Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa kujadili mauaji ya Albino na Vikongwe katika mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Hilary Bujiku
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
SERIKALI imetangaza kufuta leseni zote za waganga wa jadi kuanzia Ijumaa Jan. 23, 2009 ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya mauaji ya Albino na Vikongwe nchini.
Amri hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika mkutano wa hadhara mjini Shinyanga leo mwishoni mwa ziara yake ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhamasisha mapambano ya Serikali dhidi ya mauaji hayo.
Waziri Mkuu alisema kuwa aliwasiliana na Mwanasheria Mkuu kuhusu uamuzi wa kuchukua hatua hiyo ya kufuta leseni hizo na Mwanasheria Mkuu akasema jambo hilo linawezekana.
"Kuanzia leo leseni zote za waganga wa jadi futa… Mtu yeyote akiendelea na kazi hiyo mfuatilieni," aliwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakuu wa Halmashauri zote za Jiji, Miji na Wilaya nchini.
Waganga wa jadi wamekuwa wakituhumiwa kuwa ndiyo chimbuko la mauaji hayo kwa vile wao ndiyo hupiga ramli za kuelekeza hivyo.
Katika mikutano na viongozi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Tabora na Shinyanga, wachangiaji wengi waliitaka serikali kufuta leseni hizo. Hata baadhi ya waganga wa jadi waliochangia walikiri.
Waganga wa jadi husajiliwa na kupewa leseni za kufanya kazi zao na Halmashari kwa utaratibu wa kiutawala. Ipo sheria ya mwaka 2002 kuhusu Tiba Asilia na Tiba Mbadala (Traditional and Alterntive Medicine Act), lakini Kanuni za utekelezaji wake zilikuwa hazijatengenezwa.
Waziri Mkuu alisema mganga wa jadi ambaye anaweza kuruhusiwa baadaye ni yule ambaye dawa zake za mitishamba au za asili zitakuwa zimethibitishwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Tiba Asili cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa kweli zinatibu.
Mgonjwa naye atatakiwa awe na cheti kutoka hospitali kitakachothitisha maradhi yake na kuwa tiba yake hopitali imeshindikana. "Waganga hawa ni waongo wakubwa…Siyo lazima kuwa nao.
Wangekuwa waganga wa kweli magonjwa mengi yangepungua nchini, lakini magonjwa yapo na sasa wanapiga ramli na kuwa kichocheo cha mauaji. Mkoa wa Shinyanga unasemekana unaongoza kwa idadi ya waganga wa jadi waliosajiliwa na wako 1,104 na 94 ambao hawakusajiliwa.
Wilaya ya Kahama peke yake ina 763. Waziri Mkuu aliuambia umati uliofurika kwenye uwanja wa Chuo cha Biahshara cha Shinyanga (Shycom) huku akishangiliwa kuwa mapambano dhidi ya mauaji ya Abino ni vita na ndiyo maana anataka ulinzi wa jadi wa Sungusungu urejeshwe kusaidiana na vyombo vya dola kukabiliana na hali hiyo.
Aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa kufnya kazi zao kwa ufanisi zaidi na "kujipanga upya na kuteremka hadi ngazi ya chini" kusimamia mapambano dhidi ya mauaji ya Albino na Vikongwe.
"Inapotokea kuwa Albino au Kikongwe anauawa katika eneo fulani, mimi nitamshukia Mkuu wa Mkoa na kumuuliza kwa nini aliacha hali itokee hivyo. Mkuu wa Mkoa naye atamshukia Mkuu wa Wilaya na vivyo hivyo," alisema.
Aliongeza: "Tukijumuika wote kwa pamoja tutashinda vita hii kama tulivyoshinda vita dhidi ya nduli Idi Amin wa Uganda". Waziri Mkuu pia alisema atamwomba Jaji Mkuu kuwa zile kesi za mauaji ya Albino ambazo ziko tayari zinapangiwa majaji maalum ili zikamilike na hatima yake ijulikane haraka.
Tangu Juni mwaka 2007 mpaka Novemba mwaka 2008 jumla ya Albino 34 wameuawa nchini kwa imani za ushirikina kuwa eti viungo vyao vinasaidia kupata utajiri.
Idadi yao kimkoa kwenye mabano ni Mwanza (19) Mara (4) Kigoma (3) Shinyanga (4), Kagera (3) na Mbeya (1). Mwaka huu tayari wameuawa watatu.
Jumla ya vikongwe waliouawa nao kwa kushukiwa wachawi ni 2583 ambapo idadi yao kimkoa kwenye mabano ni Mwanza (696), Shinaynga (522), Tabora (508), Iringa (256), Mbeya (192) Kagera (186), Singida (120) na Rukwa (103).
