Sheikh Yahya Hussein

Mtabiri maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, amemtabiria ushindi wa kishindo Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu mwakani na kwamba Serikali yake itakuwa ya Muungano wa Vyama vya Siasa.

Shehe Yahya amesema pia kuwa ushindi wa Kikwete utatokana na mwendelezo wake wa kufichua mafisadi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila woga na kwamba katika uchaguzi huo, hakutakuwa na wizi wa kura, bali watu watashughulikia kutafuta fedha na mtandao wa mafuta.

Mtabiri huyo alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya utabiri wake kwa mwaka huu kwa waandishi wa habari.

Kuhusu ushindi wa Kikwete na hali ya kisiasa kuelekea mwaka wa uchaguzi, alisema utabiri wa mwaka huu uliopewa baraka zote na Umoja wa Mataifa, kuwa mwaka wa kuongozwa na nyota duniani, unaonyesha kuwa kiongozi mwenye jina lenye herufi J na K nchini, ndiye anayeongoza nchi.

HABARI KAMILI

MTEMBELEE SHEIK YAHYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. WATANZANIA LAZIMA TUJIFUNZE KEFANYA KAZI KWA BIDII.
    KUNA WATU WATAKAO AMINI KATIKA HILI LA SHEIKH YAHYA, WATALALA MLANGO WAZI, NA HAWATAENDELEA KAMWE!!!
    UTABIRI WA AINA HII NI KUENDEKEZA USHIRIKINA TU-HAMNA KITU HAPA KATIKA UTABIRI.

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee asilete utatanishi.Kwani nani asiyefahamu kuwa vipindi vya urais Tanzania ni viwili.Hiyo tukita tusitake, na ingelikuwa inawezakana kubadilisha katiba na kumpa mtu zaidi ya vipindi viwili, basi ungeona watu wanavyo geuka na kuwa wafalme.

    ReplyDelete
  3. Huyu zuga tu, anaona uelekeo ndio anajifanya anatabiri. UWIZI MTUPUzzzz

    ReplyDelete
  4. OLD NEWS !

    ReplyDelete
  5. Mapepo hayo,hayana nafasi katika ufahamu wa kizazi hiki.No way for your thoughts.

    ReplyDelete
  6. HUYU NI MSANII MTUPU, HAIWEZEKANI MTABIRI AKAWA UTABIRI WAKE NI CCM, VIONGOZI NA VYOMBO VYAKE TU KILA KUKICHA! MARA GAZETI LA UHURU LITAPAA, MARA CCM ITAPAA, MARA KIKWETE HANA MPINZANI YA NINI YOTE HAYA SHEHE SI MUOMBE KAZI KIKWETE HATA KAMA YA UDISII. MUAMBIE MHESHIMIWA MZEE WAKO NIMECHACHA NITAHADHIRIKA NIOKOE, NINAAMINI ATAKUSAIDIA TU.

    ReplyDelete
  7. king pin!!!!!

    kila mtu anajua JK lazima atashinda
    wee mzee wacha longolongo

    ReplyDelete
  8. Mungu mtu kaaaaziiiii kwelikweli

    ReplyDelete
  9. vipi ndugu zetu maalbino bado wataendelea kutaabika ????? au sio issue kwako we mungu m2

    ReplyDelete
  10. Pepo liko kazini,litawamaliza!

    ReplyDelete
  11. Hawa hawa ndio walee wa mambo ya albino. Huyu jamaa anachezea sana akili za raia wa jamhuri. wakiendelea kumuachia na vile vipindi vyake kwenye TV anaweza kusababisha matatizo. Hakuna siri ya mafanikio mbali na kufanyakazi kwa bidii katika kila jambo. Hakuna dawa ya mapenzi mbali ya kumpenda mwenzako kama unavyojipenda wewe. Mambo anayozungumzia kila siku kwenye runginga na kwenye vile vigazeti vya sh 100. ni kuibia tu raia hakuna swali ambalo huwa anajibu kwa anavyoita kinyota modern sayansi haina jibu lake, aache kujenga imani potofu katika mioyo ya raia walio choka na maisha na hatimaye kuwachukulia hata hicho kidogo walicho nacho.

    Etii kama unataka kupata jibu la swali hili njoo ofisini kwangu pale magomeni mikumi..mta waa... nyumba namba.... ukisikia hivyo ujue umeshaibiwa.
    Watanzania sio mabwege tena

    ReplyDelete
  12. Huyu anaongea nini???
    Hii sio karne ya elimu hii. Sema jingine hili kila mtu analitambua haliitaji utabiri.

    Thank u

    ReplyDelete
  13. Huyu !mbona ni maarufu kwa mambo
    ya uzushi na istoshe mlevi

    ReplyDelete
  14. THANKS BROTHER MITHUPU KWA KUONYESHA KUWA WATANZANIA WA LEO SI WALE WA WAKATI WA BABU ZETU.
    WATU NI WASOMI NA OUNGO WA WAZI TUNAUONA MAPEMA.
    WALE WANAOENDA KWA HUYU JAMAA MAGOMENI WANA WALAKINI NA KATIKA MTANDAO WA HESHIMA KAMA HUU HAPA SI MAHALI PAKE.
    NSHOMIRE ....BWANA

    ReplyDelete
  15. Huyu Mzee aendelee na kutabiri mambo mengine na siyo siasa za kujipendekeza kwa Kikwete. Sikubaliani na mawazo yake kuwa Kikwete ndiyo aliyewafichua mafisadi. Asiwahadaa watanzania, wanzania wa leo si wale wa enzi zake. Suala la kufichuliwa kwa mafisadi ni kazi Dr. Slaa na Zitto kabwe. Hao ndio watanzania wenye uzalendo na wenye kuipenda Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  16. Mbona hajatwambia siku yake ya kufa? Kama anaweza kutabiri ya wenginne, kwa nini asitwambie atakufa lini?

    Kunradhini Waislamu wenzangu. Lakini huyu mtu na AMNUT (All Muslin National Union of Tanganyika)yake!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. KAMA KWELI NI MTABIRI ATUTABIRIE NANI ATAKUWA BINGWA WA WORLD CUP 2010 SASA HIVI. MIPIRA HUWA ANAIKIMBIA SANA HUYU... BASI ATUTABIRIE NANI ATAKUWA MSHINDI WA PILI WA LIGI YA BARA MAANA BINGWA IKO WAZI KIDOGO..

    MZOZAJI

    ReplyDelete
  18. Huyu Mzee Bana Hajaacha Tu Kuwafunga Kamba Marais?? Kawafunga Moi ,Museven na Mkapa Sana kamba sasa Anamtaka JK hahaha Ila Kwa Kwere Atampata Maana Wabagaomoyo

    ReplyDelete
  19. Wewe babu ndio ujifunze kutofunga watu kamba au kama huna shughuli kamata jembe ukalime!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...