Mtabiri maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, amemtabiria ushindi wa kishindo Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu mwakani na kwamba Serikali yake itakuwa ya Muungano wa Vyama vya Siasa.
Shehe Yahya amesema pia kuwa ushindi wa Kikwete utatokana na mwendelezo wake wa kufichua mafisadi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila woga na kwamba katika uchaguzi huo, hakutakuwa na wizi wa kura, bali watu watashughulikia kutafuta fedha na mtandao wa mafuta.
Mtabiri huyo alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya utabiri wake kwa mwaka huu kwa waandishi wa habari.
Kuhusu ushindi wa Kikwete na hali ya kisiasa kuelekea mwaka wa uchaguzi, alisema utabiri wa mwaka huu uliopewa baraka zote na Umoja wa Mataifa, kuwa mwaka wa kuongozwa na nyota duniani, unaonyesha kuwa kiongozi mwenye jina lenye herufi J na K nchini, ndiye anayeongoza nchi.
HABARI KAMILI
MTEMBELEE SHEIK YAHYA
WATANZANIA LAZIMA TUJIFUNZE KEFANYA KAZI KWA BIDII.
ReplyDeleteKUNA WATU WATAKAO AMINI KATIKA HILI LA SHEIKH YAHYA, WATALALA MLANGO WAZI, NA HAWATAENDELEA KAMWE!!!
UTABIRI WA AINA HII NI KUENDEKEZA USHIRIKINA TU-HAMNA KITU HAPA KATIKA UTABIRI.
Huyu mzee asilete utatanishi.Kwani nani asiyefahamu kuwa vipindi vya urais Tanzania ni viwili.Hiyo tukita tusitake, na ingelikuwa inawezakana kubadilisha katiba na kumpa mtu zaidi ya vipindi viwili, basi ungeona watu wanavyo geuka na kuwa wafalme.
ReplyDeleteHuyu zuga tu, anaona uelekeo ndio anajifanya anatabiri. UWIZI MTUPUzzzz
ReplyDeleteOLD NEWS !
ReplyDeleteMapepo hayo,hayana nafasi katika ufahamu wa kizazi hiki.No way for your thoughts.
ReplyDeleteHUYU NI MSANII MTUPU, HAIWEZEKANI MTABIRI AKAWA UTABIRI WAKE NI CCM, VIONGOZI NA VYOMBO VYAKE TU KILA KUKICHA! MARA GAZETI LA UHURU LITAPAA, MARA CCM ITAPAA, MARA KIKWETE HANA MPINZANI YA NINI YOTE HAYA SHEHE SI MUOMBE KAZI KIKWETE HATA KAMA YA UDISII. MUAMBIE MHESHIMIWA MZEE WAKO NIMECHACHA NITAHADHIRIKA NIOKOE, NINAAMINI ATAKUSAIDIA TU.
ReplyDeleteking pin!!!!!
ReplyDeletekila mtu anajua JK lazima atashinda
wee mzee wacha longolongo
Mungu mtu kaaaaziiiii kwelikweli
ReplyDeletevipi ndugu zetu maalbino bado wataendelea kutaabika ????? au sio issue kwako we mungu m2
ReplyDeletePepo liko kazini,litawamaliza!
ReplyDeleteHawa hawa ndio walee wa mambo ya albino. Huyu jamaa anachezea sana akili za raia wa jamhuri. wakiendelea kumuachia na vile vipindi vyake kwenye TV anaweza kusababisha matatizo. Hakuna siri ya mafanikio mbali na kufanyakazi kwa bidii katika kila jambo. Hakuna dawa ya mapenzi mbali ya kumpenda mwenzako kama unavyojipenda wewe. Mambo anayozungumzia kila siku kwenye runginga na kwenye vile vigazeti vya sh 100. ni kuibia tu raia hakuna swali ambalo huwa anajibu kwa anavyoita kinyota modern sayansi haina jibu lake, aache kujenga imani potofu katika mioyo ya raia walio choka na maisha na hatimaye kuwachukulia hata hicho kidogo walicho nacho.
ReplyDeleteEtii kama unataka kupata jibu la swali hili njoo ofisini kwangu pale magomeni mikumi..mta waa... nyumba namba.... ukisikia hivyo ujue umeshaibiwa.
Watanzania sio mabwege tena
Huyu anaongea nini???
ReplyDeleteHii sio karne ya elimu hii. Sema jingine hili kila mtu analitambua haliitaji utabiri.
Thank u
Huyu !mbona ni maarufu kwa mambo
ReplyDeleteya uzushi na istoshe mlevi
THANKS BROTHER MITHUPU KWA KUONYESHA KUWA WATANZANIA WA LEO SI WALE WA WAKATI WA BABU ZETU.
ReplyDeleteWATU NI WASOMI NA OUNGO WA WAZI TUNAUONA MAPEMA.
WALE WANAOENDA KWA HUYU JAMAA MAGOMENI WANA WALAKINI NA KATIKA MTANDAO WA HESHIMA KAMA HUU HAPA SI MAHALI PAKE.
NSHOMIRE ....BWANA
Huyu Mzee aendelee na kutabiri mambo mengine na siyo siasa za kujipendekeza kwa Kikwete. Sikubaliani na mawazo yake kuwa Kikwete ndiyo aliyewafichua mafisadi. Asiwahadaa watanzania, wanzania wa leo si wale wa enzi zake. Suala la kufichuliwa kwa mafisadi ni kazi Dr. Slaa na Zitto kabwe. Hao ndio watanzania wenye uzalendo na wenye kuipenda Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteMbona hajatwambia siku yake ya kufa? Kama anaweza kutabiri ya wenginne, kwa nini asitwambie atakufa lini?
ReplyDeleteKunradhini Waislamu wenzangu. Lakini huyu mtu na AMNUT (All Muslin National Union of Tanganyika)yake!!!!!!!!!!!!!!!!
KAMA KWELI NI MTABIRI ATUTABIRIE NANI ATAKUWA BINGWA WA WORLD CUP 2010 SASA HIVI. MIPIRA HUWA ANAIKIMBIA SANA HUYU... BASI ATUTABIRIE NANI ATAKUWA MSHINDI WA PILI WA LIGI YA BARA MAANA BINGWA IKO WAZI KIDOGO..
ReplyDeleteMZOZAJI
Huyu Mzee Bana Hajaacha Tu Kuwafunga Kamba Marais?? Kawafunga Moi ,Museven na Mkapa Sana kamba sasa Anamtaka JK hahaha Ila Kwa Kwere Atampata Maana Wabagaomoyo
ReplyDeleteWewe babu ndio ujifunze kutofunga watu kamba au kama huna shughuli kamata jembe ukalime!!!!!!
ReplyDelete