Ziara ya Waziri Mkuu Pinda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa inamalizika leo kwa majumuisho yatakayowahusisha viongozi wa mikoa hiyo. Alianzia Kagera na badaye kutembelea mikoa ya Mwanza, Tabora na Shinyanga.
Mkoa wa Mara ulijumuishwa kwa viongozi wake kuhudhuria mkutano wa viongozi Mwanza.
Ni Ushauri Hivi sisi TZ tunaelewa kuwa nguo inapokuwa nyeusi na kuivaa wakati wa juwa kali inaletea juwa likupige sana na kuingia katika mwili wako ?cha kushangaza hapa joto na juwa kali kama hili la hapa Bongo tunaonekana wengi wetu na suti nzito tena nyeusi katika hali ya juwa kati inashauriwa kuvaa nguo nyeupe kusaidia ile hali ya juwa kali kuingia katika mwili wako na tegemea ujumbe huu kama utafikishwa utaweza kusaidia japo watu wawili na kubadilisha hali hiyo
ReplyDeleteyaani wewe katika yote hapo juu uliloona ni swala la kuvaa nguo nyeusi...?kama huna la kuongea basi acha wenye kitu cha maana waongee...
ReplyDeletefire brigade hiyooooooooooo!!!
ReplyDeleteje umefanyika uchunguzi wa kutosha hadi kufikia kuwafutia leseni waganga wote wa jadi?
pia ikumbukwe kuwa waganga wa jadi hawahitaji leseni hususan wale waliokuwa wanafanya vitendo vya kushirikiana na wauaji wa albino. jambazi hahitaji leseni kufanya ujambazi!!! ninaona hapa WM amekurupuka kama ilivyo kawa yetu
mwananchi.co.tzDate::1/23/2009
ReplyDeletePinda ataka jino kwa jino
Na Victor Kinambile, Tabora
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.
Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.
Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi.
Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.
Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.
"Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.
Aliviomba vyama vya siasa kushirikiana na wananchi kuhakikisha suala hili la mauji linakwisha kwani wauji "tunaishi nao na ni rahisi kulimaliza iwapo tutakuwa kitu kimoja katika kuondoa kashifa hii ambayo imekuwa mbaya kwa nchi yetu".
Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana.
"Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya watu wanaoonekana kuwa ni wa "serikali" waliwafuata baadhi ya waandishi wa habari, akisihi suala hilo lisiripotiwe magazetini kwa madai kuwa kauli hiyo ya Waziri Pinda inaweza kusababisha matatizo.
Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine.
Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi.
"Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa," alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao.
Akitoa takwimu za mauaji ya vikongwe na malbino alisema mwaka 2003 waliuwawa vikongwe 517, mwaka 2004 waliuawa vikongwe 444, mwaka 2005 (494), 2006 (vikongwe 386), mwaka 2007 (vikongwe 526) na albino sita na mwaka 2008 (vikongwe 526 na albino 28).
Alisema tayari mwaka huu wameuawa albino watatu hivyo kufanya albino na vikongwe waliouawa kufikia kuwa jumla 2,900.
Waziri mkuu ameanza ziara ya siku nne kutembelea mikoa ya Shinyanga, Tabora na Mwanza ili kuhamasisha wananchi watokomeze vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu weye ulemavu wa ngozi.mwananchi.co.tz
Hiyo ndio yenyewe, binafsi ninakubaliana kabisa na WM, Futa hizo leseni. Ila viongozi wetu watapata waganga wapi? Maana wao ndio wenyewe kwa ushirikina a.k.a. kutafuta vyeo kwa waganga badala ya kuchapa kazi na kujiendeleza ki-elimu.
ReplyDeleteBongo tambarare.
Baadhi ya vipengele vya dawa asilia, hasa mitishamba, vinahitaji tafakari zaidi na subira. Naongelea suala la mitishamba tu, sio suala la mauaji ya albino, kwani kuhusu suala la albino, naungana na kila mtu anayelaani na kutaka mauaji hayo yakomeshwe hima na wahusika waendelee kusakwa na wachukuliwe hatua ipasayo.
ReplyDeleteSuala la mitishamba ni suala la taaluma asilia, na katika dunia ya leo, tunaongelea suali la haki ya waganga wa mitishamba na jamii zao kuendelea kutambuliwa kama wamiliki wa ujuzi walio nao. Leo hii, makampuni ya kimataifa yanaiba ujuzi wa mitishamba na kujipatia haki miliki, na kisha kutengeneza madawa ambayo wanauza. Ni hujuma nzito na imekuwa tishio duniani kote. Kwa hivi, wazo la kupeleka mitishamba Muhimbili lina utata.
Suala la haki miliki katika nyanja mbali mbali, kama vile sanaa, bado linayumba sana Tanzania, na wasanii wanahujumiwa. Je, hili suala la kupeleka mitishamba Muhimbili tumeliandaa vipi ili isitokee hujuma dhidi ya haki za wale wenye ujuzi wa mitishamba hiyo? Hayo ni masuala mazito, yanayotambuliwa na taasisi za kimataifa kama vile UNESCO.
