Kaimu mkurugenzi wa wilaya ya kasulu, ndugu Alphonce Sebukoto akiwaongoza majumbe wa kamati ya Bunge inashughulikia ya mhesabu ya serikali za mitaa (LAAC) kukagua miradi ya maendeleo katika hospitali ya wilaya kasulu. Nyuma ni makamu wa kamati hiyo mhe. Mgana msindai
Mwenyekiti wa mradi huo ndugu amosi kayagwe akiwaonyesha jinsi wanavyootesha katika vitalu

Afisa kilimo wa wilaya ya kigoma vijijini ndugu Daniel kamwela, akiwaeleza waheshimiwa wabunge jinsi wanavyootesha miche ya kahawa inayostahimili magonjwa sugu walipotembelea mradi wa kuzalisha kahawa hiyo kijiji cha nyarubanda wilaya ya kigoma vijijini
Baadae walipata nafasi ya mwenda kumfariji mhe. Daniel Nsanzugwako (wa pili shoto) nyumbani kwao kasulu ambaye amefiwa na baba yake. Anayetoa salama ni mhe. Ernest Mabina mbunge wa Geita na mjumbe wa kamati hiyo.
(Picha zote na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge)

Kamati ya LAAC ipo katika ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika halimashauri za mikoa ambapo imejigawa katika kanda kukagua mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwa , Arusha, Kilimanjaro na manyara, na kanda ya Mwanza, mara na kagera, lengo ni kujionea maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopewa ruzuku na serikali katika kupeleka huduma vijijini,
katika kanda ya kigoma, rukwa na kigoma imewakilishwa na
mhe. Mgana msindai - makamu mwenyekiti
mhe. ernest Mabina - mjumbe
mhe. mwanne ismail mchemba -mjumbe
mhe. Halima kimbau - mjumbe




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ama kweli mahesabu mwili wenyewe wa jamaa unaonyesha mahesabu teh.

    ReplyDelete
  2. Sikujua na sisi tuna heavy set namna hii. duh

    ReplyDelete
  3. ok , am bringing you back kidogo, there is one kamati ya bunge that asked for dowans not to get into the procurement stages with tanesco ; the were of the opinion tht its already been used so its used goods ( used for a year ! ) right now demand is 700megawatt and it is growing at an alarming rate of 100megawatt per year or more depending on development, now the 'old dowans' which is cheaper coz it uses gas was going to substatiante tht amount, look into the other option conversion of IPTL which is way tooo old and quite expensive ( to covert and use )IPTL uses diesel which has to be imported coal is locally here;
    sasa kipi bora? tanesco's installed capacity is 586megawatt IPP's have to be used...i dare the kamati ya bunge to think of nation's favour when those rains stops and our dams get below capacity than cheap popularity, i would go for dowans before they are removed here and brought back in a hefty and brand new price.. do i hear someone shout TRAITOR! at me?? on this case.. so be it !

    ReplyDelete
  4. Bibi Umeme, mbona unapotoa maoni yako wengine tunashindwa kuelewa vizuri? Aidha unaandika ukiwa na jazba au unachanganya lugha sana na huipitii comment kabla ya kuweka hewani. Tafadhali zipitie tena utueleweshe na sie kwani unaonekana kama unakuwaga na tu pointi

    ReplyDelete
  5. samahani anony wa 12;19 nadhani niliandika kwa jazba sana, naomba radhi kwa hilo, kama mdau wa umeme nchini ninapenda maendeleo ya umeme, na nilishtushwa na kamati ya bunge kusitisha mchakato wa kununua mitambo ya dowans kisa ilishatumika hivyo nzee ( imetumika 2 years only ), na kuhimiza IPTL conversion ifanyike, kwa akili ya kawaida IPTL inatumia diesel na dowans coal vilevile IPTL ni"nzee" kuliko dowans, zote ni megawtt mia, dowans ni cheaper to run, IPTL yabidi ibadilishwe kutumia gas, huo mbadiliko is a trip on its own, manake ni mambo mengi ya kiufundi na fedha !! sasa tusipokuwa na chanzo cha umeme wa dharura nchini, tutaishia mgao na vilevile tanesco ina uwezo wa kuzalisha megawati 586 au 600 ukiingiza na ubungo gas plant.. ndio niliomba wakati sasa tukitaka kununua mitambo baada ya hii iliyopo kuondolewa nchini, gharama za kusafirisha peke yake zitatutoa kamasi... na kama ni maslahi ya nchi au ni majibu ya kisiasa ili wapiga kura wakuchague tena enyi kamati teule ya bunge, naomba mniite msaliti kwa hili !

    ReplyDelete
  6. Anony 09th Jan 2009, kuwa muwazi kuwa Bibi Umeme kiingereza chake ni kibovu mno ndio maana hata tunaoongea Kiswahili hatuwezi kukielewa kiingereza chake, sijui kama watani wetu wa jadi wasiojua kiswahili vizuri kama wataweza kuambulia chochote cha mdau Bi Umeme.

    Kwa vile Bibi Umeme anapenda sana kutumia mtandao awe pia anatumia mtandao kuboresha kiingereza chake.

    Hivyo Bibi Umeme nakushauri ingia ktk webusaiti:
    *www.primaryresources.co.uk/english
    *http://www.bbc.co.uk/worldservice/learningenglish/grammar
    *wwww.VOAnews.com/special english

    Hapo mie ndipo ninapo kiboresha kiingereza changu kila siku.

