MICHUZI HEBU ANGALIA HATARI HII................
P- W- D- L- GD- Pts
Uganda 3- 2- 1- 0- 8- 7
Tanzania 3 -2- 0- 1- 2- 6
Zanzibar 3- 1- 1- 1 -3- 4
Rwanda 3- 1- 0- 2 -4 -3
Somalia 4 -1- 0- 3 -9 -3
Uganda 3- 2- 1- 0- 8- 7
Tanzania 3 -2- 0- 1- 2- 6
Zanzibar 3- 1- 1- 1 -3- 4
Rwanda 3- 1- 0- 2 -4 -3
Somalia 4 -1- 0- 3 -9 -3
MECHI YA KWANZA SAA 10 NI BARA NA UGANDA.
IWAPO TUTATOKA SARE YOYOTE ILE, ZENJI ANAHITAJI KUSHINDA 1-0 TU NA ANAKWENDA NUSU FAINALI NA SISI TUNATOKA, HATA KAMA NI SARE YA MABAO 1,000 KWA 1,000.
KWA KUWA CECAFA WANAFUATA SHERIA YA GOAL DIFFERENCE (GD), TUKITOKA SARE TUTAKUWA NA GD YA 2 NA POINTI 7 TU, WAKATI ZENJI HADI SASA WANA DG YA 3, HIVYO WAKISHINDA 1-0 WATAFIKISHA POINTI 7, NA GD YA 4.
MDAU,
WASHINGTON DC.
Mdau wa Woshingitoni mbona unachanganya habari? Zenji alimfunga somalia 2-0, akatoka suluhu na UG na bara wakamchapa 2-1, hii ina maana kafunga goli 3 kafungwa 2 na goaldiff yake ni goli 1 na sio 3 kama unavosema. ina maana akishinda 1-0 na tz (ambayo ina GD ya goli 2- imefungwa na somalia 1-0, imeifunga zenji 2-1 na rwanda 2-0 hivo imefunga bao 4 na imefungwa 2)ikatoa suluhu ya 0-0 bado bara inasonga mbele, au sio wadau?
ReplyDeletenani wanacheza saa saba mchana? kama kili tunacheza saa kumi jioni! ni kweli mdau wa washinton kachemcha zenj wana goli moja tu na pointi nne sisi tuna bao mbili na pointi sita
ReplyDeleteHiyo "SISI" inasimama badala ya nini? Hii Blog ya Bara? Viziwani? Jamii? ama vp? Jamani tuangalie hizo lugha tunazotumia!
ReplyDeleteMdau wa Washington DC 'table' inaonyesha Somalia wameshacheza mechi 4, je walicheza na 'maruhani' kufikisha mechi nne? maana 'table' inaonyesha timu zingine zote zimeshacheza mechi 3 tu!
ReplyDeletemichuzi timu ya tanzania una maanisha ni pamoja na zanzibar kwahio bora uiite kilimanjaro tu au bara
ReplyDeletekwako mdau ulieuliza SISI inasimama badala ya nini...SISI INA MAANA WAO WA KINA MICHUZI YAANI WAO KINA MICHUZI(KILIMANJARO STARS)MAANA HAPO UNAMUONEA TU MICHUZI KWAVILE MICHUZI HATA UFANYEJE YEYE SIO MZENJI ATABAKIA KUWA NI M`BARA TU SO HE WAS RIGHT TO SAY SISI
ReplyDeleteHii biashara ya Tanzania na Zanzibar sijui ina maana gani? Ni utata tu wa muungano ambao wakubwa wanagofya kuushughulikia kikamilifu.
ReplyDeleteHuwezi kuwa na Tanzania halafu ukawa na Zanzibar au ukawa na Tanzania Bara na Zanzibar zote haziji ni sawa na kusema UK imeifunga Scotland.
Aidha iwe Tanzania Bara na Tanzania visiwani(wala haijitoshelezi maana je Mafia, Ukerewe itakuwaje!!)
au tuwe na Tanganyika na Zanzibar hii ndio muafaka.
Muungano wa kwetu uko katika mfumo wa UK( Kiswahili sijui maana Uingereza ni England) wa sasa ambapo England haina serikali yake kama ilivyo Tanganyika wakati Wales, Scotland na Nothern Ireland zina serikali zao za ndani pamoja na kwamba wamo pia katika serikali ya UK( Mfano Gordon Brown ni mscoti).
Muungano uliofanyika mwaka 1964 kwa kiasi kikubwa kwa rihaa ya watu wawili ambapo wataalamu ndani ya nchi walikuwa ni wachache sana na pia upeo na muono wa wengi ulikuwa ni mfinyu sana hauna budi kuangaliwa upya ili urekebishwe na kuimarishwa, kuendelea kudekeza kidonda mwisho mguu utakatwa.
Na hili sio swala la Chama bali ni la kitaifa maana mmiliki wa muungano ni wananchi na sio chama.
Upo umuhimu wa wabunge wenye upeo wa kuleta hoja binafsi bungeni ya kuangalia upya swala la muungano maana viongozi wa juu wanaonekana kuliogopa bila sababu za msingi.
Tokea 1995 tena baada ya damu kumwagika Mkuu wa nchi aliahidi kushughulikia kero za muungano hadi leo hakuna hata dalili za juhudi ya maana ya kitaifa zaidi ya vikao vya vyama.
Katika hotuba ya kwanza ya Raisi JMK kwa Bunge nae pia aliahidi kushughulikia lakini akaanzissha vikao vya vyama.
Sasa watanzania sio wote wanavyama lakini wote ni wanamuungano hivyo tungetegemea hili swala alitoe kwenye vyama kwa kutumia kofia ya Raisi wa nchi na aanzishe zoezi la kitaifa kulishughulikia maana lasivyo tutashuhudia tena vioja na uvunjaji wa haki katika uchaguzi ujao. Hii inapandikiza mbegu mbaya ndani ya nchi.
Tumeshashuhudia kuwa Raisi wa sasa anapenda kufuata utaratibu,kuzingatia sheria na pia kuvieheshimu na kuvipa uhuru vyombo vya Dola sasa badala ya kufanya Muungano ni wa Bwana Makamba na Hamad kutatua basi ashirikishe Watanzania wote.
Aidha kwa kutumia tume kama tulivyozoea au aanzishe majadiliano ya kitaifa.
Wadau naomba nitoe hoja maana nisingependa kesho nianze kukurupushana na marafiki wangu wa wazanzibari kwa kuwa Viongozi leo wamekuwa waoga wa hoja tofauti au mabadiliko.
Asanteni
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu iokoe Tanzania.
Mzawa