Nampongeza sana waziri
ReplyDeletePinda kwa uamuzi aliochukua. Nadhani kuna haja ya kuchunguza na kutoa hizo leseni upya kwa wale tu wanaostahili. Zaidi ya hapo kuna haja kubwa ya wizara ya afya kushirikiana na wizara nyingine za maendeleo ya jamii kuendelea kuelimisha wananchi. Wananchi wengi hudanganyika kirahisi mara wamapopatwa na shida kwa sababu ya kukosa upeo mkubwa juu ya maumbile ya binadamu na tofauti za maumbile hayo. Swala jingine ni umaskini, ambao unadhuru hadi uwezo wa kufikiri. Adui hao watatu wakuu: UJINGA, UMASKINI, NA MARADHI, wakishambuliwa, matatizo kama haya yatapungua sana.
NI HATUA NZURI YA KUPONGEZWA KWA SERIKALI KUFUTA HUO UPUUZI.ETI WAGANGA....SERIKALI ILIPASWA KUCHUKUA HATUA HIYO SIKU NYINGI SANA,HAO WANAOJIITA MAPROFESA,WAGANGA WA KIENYEJI HAWASAIDII JAMII KWA NJIA YOYOTE ILE ZAIDI YA KUWADANGANYA.IMEKUWA NAFUU WAMEFUTIWA LESENI ILIKUWA AIBU KWA TAIFA KUWA NA WACHAWI(WAGANGA WA KIENYEJI)TULIKUWA TUMERUDISHWA KATIKA KARNE YA 16.
ReplyDeleteanon wa 2,
ReplyDeleteasante.
Huyu anon wa kwanza mgonjwa wa akili. This's a very sensitive issue, not only in TZ, lakini dunia nzima. This's a human rights issue, watu wasio na hatia wanapoteza maisha, we unaongelea kuvaa nguo nyeusi kuna leta joto? who doesn't know? kichwa maji we!
Yaani sina maneno ya kusema kuhusu jamaa aliyeongea kuhusu nguo wakati ndugu zetu wanauawa.... Mbona sioni mkoa wa Pwani? inamaana hawa wenzetu mimi nilidhani wasomi ndio wamedata kuliko sisi Wazaramo na Wakwere? Hii ni aibu kubwa kwa Taifa I hope tabia hii inakoma mara moja.. Somebody get to work and stop this National Embarassment!!
ReplyDeleteMdau, Boston, US
MIMI SIUNGI MKONO HATUA HIYO KWANI HAITAZUIA WATU KUUWAWA, IT IS JUST A POLITICAL GIMMICK, KWANI KWA MFANO WIZI HAURUHUSIWI MAHALA POPOTE PALE DUNIANI LAKI WATU BADO WANAIBA, KUUA HAKURUHUSIWI MAHALA POPOTE PALE DUNIANI LAKINI WATU BADO WANAUANA KWA SILAHA ZA AINA MBALIMBALI YEKIWEMO MAPANGA NA WALA SIJAWAHI SIKIA MAPANGA YASIUZWE TENA, UKWELI SIONI JINSI GANI HATUWA HIYO ITAZUWIA MAUAJI HAYO, HIYO SI HATUA MUAFAKA. SHERIA ZILIZOPO ZINATOSHA KULIKABILI JANGA HILO TATIZO KUNAUPUNGUFU WA UTENDAJI WA KAZI NA VYOMBO HUSIKA VYA USALAMA WA JAMII NA MALI ZAO AMA KWA KUKOSA UJUZI MUAFAKA AMA UZEMBE TU PLUS LACK OF POLITICAL AND CENTRAL EXECUTIVE LEADERSHIP ON IT. EBU KAANI CHINI MUNIELEZE LESENI KUFUTWA ITASAIDIAJE KUKOMESHA MAUAJI, HICHO NI KICHEKESHO KIKUBWA, HAPO ANATAKA KUONYESHA WANAFANYA KAZI NA KUMBE NI ZERO TUPU. WAGANGA WATAENDELEA KUTOWA HUDUMA ZAO KWA KIFICHO MANANE YA USIKU KWANI KUNA WAGANGA KIBAO HAWANA LESENI NI WACHACHE TU WENYE HAYO MAKARATASI MNAYOYAITA LESENI, PLEASE LET US BE SCIETIFIC AND PROFESSIONAL.
ReplyDeletesafi sana serikali, bravo lazma mambo ya kishirikina yateketee tz na iko siku watu wataamini hili.