    Mdau
    Uingereza.

    ReplyDelete
  7. Mgana Msindai anahitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu afya yake. Ni Hayo tu!

    ReplyDelete
  8. mbona mradi wenyewe hauonekani? naona kama kuna vijimajani majani tu, au mimi ndio sioni

    ReplyDelete
  9. mdau uingereza, thanks for the places to brush up my english, at this stage, i communicate well with both speakers so i dont need to further it, ironically we communicate very well in both languages and i havent heard any complaints, since am blogging, i use blog jargon and shorten words; but i admit i am not a master of either languages, thanks for the sites, i wont visit them unless i want to do a PHD of either of the two languages.

    ReplyDelete
  10. Bibi Umeme mimi ni mwalimu kitaaluma, hapo ulipomjibu anony wa Uingereza kuhusu kuboresha uwezo wako wa kiingereza inatakiwa ukubali, kwa nini nasema hivyo?

    Ulipojaribu kutoa maoni yako kuhusu IPTL,Tanesco na Dowans kama ungekuwa mtihani ningekupa alama 15 kwa 100 kwa kiingereza chako.

    Katika majibu yako kwa Mdau wa Uingereza kwamba uhitaji kuboresha kiingereza chako ningekupa alama 80 kwa 100 kwa ulivyoandika kiingereza.

    Sasa basi inakuwaje upate bad failure ktk kazi moja na nyingine upate 'very goood'? hapo lazima kuna mushkeli ya kufanyiwa mtihani na mtu 'maruhani' na ndio maana unafikiri kuboresha lugha ni lazima uwe unataka kupata PhD, wakati sie lugha ni ya 'kuombea maji'. Kwa ujanja huo hufiki mbali.

    ReplyDelete
  11. Ebu nyie watanzania wachache acheni huo ujinga wa kukosoa kiingeleza cha mwenzenu discuss issues. Kwa mtindo huu hutatafika mie niko huku ughaibuni tupo mataifa kiboa wasiojua english hata tone kama wachina , lakini hukuti mzungu anacheka english ya mtu hivyo inakupa courage kila siku kuongea. Sasa nyinyi vipi? Mbona hamuandiki zenu? Mwalimu gani wewe unayekatisha tamaa wenzio? Acha hizo wewe

    ReplyDelete
  12. haha kuna kupewa na marks humu??hapa kiingereza chako ulipata..this pale ulipata 100..haahhahahhaa yeleeeeeeeeeeeeeeeee mnh???!

    ReplyDelete
  13. Huyu lazima ni mwalimu the "maimuna type" and I am troubled by you. You haven't stated why you should give him 15 on one piece and 80 on the other..it seems like your emotions to award those scores and I feel sorry for your students.
    Mdau,
    Chapel Hill, NC

    ReplyDelete
  14. Huyo mheshimiwa mwenye heavy set...Mgana Msindai aangalie sana! Siko yoyote anaweza kuanguka kwa 'heart attack' alafu mtasema " Ni mapenzi ya mwenyenzi Mungu"!!!! Come on man! take control of your destiny, that is very unhealthy and you may die prematurely. I wish you the wisdom to understand this comment.

    Mdau Toronto.

    ReplyDelete
  15. Wadau tuwe na utamaduni wa kukubali mapungufu yetu ndo ubinadamu. Kuna Mh. hapo ana aswa kuhusu kuangalia afya yake pia kuna mdau anapewa shavu afanye bidii ktk kuchangia ktk lugha ya kiingereza. Na kitu kizzuri ni kuwa wote waliochangia humu wametumia lugha ya kiasi ambayo ndio inastahili.
    Idumu blogu ya jamii.

    ReplyDelete
  16. Brother Mithupu , huyu jamaa Mbunge Mgana Msindai tafadhali mpe ujumbe huu-
    -aende JKT miezi mitatu tu
    -unene alio nao ni ugonjwa na asipishughulikia swala hili vifuatavyo vita mwandama,BP na magonjwa ya aina hiyo,kisukari,mifupa ya mgongo kusagika(verterbral discs),kirungu cha femur joint chaweza kuachia.
    Tunampenda kwa michango yake bungeni, afanye hima

    ReplyDelete
  17. huyu jamaa anayeoengea kuhusu dowans and iptl haelewi kitu kimoja, IPTL ni mitambo iliyokuja mipya kabisa, dowans ni second hand toka iingie bongo. So hawezi kusema dowans ni mipya kuliko iptl unless alete ushahidi. Pili hiyo dowans ameiona plant yake then alinganishe na iptl? Naomba waandishi wa habari wajaribu kuwaonyesha watz mitambo yote miwili then tuweze kujua. Tatizo la tz watu wanapenda kudandia hoja za mafisadi bila kufanya utafiti. Kwa mfano mafisadi walitudanganya kuwa dowan ingezalisha umeme ndani ya miezi miwiwli toka wapewe contract then wakachukua mwaka mmoja kipindi ambacho kingeweza kutumika kuagiza mitambo mipya na ikawa mpaka leo inamilikiwa na serikali.

    ReplyDelete
  18. kibongo bongo mwili wa fweza hua ama hamjui na pia pentejeee lazima awe na tumbo kubwa ebo mmeishi nje sana mmesahu utamaduni wenu hahahaha gym si atazivunja zote jimu gani itamkubali lol may be afanye Boxing au vp wadau mkumbuke miili mingine ya kurithi araa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...