiandikia comment mwenyewe???
Gari hilo unauza bei ghali sana. Halafu unauzia kwenye yadi japani.watu wajanja siku hizi.
Subiri WANYARUGUSU WAJE TOWN.Sidhani pia, kama utawapata.
ndugu zangu wa-Tanzania, unajua kama huwezi kununua bidhaa unakaa kimya.Kwnai huwa unaenda dukani ukiona kitu ni bei ya ghali unaanza kumpondea muuza duka? kama bei huwezi basi nenda kanunue huko unakoona ni cheap, kukatishana tamaa na kuharibiana biashara ni kurudishana nyuma kimaendeleo, kama huna vijisenti kuna watu wanavyo na ambao mnabeba mabox siku nyingi hamjafika dar, fanyezi utafiti kuhusu kodi za gari kama hiyo baada ya kuitoa japan, jamaa anasema imeshalipiwa kodi zote. Think!!!
ReplyDeleteSkia mtu wangu,
ReplyDeletehata kama hiyo ni bei ya kuanzia, lakin umeanza mbali sana,
hata FOB ya 4,578 alietaja jamaa hapo juu ni kubwa sana,
Kwa taarifa yako hizo gari zaianpatikana kwa mpaka FOB ya 3,750, na makoro koro mengine haizidi 8,000 mpaka iingie barabarani,
Labda useme unauza gari mbili kwa bei hiyo ndo angalau utampata mtu.
MUOSHA KINYWA ORIGINAL
(a.k.a SENENE)
Laana za kifisadi za mapepo wachafu wa US BLOGGER zimewafikia hadi na usenene wake mnaionea hadi gari wivu
ReplyDeleteMh.Mashaka inabidi urudishe economic crisis ili haya masenene yashike adabu. Kweli tumelogwa
haya majitu yenye wivu ni mabeba boxi ya majuu.... Hayana kazi zaidi ya majungu na U Us blogger
ReplyDeleteYalaaniwe kwa jina la baba
Yaani mimi sihitaji kununua hii gari ila nimekerwa sana na hawa watu wnaolalamika kwamba bei ni kubwa. si ajabu ndio maana watu wengine wanaweka namba bila kutaja bei. watu wa aina hii kawaida hawana magari kabisa ni sawa na wale wanaosema mark 2 hazina dili ukimwangalia hata corolla hana.
ReplyDeletekwa mawazo yangu hiyo bei iko reasonable. ingekuwa vyema tukajadili kuhusu usumbufu wa kutoa mizigo bandari ya dar. na wale mnaoponda jaribu kusafirisha hata honda civic alafu ujue ni jinsi gani inavyosumbua kuagiza gari kutoka nje.
Kuna kitu tunaita "CAVEAT EMPTOR" (Buyer Beware). Tunachofanya hapa ni kuwafanya wanunuzi kuwa na ufahamu tu wa nini kilichoko sokoni. Kwa kuwa wewe muuzaji umeleta kwenye blog ya jamii kifaa chako basi sisi tunachofanya ni kuiweka jamii hiyo hiyo makini ili mtu akiamua kukuzawadia $20,000 ili ukanunue zingine mbili asije akajuta hapo baadae kuwa wadau tulimwacha akavutiwa machakani ni kuchunwa ngozi na wamachinga wa magari. Hapa hatujakataza watu wasinunue la, ila tuwapa hali halisi waujue mtaa wa Congo, kitu cha shs 200 unauziwa Shs 2,000
ReplyDeleteKama lengo la muuzaji ni kukuza mtaji basi akakope bank vinginevyo humu ni USENENE Kwenda mbele, huwezi tangaza bei ya magari mawili kwa moja be reasonable!
Siku ingine kalipie TBC au Daily news matangazo watu wakiona/wakisoma hawazi kuweka comment Ukazisoma.
Ila hapa TUNAKONGOLI Tu unagoogle unapata kitu unaona ukweli then unarudi "SENENE" laini kama unanawa vile, na wewe mw
Kweli nimeona lina number ya Japan! Bongo kweli Bongo!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMdau wa Nagoya, japan
ukiwasikiliza wabongo hutofanikiwa,wanaongea sana,hao wanaocomment vitu vya watu hadi leo hata baiskeli hawana,na mungu anajua watu wa kuwapa riziki,mtabaki hivyo hivyo, na miwivu
ReplyDeleteNawafagilia wote waliotoa komrnti kuponda bei kama bei ni mara dufu ya bei halali.
ReplyDeleteEti biashara, kwahiyo aweke bei kubwaaaaaaa. Acheni hizo.
Usijifanye mstaarabu wakati usitaarabu wako una viji-elements vya kifisadi. Yaani unafurahia mtu kudouble bei?
Big up sana kwa wale wazowefu wanaotoa bei za kweli. Zero matrix kwa wale wenye usitaarabu wa kifisadi.
Hapa ni katika Jamii, kila kitu kiwe na faida ya jamii,. Hivi sasa nchi imekamatwa na mafisadi wananchi tunalia, hali ngumu, hakuna uzalendo, halafu mijitu mingine bado inaendeleza ufisadi kwa kutumia web za jamii kama hii.
ReplyDeleteMuuaji ni muuaji tu, hata kama anakuua taratibu huku anakubembeleza. Hii iwe fundisho, mtu akitaka kuuza kitu hapa, basi awe reasonable.
Sounds like a I want to make a profit, a 2009 model costs 30,000 Dollars.
ReplyDeleteGood luck but that price is just too steep.with that much I can get two 1999 Lexus RX 300(which looks like Harrier).
Namfagilia kapili,
ReplyDeleteInaonekana ni Mchangiaji makini sana,
Sio mtu unakurupuka tu na kuanza kutaja bei ambazo refernce zake hazijulikani ilikotoka,
We kama umeuziwa kwa bei kubwa huko ulikonunu basi ni wewe,
Ufisadi hauusiani na EPA tu,
hata ku-double price ni element hizohizo,
Ahsante kapili umenifungua macho, ntaagiza kwa hawa jamaa,
meanwhile naomba Kapili tuwasiliane kwa shaqeir@yahoo.com
Wewe unayeataka e-mail ya kapili usiwe ni mwenye gari, baada ya michuzi kubania maoni yako ya kumponda kapili kwa kazi nzuri sasa unata e-mail yake umalizie hasira zako. Kwa nini hicho unachotaka kuwasiliana na kapili usikiweke hapa wote tukaona?. Kapili usikubali anataka kukurarua kwe e-mail yako baada ya kushindwa kufanya hivyo hapa. LOL!
ReplyDeleteHiyo bei yako ipo juu.
ReplyDeletecheck link hapa.
http://www.lucusjapan.com/en/vehicles?category=&maker=83&model=502&year_min=&year_max=&chassis_num=&id=