ReplyDeleteAisee sio tuwe tunakurupuka kuchangia tu bila kusoma na maoni ya wachangiaji wenzako nao ukapima muelekeo nawaomba wote tuzisome comments za mdau anaejiita MBELE.huyu bwana anahoji uhalali wa madokta wajanja wajanja wa muhimbili wakimilikishwa majukumu ya kuihalalisha na kutokuihalalisha mitishamba ya wanakijiji walio mbali kidogo na hii teknojia ya mtandao patakosekana hujuma kweli hapo kwa wengine kuwafanya wenzao ngazi na kuiba teknolojia kutoka kwao???
ReplyDeletejapokuwa watu weeengi wanashededia uamuzi wa WM, mimi ninamuunga mkono anony wa Jan, 25-4:04AM. Nionavyo mimi kufuta leseni wala sio suluhisho la tatizo la mauaji ya hawa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi. Ukiangalia sana utagundua kuwa kwanza wenye leseni ni wachache mnooooo!! amini usiamini. Na vile vile hawa wengi wao ni hebalist na wala sio wale waganga wa jadi. Hivi kwanza mnawafahamu waganga wa jadi nyie mnaoshabilia leseni zimefutwa?? kule kwetu usukumani wanaitwa "bafumu" na wanaongozwa na "masamva" yaani hawahitaji TBS wala TRA kufanya kazi zao. Lilolopo, nina uhakika hawa waganga wenye leseni wanaweza kwa asilimia kubwa kuwa wanawafahamu wenzao wanaofanya vitendo viovu vya kuwaua binadamu wenzetu, na bila kufuta leseni zao, hawa ndo wangetumiwa chambo basi kama leseni zao ndo ID. Yaani ingewekwa kuwa, akiuawa albino eneo fulani basi kamata waganga wote wa eneo hilo, watatajana tu, na hata kama wanatumia uchawi, watatumia hizohizo njia za uchawi kutambua nani mwenzao aliyehusika, sio kukurupuka tu kufuta leseni.
ReplyDeletePale UD tunao anthropologists wengi tu, akina Dr. Mesaki na Masanja kwa mfano tu, ebu watumiwe pia kufanya analysis ya kwanini matukio yameongezeka kwa kasi ya ajabu hivi na hususan baada ya vyombo vya habari kuanza kutangaza???
Natoa pongezi kwa uamuzi uliotolewa kwa halmashauri zote nchini kuwa albino wote wanaosome secondary wawekwe boarding schools, hizi ndo baadhi ya solution na sio kuleta siasa mahala ambapo hapastahili.
Mwisho naomba jamani, hili tumeshaoina ni janga, na kwa kweli watu wenzetu wanauawa, sasa na albino wenyewe wawe makini, wazazi wenye watoto albino pia wawe makini, unajua pamoja na kuwa serikali na wadau mbalimbali wanawatetea na mimi naunga mkono utetezi huo kabisa, lakini nao wawe makini. Ni kama ukiwa unafuga kondoo, kijiji kikiingikiwa wa simba lazima uwe makini na mifugo yako. Wenzetu wawe makini, ikiwezekana wageni wanaokuja usiku nyumbani wasikaribishwe na mambo mengine kibao, sasa unakuta mwanamama anaye mtoto mdogo albino, anatembea tu barabarani peke yake mida ya jioni au sehemu zisizokuwa na watu, au anamtuma mtoto dukani peke yake, akamtwe kisha tulaumu??? kweli??? tuchukue tahadhari wakati tukijaribu kuwatafuta wahusika ni akina nani.
Halafu wanasiasa wanafuta leseni??? huu ni uongo wa wazi wazi, kwani siasa za Tanzania zimegubikwa na uchawi mtuuuuupu, na wao ndo wateja. Leo waganga wakitoweka sijui wanasiasa wetu uchuro wataenda wapi, wanatufanyia dangaya danganya tu hiyo. Nawasilisha
hili swala linaitia Tanznania katika hali mbaya sana ya kujitangaza na kujivunia amani yetu.Kwenye nchi za ngambo wanaliita unazist. yaani ni ubaguzi na ni ugonjwa. Ni aibu tupu kwa mtu Kufikia katika hali hiyo(eti imani?,imani gani ambayo haikubaliki na jamii?kama wanaimani basi wafanye kitu cha maana cha maendeleo cha kuigwa na jamii)
ReplyDeleteHao (mashetani)WABUMBUWAZI waache kazi yao ya kuuwa hao ndugu zetu albino kwani haitawasaidia kitu chochote!!!
Hongera bwana Michuzi kwa kutuletea habari ya maendeleo na jitiada ya kujikwamuwa kwa nchi yetu kuelekea kwenye maendeleo,naamini iko siku Tanzania itakuwa moja ya nchi tajiri na za mfano wa kuigwa hapa duniani,ila cha umuhimu ni ushirikiano na upendo wa dhati.